Bunge la 2005-2010: Mhagama, Slaa ndio wachangiaji hodari. Rostam Aziz ashika mkia.

epigenetics

JF-Expert Member
May 25, 2008
269
80
Kwa kipindi cha bunge 2005-2010, Mhe. Jenista Mhagama (CCM, Peramiho) amekuwa mbunge hai (active) kati ya wabunge wote (zaidi ya 270). Katika bunge hilo (2005-2010) Mhe. Mhagama aliuliza maswali ya msingi 25, maswali ya nyongeza 65, na ya kuchangia 272 na hivyo kuweka jumla ya michango yake kufikia 362.

Yeye anafuatiwa na Mhe. Ndugai (CCM, Kongwa) aliyekuwa na jumla ya michango 286, na nafasi ya tatu ikishikiliwa na Mhe. Dr Slaa (Chadema, Karatu) mwenye michango 265. Wa nne ni Zitto Kabwe (Chadema, Kigoma Kaskazini) aliyekuwa na michango 239.

Mhe. Rostam Aziz ameshika mkia kwa kutokuwa na ushiriki wowote wa kuuliza maswali ya msingi, maswali ya nyongeza, au michango kwa kipindi chote cha ubunge wake (kati ya 2005-2010) . Mbunge huyu ni pekee kutofanya hivyo katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.

Source: Do they work for us?
 
ninampenda sana jenesta mhagama...amedhihirisha kuwa uwezo wa kuongoza anao....natamani awe spika siku moja
mix with yours
 
ninampenda sana jenesta mhagama...amedhihirisha kuwa uwezo wa kuongoza anao....natamani awe spika siku moja
mix with yours

Ukitilia maanani kuwa alikuwa mmoja wa wenyeviti wa bunge ambaye mara nyingi alikuwa katika kiti cha spika ni wazi mama huyu ana mapenzi ya dhati na kazi ya kuwawakilisha wananchi. Hongera Mama Mhagama.
 
Back
Top Bottom