Hiyo sheria hawakufiria hata kidogo.... Kwa wafanyakazi wa serikali hilo wanatambua cku zote na hawana ndoto ya withdrawal benefit ila kwa secta binafsi hapo walichemka kutaka kutoa hiyo kitu.
Hata wafanyakazi wa serikali nao wana uhuru wa kuacha kazi wakati wowote kwa kutoa notisi ya saa 24 au miezi mitatu. Sheria ya hifadhi ya jamii iweke fao la kujitoa kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii. Pia sheria iruhusu wanachama wa mifuko hiyo kukopa fedha katika mifuko hiyo kwa ajili ya maendeleo yao. Tunachokiona sasa hivi ni watu wasio wanachama kufaidi na fedha za wafanyakazi.Tuwakumbushe wabunge wetu; naanza kumpigia mbunge wangu na kila mtu afanye hivyo