Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Rais Kikwete atavunja Bunge leo kuashiria kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu. Jambo moja ambalo nimeamini lina make sense kuanzia sasa ni kuwa hakutakuwa na uhalali wowote wakufanya tena vikao vya bajeti kwa miezi mitatu kama tunaweza kuvifanya kwa wiki tano na tena tukanikisha vizuri. Kwa hili Bunge imeonesha njia ya kufuata.
Tunasubiri kusikia/kuonahotuba ya Kikwete ya kuvunja Bunge itakavyokuwa na majigambo ya mafanikio ya serikali yake. Lakini zaidi ni nahamu ya kusikia maono yake ya Bunge jipya yatakuwaje. Kuna baadhi ya wabunge ambao kwa kweli sitosikitika kama hawatorudi Bungeni na wengine wasiporudi itakuwa ni masikitiko.
Vyovyote vile ilivyo, leo yawezekana ni mwanzo wa mabadiliko tunayoyataka; au yaweza kuwa ni marudio ya tulikotoka.
Tusubiri Vitu!