Bunge La 10 Lafunguliwa Rasmi

Kenyan-Tanzanian

JF-Expert Member
Nov 7, 2006
302
2
_44473687_kibodi_416_afp.jpg


"Nani bora kati ya Yanga na Simba?"

Marehemu Tanzanian musician Cool James aliuza.​



Wakuu hayo tuachie wazushi bcoz tunaeza kesha tukibisha.

Bunge lilifunguliwa leo rasmi. Kabla ya ufunguo huo vyama hasimu vya ODM na PNU (ikiwa na ODMK) vilifanya mkutano wa wajumbe wao wa pamoja chini ya Waziri Mkuu Mteule Raila Odinga na Rais Mwai Kibaki.

Kwa mara ya kwanza ndani ya historia ya kisiasa ya Kenya tangu kurejeshwa kwa siasa vya vyama vingi 1992, Bunge la Kenya halina Upinzani. Wajumbe wa pande zote mbili wameamua kufanya kazi chini ya serikali mseto au ukipenda Grand National Coalition ili kuinga mkono Mswada wa Annani na kuleta uwiano baina ya wananchi.

Baada ya ufunguo rasmi wa Bunge leo adhuhuri, limehairishwa hadi wiki ijayo. Kibaki aliwasihi wabunge wawajibike kwenye kuzipa kipa umbele na kuzipitisha miswada zifuatazo na zinazoashiriwa kutengeza mazingira mapya ya utawala nchini:

1. Bill ya National Accord and Reconciliation (Ambaye ndio itatengeza u PM wa Raila)
2. Bill ya Constitution of Kenya (Amendment) Bill (itaunda mazingira ya muungano)
3. Bill ya Establishment of Truth, Justice and Reconciliation Commission Bill
4. Bill ya Establishment of the Ethnic Relations Commission of Kenya Bill.

Hizo mbili za nyuma zitafukua na kufanyia kazi sababu za kihistoria za michafuko ya hivi juzi zaidi zikizingatia ukabila na uhasama dhidi ya Jamii za Kenya.


Kibaki, aliyecheza gemu chafu Desemba, sasa yaonekana amekubalika kama Rais ili mradi tuu Kenya iendelee kama nchi moja na watu wasiumie zaidi au kupoteza mali nyingi kuliko miezi mbili zilizopita.

Kwa maoni yangu binafsi bado naona kimbunga huko kwenye upeo kikiyumbayumba lakini kikiashiria bado kuna malumbano makali in future wakati Waziri Mkuu ataanza kutimiza majukumuu yake. Shida sio kuikubali pendekezo la Annan. Shida pia sio kuitekeleza iwe sheria. Kama kwingine kote Afrika, shida huwa kutimiza zilizowekwa saini kama mkataba baina ya kundi mbili hasimu. Hii ndio shida babu kubwa Afrika. Mikataba kibao lakini kuzizingatia au kuzifaulisha hatutaki!

Nawatakieni wikendi njema....alafu niulize naambia mnenguaji nambari wani Aisha Mandinda amerudi kwenye fomu baada ya kuuguza jeraha la mguu kwa mda. Kama hili ni la hakika basi Njenje sasa watapata kompetisheni kali toka kwa Twanga kwa mara nyingine tena

Mpole

Kenyan-Tanzanian.
 
Mkuu K-T,
Many thanks hizi info umezipa summary safi sana.
Mimi nafikiri kwamba hawa jamaa watajitahidi kutimiza yale yaliyoko katika mapendekezo ya Annan! Sidhani kama kuna mtu ndani ya Kenya anatamani ile hali ya Dec-feb ijirudie ila tu pale itakapobidi.
Huu ni muda wa Wakenya wote kukaa chini na kutafakari ili kupata suluhu ya uhasama uliojengeka kati ya makabila. Ni muda mzuri wote wafanye kazi kwa lengo moja la kuiinua kenya iwe zaidi ya pale ilipokuwa zamani...

Mungu Ibariki Afrika...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom