Bunge letu Dodoma Kuwa Wakunga wa Katiba Mpya au 'Tahrir Square' ya Tanzania?

Ni vita ya Chadema, CUF bungeni

Tuesday, 08 February 2011 21:10

mdee%20hoja.jpg


Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee akichangia hoja.

Exuper Kachenje na Habel Chidawali, Dodoma VITA ya CUF na Chadema iliyotokana na Chadema kutotaka ushirika na vyama vingine kwenye kambi yake ya upinzani, imehamia bungeni baada ya wabunge wa vyama hivyo jana kupeana mipasho katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Bunge la Kumi, ulioanza mjini Dodoma.

Kabla ya mkutano huo wa Bunge, Chadema ilieleza kuwa imeamua kuvitenga vyama hivyo kwa kuwa vinashirikiana na CUF ambayo kwa mtazamo wake, haina tofauti na CCM.

"CUF na CCM wameamua kuungana Zanzibar na kuunda Serikali ya Mseto na kwa kuwa sheria ya vyama ya Zanzibar ndiyo inayotumika pia Tanzania Bara, Chadema imeona CUF na CCM ni wamoja," alieleza Katiba Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alipokuwa akitoa tamko la Kamati Kuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam mwezi uliopita.

Hata hivyo, siku chache baadaye CUF, ilifanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa haina mpango kuilamba miguu Chadema ili iwaunganishe kwenye kambi hiyo ya upinzani, badala yake inaandaa barua kuliomba Bunge lipitishe kuwa na kambi mbili za upinzani bungeni.

Hoja hiyo jana ilifanya mkutano kuanza kwa moto pale Naibu Spika, Job Ndugai alipowasilisha azimio linalotoa tafsiri ya nini maana ya ‘Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni' akitaka lipitishwe na Bunge hali ambayo ilitafsiriwa kuwa ni mkakati wa "kuivunja nguvu za kisheria Chadema".

Mkutano huo ulitoa tafsiri inayobainisha kuwa kambi rasmi ya upinzani bungeni ni mjumuiko wa wabunge wote wa upinzani bila kujali vyama wanavyotoka hivyo kutoa fursa kwa wabunge hao kuwa na haki ya kuchaguliwa kuongoza kamati tatu za bunge zinazohusika na Hesabu za Serikali.

Kamati hizo kwa mujibu wa kanuni za Bunge ni Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).

Hata hivyo, tafsiri iliyoongezwa katika kanuni hizo za Bunge haimwondolei uwezo Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kuteua wabunge anaowataka pale atakapokuwa akiunda Baraza la Mawaziri Kivuli.

Wakati wa mjadala huo, baadhi ya wabunge waliugeuza Ukumbi wa Bunge kuwa jukwaa la mipasho na mabishano.

Hali hiyo imejitokeza baada ya michango ya wabunge hao kuingiliwa kati na kukatishwa na wenzao waliokuwa wakichomeka maneno ya kebehi bila utaratibu, huku wengine wakiomba mwongozo wa spika na kutoa taarifa kadhaa.

Mjadala huo ulimlazimu Spika wa Bunge, Anne Makinda kusimama mara kwa mara na kutoa maelezo huku akionekana kuachia baadhi ya vijembe na kebehi zilizopenyezwa na wabunge hao.

Mabadiliko hayo yaliyogusa kanuni ya 15 kifungu cha kwanza yametokana na Msimamo wa CUF na NCCR Mageuzi kutaka Bunge liwe na kambi mbili za upinzani.

Naibu Spika wa Bunge, Ndugai aliewaeleza wabunge kuwa maombi hayo yaliyowasilishwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed.

"Maneno ya kambi rasmi ya upinzani sasa yatasomeka, kambi inayoundwa itakuwa ni ya vyama vya upinzani vyenye wawakilishi bungeni," alisema Ndugai na kuongeza: "Azimio la Kamati ya Kanuni ambayo mimi ni makamu wake inaona upo ulazima Kanuni za Bunge za mwaka 2007 zikaongezewa tafsiri na kutengua kanuni ya 15 kifungu cha kwanza."

Baada ya maelezo hayo ya Naibu Spika, Spika wa Bunge, Makinda ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni za Bunge alisimama na kueleza kuwa wenye uamuzi ni wabunge ambao watachangia hoja na baadaye kulipigia kura ambapo Kafulila alikuwa mchangiaji wa kwanza kati ya wachangiaji nane.

Akichangia hoja kabla ya kupigwa kura na kupitisha azimio hilo, Kafulila alisema mabadiliko aliyopendekeza yeye na Hamad Rashid, yataondoa mgogoro ulioibuka kati ya wapinzani na kuwezesha wabunge wengine kuwemo na kuchaguliwa kuongoza Kamati za Bunge na uwaziri kivuli.

Kafulila alisema wachache wanaopinga suala hilo, kimsingi hawana hoja zaidi ya ubinafsi wao na ubaguzi. "Wachache ambao wanapinga azimio la mabadiliko haya, sioni kama wana hoja zaidi ya ubaguzi.

Kama leo wapinzani tumepata asilimia 20 ya viti tunapingana, je itakuwaje tukipata asilimia 60?," alihoji Kafulila huku akipigiwa makofi na wabunge wengi wakiwa ni wale wa CCM.

Aliongeza: "Tuonyeshe muafaka wa kitaifa, kama umepewa kidogo huonyeshi upendo, je ukipewa 60 itakuwaje. ni muhimu tufanye kazi pamoja tofauti zetu ziwe nje na si ndani ya Bunge, tukubaliane pamoja anayekwenda kinyume awajibishwe nasi NCCR tutakuwa watiifu kwa kiongozi wa upinzani.

Bunge hili ni alama ya demokrasia." Hamad Rashid alianza kuchangia hoja hiyo kwa kukanusha kuwa CUF sio kibaraka wa CCM. Aliunga mkono hoja hiyo na kueleza kuwa CUF nayo ina haki ya kuingia katika kambi ya upinzani kama ilivyo kwa Chadema.
Hamad awaita Chadema ‘watoto'

Kiongozi huyo wa upinzani katika Bunge la Tisa alisema kuwa kinachowasumbua ndugu zao wa Chadema, ni hali ya mambo aliyoyaita ya 'kitoto' ambayo wanashindwa kufafanua mambo kwa utu uzima huku akikumbushia machungu ya Muungano kufuta kauli za Chadema wa wabunge wa Zanzibar wanachaguliwa na idadi ndogo ya wabunge.

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee ambaye hotuba yake alichangia hoja hiyo huku ikikatishwa mara kwa mara na wabunge kutoka CCM na CUF wakitaka mwongozo wa Spika, alisema wabunge wa Chadema wanalazimishwa kuungana na watu ambao haikubaliani nao kimsingi, kikanuni na kwamba huo ni mpango wa CCM.

Mdee awabatiza wapinzani wengine ‘CCM B'

"Huwezi kumlazimisha kiongozi wa upinzani bungeni, kuunda kambi ya pamoja na wabunge wa vyama vingine ambao kikatiba na kikanuni hawakubaliani, na kwamba wabunge hao ni sawa na 'CCM B' ,"alisema Mdee.

Mdee ambaye alikuiwa akitumia maneno ya ukali wakati wote wa hotuba yake alisema kama mpango huo unalenga kuzima moto wa Chadema, basi hilo halitawezekana na kwamba moto wa chama hicho utabaki ule ule.

"Kama mpango, huo ni kuzima muziki wa Chadema, nawahakikishia kuwa hamtaweza kuuzima kwani muziki wa Chadema utakuwa mkubwa zaidi bunge hili.

Hao CUF wanaotaka kutulazimisha, mbona wao mwaka 2005 waliunda kambi yao hadi walipolazimishwa, sasa waache unafiki," alisema Maneno hayo ya Mdee yalisindikizwa pia na kauli zisizo rasmi za wabunge waliosikikika wakisema, "Wanunue vyombo waanzishe bendi."

Akichangia mjadala wa azimio hilo,Tundu Lisu ambaye pia ni Mnadhibu wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni pia alipinga azimio hilo na kwenda mbali zaidi akidai kuwa Bunge linataka kuwafungisha ndoa ya lazima ambayo wao Chadema hawaitaki.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki alisema kubadilishwa au kutolewa kwa ufafanuzi ya kanuni hiyo, kunalenga kuua upinzani bungeni na kuhoji kuwa haiwezekani CCM ambayo inaongoza Serikali ikaweka utaratibu wa kuwaundia kamati za kusimamia fedha za umma.

"Hapa inaonyesha kuwa tunataka kufungishwa ndoa ya lazima kama walivyofanya kule ng'ambo ya bahari (Zanzibar), hivi kuna maana gani kwa mbunge anayetoka chama chenye mbunge mmoja katika nchi akapewa jukumu la kusimamia fedha za umma au mbunge kutoka Zanzibar ambaye wapiga kura wote wa wabunge hao hawafikii idadi ya wapiga kura wa mbunge mmoja tu John Mnyika wa Ubungo," alihoji Lisu na kuongeza: "....Kamwe haitawezekana, watu tunaotaka kuwaondoa madarakani, leo hii tuwape madaraka ya kutuundia kambi ya upinzani bungeni.

