Bulyanhulu/Kakola waandamana kudai maji Barrick

Msolopagazi

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
663
153
Wakazi wa Bulyanhulu na vijiji vya jirani wakiongozwa nadiwani wao wa Chadema leo wamefanya maandamano ya amani kwa kuwapa Barrick siku 30 wawe wameleta maji kakola kwani wanaishi jirani na mgodi unaotumia maji toka ziwa Victoria pia mwaka 2006 meneja alitoa dola 60,000 kwa ajili ya maji kwa kusign contract but cash haijafika kijijini mpaka leo
 
safi sana wananchi wa Kakola na Bulyankulu,naunga mkono maandamano yenu kwani huyo mwekezaji wa mgodi wa Bulyankulu hajatekeleza baadhi ya mambo yaliyo kwenye mkataba wake kama vile kuwaletea maji wana vijiji wanaouzunguka mgodi pia hajajenga shule kama alivyoahidi kipindi anauchukua mgodi toka kwa wachimbaji wadogo wadogo.
 
Hapo hapo shikamaneni waepukeni wanao wazuia kuandamana, mwishin wa siku wataleta maji hao wezi wa raslimali zetu
 
Kitu si kuomba haya ni mahitaji ya binadamu na tangu lini taifa linakuwa na mgodi unauza madini nje kwa faida lakini wakazi wa hilo eneo wanakosa kitu hata maji na kuwa na maisha mabovu? Anayehusika na kukudanya mapato ya serikali ni nani? Anayehusika kukuchunguza inform za wamiliki ya migodi na kujua kiasi gani hawa wanasema ukweli kwenye mapato ni nani? Kwanini wahusika wanakijiji hasa mkuu wa kijiji hawapewi power ya kuingia ndani ya hili jengo anytime ni nani? Aliwapa ulinzi haya makampuni ni nani? Huu ni ndio ukandamizaji na katiba mpya haitabeba dhambi za namna hii ...
 
hizo ni sera mbovu za chama cha MAGAMBA. wao wizi ndo sera zao. chadema plse tukomboeniii
 
hizo ni sera mbovu za chama cha MAGAMBA. wao wizi ndo sera zao. chadema plse tukomboeniii

Kuwa sehemu ya ukombozi kwa kuunga mkono jitihada za CHADEMA mkuu, usikae pembeni kuiomba ikukomboe! Tuungane kwa pamoja tuikomboe nchi yetu hata wanachama wa CCM wenyewe wamepigika kwa sababu wanaonufaika nayo ni hao mafisadi akina Kikwete na watoto wao akina Rizwani!!
 
huu ujio wa pipoz unafaidisha kila kiumbe hadi hao kina nape wapiga domo(mavuvuzela)
 
lakini pia inawezekena hao wenye migodi huwa wanatoa hela za maendeleo ya vijiji jirani ila zinaliwa na wajanja wachache hao ndio kwanza waahidiwe afu wenye migodi wafawatwe no stne to be left unturned
 
walijenga bugarama secondary mwaka 2005,pia walitakiwa kujenga barabara kwa kiwango cha lamo toka kakola hadi makutano ya barabara ya kahama ushirombo tangu walipochukua mgodi lkn hawajafanya hivo
 
Afrika tumelogwa na nani maana rasilmali zinakombwa kama hazina mwenyewe ni heri nchi zetu zisingejaliwa kupata rasilmali yeyote. Angalia nchi kama DRC Congo pamoja na kuwa na kila aina ya rasilmali lakini wananchi maisha yao kila kukicha afadhari ya jana kila kinachopatikana kina wanufaisha mibaka uchumi Nao wazungu wanahakikisha vita vya wazawa (wenyewe kwa wenyewe) haviishi kwa kuuza silaha kwa pande zote hasimu maanake katika vurugu hizo wanapata muda mzuri kujipanga wakuwaibia. Kama yaliyotokea Sierra Leone au yaliyompata Ken Sarowiwa huko Ogoniland nchini Nigeria. Hapa kwetu wazawa wanauawa aidha na risasi za moto au na kemikali zinazotoka kwenye migodi hayo yote eti kwa ajili ya kuwafurahisha wanaojiita wawekezaji wananaotuachia mrahaba wa asilimia tatu mashimo na ahadi uchwara zisizo tekelezeka zakuchangia huduma za maendeleo ya jamii iliyozunguka migodi.
Ama kweli Afrika ni shamba la bibi.
 
Back
Top Bottom