Bunge lawaka moto: Lissu, Msigwa na Lema watolewa nje!

Lusambara

Member
Oct 31, 2010
38
9
Sasa Bunge limepasuka tayari,

Wabunge watatu wametolewa nje ya ukumbi, Tundu Lisu, Msigwa na G. Lema
 
Wametolewa nje na Naibu speaker kwa kosa la kuongea/Kuwasha MIC bila ruhusa ya Naibu Speaker
Kuna haki hapo?
 
Kisa ni kitendo cha Naibu wa Spika kumpatia muda mrefu Lukuvi kuongea kuitetea serikali kuhusu na Hotuba ya Lema, Kambi ya upizani wamekataa kitendo hicho cha kupatiwa muda mrefu wakati si hotuba. Naibu wa spika ametumia kiti kuwatoa nje ya ukumbi kwa kazi za siku ya leo. Mambo yalikuwa magumu kweli kiasi cha hata Lukuvi mwenyewe kushindwa kumalizia hotuba yake.
 
Tundu lissu,Godbless lema,na Mch Msigwa wametolea nje kwa kukiuka utaratibu wa bunge unaowazuia zungumza pasipo ruhusa ya mwenyekiti.
 
HiVI HAWA WABUNGE WATATOANA BUNGENI MPAKA LINI?
JANA WENJE,LEO TUNDULISU,LEMA, NA MSIGWA SIJUI KESHO? KAMA MCHEZO VILE!
 
Inakuaje m'bunge atolewe njee ya ukumbi wa bunge pale anapotetea maslahi ya taifa,? Kweli ina maana gani ya kuwepo wabunge wa upinzani bungeni? Ni aibu tupu.

Mh. Lema, lisu na mchungaji wametolewa njee ya bunge kwa kusema tanzania haina amani bali ni nidhamu ya uoga? Nini kazi ya wabunge wa upinzani bungeni kama sio kuikosoa serekali..? Kwa stahili hii ni bora au nashauri wabunge wote wa upinzani waligomee bunge tuu kuliko kudhalilishwa hivi kwa mnaofuatlia bunge nadhani mmenielewa naomba kuwakilisha


mungu ibariki tanzania
 
Wametolewa nje na Naibu speaker kwa kosa la kuongea/Kuwasha MIC bila ruhusa ya Naibu Speaker
Kuna haki hapo?

Nadhani Bungeni linatawaliwa na sheria,kanuni na taratibu.Je kila mbunge akiongea bila kufuata utaratibu bunge litaendeshwa vipi ?.Anyway hakuna umeme sijui Naibu spiker kama katumia jazba ili chama chake kimfikirie siku za usoni nafasi ya uSpeaker.Nawashangaa sana magamba pamoja na wingi wake bungeni bado wanahitaji ulinzi wa kiti cha speaker.
 
Ni ule ule utoto wa CDM, Hata ningekuwa spika ningewatoa nje wanaozomea wakati wenzao wanaongea. Haiwezekani CDM tu wajione ndio wana haki ya kuongea.
Ndungai anafanya kazi kichama zaid kama mmeshndwa kuendesha bunge achieni kiti
 
Dah! Lukuvi alikuwa anamwaga hotuba ndogo, anataka mwongozo huku anachambua kila aya ya hotuba ya Lema, mh.msigwa uvumilivu umemshinda kamchana live speaker.
 
Kama wamekose sawa ni haki yao kutolewa but swali linakuja mbona magamba huwa hawatolewi!
Hapo ndo kunatatizo hata mimi napenda sheria zifuatwe lakini kwanini iwe kwa wapinzani tuu!
Magamba yanaendelea!
 
Daaaa JOB NDUGAI NAIBU SPIKA ametumia power yake ya kanuni kwa kuwatoa Wabunge tajwa kwa kushindwa kufuata utaratibu lkn imekaa kiupendeleo fulani vile kwani ata LUKUVI alikuwa amekosea au sabu ni Wazir anyway tujiachie wenyee Watz Bunge letu lilivyo
 
Back
Top Bottom