Tetesi: Bulembo kumrithi Kinana, katibu Mkuu CCM

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,395
Kwa taarifa za ndani kabisa, ni kwamba Mwenyekiti wa wazazi wa CCM, Addalla Bulembo ambaye ni darasa la saba kielimu anatarajiwa kumrithi Kinana ifikapo May hapo Rais Magufuli atakapoachiwa chama...

Yasemekana Rais Mstafu Kikwete, ambaye ni Mkt wa CCM kaamua kuachia kiti hicho ifikapo Mei ili ampe nafasi Rais Magufuli.
 
Elimu ya Abdalla Bulembo unaijua? Ni darasa la saba hawezi kumudu madaraka ya katibu mkuu, ilimu yake ni shida
 
Ikiwa kweli tusubiri mipasho na matusi. eg
"H....hujazaa kwa nini unazungumzia wodi ya wazazi"-----Bulembo
Akili ya darasa la saba
 
Kwa kweli tukivuta kumbukumbu wakati wakuteuliwa mpeperusha bendera ndani ya CCM,usingekuwa ujasiri wa E.Nchimbi,
S.Simba na Kimbisa kukataa majina ya mfukoni kwa sasa Magufuri ingekuwa ni historia kuwa naye alifika 5 bora.Hivyo kwa akili yangu,hawa watu Magufuri asingewaacha kama ilivyo sasa.
 
Mbowe,Kubenea,Sugu,Lema mbona wao elimu zao ni za hapa na pale lakini ndio wabunge na viongozi wa chadema.

Kwenye siasa za Tanzania elimu haitakiwi kinachotakiwa ujue kuropoka na kupiga majungu.
 
Kwa taarifa za ndani kabisa, ni kwamba Mwenyekiti wa wazazi wa CCM, Addalla Bulembo ambaye ni darasa la saba kielimu anatarajiwa kumrithi Kinana ifikapo May hapo Rais Magufuli atakapoachiwa chama...

Yasemekana Rais Mstafu Kikwete, ambaye ni Mkt wa CCM kaamua kuachia kiti hicho ifikapo Mei ili ampe nafasi Rais Magufuli.
Hao wenye elimu ya Chuo Kikuu wamefanya lipi tofauti na wa la darasa la saba,Zuma anaongoza SA.Kuna wengine hawajafika Chuo Kikuu lakini wana uwezo mkubwa wa kuongoza,ungesema Bulembo anapewa Uwaziri wa Fedha hapo ndio ningepata shida,lakini kwa ukatibu mkuu wa siasa mkuu hapo sioni shida.
 
Hapo kama huku Mwenyekiti Mzee Pombe, Katibu mkuu Bulembo basi ili timu hiyo icheze kama Barcelona inabidi itikadi na uenezi ambaye ni kiungo mchezeshaji apewe mheshimiwa sana Livingstone Lusinde.
Nahakika chama kitakuwa bora haijapata kutokea
 
Majuzi walipoitwa wasanii Ikulu nayeye alikuwepo sasa sijui na yeye ni msanii .
 
Back
Top Bottom