Hivi hapo tunategemea kupata nini ndani? Hapa tutapoteza usimamizi wa fedha za Serikali," alisema Lisu. Kauli hiyo ya Lisu ilimkera Mbunge wa Bariadi, Mashariki na mwenyekiti wa UDP, John Cheyo aliyeingilia kati, bila ruhusa ya spika na kusikika akisema, "This is not true, (hii si kweli), mimi nimeongoza kamati hiyo, kwa ufanisi na uadilifu mkubwa," alisema Cheyo na kutoa karipio akimtaka Lisu kufunga mdomo.

Cheyo ataka wabunge wa Chadema wapunguze jazba Katika mchango wake kabla ya Lisu, Cheyo aliwataka wabunge wa Chadema kupunguza hasira na jazba badala yake kukubaliana na wabunge wa vyama vingine kuwa mbunge yoyote wa upinzani anaweza kuongoza kamati za fedha.

"Chadema punguzeni hasira ili tutengeneze bunge linalotegemewa na Watanzania wote, lakini na ninyi CCM kwa kuwa kura zimepita hebu tawaleni na mtu akitaka kuwaletea kitu cha ajabu mnyamazisheni mara moja," alisema Cheyo.

Wabunge wa CCM waliochangia hoja ya azimio la mabadiliko hayo ya Kanuni za Bunge walikuwa ni George Simbachawene (Kibakwe) na Angela Kairuki (Viti Maalum) ambao wote waliunga mkono mabadiliko hayo huku wakiitupia madongo Chadema kuwa kina ubinafsi.

CHANZO: Ni vita ya Chadema, CUF bungeni

MAONI YANGU:

Jitihada za kupindisha kanuni za Bunge, kukiukwa kwa tamko la sheria za vyama vingi na misingi yake yote, dhamira ya makusudi kuleta mzaha kwa maelekezo ya dhana zima ya Demokrasia na utekelezaji wake Bungeni, yote kwa pamoja na MWAFAKA WA CCM na CUF kuwa vyama tawala Visiwani katika ardhi yetu hii hii ya Tanzania yaweza kuleta matatizo makubwa sana endapo wanaocheza danadana hii hawatofikwa na busara kwa haraka zaidi.

Wananchi kila mmoja wetu tuwakanye waheshimiwa wabunge wetu kwa dhati kabisa juu ya swala hili nyeti kiasi cha kuweza kushupaliwa na washikadau mbalimbali na tafsiri kupatikana kwamba kumbe hata hivyo CCM na CUF kwa kitendo chao hicho peke yake walishavunja Muungano wetu wa Jamhuri wa Tanzania bila kutushirikisha sisi wananchi wa upande wa Tanzania Bara katika hilo zoezi.

Kama kuna mtu yeyote atakuwa analiona hili nadhani watakimbilia haraka sana kwa CHADEMA na kuwapigia magoti ili chakato wa mgogoro wa kikatiba ambao mpaka sasa uko wazi nchini wasije wakalishikilia bango kwa ahadi kwamba TUTALIREKEBISHA NDANI YA KATIBA MPYA ambayo nayo mchakato wake utaanza hivi karibuni.

Wake up CCM and CUF Members of parliament!!!
 
Chadema MPs walk out of House

By Patrick Kisembo

9th February 2011

headline_bullet.jpg
Says MPs bent on forcing the leading opposition party into `forced marriage`
headline_bullet.jpg
Speaker: Opposition camp is headed by the party with majority opposition MPs in Parliament

Main%2859%29.jpg


Chadema legislators storm out of the National Assembly in Dodoma yesterday, protesting redefinition of the composition the official Opposition camp in the House. (Photo: Tryphone Mweji)

Drama ensued in the National Assembly in Dodoma yesterday with a walkout by furious Chadema MPs, this time over plans to make drastic changes to the composition of the opposition camp in the House.

Members of Parliament clashed over the formation of the camp, with the deputy Speaker maintaining the opposition camp should comprise all opposition parties which have representatives in the Parliament.

The controversy erupted following a motion presented in the House by the deputy Speaker, Job Ndugai, seeking to define opposition camp and its formation, as provided for in the Parliamentary Regulation 152 (1) and (3) of Parliamentary Standing orders.

Presenting the motion Ndugai said Hamad Rashid Mohamed -Wawi – CUF and David Kafulila -Kigoma South –NCCR-Mageuzi had presented their proposal to the Speaker in writing for the amendment of section (11) of Parliamentary Standing Order 113 of 2007.

"We have gone through the proposals and found out that no changes or amendments were needed. That's why I am presenting this motion in order to provide a clear definition of the opposition camp," said Ndugai.

According to the deputy Speaker, the opposition camp is clearly defined in the Section 2 of the Parliamentary Standing Order No. 14.

"That the official opposition camp in the parliament means an opposition which comprises all opposition parties which have representatives in the House," he said.

Contributing to the debate, the Kigoma South MP, Kafulila said the major aim of forming official opposition camp in parliament was to reduce conflicts among members of the opposition parties themselves.

"We have already created the concept of having an opposition within opposition parties. I think if this amendment is made, which I support, it will contribute a lot to cementing the relationship between political parties," he said.

He stressed that there was need for all opposition parties to work as one for the interest of the nation and the people they lead.

"I do not see the reason why a few people are pushing to become the official opposition party, when opposition parties are so many," said Kafulila.

He said once the regulation is amended, it will enable them to form a strong official opposition camp in the House, strengthening the running of parliament.

For his part, the Wawi MP, Hamad Rashid Mohamed told the House that CUF and NCCR-Mageuzi never influenced the parliamentary committee to make changes.

"What the committee did was to interpret the regulations. We do not want to be seen as if we have been favoured by CCM," he said.

Kawe legislator-Chadema, Halima Mdee hit back saying it was a shame for the opposition to seek applause from the CCM MPs.
"The so-called opposition parties have turned CCM–B and I see the Zanzibar issue penetrating into this Union House to forge a common ground," she said.

Mdee, who most of the time was being interrupted by MPs who raised points of order, said it was impossible for the parliament to force the leader of opposition to work with people whom he does not cope with.

"This contradicts the whole meaning of parliamentary regulations and its operations and we are sure that there is a hand of the ruling party in this," she said.

Bariadi East MP for UDP, John Cheyo was of the view that the opposition has to form one opposition camp in order to be strong.

"Tanzanians need a strong opposition camp," he said advising the ruling party MPs to support the president in his endeavour to develop the country.

"We have finished elections, now it is time for governing the country," he said.

Opposing the views of many who were supporting the changes, Chadema Chief whip, Tundu Lissu, Singida East- MP said of the other MPs, Kafulila and Hamad: "They want standing order 113 section 11 to be amended to allow them to vie for the chairmanship and not otherwise."

"If that's the case, Madam Speaker, we are breaking commonwealth traditions…and intentionally or unintentionally, we are killing the opposition in parliament," insisted Lissu.

"And what we are seeing here is for the so called opposition parties to depend on favours of the ruling party in votes. We cannot work with such people," he said.

Freeman Mbowe, official opposition leader said what the MPs were trying to achieve was to force the opposition into ‘forced marriage'.

"We don't see the meaning of continuing with the discussions," he said, leading a walk-out by Chadema legislators from the debating Chamber.

Clarifying, Ndugai said his motion did not intend to change the parliamentary standing orders, but to "define the meaning of opposition in the Parliament."

Speaker, Anne Makinda said: "The Opposition camp is headed by the party which has majority opposition MPs in Parliament. Rules and regulations allow the party to form the shadow cabinet…I don't know why Chadema legislators are always walking out."

Meanwhile, the High Court in Dodoma yesterday delivered a summons in parliament to MP for Singida-East Tindu Lissu, requiring him to report to High Court Judge Mwangesi.

The MP sought clarification on the procedure from the National Assembly Speaker Anne Makinda who said what was done was contrary to Article 11(1) of the National Assembly's procedural rules.

"When a Member of Parliament is attending the National Assembly as is the case now he or she is protected by Parliamentary immunity.

If there is any order requiring a legislator to be out of the House it has to go through the House and not otherwise," she said. Until we went to press, it was not clear what MP Lissu was being summoned for.

SOURCE: THE GUARDIAN

MAONI YANGU:

Je, tunapozungumza Kidemokrasia na kwa kuzingatia misingi yote ya UTAWALA BORA hapa nchini kwetu, serikali yetu kweli inafahamu maana halisi na tafsiri ya SAUTI YA KIKUNDI CHA WATU WACHACHE (Minority Voices) WANAPOCHUKUA HATUA YA KUTUMIA SILAHA YA KIDEMOKRASIA KUTOKA NJE YA BUNGE pindi wanapopinga jambo wasiloliafiki kimsingi??

Silaha hii ya kutoka nje ya bunge, kwa wale wanaoelewa vema demkrasia katika vitendo halisi, ni silaha hatari sana ambayo hutumika na waunguana badala ya kupigana ngumi kufuatia mijadala fulani. Silaha hii hutumika hasa pale ambapo KIKUNDI FULANI CHA WATU WENGI KINAPOTUMIA WINGI WAO VIBAYA (Majority Force) kulazimisha jambo BILA KUZINGATI MANTIKI INAYOTAWALA JAMBO HUSIKA NA AU SHERIA, TARATIBU NA KANUNI zilizopo.

Endapo itabainika kwamba serikali yetu chini ya CCM hujionea tu jambo hili kama kiji-sinema wabunge wa chama chochote wanapotibuliwa kupita kiasi na kujiamulia tu kutumia hii salaha kama hatua ya mwisho kabisa kuonyesha KUTOKUAFIKI JAMBA FULANI na pengine serikali hata ikaendelea tu kujifariji kwamba kimataifa LUGHA HII YA MWILI KIDEMOKRASIA haina gharama yake kwa taifa letu, basi watakua wanajidanganya sana mchana mchana. Lakini naamini kwamba watu wengi sana tu wenye upeo mkubwa ndani ya taifa hili wanaelewa fika tafsiri ya lugha hii.

