Bunge kutooneshwa live kwenye TV, kisa CHADEMA

Wakifanya hivyo itakula kwao vibaya mno. Hawana namna yoyote ya kuwadanganya wananchi waeleweke. Halafu chama chochote kikiwaahidi wananchi kuwa kikipewa madaraka kitaondoa usiri kenye mikataba ya uwekezaji na kurudisha utaratibu wa bunge kuwa live kitakuwa kimeipiga bao ccm.
 
Wadau,

Leo nimesoma makala kurasa za mwisho mwisho ktk gazeti la Rai la wiki iliypita ( siyo la jana) kuwa kuna mjadala wa kichini chini kwamba bunge lisioneshwa live ili kupunguza aibu ya serikali inayotokana na wapinzani haswa CHADEMA. Ieleweke kuwa mwandishi wa makala naye ameliweka kama tetesi.

Mwandishi amejenga hoja ktk mfumo wa uandishi wa kichokonozi. Wengine wanaweza kuisoma gazeti hilo. Hizi tetesi ningezikuta ktk gazeti jingine nisingezileta humu Jf.
Rai naiheshimu sana.

Fufununu hizi zinakuja wiki chache baada ya mbunge wa CCM kuonesha nia ya kutaka kupeleka hoja binafsi bungeni ili kuondoa maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu kwamba hayana tija.

Nawasilisha.

Mkuu Rai ilikuwa Zamani miaka ya 90 siyo Rai ya sasa.
 
Wadau,

Leo nimesoma makala kurasa za mwisho mwisho ktk gazeti la Rai la wiki iliypita ( siyo la jana) .
Mkuu Mwana wa Daudi
Nafikiri ulisoma kwenye gazeti la Raia Mwema ilikuwa ni Makala ya Chesi Mpilipili, labda kama makala inayofanana iliandikiwa kwenye Rai pia
 
Hii ndiyo taabu ya kuwa na magazeti ambayo yameajiri waandishi vilaza.

Wasiojua mantiki inabidi tuwafundishe kwamba bunge la Tanzania halikutaka kamwe session zake ziendeshwe kwa camera ya TV. Lilikubali hivyo kwa kushinikizwa na dhana ya transparency kwa mabunge duniani.

Kama wakifanya hivyo basi wajiondoe kwanza kwenye Commonwealth Parliaments team waende kivyao. Je, wana ubavu huo wakati rais wao kila kukicha anachanja mbuga hukohuko msikotaka bunge liige?

Hivyo usitarajie wazo hilo la RAI lipitishwe bungeni japo ninaamini CCM wote wangependa iwe hivyo.

Kumbuka kwamba hata ile kuwa na website ya bunge hawakupenda bali walilazimishwa kwamba kila Pucli Sector duniani iwe na website yake kama central information centre. Website kama hiz ndizo zimefanya tunataka law oyote hatukimbizani kwenye Goverment Shop tunakaa chumbani tuna-download.

Sijaliona hilo gazeti la RAI kwa sababu huwa silisomi. Lakini nikitoka kazini nitapita kulinunua na kama mwandishi ameweka namba ya simu nitaishia kumpa pole kuwa hilo wazo lake ni impracticable daydream!
 
hapo ndipo watajimaliza zaidi ya hapa maana hata umbea tu watu wata amini kuwa ni kweli pia Wafahamu kuwa kwa kizazi hiki hakuna siri waangalie hata vikao vyao vya ndani vya siri kesho yake tunapata habari zote tena kwa kina
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom