Bunge letu na kombe la Kagame

Pole sana mtani, najua usimba ndio unaokusumbua, ila jifunze kujua kuwa Yanga ni timu ya Tanzania hivyo ina haki ya kwenda Bungeni kama watanzania wengine. YANGA DAIMA MBELE.........

Well said Mkuu na kwa kuongezea tu,
Club ya Taifa iliyoipeperusha bendera ya Taifa vizuri kwa kuzishinda team za mataifa mengine zaidi ya 10
 
Wadau,

Wadau wenye upeo katika medani za kimataifa ni bunge lipi jingine ulimwenguni hufanya hivi?


Spika na waheshimiwa MPs kama mnapita humu hebu msitupotezee muda kesho na makombe mjengoni.....
....

Pole, wivu hauko kwenye mapenzi tu hata huu wako ni wivu tena ule wanosema wivu kidonda...pole sana
 
Hakuna userious wowote huko. Watu badala ya kuwaza mambo ya msingi kuwaondoa wananchi kwenye shida wao wanafikiria kushangilia kombe la Kagame ama Ngao ya Hisani. Bunge letu linasikitisha. Badala ya kutafakari na kusoma kwa makini miswada ya sheria kabla ya kuipitisha wao wanawaza ushabiki wa Simba na Yanga. Hawana muda wa kujadili hoja lakini wana muda wa kushangilia Kombe la Kagame ama Ngao ya Hisani. Kuna siku nitapeleka kombe la Mbuzi ama Kombe la KImbunga ndani ya Bunge. Afadhali ingekuwa kombe ambalo limetwaliwa na timu ya Taifa badala ya vilabu. Nimekereka kweli

Mhe. Kimbunga, unasema sahihi kuwa hawatumii muda wao vizuri kwa kuongelea mambo ya ajabu kama vilabu kutwaa ubingwa n.k. Tatizo hapa kwetu ni kwamba hata hao wanaokuwa wanaongelea mambo ya msingi wengi wanaongea upuzi! Na kuhusu kuw angalau ingekuwa timu ya taifa ndio imetwaa ubingwa, si ndoto ya kutegemea mara kwa mara kwa sababu ni bidhaa adimu sana kupata taji la timu ya taifa...

Si umesikia hata wawakilishi walioenda London kuiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya kuogelea walienda kujifurahisha? Kwa nini wasingeenda Bagamoyo, au hata pale Ferry wakaogelea, wakajifurahisha hadi wakachoka. Kwa namna hiyo ni lini tunategemea ushindi wa taifa?
 
Heading imenishangaza sana, Kombe lilikuwa halijafika Bungeni umeshaanza kulalama, umekuwa MTABIRI! Ungesubiri lifike Bungeni ndio uanze kutoa kasoro la Bunge letu

Mkuu limeshafika sasa....yaleyale
 
Mkuu Bovidae ina maana kwa kuwa timu za taifa hazishindi ndio maana wabunge wanakuwa na hamu ya makombe hadi kukubali hata ngao ya hisani na mwishowe watakpokea kombe la mbuzi! Nimesikia kesho Spika atapokea Bao na watacheza bao kati ya CCM na wapinzani!

Mkuu hiyo ya Olympic mimi nasubiri bifu la Filiberf Bayi na Gidabudai.
 
Last edited by a moderator:
Mhe. Kimbunga, unasema sahihi kuwa hawatumii muda wao vizuri kwa kuongelea mambo ya ajabu kama vilabu kutwaa ubingwa n.k. Tatizo hapa kwetu ni kwamba hata hao wanaokuwa wanaongelea mambo ya msingi wengi wanaongea upuzi! Na kuhusu kuw angalau ingekuwa timu ya taifa ndio imetwaa ubingwa, si ndoto ya kutegemea mara kwa mara kwa sababu ni bidhaa adimu sana kupata taji la timu ya taifa...

Si umesikia hata wawakilishi walioenda London kuiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya kuogelea walienda kujifurahisha? Kwa nini wasingeenda Bagamoyo, au hata pale Ferry wakaogelea, wakajifurahisha hadi wakachoka. Kwa namna hiyo ni lini tunategemea ushindi wa taifa?

Bovidae..watu hawana userious kabisa..hata humu tunawalaumu viongozi wakati sisi wenyewe tuna misimamo hiyohiyo ya kishabiki..nimemsikiliza spika anaongea vitu visivyo na msingi
hatusemi hapa kwa kuwa ni Yanga..hata ingekuwa simba ama azam hata jamhuri isingefaa...tunajenga utamaduni gani
Inanikumbusha uzi wa mdau mmoja kule siasa inasema bunge letu si tukufu....kila kitu kinaingia kama kimbunga alivyotanabaisha kupeleka kombe lake siku moja.imagine kuna challenge,Tusker,shirikisho,Club championiship etc..sounds good kama ingekuwa ngazi ya timu za taifa
 
Wenye nchi wamenda bungeni ile ndo tanganyika bwana wengine feki,. Yanga juuuuu,,..
 
Wabunge Simba, Yanga 'wapigana vijembe' Send to a friend
Monday, 06 August 2012 22:22

Oliver Albert na Reginald Miruko, Dodoma
BAADHI ya wabunge wa Bunge la Muungano, jana waliligeuza Bunge, kama 'kijiwe' cha muda cha kupigana vijembe vya soka, wakati mabingwa wa Kombe la Kagame, Yanga walipotinga ndani ya Ukumbi wa Bunge ili kutambulisha taji lao kwa mwaka wa pili mfululizo.
Yanga walitwaa taji la Kagame wiki mbili zilizopita, baada ya kuifunga Azam FC mabao 2-0 katika mchezo wa fainali kwenye Uwanja wa Taifa, hiyo ikiwa ni mara ya pili, baada ya mwaka jana kufanya hivyo walipoifunga Simba bao 1-0 kwenye uwanja huo.
Vijembe hivyo vilianza muda mfupi baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kulitambulisha Bunge uwapo wa wachezaji na viongozi wa Yanga ndani ya ukumbi.
Wakati wabunge mashabiki wa Yanga wakilipuka kwa nderemo na vifijo kufuatia utambulisho huo, hali ilikuwa tofauti kwa wabunge mashabiki wa Simba ukumbini hapo.
Katika kujipoza, wabunge wa Simba, waliwajibu wenzao kwa kuwanyoshea mkono mmoja, ikiwa ni ishara kuwakumbusha kipigo cha mabao 5-0 walichopata kwenye mechi ya Ligi Kuu msimu uliopita.
Pamoja na uchache wao bungeni na kufunikwa na makofi na kelele za wabunge mashabiki wa Yanga, bado wabunge mashabiki wa Simba hawakuwa nyuma kuwajibu.
Kelele za 'tano bila...tano bila', zilisikika kutoka kwa baadhi ya wabunge wapenzi wa Simba, huku wale wa Yanga wakionyesha ishara ya mkono mmoja (maama yake ni kwamba Yanga imetwaa Kombe la Kagame mara tano).
Aliyekuwa wa kwanza kunyoosha mkono, ni Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage (Mbunge Tabora Mjini) kisha kufuatiwa na mbunge kijana Joshua Nassari (Arumeru) ambaye mbali na kunyosha mkono, alisema: "Tano bila... tano bila."
Awali, wakati akiwatambulisha Yanga, Spika Makinda aliwapongeza kwa kufanikiwa kutwaa taji hilo kubwa la vilabu kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
"Jamani kama watu wameleta kitu kizuri bungeni lazima niwapongeze...Yanga hongereni sana," alisema Makinda na kushangiliwa na wabunge mashabiki wa Yanga.
Aliongeza: "Lakini acheni tabia kwamba, kwa sababu nimetoa pongezi, basi mimi ni shabiki wa Yanga...siku nyingine nikiwapongeza Simba, mtasema mimi ni Simba."
Nje ya Ukumbi wa Bunge, jana hiyo kulifanyika sherehe ya kuzindua tawi jipya la wabunge wanachama wa Yanga, ambapo wachezaji na viongozi wa klabu hiyo ya Jangwani walishiriki.
Sherehe hizo zilifanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Fatma Karume. Mbunge Mohamed Misanga (Singida Magharibi), alichaguliwa kuwa mwenyekiti, huku nafasi ya Katibu ikienda kwa Geofrey Zambi (Mbozi).
 
Back
Top Bottom