Hakika, utawala bora ni pamoja na KULINDA VILIVYO MINORITY VOICES na pale tunaposhindwa kufanya hivyo basi mjue ya kwamba dereva wa gari lililobeba wale watu wengi huenda asifike salama; atawamwaga njiani abiria wake kabla safari haijakamilika kimatarajio. Kipimo halisia wa utawala bora katika nchi hupimika zaidi kutokama na ujumbe usiokua wa maneno tunaoupata usoni mwake mnyonge.

Mfano mzuri nchini ni kwamba bila Mwalimu Nyerere kutambua ukweli huu leo hii nchini mwetu tusingekua na huu Mfumo wa vyama vingi kamwe.

Dunia inatuangalia sana tunavyoenenda katika kujitawala huku na pengine hata kutucheka jino-pembe kama taifa lililosheheni wanadiplomasia mahiri sana kwa viwango vya kimataifa LAKINI WASIOKUA NA MAANA YOYOTE KWA SEHEMU MUHIMU YA JAMII YAKE YENYE SAUTI DHAIFU!!!

Mhesimiwa Spika, Mama Anna Makinda, kama referee kwenye jumba letu la mijadala Dodoma, wala hatuhija mtu kutukumbusha kwamba wajibu wako namba moja bungeni humo ni KUHAKIKISHA WAKATI WOTE KWAMBA SAUTI DHAIFU INAPEWA SANA UZITO, HULINDWA NA HUPEWA MOYO WA USHIRIKI SALAMA. Mimi naamini sana kwamba hali hii inaweza kabisa ikazuiliwa kwa kupendelea zaidi kutenda haki wakati wote uwapo kazini hapo.

Kinyume cha hapo mama yetu utakapoponyokwa miiko ya usimamizi wa mijadala kwa kulinda HAKI na kuanza KUTIA TIMU kwenye kile kikundi cha 'wasakata kabumbu ya nyumbani' basi hapo ndipo utakapofanikiwa sana kupanda mbegu mbaya sana (Political Animorsity) ya chuki ndani ya taifa letu. Hata kule Pemba na Unguja ile sura mbaya ya vipindi vilivyopita haikunyesha tu kama mvua; tuliilea sisi wenyewe kwa kutovutiwa sana kutenda haki!!!

Na uzoefu unaonyesha kwamba kwa hali ya aina hiyo wewe mwenyewe utakua unasaidia kwa kiasi kikubwa sana kukiangamizi hicho kikundi kipenzi au kiwakilishi chake na wananchi nao kusubiri kukirudishia KURA ZA CHUKI hivo hivo kama ishara ya kutaka kumtetea mnyonge aliyeonekana kunyongwa hadi na HAKI YAKE bungeni - Ndugu Ndugai, hebu litafakari kidogo hili ninalolisema hapa kwa faida ya mijadala ijayo!!!

Taifa lisiloweza kulinda vilivyo sauti dhaifu katika ngazi yoyote ya jamii haina tofauti sana na wanaukoo wanaogombania mali ya marehemu na kuwaacha solemba wajane na yatima huku wakijipongeza kama zuzu tonge linalobana kwenye koo!!!!

 
UENYEVITI KAMATI ZA BUNGE NA MASLAHI ZITAKAZOFICHULIWA TU NA
WAKATI KWA MAJONZI ZAIDI KWA UMMA NDANI YA TAIFA LETU


Kati ya wenyeviti wote wa kamati mbalimbali za bunge letu walioteuliwa siku chache zilizopita, wala sipati taabu sana nani kashika kitu gani bali zaidi jicho langu liko kwenye MASLAHI GANI itakayokua imewapeleka Waheshimiwa Lowassa na Dogo Makamba kwenye kamati husika.

Hadi hapa ni sharti kila mwananchi akodoe zaidi macho hapa bila hata simila la kutaka kusinzia kitu ndipo tutakapopata jibu nyuma ya ugawanywaji huu wa keki ya taifa bila hata ya CHADEMA kuambulia kitu huku chama fulani chenye mbunge mmoja tu kikiibuka na ushindi WA KISHINDO kushika maswala ya mahesabu ya serikali za mitaa.

Ukistaajabu ya Musa ndipo utakapojua wabunge ambao ni wapinzani mchana na usiku ni CCM ni akina nani pale mjengoni Dodoma. Hapa mtu lazima atasamehewa kabisa atakapofikiria ya kwamba kwa baadhi ya waheshimiwa wabuge wetu mwongozo wao ni: TUMBO MBEEELE KAMA TAI, UZALENDO UNAWEZA UKASUBIRI KWANZA!!!!
 
Ajali ya Maspika Bungeni Dodoma Kuteleza Jukumu la Kutetea
'Sauti za Wachache' (Minority Voices) Na Hatari yake

Kukuza Mbegu ya Siasa za Chuki kwa Taifa letu
Main%2859%29.jpg


Je, tunapozungumza Kidemokrasia na kwa kuzingatia misingi yote ya UTAWALA BORA hapa nchini kwetu, serikali yetu kweli inafahamu maana halisi na tafsiri ya SAUTI YA KIKUNDI CHA WATU WACHACHE (Minority Voices) WANAPOCHUKUA HATUA YA KUTUMIA SILAHA YA KIDEMOKRASIA KUTOKA NJE YA BUNGE pindi wanapopinga jambo wasiloliafiki kimsingi??

Silaha hii ya kutoka nje ya bunge, kwa wale wanaoelewa vema demkrasia katika vitendo halisi, ni silaha hatari sana ambayo hutumika na waunguana badala ya kupigana ngumi kufuatia mijadala fulani. Silaha hii hutumika hasa pale ambapo KIKUNDI FULANI CHA WATU WENGI KINAPOTUMIA WINGI WAO VIBAYA (Majority Force) kulazimisha jambo BILA KUZINGATI MANTIKI INAYOTAWALA JAMBO HUSIKA NA AU SHERIA, TARATIBU NA KANUNI zilizopo.

Endapo itabainika kwamba serikali yetu chini ya CCM hujionea tu jambo hili kama kiji-sinema wabunge wa chama chochote wanapotibuliwa kupita kiasi na kujiamulia tu kutumia hii salaha kama hatua ya mwisho kabisa kuonyesha KUTOKUAFIKI JAMBA FULANI na pengine serikali hata ikaendelea tu kujifariji kwamba kimataifa LUGHA HII YA MWILI KIDEMOKRASIA haina gharama yake kwa taifa letu, basi watakua wanajidanganya sana mchana mchana. Lakini naamini kwamba watu wengi sana tu wenye upeo mkubwa ndani ya taifa hili wanaelewa fika tafsiri ya lugha hii.

Hakika, utawala bora ni pamoja na KULINDA VILIVYO MINORITY VOICES na pale tunaposhindwa kufanya hivyo basi mjue ya kwamba dereva wa gari lililobeba wale watu wengi huenda asifike salama; atawamwaga njiani abiria wake kabla safari haijakamilika kimatarajio. Kipimo halisia wa utawala bora katika nchi hupimika zaidi kutokama na ujumbe usiokua wa maneno tunaoupata usoni mwake mnyonge.

Mfano mzuri nchini ni kwamba bila Mwalimu Nyerere kutambua ukweli huu leo hii nchini mwetu tusingekua na huu Mfumo wa vyama vingi kamwe.

Dunia inatuangalia sana tunavyoenenda katika kujitawala huku na pengine hata kutucheka jino-pembe kama taifa lililosheheni wanadiplomasia mahiri sana kwa viwango vya kimataifa LAKINI WASIOKUA NA MAANA YOYOTE KWA SEHEMU MUHIMU YA JAMII YAKE YENYE SAUTI DHAIFU!!!

Mhesimiwa Spika, Mama Anna Makinda, kama referee kwenye jumba letu la mijadala Dodoma, wala hatuhija mtu kutukumbusha kwamba wajibu wako namba moja bungeni humo ni KUHAKIKISHA WAKATI WOTE KWAMBA SAUTI DHAIFU INAPEWA SANA UZITO, HULINDWA NA HUPEWA MOYO WA USHIRIKI SALAMA. Mimi naamini sana kwamba hali hii inaweza kabisa ikazuiliwa kwa kupendelea zaidi kutenda haki wakati wote uwapo kazini hapo.

Kinyume cha hapo mama yetu utakapoponyokwa miiko ya usimamizi wa mijadala kwa kulinda HAKI na kuanza KUTIA TIMU kwenye kile kikundi cha 'wasakata kabumbu ya nyumbani' basi hapo ndipo utakapofanikiwa sana kupanda mbegu mbaya sana (Political Animorsity) ya chuki ndani ya taifa letu. Hata kule Pemba na Unguja ile sura mbaya ya vipindi vilivyopita haikunyesha tu kama mvua; tuliilea sisi wenyewe kwa kutovutiwa sana kutenda haki!!!

Na uzoefu unaonyesha kwamba kwa hali ya aina hiyo wewe mwenyewe utakua unasaidia kwa kiasi kikubwa sana kukiangamizi hicho kikundi kipenzi au kiwakilishi chake na wananchi nao kusubiri kukirudishia KURA ZA CHUKI hivo hivo kama ishara ya kutaka kumtetea mnyonge aliyeonekana kunyongwa hadi na HAKI YAKE bungeni - Ndugu Ndugai, hebu litafakari kidogo hili ninalolisema hapa kwa faida ya mijadala ijayo!!!

