Bunge letu na kombe la Kagame

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Wadau,
mara nyingi spika ama wenyeviti wabunge hulalamika kuwa muda wa kuchangia wa wabunge ni mchache kwa hoja mbalimbali na hili hudhihirika hata kwa wachangiaji kujikuta wakipigiwa kengela za kukatizwa michango yao
pia hoja nyingi binafsi kama hii ya fao la kujitoa ya SSRA pia ni yamkini zikakosa kujadiliwa kutokana na kutokuwa na muda wa

Tukirudi nyuma kuhusiana na hoja yangu kama thread heading inavyosema inashangaza bunge hilohilo lisilopata muda wa kujadili mambo mbalimbali ya msingi kwa taifa na watanzania huweza kupata muda wa kuingiza makombe ya vilabu(not national team) na kuanza kupigana vijembe

Wadau wenye upeo katika medani za kimataifa ni bunge lipi jingine ulimwenguni hufanya hivi?
Spika hukatiza hoja za wabunge na kuanza kutumia dakika kadhaa kutambulisha wanafamilia wa wabunge!
Mawaziri kutumia muda mwingi kuwataja wachangiaji kwa majina....je haitoshi kutaja idadi tu ya wachangiaji wa maandishi na wa mdomo?

Enyi wabunge are you serous kweli na TIME...dou you value muda wenu kweli na kujali gharama zinazoteketea kila siku huku serikali hiyo hiyo ikishindwa kuwakimu walimu,askar,madaktari na watumishi wengine
Lets wake up in this deep sleep and utilise the valuable time for essential issues

Spika na waheshimiwa MPs kama mnapita humu hebu msitupotezee muda kesho na makombe mjengoni mjue tunawaona na 2015 is at your door step
Enyi wabunge makini tusaidieni kwa hili....ama wenzangu Mnalionaje hili??

Pls tuchangie bila kuweka uYanga na uSimba....
 
Hakuna userious wowote huko. Watu badala ya kuwaza mambo ya msingi kuwaondoa wananchi kwenye shida wao wanafikiria kushangilia kombe la Kagame ama Ngao ya Hisani. Bunge letu linasikitisha. Badala ya kutafakari na kusoma kwa makini miswada ya sheria kabla ya kuipitisha wao wanawaza ushabiki wa Simba na Yanga. Hawana muda wa kujadili hoja lakini wana muda wa kushangilia Kombe la Kagame ama Ngao ya Hisani. Kuna siku nitapeleka kombe la Mbuzi ama Kombe la KImbunga ndani ya Bunge. Afadhali ingekuwa kombe ambalo limetwaliwa na timu ya Taifa badala ya vilabu. Nimekereka kweli
 
Poleni sana MIKIA!!!! Ibadilishe heading iendane na maelezo yako ama sivyo imekaa kiuSIMBA.
Mkuu umeonyesha rangi yako....nilijua mpo wa mawazo hayo lakini mimi sipo huko...yupe mchango wako acha unazi
 
Hakuna userious wowote huko. Watu badala ya kuwaza mambo ya msingi kuwaondoa wananchi kwenye shida wao wanafikiria kushangilia kombe la Kagame ama Ngao ya Hisani. Bunge letu linasikitisha. Badala ya kutafakari na kusoma kwa makini miswada ya sheria kabla ya kuipitisha wao wanawaza ushabiki wa Simba na Yanga. Hawana muda wa kujadili hoja lakini wana muda wa kushangilia Kombe la Kagame ama Ngao ya Hisani. Kuna siku nitapeleka kombe la Mbuzi ama Kombe la KImbunga ndani ya Bunge. Afadhali ingekuwa kombe ambalo limetwaliwa na timu ya Taifa badala ya vilabu. Nimekereka kweli
Well said Kimbunga...:A S 465::A S 465:
 
Mkuu umeonyesha rangi yako....nilijua mpo wa mawazo hayo lakini mimi sipo huko...yupe mchango wako acha unazi

Heading imenishangaza sana, Kombe lilikuwa halijafika Bungeni umeshaanza kulalama, umekuwa MTABIRI! Ungesubiri lifike Bungeni ndio uanze kutoa kasoro la Bunge letu
 
Dah hivi ulikua hujui why wanasema Yanga Team ya wananchi? Ok Mods toeni hii bla bla hapa sio mahala pake.
 
