Bunge la Miongozo ya Spika, Jee Mhe, Spika ni Dhaifu, Dikteta au?

Ukweli Lema aliomba muongozo na hakumtuhumu waziri mkuu.ila kwasababu ya udenti na jazba za kitimaalum spika,kila jambo analipeleka kidikteta.Slaa unajua mengi na ukweli wote wa Arusha.baada ya Lema kusema,ntafurahi kukuona ukizungumza.hatuwezi kukubali kuona pinda anachafua chama flan kwa interest zake binafsi eti kisa ye waziri mkuu.Haihuu...
 
jamani..huyu pinda origin yake ni usalama wa taifa na amekuwa raised huko.... na hawa jamaa unawajua kazi yao kubwa ni unafiki na ukandamizaji kwa maslahi ya watawala.... na si kuhakikisha taifa lina usalama kwa maslahi ya wananchi
 
jamana kwa mliokua mnafatalia bunge la jana, mh. Mbunge wa arusha mjini Godless Jonathan LEMA, aliomba mwongozo kuwa,endapo waziri mkuu atalidanganya bunge inakuaje?? au ni mbinu za kutaka kum'bambikizia kesi kuwa kamchafulia jina waziri mkuu??

Asante sna bibie kwa kulikumbuka hili maana hata mm nilikuwa nikijiuliza maswali mengi sana kuhusiana na alichofanya mh. spika,alichokifanya Godbless Lema ilikuwa ni kuomba tu mwongozo kwa maana ya ufafanuzi.Aliomba mwongozo
https://www.jamiiforums.com
 
Kwa jinsi mambo yalivyokuwa nimeshangaa kwa nini kibao kimegeuzwa kwa Lema. Alichotaka yeye ni utaratibu wa kama waziri Mkuu analiongopea Bunge anaweza kuchukuliwa hatua gani? kwa kawaida, hapa budern of proof ilikuwa kwa PM, alithibitishe kuwa aliyoyasema hayakuwa kweli, ndio tulivyozoea siku zote. Katika uzoefu wangu mfupi wa masuala ya Bunge, sijawahi kusikia mbunge anayeomba mwongozo ndiye anatakiwa athibitishe kuhusu kile anachokiomba.

nadhani baada ya lema kutoa kauli yake, ilipaswa PM apewe nafasi ya kuthibitisha kuwa alichokisema Bungeni ni kweli.

Kama Spika ameshaanza kutilia shaka maneno ya Lema na kumbambikia mzigo ambao hakustahili, sidhani kama haki itatendeka katika hili.

Lakini kwa kuwa Lema amesema ana nindo zote, tusbiri tuone watakavyomchakachua wiki ijayo
 
yule mama kweli hilenafasi haiwezi.yuko pale kuwalinda wabunge wa sisiemu tu.alafu anakua atention sana pale mbunge yeyote wa chadema anaposimama,hatakama alikua anasoma au kuandika ataacha mpaka ahakikishe huyo mbunge amemaliza.sioni kama lema analakulitolea ufafanuzi pale,yule mama kakurupuka.
 
Hizo hamaki changanya na ule uso wenye makunyanzi, na yale meno.. loh,
Cynic, niliomba ombi lifuatalo
Wanabodi,
Angalizo: Mhe. Anna Makinda ndio Spika wetu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo anastahili heshima yake kama kiongozi mkuu wa moja ya mihimili ya dola, naomba tujadili hoja hii kwa heshima na lugha ya staa huki tukiondoa any personal attacks, tujadili speakership as an institution na sio Mhe. Anna Makinda as an individual.
Pasco.

Hata kama pen name yako ndio hii, why?. Naomba tuwe wastaarabu, tuwe na heshima na utu, tusianze personality attack, japo siujui umri wako, Mama Makinda anaweza kuwa ni mama yako au bibi yako, just imagine hayo uliyoyasema ndio angeambiwa mama yako wa kukuzaa?.
Tumkosoe tumshambulie tumbeze kwenye utendaji wake, tusiingilie maisha yake binafsi wala kuubeza utu wake!..Please!.
Tujifunze kutenganisha mtu na taasisi. Uspika ni taasisi inayashikiliwa na mtu. Naomba tujikite kwenye taasisi ya uspika na sio kwa utu wa kiongozi wa taasisi hiyo!.
 
Anna Makinda ni mtu wa Lowassa sana tu. Hapa anatafuta kummaliza Mh Pinda kiaina kwani aliongopa sana.
 
Hili ndio tatizo ninaloliona, si wananchi wala wabunge tunachotaka kuona ni makinda akiadabishwa kwa kupelekwa puta na akina lissu,lema,mnyika,zitto nk, kilichopo sasa ni nani mjuaji zaidi zaidi miongozo ya kipuuzi yenye kukamiana na kukomoana ndio inayotazamwa na kupewa heading kubwa.
Mama makinda nakupa pongezi sana kwa msimamo wako, niwakati wako kudhihirishia umma kuwa ur strong than they think. daima kanuni za bunge ndizo mwongozo.
Najua ufisadi na uozo mwingi wa ccm unawatia watu upofu na kutoona kile unasimamia ni kwa mujibu wa kanuni za bunge na sera za chama chako sababu hii ndio politics.
Tambua unafanya kazi na watu wao wanachotaka ni kukuvuruga ili uvurunde wapate cha kusema na usitegemee kusikia mazuri yako toka kwao,daima tegemea madongo maana hii ndio siasa.
Ni wachache wanaoweza kujua ni busara gani umetumia kumpa muongozo lema wa kuwasilisha uongo wa PM, bahati mbaya tupo wepesi kusahau ila kama sikosei zito amewahi kuombwa athibitishe uongo bunge lilopita.
Go makinda go spika

ndugu angalia tena vizuri hapo kwenye bold. umesema kanuni za bunge pekee ndio muongozo kisha unarudi kusema kuwa ametumia busara kumpa lema muongozo. lakini unajua kabisa alichompa lema siyo muongozo. waliotuhabarisha wanasema alimpa vitisho na kumtaka atoe uthibitisho wa madai yake. sasa hizo ndizo kanuni za bunge? kama ndizo kanuni za bunge, kazinukuu toka kifungu gani?

narudia tena kwa mantiki ya wazi zpoika hakutoa kanuni za bunge kwa lema bali alitoa agizo la kuletewa ushahidi kitu ambacho hata lema akikataa kuleta ushahidi atakuwa sawa kwa sababu kimsingi bado hajasema kama pinda kasema uongo. nionavyo mie mnyika ndiye aliyemsaidia spika katika hilo ka muongozo kwa kumsaidia vipengele vya kanuni za bunge vinavyohusika na hata spika aliappreciate kwa kubadili sehemu ya maagizo yake.

ujasiri bila hekima kwa nafasi kama spika ni aibu ndugu yangu. hata kama ni mshabiki wake, naomba utambue kuwa na mimi ni mshabiki wake pia. kama mwanamke napenda kuona akifanikiwa na kuondoa kabisa imani potofu kuwa wanawake hawawezi. sasa hili la kusaidiwa hata jamabo wazi kama hili haliwezi kupita bila kukosolewa.

samahan ndugu na pasco naona naye ankuunga mkono kla unalosema kwa kuwa naye kishamhukumu lema
 
mkuu msanifu...hapa suala ni dogo huyu naibu spika kashazoea kukurupuka..mfano bunge la 9 ndugu spika6aliwah kumkemea asikurupuke...wakuu hli lisiwashangaze cdm nimakin daima
 
Nje ya Bunge Lema akihojiwa na ITV Lema amekiri kwamba Waziri Mkuu alisema uongo na ataonyesha uongo huo tarehe 14 Feb. Wala hatuna sababu ya kupindishan maneno. Hapa Spika kama alifikiri anamsaidia PM kamkaanga mno kwa sababu sasa dunia nzima itajua jinsi ambavyo serikali imechakachua swala la Arusha. Ni nafasi nzuri mno ya CDM kuanika ukweli kuhusu kilichotokea Arusha na hapa ndipo Makinda atakapojuta. Ni rahisi kutabiri kitakachotokea: Spika atakaata ushahidi wa Lema usiwasilishwe Bungeni, lakini Lema atapata nafasi ya kumwaga ukweli wote kwa waandishi wa habari na umma. It's the first terrible mistake that this lady has done to CCM, but a great service to the country. Mimi nampongeza sana Mhe Anne Makinda, mwanamke wa kwanza kuwa Spika wa Bunge letu tukufu pamoja na kwamba hakujua alichokuwa anakifanya katika sakata hili la Lema!
 
Anna Makinda ni mtu wa Lowassa sana tu. Hapa anatafuta kummaliza Mh Pinda kiaina kwani aliongopa sana.

wabunge wa chadema ni makini kuliko vichwa vya ccm+president combined,wanachofanya chadema ni kumwingiza kwenye mitego huyu mama sababu wanajua ni kilaza na tayari ameshaingia,mtu anataka mwongozo kama waziri mkuu atakuwa analidanganya bunge,badala ya kutoa jibu anamwambia anayetoa mwongozo adhibitishe,..lema amemtuhumu pinda kuongopa between the lines lakini hakuna ushahidi kuwa kamtuhumu
 
Anne Makinda ni Spika wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Yeye ni kiongozi na ni kati ya wabunge wakongwe wa Bunge lililopo.Yeye kama kiongozi wa Bunge,anawajibika kuwalea,kuwaelekeza kwa upole na kuwaonya wabunge(makinda yake) kama ana sababu ya kufanya hivyo.Lakini,Spika Makinda yaonekana dhahiri amejawa na u-CCM na ukandamizaji wa upinzani ndani ya Bunge hasa watokao CHADEMA.Kama Lema anatakiwa kuthibitisha uongo wa Pinda,kwanini Pinda hajathibitisha habari zake 'za kuambiwa'?.Pinda ni mwanasheria.Anajua madhara ya 'hearsay evidence'.Haki ya Mungu! Makinda anayashindwa mapema makinda yake.Anaweza kusababisha ndundi Bungeni.....
 
Nje ya Bunge Lema akihojiwa na ITV Lema amekiri kwamba Waziri Mkuu alisema uongo na ataonyesha uongo huo tarehe 14 Feb. Wala hatuna sababu ya kupindishan maneno. Hapa Spika kama alifikiri anamsaidia PM kamkaanga mno kwa sababu sasa dunia nzima itajua jinsi ambavyo serikali imechakachua swala la Arusha. Ni nafasi nzuri mno ya CDM kuanika ukweli kuhusu kilichotokea Arusha na hapa ndipo Makinda atakapojuta. Ni rahisi kutabiri kitakachotokea: Spika atakaata ushahidi wa Lema usiwasilishwe Bungeni, lakini Lema atapata nafasi ya kumwaga ukweli wote kwa waandishi wa habari na umma. It's the first terrible mistake that this lady has done to CCM, but a great service to the country. Mimi nampongeza sana Mhe Anne Makinda, mwanamke wa kwanza kuwa Spika wa Bunge letu tukufu pamoja na kwamba hakujua alichokuwa anakifanya katika sakata hili la Lema!

ngoja nimprintie hii post nimtumie kwenye email address yake ya spika@bunge.go.tz
 
It's the first terrible mistake that this lady has done to CCM, but a great service to the country. Mimi nampongeza sana Mhe Anne Makinda, mwanamke wa kwanza kuwa Spika wa Bunge letu tukufu pamoja na kwamba hakujua alichokuwa anakifanya katika sakata hili la Lema!

mkuu haya maneno huyu mama akiyasoma..., anaweza kuugua kabla ya huo ushahidi haujatolewa...je ushahidi ukitolewa...? kazi kweli kweli
 
yule mama kweli hilenafasi haiwezi.yuko pale kuwalinda wabunge wa sisiemu tu.alafu anakua atention sana pale mbunge yeyote wa chadema anaposimama,hatakama alikua anasoma au kuandika ataacha mpaka ahakikishe huyo mbunge amemaliza.sioni kama lema analakulitolea ufafanuzi pale,yule mama kakurupuka.

Ultimately kiti kile kitarudi kwa Samwel Sita! Hakiwezi. mwisho tutaomba mwongozo wa Spika "Endapo Spika atashindwa kusimamia kanuni za bunge kwa sababu ya jaziba, nini kitafanyika?"
:clap2:
 
nchi hiiinatashangaza sana hata kwa yale mambo yaliyo wazi kwa Mungu na mwanadamu bado yanapindishwa. nasema mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko kwa kuwa ni Jubilee ya miaka hamsini tangu kupata uhuru. Mungu anajua kipi cha kuwapa watu waongo kwa kuwa anasema waongo na wanafiki hawatauona uso wa Mungu kwa sisi wakristo nadhani hata waislam wanahaya inayosema kwamba mnafiki anasura tatu ya kwanza akiaminiwa haaminiki, akisema anasema uongo na akiahidi atekelezi. sasa kwa hapa naona mambo yanakuwa magumu hata wanashindwa hata kiswahili chepesi wanashindwa kuelewa. Lema kaomba mwongozo lakini majibu yake ni kwamba ameambiwa alete vielelezo. sasa basi huko nyuma na siku ya kwanza ya bunge wabunge wengi waliomba mwongozo lakini hawakutakiwa kuleta vielelezo sasa sijui utaratibu umebadilika jana au inakuwaje? Nadhani ni wakati wa kuacha uongo na unafiki na kusema kweli daima kama ahadi ya TANU inayosema 'NITASEMA KWELI DAIMA UONGO KWANGU NI MWIKO'.
 
Kawekwa pale kuua upinzani..

Na kusimamia maslahi ya mafisadi
 
suleiman alimwomba mungu ampatie hekima na busara ili kuweza kuwaongoza watu wake. CCM wanamwomba mungu kuwapatia uwezo wa kuiba na kutetea uongo.
 
nchi hiiinatashangaza sana hata kwa yale mambo yaliyo wazi kwa Mungu na mwanadamu bado yanapindishwa. nasema mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko kwa kuwa ni Jubilee ya miaka hamsini tangu kupata uhuru. Mungu anajua kipi cha kuwapa watu waongo kwa kuwa anasema waongo na wanafiki hawatauona uso wa Mungu kwa sisi wakristo nadhani hata waislam wanahaya inayosema kwamba mnafiki anasura tatu ya kwanza akiaminiwa haaminiki, akisema anasema uongo na akiahidi atekelezi. sasa kwa hapa naona mambo yanakuwa magumu hata wanashindwa hata kiswahili chepesi wanashindwa kuelewa. Lema kaomba mwongozo lakini majibu yake ni kwamba ameambiwa alete vielelezo. sasa basi huko nyuma na siku ya kwanza ya bunge wabunge wengi waliomba mwongozo lakini hawakutakiwa kuleta vielelezo sasa sijui utaratibu umebadilika jana au inakuwaje? Nadhani ni wakati wa kuacha uongo na unafiki na kusema kweli daima kama ahadi ya TANU inayosema 'NITASEMA KWELI DAIMA UONGO KWANGU NI MWIKO'.

kauli ya mheshimiwa Leme iliishia na nukta (.) au kweshenmak ( ?)

nauliza
 
Back
Top Bottom