Bundi wazua tafrani mkutano wa CCM Kahama! Watua meza ya Lembeli, Mgeja... Wagoma kutoka ukumbini!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
  • BUNDI WAZUA TAFRANI MKUTANO WA CCM KAHAMA,
  • WATUA MEZA YA LEMBELI, MGEJA,
  • WAGOMA KUTOKA UKUMBINI,
  • DIWANI ASEMA MATUKIO YA USHIRIKINA LAZIMA YAKEMEWE

Na Patrick Mabula, Kahama

KATIKA hali ya isiyo ya kawaida Bundi wawili wameingia kwenye ukumbi wa mikutano kisha kutua meza kuu wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Kahama uliofanyika Shule ya Msingi Rocken Hill.

Kituko hicho kilitokea jana wakati ndege hao aina ya bundi walipotua katika meza waliyokaa Mbunge wa Jimbo la Kahama, Bw.James Lembeli na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bw.Hamis Mgeja.

Mbali na kutua kwenye za watu hao ambao ni mahasimu kisiasa, pia waliendelea kukaa ukumbimbi wakati shughuli za uchaguzi zikiendelea hali iliyozusha hofu miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo.

Shuhuda wetu alieleleza kuwa tukio hilo lilitokea wakati wajumbe wakijiandaa kuchagua viongozi wao, ndipo bundi ha wawili wawili waliingia kwenye ukumbi wa mikutano. Kitendo cha bundi hao kuvamia mkutano huo kiliwafanya wajumbe kutaharuki na kila mmoja akitafasiri tukio hilo kwa mtazamo wake na wengine kulihusisha na imani za ushirikana.

Wakati wajumbe wakiwa wamekaa ukumbini ghafla bundi hao waliingia ukumbini na kisha waliruka hadi kwenye meza ya Bw. Lembeli na Bw. Mgeja, kisha kusababisha matafaruku mkubwa kwa wagombea nafasi mbali mbali.

Diwani wa Kata ya Chambo Bw.Damas Joseph, alisema mambo hayo yanayodhaniwa kuwa ya kishirikina katika chaguzi za CCM ni lazima yakemewe kwa vile yanawapa hofu mbalimbali na kuwafanya baadhi kutojiamini .

Bw. Deo Ndimila tangu Kata ya Ukune alithibitisha vitendo vya kishirikina katika chaguzi za CCM mara nyingi zimekuwa zikitawala kwa baadhi ya watu kuendekeza imani hizo potofu.


Chanzo: Majira
 

Vyeo hivi JAMANI... BASI TU... MBONA VISA? Nimecheka Mpaka Mkoja karibia Utoke...
 
Hii mpya Bundiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, lakini ni kawaida maana uchawi wa wasukuma ni bundi na fisi
 
Kama sio chama cha mabundi basi ni cha shetani! Manaake mabundi mkutaanoni tena! Nadhani hata freemason hawako hivyo!
 
  • bundi wazua tafrani mkutano wa ccm kahama,
  • watua meza ya lembeli, mgeja,
  • wagoma kutoka ukumbini,
  • diwani asema matukio ya ushirikina lazima yakemewe

na patrick mabula, kahama

katika hali ya isiyo ya kawaida bundi wawili wameingia kwenye ukumbi wa mikutano kisha kutua meza kuu wakati wa mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi (ccm), wilayani kahama uliofanyika shule ya msingi rocken hill.

kituko hicho kilitokea jana wakati ndege hao aina ya bundi walipotua katika meza waliyokaa mbunge wa jimbo la kahama, bw.james lembeli na mwenyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga bw.hamis mgeja.

mbali na kutua kwenye za watu hao ambao ni mahasimu kisiasa, pia waliendelea kukaa ukumbimbi wakati shughuli za uchaguzi zikiendelea hali iliyozusha hofu miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo.

shuhuda wetu alieleleza kuwa tukio hilo lilitokea wakati wajumbe wakijiandaa kuchagua viongozi wao, ndipo bundi ha wawili wawili waliingia kwenye ukumbi wa mikutano. Kitendo cha bundi hao kuvamia mkutano huo kiliwafanya wajumbe kutaharuki na kila mmoja akitafasiri tukio hilo kwa mtazamo wake na wengine kulihusisha na imani za ushirikana.

wakati wajumbe wakiwa wamekaa ukumbini ghafla bundi hao waliingia ukumbini na kisha waliruka hadi kwenye meza ya bw. Lembeli na bw. Mgeja, kisha kusababisha matafaruku mkubwa kwa wagombea nafasi mbali mbali.

diwani wa kata ya chambo bw.damas joseph, alisema mambo hayo yanayodhaniwa kuwa ya kishirikina katika chaguzi za ccm ni lazima yakemewe kwa vile yanawapa hofu mbalimbali na kuwafanya baadhi kutojiamini .

bw. Deo ndimila tangu kata ya ukune alithibitisha vitendo vya kishirikina katika chaguzi za ccm mara nyingi zimekuwa zikitawala kwa baadhi ya watu kuendekeza imani hizo potofu.


chanzo: majira

ok kumbe na wao ni chama cha washirikina siyo
 

Wajameni KUNA NINI HUMO NDANI ya CCM-NEC ? MAPESA YA GAS nini ?
 
Kama sio chama cha mabundi basi ni cha shetani! Manaake mabundi mkutaanoni tena! Nadhani hata freemason hawako hivyo!

Hapa hata shetani atawavulia kofia CCM kwani kwa kiwango chake shetani hajawafikia na hafui dafu kwa chama kikuu cha mashirikina aka CCM
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom