Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

nguna.jpg

Je bajeti yetu itaweza kuondoa kazia kama hizi za mlo mmoja watu kumi?..Maisha bora kwa watanzania bado yataendelea kuwa ndoto za mchana!

Duu..hapo ni mtu dozen...!!! kweli bado..
 
Samora10

Ndio mkuu. Itakapofikia watu hata mlo mmoja wa kula ni shida, na serikali inakata mishahara ya watu kama Ugiriki na Ureno ndio utaelewa kitu gani nasema. Sasa hivi watu wanaona hali ngumu but mambo yanaenda. Nasubiria niisome hiyo bajeti sitaki habari za kuambiwa au kuhadithiwa.
 
TBC 1 LIVE Mustafa Mkulo anashusha mistari yenye vina kuhusiana na bajeti 2011 -2012 pata uhondo!
Mustafa-Mkulo.jpg

Mistari yenye vina ipo na ni kawaida ya Serikali ya kisanii ya Jakaya lakini tatizo lipo kwenye utekelezaji wa hiyo mipango.Kwa kawaida mipango ya kwenye makaratasi huwa inawapumbaza wengi pmj na wewe lakini Kama mngepata nafasi ya kuwahoji hawa waheshimiwa ukapata fursa pia ya kutembelea hiyo wanayosema kuwa wameshaifanya itakuwa ni kichekesho.
 
hiyo kitu inasomwa saa ngapi? mi nataka kuona bajeti mbadala itakyosomwa na mh zitto kabwe..
 
Tafadhali tujuzeni yatakayokuwa yanajuishwa kwenye bajeti za africa mashariki leo.
Wale mlioko
TANZANIA,
KENYA,
UGANDA,
RWANDA,
BURUNDI.

Fuatilieni bajeti zinaposomwa ili mtujulishe live.
Asanteni wadau.
 
hiyo kitu inasomwa saa ngapi? mi nataka kuona bajeti mbadala itakyosomwa na mh zitto kabwe..

Kawaida budget huwa inasomwa kuanzia saa kumi jioni. Hiyo mistari huenda ikawa ni hali ya uchumi wa nchi na mwelekeo wa budget ya 2011/12 na siyo budget yenyewe.
 
Sasa watanzania muda si mrefu na wafanyakazi wa mashirika ya sekta binafsi kufungashiwa viporo majumbani mwao na kwenda kuvilia kazini wakati wa mlo wa mchana, kwakua huku tuendako hata garama za kula kwakina mamalishe nahisi tutakuja kuzishindwa! kila kukicha sasa hivi kwa maisha ya mtanzania nafuu ya jana!
 
Kawaida budget huwa inasomwa kuanzia saa kumi jioni. Hiyo mistari huenda ikawa ni hali ya uchumi wa nchi na mwelekeo wa budget ya 2011/12 na siyo budget yenyewe.
Upo sahihi Mkuu, nilitaka kushangaa kama leo Mkulo amekiuka utaratibu
 
Tujulisheni saa bajeti itasomwa katika nchi uliyopo tafadhali.
TANZANIA?
KENYA?

UGANDA?
RWANDA?
BURUNDI?
 
Upo sahihi Mkuu, nilitaka kushangaa kama leo Mkulo amekiuka utaratibu

Mkuu mimi sijamuona anachokifanya lakini kwa utaratibu huwa hivyo. Kuna utaratibu kwamba budget zote za EAC zisomwe kwa siku moja kwa wakati mmoja, sasa huku Lokichogio hatuoni kama waziri wetu anasoma budget na tumeambiwa itarushwa live kuanzia saa kumi.

Jamani mbona leo makamanda wetu wa JF hawako mstari wa mbele yaani hadi sasa nakala ya budget haijatinga jamvini, kulikoni? Kamandaz wake up and walk to work! Tupeni nakala jamani
 
Mkuu hotuba ya budget haijasomwa wewe unasema umekoshwa!! Umekoshwa na nini sasa? Au unayo hotuba ya budget utuwekee hapa tuidurusu?

Jamani... budget ya nchi inangaliwa na overview ya uchumi wa nchi ambako asubuhi ya siku ya budget waziri wa Mipango (kama kungekuwa na wizara separate) anasoma mwelekeo wa uchumi nadhani kwa miaka mitatu... hotuba ya saa 10 jioni ni budget ya mwaka wa fedha... current year (inassomwa na waziri wa fedha)... wasomi wazuri wanaangalia zaidi hii ya asubuhi kwa kuwa huwa inatoa muelekeo wa kinachokuja saa kumi jioni na miaka 2 mbele.
 
Hatimaye Mkulo ameshaingia tena ndani ya bunge! Ngoja tuendelee kumsikiliza akifloor kuhusiana na bajeti! lakini chakushangaza ni kua anatupotezea muda kwa kuwashukuru wananchi saaana eti kwa kuchaguliwa kwa raisi Kikwete!
 
Back
Top Bottom