Taifa lisiloweza kulinda vilivyo sauti dhaifu katika ngazi yoyote ya jamii haina tofauti sana na wanaukoo wanaogombania mali ya marehemu na kuwaacha solemba wajane na yatima huku wakijipongeza kama zuzu tonge linalobana kwenye koo!!!!
 
Clerics snub ‘prophets of doom'



By BILHAM KIMATI, 9th February 2011

RELIGIOUS leaders have denounced acts of manipulation perpetrated by some politicians which are designed at dividing the people to the detriment of the nation.

The clerics who met in Dar es Salaam on Wednesday under the auspices of Inter-religious Committee also challenged the government to respond promptly to signs of breach of peace instead of waiting for the worst.

In his presentation under the theme 'The Role of Religious Leaders in Fostering Peace', Sheikh Hamisi Mataka, said peace, Justice and stability were intertwined entities and clerics would never remain silent when peace and justice were under threat.

"In the absence of peace there is hunger and fear. Law enforcers and other government authorities have the responsibility to cherish peace and more importantly address threats to peace. "We will always speak out loudly to highlight weaknesses," Sheikh Mataka said.

For example, he questioned the legality for the widespread tradition of people taking law into their own hands and set ablaze vehicles or kill suspects for minor offices, adding perhaps people have lost confidence in state organs.

"Why should loans be issued to students after going into rampage? Why should road bumps be installed after pupils barricade roads? There must be some degree of irresponsibility somewhere which must be addressed without delay," he said.

He said clerics always advocated for peace and should always be involved early enough to help sustain peace instead of being consulted after things have gone astray. Presenting his paper, Bishop Charles Salala from the African Inland Church, said peace was the fruit of justice, adding that where justice was denied peace also would be at risk.

"Tanzania does not belong to any political party. The country belongs to God and leaders are the entrusted guardians of peace and justice.

"Any symptoms of breach of peace must be dealt with accordingly. The culture of tolerance among different social groups must be treasured," Salala explained.

The chief guest, the IPP Executive Chairman, Mr Reginald Mengi, commended clerics for conveying God's message of peace throughout generations and urged them to continue promoting peace which begins with individuals and later communities and the nation at large.

"In the absence of peace there is chaos, conflicts, derogative remarks, fighting, hatred, irresponsibility and disregard of human dignity. We don't need any of that in Tanzania. Sometimes it is not easy to recognize the value of peace until it evaporates," Mengi said.

In their resolutions, the clerics agreed to cooperate, respect each other and exercise tolerance among different denominations.

They also agreed to form a forum to issue statements on issues pertaining to welfare of the nation. They also agreed to organise common prayers for peace in the country and other related issues in the society at large.

The clerics agreed to remind government leaders of their responsibility to address national issues at the right time instead of doing that when it was too late.

SOURCE: Daily News | Clerics snub ‘prophets of doom'

MAONI YANGU:

Yale yoote aliyoyasema huyu kiongozi wetu wa kiroho ni sahihi kabisa ka JUKUMU LA MSINGI YA DINI MBALIMBALI isipokua tu alisahau neno moja tu, ambayo hadi sasa nimeliongeza na kulikolezea wino mwekundu hapo juu.

Neno lenyewe ni HAKI; haki ikishamiri mote na kila mmoja wetu akaonekana kuhisi na kuishi uwepo wake basi kwa haraka tu utaona UMASIKI ukitoweka, amini ikireje kwa uhiari wa kila mmoja wetu na hali ya utengamano kutufunika soote kwa pamoja kama barua ndani ya bahasha.

Hivyo basi kitendo cha kiongozi wetu wa kiroho huyu kutoa somo juu ya jukumu la madhehebu katika taifa halafu akaamua tu kuliruka neno hili manaana yake ni kwamba tayari upungufu huo unatuelekeza kama taifa jinsi ambavyo tumekua tukikosewa kumbe na viongozi wetu hawa tunaowathamini sana lakini kumbe wanazungumza na wanasiasa wao hujiamulia kulionea aibu neno hili.

Sasa naanza kuona sababu zilizowafanya baadhi ya viongozi wetu wa kiroho kuwa na mitazamo tofauti juu ya tukio moja la malamiko juu ya taratibu za uchaguzi wa meya kule Arusha. Kumbe tatizo ilikuwa ni kwamba kundi moja huenda ilikua ikitete Haki, amani, na utengamano wakati kundi la pili halikuwa na neno HAKI kwenye MENU yake ya yale ya kuzungumzia!!!

Hili ni fundisho kubwa sana.


Kwa kuhitimisha, nawaomba viongozi wetu wote wa kiroho waanze kwa haraka kidogo kutufundisha juu ya haki na kulitetea wakati wote hata kama viongozi wa kisiasa wasipata cha kuwafanya wafurahike vya kutosha.
 
Taswira ya CCM haitarejea kwa staili ya Kikwete

Mwandishi wetu
FEBRUARI 5 mwaka huu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilisherehekea miaka 34 tangu kuanzishwa kwake. Kilele cha maadhimisho hayo, yalifanyika mjini Dodoma ambapo Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete, alizungumza na wananchi.

Rais Kikwete, alizungumzia mambo mengi yanayohusu chama hicho na nchi yetu kwa ujumla.

Hata hivyo si nia ya makala hii kujadili mambo yote aliyoyazungumza yakiwamo yale ambayo tayari yameonyesha kupokewa kwa maoni tofauti na wananchi wa kada mbalimbali kama ambavyo tumeona katika vyombo vya habari mbalimbali.

Moja ya mambo yanayojadiliwa sana baada ya hotuba yake ni kauli yake kwamba yeye hawajui wamiliki wa Dowans na kwamba eti hata yeye hataki walipwe. Hilo tuliache.

Lengo la makala hii ni kujadili eneo jingine kabisa katika hotuba hiyo nalo likiwa ni kupotea kwa taswira ya CCM na nia ya kufanywa mabadiliko makubwa ya uongozi ndani ya chama hicho.

Kwanza nianze kwa kumpongeza kwa kuthubutu kuwaambia viongozi wenzake waliomwezsha kushinda uchaguzi mara mbili katika kipindi kizishozidi miaka mitano kwamba chama chao kimepoteza taswira nzuri na mvuto mbele ya umma na kwamba wengi wao ni lazima waondolewe ili kukijengea taswira mpya na bora zaidi.

Mimi kama mwananchi wa kawaida kabisa ambaye ni mwanachama ninayeyumba kutokana na mikanganyiko mingi iliyojitokeza katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya utawala wake.

Naweza kusema kuwa ni miongoni mwa watu waliofurahi kusikia kwamba kwa mara ya kwanza kiongozi wa juu kabisa wa chama amekuwa na mawazo ya kuchukua hatua za kuwawajibisha watendaji ambao wamekuwa mzigo kwa chama.

Lakini ninatatizika kidogo kuelewa viongozi hao ambao uongozi wa juu una madaraka ya kuushughulikia ni upi?

Maana tumekuwa na watendaji wengi ambao walikuwa wanasimamia zoezi la rushwa wakati wa kura za maoni ambao wanaanzia katika ngazi za matawi, kata wilaya hadi mkoa.

Ni dhahiri viongozi waliohusika katika rushwa hawakuwa katika ngazi ya taifa ambako taratibu zake ziko wazi na zilizo katika mazingira ambayo huwezi kutoa rushwa kwa yoyote.

Utampa rushwa Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Mwenyekiti au Katibu mkuu utaanzaje?

Katika ngazi hiyo, hupokewa matokeo ya kila jimbo na mapendekezo ya mikoa na wilaya tayari kwa uchambuzi wakati zoezi la rushwa likiwa limekwisha kufanyika katika ngazi hizo.

Sasa Rais Kikwete anaposema viongozi watashughulikiwa ili kujenga taswira ndipo ninapojiuliza, viongozi gani? Wale walioajiriwa na CCM au wale wanaoteuliwa na mwenyekiti?

Ukiangalia katika ngazi za wilaya na mkoa, kuna watendaji wengi ambao hufanya kazi za chama ambao hushiriki katika kupanga na kutoa maamuzi makubwa katika chama katika ngazi zao ambao naamini si mwenyekiti au mwingine yeyote anaweza kuwaondoa bila kutumia utaratibu wa nyakati za uchaguzi wa chama.

Katika kundi hili, wapo wenyeviti, makatibu wa Itikadi na Uenezi, makatibu wa Uchumi na Fedha, wajumbe wa Halmashauri Kuu na wale wa Kamati za Siasa katika ngazi zote (tawi, kata, wilaya, mkoa hadi taifa).

Binafsi najiuliza, hivi wakishughulikiwa wachache tu, tena wale walioajiriwa na chama, ndiyo taswira ya chama itajengeka upya?

Hata hivyo mtizamo huu mimi unanipa tabu kidogo kwa maana naamini kwamba wananchi wa kawaida hawana jambo lolote wanalofanyiwa moja kwa moja na chama, linalowafanya wakichukie chama chao au kuharibu taswira.

Binafsi naamini, chombo kinachoweza kuharibu taswira ya chama ni serikali kutokana na wananchi wanavyoweza kutokubaliana au kulalamika kwa jinsi serikali inavyochukua maamuzi mbali mbali ambayo wao wanaona yanawaumiza.