Hakuna userious wowote huko. Watu badala ya kuwaza mambo ya msingi kuwaondoa wananchi kwenye shida wao wanafikiria kushangilia kombe la Kagame ama Ngao ya Hisani. Bunge letu linasikitisha. Badala ya kutafakari na kusoma kwa makini miswada ya sheria kabla ya kuipitisha wao wanawaza ushabiki wa Simba na Yanga. Hawana muda wa kujadili hoja lakini wana muda wa kushangilia Kombe la Kagame ama Ngao ya Hisani. Kuna siku nitapeleka kombe la Mbuzi ama Kombe la KImbunga ndani ya Bunge. Afadhali ingekuwa kombe ambalo limetwaliwa na timu ya Taifa badala ya vilabu. Nimekereka kweli

Hapo bado hujazungumzia utoro. Wabunge wetu ni watoro kupita kiasi au kutohudhuria bunge kwa sababu zisizokuwa na mantiki.

Mtu anaacha kikao cha Bunge, anaenda jimboni kushamirisha vijana kwenye siasa. Mtu anaacha kikao kinaendelea yeye hahudhurii, anaenda jimboni kwa Mbunge mwengine kupiga kampeni ya chama

Ni vitu visivyoweza kutokea nchi nyengine
 
mimi nashauri mama makinda asiikarishe yanga bungeni,ila aunde tume kuchunguza pesa za rambirambi zilizoliwa na akina kaburu huu ni ufisadi mkubwa sana.
 
Sijawahi sikia wala kuona eti UEFA CHAMPION TROPHY inepelekwa HOUSE OF COMMONS (Bunge la Uingereza) kisa team ya uingereza imelichukua. Au Wabunge walisimama baada ya NEW CASTLE kushuka daraja kisa Tonny BLAIR alikua mshabiki wa tim hiyo......

Pima uelewa wa BUNGE la Tanzania kisha chukua hatua za kimapinduzi..
 
Pole sana mtani, najua usimba ndio unaokusumbua, ila jifunze kujua kuwa Yanga ni timu ya Tanzania hivyo ina haki ya kwenda Bungeni kama watanzania wengine. YANGA DAIMA MBELE.........
 
Heading imenishangaza sana, Kombe lilikuwa halijafika Bungeni umeshaanza kulalama, umekuwa MTABIRI! Ungesubiri lifike Bungeni ndio uanze kutoa kasoro la Bunge letu
Mkuu mimi si shehe wa mwembechai bali nakiona kitakachotokea kwa kulinganisha na kilichokwishatokea siku za nyuma..hata hizo club kuwa na nauli za kwenda Dodoma kutembea wakati nauli za mechi wanatembeza bakuli nayo haijakaa sawa
 
Dah hivi ulikua hujui why wanasema Yanga Team ya wananchi? Ok Mods toeni hii bla bla hapa sio mahala pake.

Mkuu,bunge na siasa ni uji na mgonjwa.. thread hii hapa ni mahali pake sahihi na ila kombe bungeni sio mahala pake
 
Hapo bado hujazungumzia utoro. Wabunge wetu ni watoro kupita kiasi au kutohudhuria bunge kwa sababu zisizokuwa na mantiki.

Mtu anaacha kikao cha Bunge, anaenda jimboni kushamirisha vijana kwenye siasa. Mtu anaacha kikao kinaendelea yeye hahudhurii, anaenda jimboni kwa Mbunge mwengine kupiga kampeni ya chama

Ni vitu visivyoweza kutokea nchi nyengine

Mkuu Gaijin hapo ulipopasema panashangaza...hivi mtu ukishakuwa MP na akili zinabadilika kuwa za kujitoa fahamu?
 
Sijawahi sikia wala kuona eti UEFA CHAMPION TROPHY inepelekwa HOUSE OF COMMONS (Bunge la Uingereza) kisa team ya uingereza imelichukua. Au Wabunge walisimama baada ya NEW CASTLE kushuka daraja kisa Tonny BLAIR alikua mshabiki wa tim hiyo......

Pima uelewa wa BUNGE la Tanzania kisha chukua hatua za kimapinduzi..
Ewaaaa...mkuu umeiona hiyo!! hapa tumetawaliwa zaidi na hisia za ubinafsi mara usimba mara uyanga hata kwenye bunge...this is too much!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom