Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,571
- Thread starter
- #21
Walau hawa wanaonekana kuchukua hatua za kiutawala na kinidhamu za kuwajibishana ,hapa kwetu tatizo ni kuwa hakuna aliyetatayari kumona hatua zikichukuliwa .
Hawa ndio watu wanaojua kile wanachokifanya kwenye Bunge, angalia ufisadi wa 6 bln mtu anag'ooka lakini hapa kwetu Mramba kwenye Alex Stuwart alikatiza salama ,Mama Meghji naye akakatiza salama kwa kusema kuwa Kagoda ni national security .
sasa ni lazima wabunge wetu waweze kuiga jambo hili na kuhakikisha kuwa fisadi halikatizi kamwe.
Our Bunge should take a page out of the Kenyan Bunge's book as it were... muda wa kuoneana aibu na kulindana umekwisha.
Bunge la Kenya jana lilimng'oa Waziri wa fedha kutokana na tuhuma za Rushwa na Ufisadi kwa kumpigia kura ya kukosa imani naye .
Waziri huyu Kivuitu nafikiri wengi mtamkumbuka jinsi ambavyo alikuwa na kiburi wakati wa kujibu maswali kuhusiana na uchaguzi mkuu akishirikiana na Amos Kimunya .
Nitawaletea taarifa zaidi hapa .
Wasiwasi wangu ni kuwa huenda huu ukawa ni muendelezo wa Mapamabano ya Raila vs Kibaki.
Hatimaye Kimunya amung'unywaHatimaye KIMUNYA amejiuzulu baada kutakiwa na Rais wake ili kupisha UCHUNGUZI.
Mbona alisema yuko tayari kufa kuliko kujiuzulu, imekuwaje amekubali kujiuzulu ama kifo ndo kitafuata?
Politics za Kenya ninazipenda sana, watu wakishupalia kitu lazima wahakikishe kinafika mwisho wake. Sasa ngoja Kimunya akakalie benchi kwanza huku akitafakari zile kauli za baada ya Uchaguzi.
Martha Karua anapiga mbinja tu maana njia sasa ni nyeupe na iko wazi ndani ya NARC-Kenya na Central Region kupitia chama chake. 2012 itawafanya mawaziri wawe na nidhamu!
Alisema pia kwamba anataka kuondoka na Waziri Mkuu Odinga na vigogo wengine!
Siasa ni hasa.