Kwa mfano suala la Netgroup Solutions, Richmond, Dowans, EPA, uuzaji wa mabenki yetu kwa bei chee badala ya kuwaruhusu wawekezaji kuanzisha benki zao, mikataba ya madini, mishahara midogo, ugumu wa maisha unaotokana na uchumi wetu kuwa wa wasiwasi, gharama kubwa ya petroli kiasi cha wananchi kutojua EWURA ipo kwa sababu gani na wenzao wa TPDC.

Kwa hakika, haya ndiyo yanayoharibu taswira ya chama chetu, bila kuyashughulikia haya hata ukifukuza watendaji wote wa ngazi ambazo una mamlaka ya kuwaondoa hakika taswira ya chama haiwezi kurudi.

Wewe mwenyewe umeona baada ya hotuba yako ya Dodoma baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wasomi na wananchi wa kawaida walivyoonyesha kutokubaliana na suala moja tu ulilolitolea ufafanuzi la Dowans kwa kusema hata wewe hutaki walipwe na kwamba huwajui wamiliki wakati waziri wako akiwa tayari ameshawataja wale ambao wananchi wameshafanywa wasiamini kwamba ndio wenyewe kutokana na taarifa za kuchanganya wanazosoma kila siku katika vyombo vya habari.

Wananchi wanaamini kuwa wahusika wa Dowans, wako ndani ya CCM, jambo linalopewa nguvu na baadhi ya mawaziri wako wanaotuhumu kwamba kuna baadhi wanataka kutengeneza fedha kwa ajili ya uchaguzi ujao wa urais.

Ndiyo maana nakwambia, kutueleza taswira ya chama itajengwa kwa kuwaondoa viongozi walioajiriwa na chama tu huku serikali ikiendelea kuleta mikanganyiko isiyoleta majibu na kueleweka ndani ya uma, bila wakosaji kushughulikiwa ni kujidanganya.

Binafsi naona wapo viongozi walioshiriki kuvuruga chama kwa nafasi zao ambao si wa kuajiriwa au walioko katika mamlaka yako ya uteuzi wakiachwa waeendelee kuvurunda, hapo ndipo ninaposema mzee wangu Kikwete mbali ya upendo wote nilionao kwako sijakuelewa.

Tunataka kuona viongozi wote waliosababisha hali hii katika serikali yako wakiondoka au kuwajibishwa ili kujenga taswira nzuri ya chama. Mbona Lowasa, Karamagi na Msabaha na wengine wameondoka?

Mzee Benjamin Mkapa kakuachia chama ukipata ushindi wa asilimia 80, zimepungua hadi asilimia 61, angalia usimuachie atakaye gombea katika uchaguzi ujao asilimia 30 kama hutacheza karata zako vizuri.

Mabadiliko uliyoyasema yawe ya heri badala ya kuleta malalamiko makubwa na mkanganyiko ndani ya chama, vinginevyo vumilia hadi katika uchaguzi wa mwaka ujao wa chama.

MAONI YANGU:

CCM inayoendeshwa katika misingi ya upendeleo, ubaguzi, udini, chuki binafsi, ubadhirifu, kiburi na kejeli nyingi za uswahilini kwetu huku tunamoishi madongo kuinama, ubinafsi, urithishwaji wa madaraka kwa wananduku, jazba, uongo takatifu, udalali na dili dili kwa kwa huduma za serikali kwa umma, fikra za miaka ya 46, na mengine mengi tu bila kuzingatia misingi ya HAKI NA USAWA wakati wote kamwe haiwezi kuleta taswira ile ya uzalendo wa hiari wa miaka ya jana, tusahau hilo.

Siku zote mmbwa mwenye njaa kali hata kidogo haiwezi kucheza kwa uwiano sawa wa furaha pindi anapocheza na yule mmbwaa aliyeshiba tena anyelishwa na kijiko huko akiimbiwa nyimbo za kumbembeleza akamezae tonge.
 
1392203750_dfe6cc0d5f_b.jpg


Courtesy of : Dodoma | Tanzania | City Gallery - SkyscraperCity

Mtihani uliopo mbele ya bunge letu safari hii ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote ule.

Matumaini ya mwisho ya wananchi waliowengi waliojikatalia tamaa na aina ya uongoi tulionao nchini sasa yapelekwa kwa Spika Mama Anna Makinda, Job Ndungai na waheshimiwa wabunge kutolea dira mambo ya msingi ambayo mpaka sasa yameshikiliwa bango kila kona na nchi.

Aina ya mtihani uliowekwa shingoni mwa kila mheshimiwa mbunge na wapiga kura safari hii, bila kujali chama chake, dini, ubara wala visiwani, ni kutaka kuwapima kwa dhati kabisa na tukapate kujiridhisha kwamba (a) UTII WAO UKO KWA MASLAHI YETU KAMA UMMA TUNAOWACHAGUA AU BORA ZAIDI (2) UTII KWA VYAMA VYAO VYA KISIASA na vikundi vinginevyo tu??

Hivyo, kwa wabunge wanaoona mbali, wenye matumaini ya kuwekeza katika ubunge wake siku a usoni hana budi kujichagulia sasa hivi kati ya hayo mambo mawili hapo juu. Makosa katika kutumia busara zao kushughulikia vuguvugu inayoendelea nchini huenda ikabadilika kuwa makosa ya kukumbukwa kwa miaka mingi ijayo.

Sasa swali langu ni kwamba je wadau wa bunge kama vile (1) Viombo vya habari, (2) Vyama vya Siasa, (3) Wanaharakati, (4) Wasomi nchini (5) Wanafuni vyuoni, (6) Vyama vya Wafanyakazi, (7) Taasisi za Kidini na (8) Wapiga Kura kwa ujumla, ambao kwa bahati mbaya sana walionekana kusinzia katika wajibu wao, safari hii tumejindaa kiasi gani na mmbo ya Bungeni Dodoma huku Taifa zima linapogeza macho na matumaini ya mwisho kupatikana huko????

Fafanua una maana gani kusema "WADAU WA BUNGE WALIONEKANA KUSINZIA KATIKA WAJIBU WAO" Ni wajibu gani huo unaouongelea?
 
Fafanua una maana gani kusema "WADAU WA BUNGE WALIONEKANA KUSINZIA KATIKA WAJIBU WAO" Ni wajibu gani huo unaouongelea?

WADAU WA BUNGE WANAPOSINZIA KATIKA WAJIBU WAO, UFISADI HUPAA, KIBURI
KAMA KAZI, NA MASLAHI YA UMMA KUTELEKEZWA OVYO WAJUMBE
WAKIKIMBILIA MASLAHI BINAFSI ZINAZOONEKANA KULIPA ZAIDI


Thatha, hili ni swali zuri saaana!!

Huko nyuma wananchi tulifikia mahala tukapumbazwa kabisaaa na KIWANGO KIKUBWA CHA UAMINIFU hasa ambao ulionyeshwa na serikali ya awamu kwanza nchi. Hili lilikua ni jambo zuri sana viongo kutozua maswali kwa tabia ao, maamuzi na hata utetezi wa maslahi ya wote. Jambo hili katika Tanzania yetu ya sasa ni ndoto kubwa kwa upigaji dili ndio inamfanya mtu awe mashuhuri mbele ya jamii.

Lakini kwa upande wa pili wa viongozi wa awamu ya kwanza kutuaminishwa kwa kiasi kikubwa sana hivyo; wananchi ndipo tukafika mahala mambo yote tukawa KUMEACHA ASIMILIMIA MIA KWA MIA kwamba hilo serikali yetu itatenda tu na wala hatuna haja ya (1) kufuatilia kitu, (2) kuhoji, (3) wala kutata ushirikiswaji wetu.

Hivyo basi Ndugu Thatha, kwa ubovu huo huo hasa katika maeneo hayo matatu kubwa zaidi, Tanzania kama taifa ghafla bin vuu tukajikuta na gharika kubwa la mambo ambayo hata siku moja hatukuwahi hata kuota kwamba yaweza kweli kutokea nchi. Mfano kiongoi kuibia watu anaowaongoza, kudanganya kwa makusudi, kuminya sauti za kuleta mtazamo wa pili, ubaguzi, upendeleo ajira / mikopo / na zabuni watu kufanya biashara na serikali. Kwa maoni ya ni sisi wananchi wenyewe ndio tumejiletea haya yote kwa usingizi wetu wa poooono!!

Nasema usingizi wa pono kutupanda kichwa kwa saba sote tunajua fika kwamba maamuzi yote mazito ya nchi hufanyika bungeni na kwamba huku maofisini ni utekelezaji tu. Sasa tunaposema bungeni tunamaanisha wabunge tuliowatuma huko. Sasa aliyetumwa anapogeuka kuwa mkubwa zaidi kuliko aliyemtuma hapo ndipo mambo yanapoharibikia na maswali kuibuka zaidi na zaidi.

Wale watu ambao huwa huwatuma wabunge kule bungeni huwa ni watu lukuki ndani ya vikundi vyao mbalimbali vyenye kuhitaji kutetewa maslahi yao KAMA AMBAVYO VIKUNDI HUSIKA VYENYEWE VITAKAPOONA INAFAA na wala si atakapoona yule mjumbe wa kutumwa bungeni atakapoona inavifaa vikundi husika. Watu hawa na vikundi vyao ndio nimewataja hapo juu kama WASHIKADAU WA SHUGHULI ZOTE ZINAZOENDELEZWA KULE BUNGENI.

