Bunge letu letu si lazima kuiga lakini tunaweza kujifunza

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
122
Kuna taarifa (breaking news) sasa kuwa yapata watu 12 wameuwawa Colorado wakiwa katika ukumbi wa sinema nadhani 16 Century. Haya ni maafa yasiyotarajiwa kama yaliyotukuta ya wenzetu Watanzania waliofariki katika ajali ya meli visiwani juzi.

Rais Obama na mpinzani wake wamesimamisha shughuli zote za kisiasa kwa ajili ya hili tukio.

Ukweli ni kwamba baada ya kuwa ma- Rais wetu wametangaza maombolezo ya tatu isingekuwa vibaya kuendelea kuahirisha shughuli za Bunge au hata ku-dedicate muda wa Bunge kujadili tu namna ya kujikinga na kujiandaa na majanga au matatizo ya ajali za vyombo vya usafiri kwa undani. Hapa naona kuwa Tundu Lissu alikuwa sahihi kuomba ruhusa ili awasilishe hoja.

Wana CCM wenzangu tafadhali sana wakati mwingine tusiwe watu wa kuwahukumu au kudharau kila hoja eti kwa sababu tu zimeletwa na watu wa upinzani. Si lazima tuige wanachofanya USA na kwingineko lakini tunaweza kujifunza somo fulani hapa.
 
Back
Top Bottom