Sasa wadau hao kama vile waandishi wa habari, wanaharakati, wanafunzi, vyama vya siasa, askari kama wewe hivi ulivyo, na wengine wengi tu, tunaposhindwa kujikita kwenye kumpangia mjumbe wetu akaseme nini bungeni, tunapoingiwa uvivu kutaka kujua kama kweli kasema na kutetea kama ambavyo tulivyomtuma na wala si kama alivyoelekezwa maslahi binafsi nyinginezo nje kabisa ya yale yetu tuliompigia kura, nasema tunaposhindwa kutuna kumbukumbu uzuri wa mambo anayoyafanya mbunge wetu ili ije iwe ama baraka au kitanzi kwake wakati uchaguzi unapoitishwa, basi hadi hapo, hata aje akatutete wakili mahiri Mhe Masumbuko Lamwai jibu sahihi ni kwamba WADAU WA BUNGE KWELI TUMESINIA KATIKA WAJIBU WETU!!!!!

Sehemu nyingi duniani, mbunge akiingia tu mkumbo wa kuunga mkono au kutokufanya hivyo ovyo ovyo tu basi wakati wote atakua anawaota PRESSURE GROUPS (Vikundi vya Wadau wenye kushinikiza mambo yaende vipi kwa wakati gani) na jinsi watakavyomparamia jimboni na maji kuchafuka kabisa huko.

Lakini kwa kuwa wadau hatufanyi kazi zetu basi ndio unaona Mhe Ndugai anadiriki kuteremka meza kuu kuja kutetea CUF na CHADEMA waoane hata kama HOFU YA VYAMA HIVYO KUAMBUKIZANA UKIMWI kwa kuwa na wame wawili ni jambo dhahiri kabisa kuzingatiwa. Sasa wadau tungekua tunafanya kazi yetu ipasavyo lazima ingebainishwa kwa haraka sana kwamba ni kikundi gani kule jimboni kwake ilimtuma kazi hiyo au maslahi gani jimbo litakua limepata.

Ni usingizi huu wa pono ndio unaoendela kutumika hata na vyama vya siasa nchini kudiriki kuelekeza wajumbe wetu washiriki vipi bungeni KWA MASLAHI YA WATU WACHACHE ndani ya vyama hivyo na MASLAHI YA WADAU WAKUU WALIOMTUMA KWA KUWA WASINGEENEA KULE MJENGONI WOTE ILI AKAWAWAKILISHE TU sasa wao maslahi yao hufunikwa kabisa chini ya zulia na hata kusahauliwa kabisaa kwa makusudi.

Nasema USINGIZI WA WADAU WA BUNGE ni mbaya sana, ni hatari mno, na inakera sana pale usingizi huo unapotumika na wajanja kama mbolea ya kujikusanjia mavuno makubwa sana bila ustahili wowote. Lakini siku huyu mdau zoba atakapozinduka na kugundua kwa serikali za nyakati hizi si zenye kuaminika hata chembe kwa lolote basi ndipo lugha zitakapoanza kupanda zaidi misamiati. Thatha, hadi hapa najaribu kujiaminisha ya kwamba walau kiu yako ya kupata ufafanuzi utakua umetulizwa japo kwa kiasi.

Endapo jibu lako ni kinyume cha hapo juu, ndugu wala tusioneane aibu kuuliza tena na tena - mlango u wazi.
 


MAMA SPIKA: NINAVYOTAMANI UFANIKIWE KAZI HII YENYE
DHAMANA KUBWA SANA KWA TAIFA LETU!!!

Mama yangu, Mhe Anna Makinda, kwa heshima na taadhima nyingi sana napenda niseme kwamba mimi ni miongoni mwa watu ninaoamini kwamba akina mama mnaweza mkipewa nafasi.

Sasa mama yangu kuamini kwangu tu hivyo wakati mwingine huenda kusiendane na hali halisi juu ya ardhi. Ni jambo lisilopingika kwamba kadri miaka inavyoendelea ndio taifa letu tunaendelea kupata aina mpya ya wabunge wenye usomi zaidi, uzoefu zaidi, mitazamo chanya zaidi na wanaoendana zaidi na mazingira ya sasa ya utandawazi.

Hivyo sina budi kukupa moyo kwamba bunge hili unaloliongoza hivi sasa linalo nafasi bora zaidi kuibuka kuwa ni Bunge linalozidi kwa viwango zaidi.

Hata hivyo mama, ili viwango zaidi viweze kuonekana wala tusitarajie kuiona ikinyesha tu kama mvua au manemane toka angani.

Juhudi za makusudi, bidiii isiotetereka, sala za Mfalme Solomoni kujaliwa busara zaidi na moyo mpana na safi kama mnyama fisi (mnyama huyu siku zote hana aleji na nyama za aina zote za nchi kavu, majini na hata angani), uvumilivu na uwezo mkubwa wa kusoma tabia sasa yake mnyama chui, na utayari wa kujiweka mwanafunzi kwa kila mmoja wetu lazima kuzingatiwa.

Mama natamani sana ufanikiwe katika kiti hiki ili historia ikajiandikishe uzuri zaidi. Sasa kwa fikra zangu tu zile za kuwahi kusimamia mijadala huko mishuleni, nakupendekezea na huyo Dogo mwenzetu Ndugai mambo yafuatayo kuzingatiwa:

MAMBO YA MSINGI KUZINGATIWA:

1. Maslahi ya Umma na usalama wake katika mjadala / maamuzi

(jenga picha akilini ya akina mama wajane, watoto yatima, wazee wasiojiweza, waathirika magonjwa yasiotibika, wapagani, machinga, wagonjwa mahospitalini, ombaomba, wafunwa ... sisi sote ni mzigo wako na tunaguswa na hayo mambo yanayopitia mikononi mwako hapo kimaamuzi)

2. Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu (Zenye kutabirika na kuzingatiwa kwa ufanano wakati wote)
3. Haki na Umoja wa kitaifa au ngazi husika.
4. Sauti Dhaifu KUSIKIKA katika mjadala.
5. Utawala Bora na misingi yake yote.
6. Nafasi ya Mungu katika maamuzi.
7. Uzoefu na tamaduni juu ya jambo fulani.
8. Idadi ya Miswada iliyopitishwa na bunge lako - KWA MASLAHI YA UMMA.

MENGINEYO YA MUHIMU KUZINGATIWA:

9. Kusoma sana Tena Sana ili tusienende kwa Uzoefu tu.

10. Kusikiliza HOJA na kuzipima na wala si Kuwapima waliotoa hoja zenyewe.

11. Kama mcheza kandanda usikubali UDHAIFU WAKO KUJIANIKO ovyo (kuhamaki) wewe ni Hakimu huna cha kupoteza lakini unapoonyesha Kupanda jazba basi tayari utakua umetangazia umma kwa lugha ya mwili wako bila kujua kwambe wewe si hakimu tu BALI PIA NI MSHIRI MWENYE MASLAHI YA KUPOTEZA kwenye mchezo husika.

12. Kutokuchukulia Mijadala ya bunge kuwa 'Personal'. Ndani ya bunge ni kama watu wa ukoo mmoja na tunajenga nyumba yetu sote sasa SPIKA anapoanza kuruhusu wabunge kunyang'anyana fito kana kwamba tunajenga nyumba tofauti hapo chuki huchukua mimba kabisaa!!

13. Kukataa mizengwe, Rushwa, na Ubaguzi kwa ujumla wake.

14. Kufanikiwa kujijengea hali ya kuaminika, kuthaminiwa na kutabirika wengi ndani ya bunge na pia akina yakhe sie huku nje.

15. Kumtanguliza Mungu katika maamuzi yako na siku zote kumuomba busara zaidi.

16. Utayari wa kuwa mwanafunzi / wala haikupunguzii kitu isipokua inakujenga zaidi.

17. Kujenga kinga thabiti dhidi ya ITIKADI MBALIMBALI katika jamii yetu

Mwisho, naomba nikushawishi kuwaona mtu yeyote anayekukosoa kama rafiki wa karibu sana na ukayachambue fikra zake kama yanafaa basi ni kuzingatia tu. Kiukweli kabisa, katika maisha ya kila siku, mtu usiemhusu kitu wala kukuthamini kwa namna yoyote ile wala hutosikia akikupongeza wala kukukosoa jambo.

Ushiriki mwema bungeni ila kwenye WISH LISTI YANGU mie namba moja ni wewe (1) kunipa fursa ya kushiriki MOJA KWA MOJA kuandika KATIBA MPYA inayoelezea misingi ambayo ningependa mtawala yeyote akayazingatie, (2) unipe Tume huru ya Uchaguzi ili ushiriki wangu kupiga kura siku za usoni uimarike zaidi na kuondoa ugonjwa sugu wa watu kutokuona sababu ya kushiriki kupiga kura.

Vile vile natamani (3) Nione Kamati zako zinavyonitayarishia mazingira mazuri ya kujitajirisha kihalali, na wao kusimamia uzuri zaidi rasilmali za taifa usiliwe na ufisadi, na (4) wewe kusaidia viongozi wetu wa ngazi mbalimbali KUTAMBUA NA KUZINGATIA UTAMADUNI WA KIISTAARABU WA KUWAJIBIKA mambo yanapopotoka - ofisi zetu za umma ziwe kwao ni utumishi kweli na wala wasione nafasi hizo kama AJIRA.

Ni hayo tu, eeehhh mama eeh. Usikose kuumwa umasikini wetu pindi unapotupita pembeni mwa barabara zetu hizi mitaani; UWEZO UNAO wa kulifanya Bunge liwe ni chombo kinachopendeka, kuheshimika kwa hiari na watu kutafuta kusikiliza habari zake sawasawa na ilivyo JESHI LA MISRI kwa wananchi wao.


Hata na mimi hapa, kama Mjomba Mpoto, nikipata nauli bungeni nitatinga kuja kukushika mkono pindi HIYO MENYU YANGU / WISH LISTitakapotekelezwa bila ujanja ujanja ndani yake. Bungeni tunajenga nyumba moja; huu ugomvi wa kunyang'anyana fito nje ya sheria, kanuni na taratibu ni ya nini?
 
MUBARAK AACHA MISRI BILA KITU HAZINA:

AVUNA ZAIDI YA TRILIONI 109,500/- ZA KITANZANIA NA
KUNG'ARA
KULIKO HATA BILL GATES KIFEDHA


images

Sasa siri ya marais barani Afrika KUNG'ANG'ANIA SAAAANA MADARAKA yajianika kweupe mezani kule nchini Misri baada ya siku 18 ya shinikizo lenye mafanikio kwa 'Nguvu ya Umma' kuingia hadi chumbani kwake Mubarak na kukumba harufu kali ya UFISADI.

Saa moja tangu Mubarak atangazwe kuachia ngazi, waandamanaji sasa wataka AKAMATWE, APELEKWE MAHAKAMANI KWA MADHAMBI YAKE na zaidi wanasikika wakisema wanataka arejesha mabilioni ya fedha ya nchi hiyo anayodaiwa kukwapua.

CNN wao wanasema Mubarak na familia yake kwa pamoja wanazo fedha Dollar za kimarekani Bilioni 73 (Tsh 109, 500,000,000,000/-). Chanzo hicho kinasema kwamba Bill Gates ambaye ni mfanyabiashara maarufu sana duniani kote bado yuko nyuma ya Mubarak kifedha kwa kuwa yeye thamani yake Dollar za Kimarekani milioni 68 hadi sasa.

Hapa kwetu nyumbani, hata hivyo, hizo fedha za Mubarak ni VIJISENTI tu kwani wakati wowote Mhe Kikwete anakusudia kuwalipa

Sasa jamani watu tujiulize kwamba yeye Mubarak alikua na biashara gani pale Ikulu ya Misri mpaka amzidi Bill Gates na fedha kiasi hiki??? Kumbe hii ndio maana viongozi wetu wengi Barani Afrika wako tayari kufanya lolote lile alimradi wabakie tu madarakani???

Kimahesabu, hicho kiasi cha fedha kwa Mubarak katika kipindi cha utawala wake wa miaka 30 (miezi 360) ni sawa na kusema kwamba kipato chake kilikua ni
Tsh 304,166,667,000/- kila mwezi endapo alikua hakatwi kodi wala kula sehemu ya kipato chake.

I mean, you guys, THIS IS JUST TOO REDICULOUS JAMAANI!!!
 
SOON AND VERY SOON 'THE PERFECT STORM OF REAL-PEOPLE CHANGE
IS TURNING SOUTH OF SAHARAN AFRICA; A REJUVINATED
WINDOW OF PROSPERITY IS COMING VERY SOON!!!


Change; an idea whose time has ultimately come to shake-off the very Dictatorial and Corrupt roots of most African governments into a rule that that is People-Focused.

I can't just help saying that SOON AND VERY SOON WE ARE GOING TO SEE THE REAL CHANGE kissing the Tanzanian Down-Trodden majorities, I can see Zimbabwe coming clean, it is no double that Kenya is soon getting a permanent people-solution and Uganda giving leadership to the MOST DESERVING person as schemer African Union Presidents are bound to meet a rude suprise on Gbagbo's back in Ivory Coast.

Yes, soon an very soon we are going to be in the driver's seat as a Nation to chart forward the type of government we NEED in Tanzania. The country is soon going to get a re-birth of our many lost glories.

As Tanzanians we have always been a very proud people unde FAIR, PEACIFUL and most Stable government. But the once unifying foundations and national pillars are worse erroded.
 




phpThumb.php

377 × 236 - Field Marshal Tantawi, see Day than vehicles
baladeyati.com

MWANAMME ALIYEANDIKA HISTORIA MPYA NA YA KIPEKEE KATIKA UKANDA WETU HUU HATA AKAKUBALIKA NA MATAIFA YA MAGHARIBI KUSHIKA DOLA!!!

Huyu ndiye jemadari wa vita mwenye Busara isiyo kifani KUKATAA KATAKATA kutumika kuua raia wa nchini mwake.

Mhe Denis Mwamnyange, Mzee Othman na Said Mwema na viongozi wetu wengu tu wa vyombo vya usalama, kama mnaweza kusoma kitu toka kwa huyu mtu kwa sisi wananchi kucharukia dhuluma haitufanyi kuwa maadui wenye kustahili tu KIFO basi Tanzania nasi huenda tukawa na sababu kubwa sana ya kujivunia uwepo wenu.

Acha wananchi tutofautiane, tusukumani, tukosoane bila kuleta fujo lakini lengo letu sote Tanzania ilio njema zaidi japo tunafanya hivyo toka kwa MITAZAMO NA ITIKADI TOFAUTI TOFAUTI lakini hili lisifanye vyombo vya ulinzi na usalama kujiingiza na kuchukua upande huku wakiwakandamiza wengine.


Be ruthlessly NON-PARTISAN, Disciplined, Professional and realistic in all stages of your duties!!
 
Leo hii Tahrir Square wakesha na sherehe za aina yake mitaani KUKARIBISHA AINA YA UHURU NA UTAWALA WANAOUTAKA wenyewe wananchi, je Bungeni Dodoma mtatufanyia hima kutuokao taifa letu kupitia njia hii ndio tukapate KATIBA MPYA, Tume Huru ya Uchaguzi na Udhibiti wa mianya ya Ufisadi kwa taifa letu???????????????
 
Leo hii Tahrir Square wakesha na sherehe za aina yake mitaani KUKARIBISHA AINA YA UHURU NA UTAWALA WANAOUTAKA wenyewe wananchi, je Bungeni Dodoma mtatufanyia hima kutuokao taifa letu kupitia njia hii ndio tukapate KATIBA MPYA, Tume Huru ya Uchaguzi na Udhibiti wa mianya ya Ufisadi kwa taifa letu???????????????

Siku yetu ya uhuru haiko mbali mkuu
 
Siku yetu ya uhuru haiko mbali mkuu
Eewe Mwenyezi Mungu na usikilize maomba ya vinywa vyetu kwa udhati wake wote ili ukatuokoe na hawa mafisadi wenye viburi vya KINYONGA KUGOMA KUTEMBEA KWA HARAKA au kobe kugeuza kila mahali chumbani kwake pa kujikunyatia tu na kuanza kulala.

Tuoko Mungu na hawa viongozi wadhalimu wasiotambua hata mateso wanayoyapata watoto yatima huko mitaani, akina mama wajane na wazee waliochoka mbaya kama wale wazee wetu watumishi wa zamani wa Afrika Mashariki.

Mungu baba, najua siku zote hujifichi unapotajwa bila unafiki; ama ukawabadilishe mioyo hawa baadhi ya Watanzania wenzetu ambao ghafla tu wamegeuka Zizi la Mi-Fisi katikati yetu, na utajiri kuwatapika kiasi kwamba pindi WAMUONAPO MTANZANIA MWENZAMASIKILI wao hishia na mijada ya kimya kimya mioyoni jinsi tulivyo wajinga tusiopenda kuwa matajiri wakati kwao utajiri uko kila mahali tu!!!!!

Tuletee mabadiliko ya kweli na kwa mtindo tuutakao sisi wenyewe vijana wa nchi hii kwa kuwa kulipa gharama kwetu tayari tumeshajikana endapo hakutokwepo yeyote mwenye busara wa kuweza kutusikiliza; si kutusikiliza kupitia maelekezo ya tumbo lake bali ni kwa kutegemea uwezo wa akili yake.

Nasi pia tumezaliwa tu na tungependa maisha matamu kama wao lakini kupitia njia nyoofu kwa wote wakati wote !!!
 
HATA NA MIMI NINGEKUWA NAJUA UTAMU WA UFISADI KUTOKA HATA KWA NYUMBA
YA JIRANI TU WALA NISINGERUHUSU KUFUNGUA AKILI YANGU KUJIFUNZA LOLOTE
TOKA TUNISIA NA MISRI - NI AMANI ALIMRADI KULA YANGU INA UHAKIKA!!!

Kuna mahala humu ndani nimesoma mtu akiandika kwamba kwa kishindo chote cha mabadiliko yalioletwa na 'Nguvu ya Umma' Misri na Tunisia yeye wala hajajifunza kitu kwamadai kwamba apenda sana AMANI nchini.

Wala sijashtuka kitu baada ya kusoma kwamba KISHINDO KILICHOTETEMESHA BARA LOTE LA AFRIKA NA GHUBA kiutawala bado na hapa kwetu Tanzania kuna watu ambao HAWAKUJIFUNZA CHOCHOTE KITU.

Huyu mpenda amani wa nchini kwetu lakini bila halki aonekana kustaajabu sana kinachowakereketua watu mpaka kwenda kuandamana mtaani. Napenda nimhakikishie kwamba kwenda mtaani si kama uamuzi wa kwenda disko Billcanas na wala haalikwi mtu huko.

Njaa, dhuluma, maonevu yakija kukufikia pomoni --- sawa na jinsi ambavyo MTU FULANI MWENYE BUSARA FUPI ALIVYOJIPANGA HIVI SASA kila idara Bungeni Dodoma akiinuia kuziba njia zote za UMMA KUSIKIKA WALA KUPITISHIWA MATAKWA YAO (Juhudi hizo wengine tunaziona kama kujaribu kujuia jua vile na ungo mwanga wake usifike duniani), kiburi, visasi, upendeleo, ujanja ujanja wa kuzuiya kusikilizwa --- mwenyewe tu utajikuta msitari wa mbele ukiongoza na kusema; aheri ya kufa kishujaa kwa sababu ya msingi kwa taifa kuliko kuishi kwa aibu kwa maslahi ya ma-mishenitauni wa kwenye misuti ma-ofisini!!

Usinisbughudhi na swali kutaka kujua kama huyu MLETA HOJA ni miongoni mwao MAFISADI wa nchi hii amba usiku huu wa leo wataelekea kitandani kulala huku mioyo ikidunda kuhusu MWELEKEO WA KAULI YA MAMA CLINTON JUU YA 'PERFECT STORM OF CHANGE' na jisi vijana wadogo wadogo walivyofanya maajabu huko Tunisia na Misri kuleta mabadiliko wanayoyataka.

Ni kweli kabisa kwamba huyu mwenzetu 'MPENDA AMANI BILA HAKI' asingeweza hata kidogo kujifunza kitu huko kaskazini mwa Afrika. Kwa wenye maono haba, usiku wala huwa hauna tofauti na mchani - kwani yote si ni majira tu katika siku!!!
 


Social media plays role in Egypt some expected in Iran

By Michael Calderone michael Calderone – Fri Feb 11, 2:39 pm ET

cairo.jpg


As Egyptians celebrated in the streets of Cairo Friday, CNN's [COLOR=#366388 ! important][COLOR=#366388 ! important]Wolf [COLOR=#366388 ! important]Blitzer[/COLOR][/COLOR][/COLOR] posed a question to activist Wael Ghonim: "First Tunisia, now Egypt, what's next? "

Ghonim, a 30-year-old Google executive who became a symbol of the country's democratic uprising against Hosni Mubarak's authoritarian regime, replied with two words: "Ask Facebook."

"I want to meet [Facebook founder] Mark Zuckerberg one day and thank him, actually," Ghonim said.

Dictators are toppled by people, not by media platforms. But Egyptian activists, especially the young, clearly harnessed the power and potential of social media, leading to the mass mobilizations in Tahrir Square and throughout Egypt.

The Mubarak regime recognized early on that social media could loosen its grip on power. The government began disrupting Facebook and Twitter as protesters hit the streets on Jan. 25 before shutting down the Internet two days later.

In addition to organizing, Egyptian activists used Facebook, YouTube, and Twitter to share information and videos. Many of these digital offerings made the rounds online but were later amplified by Al Jazeera and news outlets around the world.

"This revolution started online," Ghonim told Blitzer. "This revolution started on Facebook."

egyptfacebook.jpg


Egypt's uprising followed on the heels of Tunisia's. In each case, protestors employed social media to help oust an authoritarian government--a role some Western commentators expected Twitter to play in Iran during the election protests of 2009.

But there was no revolution in Iran, as President Ahmadinejad cracked down brutally on protesters. While "[COLOR=#366388 ! important][COLOR=#366388 ! important]Twitter [COLOR=#366388 ! important]Revolution[/COLOR][/COLOR][/COLOR]" might have made for snappy headlines, social media alone wasn't enought to topple a strongman.

For a social media to work, it still needed a deliberate mobilization of activists on the ground. So the "Twitter Revolution" talk proved premature and led to some backlash.

Evgeny Morozov writes in his new book, "The Net Delusion: The Dark Side of Internet Freedom," that only a small minority of Iranians were actually Twitter users. Presumably, many tweeting about revolution were doing so far from the streets of Tehran.

"Iran's Twitter Revolution revealed the intense Western longing for a world where information technology is the liberator rather than the oppressor," Morozov wrote, according to a recent Slate review.

In his book, Morozov writes how authoritarian regimes can use the Internet and social media to oppress people rather than such platforms only working the other way around.

The New Yorker's Malcolm Gladwell, in a much-talked-about piece in October, wrote how the "revolution will not be tweeted."
It's true that tweeting alone--especially from safe environs in the West--will not cause a revolution in the Middle East.

But as Egypt and Tunisia have proven, social media tools can play a significant role as as activists battle authoritarian regimes, particularly given the tight control dictators typically wield over the official media. Tomorrow's revolution, as Ghonim would likely attest, may be taking shape on Facebook today.

(Photo of Egyptians in Tahrir Square in Cairo, Egypt on Feb. 11, 2011: AP/Tara Todras-Whitehill. Photo taken by NBC correspondent Richard Engel and uploaded via Twitter)

UJUMBE HAPA:

Jamii Furums za nchini Misri, ushujaa wao hivi sasa na kuthaminiwa sana na jamii hiyo, na baadhi ya nyenzo za kimawasiliano pepe walizokua wakitumia kwa ufanisi mkubwa sana na kumfanya Amiri Jeshi Mkuu wa miaka ya 47 akilazimika kutimka mbio bila kuaga.

 
VIJEMBE, MIZENGWE NA MAJUNGU BUNGENI NI LESENI YA
UHAKIKA KUWAREJESHA WABUNGE UCHWARA
USWAHILINI WAKALEE WATOTO


Kwa mtaji wa hizi kura za kuchakachua huenda wapiga kura tulipitiwa hata tukawaachia watu wa darasa la saba, la kumi na mbili na wale wa darasa la kumi na nne nao pia wakawa wamejazana kwenye viti vyetu vya uwakilishi huko bungeni.

Kwa karne hii ya 21, watu kama hawa licha ya kuwa na haki kikatiba nao kutia timu, wabunge wa aina hii ni mzigo mkubwa sana kwa wapiga kura. Kazi yao kubwa ni kuvuta posho, kuchelewesha mijadala kwa kutokuelewa kinachoendelea kwa urahisi, na wakati mwingi HULAZIMIKA KUFUATA MKUMBO ILI PICHA ISIJE IKAUNGUA kwamba ni aina mojawapo wa wabunge si riziki.

Itachukua muda kuondoa bangi vichwani mwao baadhi ya wabunge wetu ambao tafsiri ya uwakilishi mzuri ni vijembe, zomeazomea, kiongozi wa fitna na mizengwe na mambo kama hayo.

Hkika inasikitisha kwamba wabunge wa aina hii BADALA YA KUFIKIRI OBJECTIVELY KWA MASLAHI YA TAIFA, WAO HUHAMISHIA UDHAIFU WAO WA UFINYU WA kupokea changamoto za mawazo pinzani na kuanza vita dhidi ya watoa hoja alimradi tu ionekane nao wako bize na kujishughulisha huko hata kama hakuna tija wanayoletea taifa kwa michango yao.

Naamini kwa Tume huru ya Uchaguzi, hakuna chuya za aina hiyo itakayopita nje ya makubaliano ya kura zetu na kufanya wabunge wabovu kujaa mjengoni tena.
 


Follow us on
February 11, 2011 A Victory for Rights in Egypt
Dear Human Rights Supporter,
Today belongs to the people of Egypt, as they celebrate their victory in their struggle for democracy and human rights.
President Hosni Mubarak's departure is a historic moment that should mark the transition to a government that respects human rights, if the military keeps its promise to protect the achievements won by the protesters.
Human Rights Watch is working with local activists to make this happen.
Many died in this struggle. Human Rights Watch scoured hospitals and interviewed doctors in Cairo, Alexandria, and Suez, counting the number of protesters killed – 302, by our conservative estimate – so that those responsible for the deaths can be brought to justice.
By sharing the stories of those harmed and detained, we're supporting Egyptians in their fight for freedoms and dignity.
This is a moment of huge emotion and a moment of great hope for Egypt and the region. The road ahead is full of challenges, but Human Rights Watch will work to protect the gains of this courageous protest movement.
Read our live updates on the Middle East uprising >>
Listen to the sounds of jubilation in Cairo >>
Our Egypt researcher writers about her own Facebook generation for The Times >>
 


Follow us on

February 11, 2011 A Victory for Rights in Egypt

Dear Human Rights Supporter,

Today belongs to the people of Egypt, as they celebrate their victory in their struggle for democracy and human rights.

President Hosni Mubarak’s departure is a historic moment that should mark the transition to a government that respects human rights, if the military keeps its promise to protect the achievements won by the protesters.

Human Rights Watch is working with local activists to make this happen. Many died in this struggle.

Human Rights Watch scoured hospitals and interviewed doctors in Cairo, Alexandria, and Suez, counting the number of protesters killed – 302, by our conservative estimate – so that those responsible for the deaths can be brought to justice.

By sharing the stories of those harmed and detained, we’re supporting Egyptians in their fight for freedoms and dignity.

This is a moment of huge emotion and a moment of great hope for Egypt and the region.

The road ahead is full of challenges, but Human Rights Watch will work to protect the gains of this courageous protest movement.

Read our live updates on the Middle East uprising >>
Listen to the sounds of jubilation in Cairo >>
Our Egypt researcher writers about her own Facebook generation for The Times >>
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom