Bukoba ya leo

vipi biashara ya hotel huko, wateja wapo, I mean kuna wageni wa kutosha au competition ikoje?

wageni wapo sana tu,ushindani wa kibiashara ndio mkubwa kwani watu wengi wamewekeza kwenye sekta hii.
 
Kuna mabadiliko chanya yanaendelea baada ya pigo kubwa la ugonjwa wa ukimwi uliosambaratisha mkoa wa Kagera. Wana Kagera wameanza tena kujivunia mkoa wao. Kufikia 2020 tutakuwa tunazungumzia mmoja wa mikoa yenye maendeleo makubwa ktk Tanzania.

Bora pigo la ukimwi kuliko tabia hii sugu ya kutokubadilika. Nimetembelea web site ya Kituo cha Utafiti wa kilimo Maruku,wanasema Bukoba inaongoza kitaifa kwa utapiamlo,wanasisitiza tabia ya kutegemea 'Kibanja System'ndio tatizo kuu...kwa wasiofahamu mfumo huu wa kibanja ni shamba la familia (migomba michache na miche ya kahawa aliyoacha babu wa baba yako)...mf.kama baba yako alilithishwa eka moja ya kibanja na akazaa watoto 8,basi mtagawiwa visehemu vidogo...samahani ndugu zangu nahisi kufunguka. Bila kukubali udhaifu wetu hata hiyo 2020 itatukuta tunatunza mashamba ya pine. Nimetumia neno kutunza kwasababu niliambiwa hiyo miti ikifikia urefu wa mita moja wenyenayo wanauza shamba kwa wawekezaji kwa bei ya hasara! Mungu wange aga magezi anga bishabo!
 
Ulivyotaja hicho kiwanja cha ndege umenikumbusha mbali sana. Kwani wakti mmoja nikiwa wizara ya fedha muungano nilisafiri kutumia ndege ya Jeshi la wananchi kutoka Dar nikiwa naenda Bukoba kikazi. nakumbuka rubani alikuwa Meja Lwena na ndege ilikuwa HS. hakika katika kutua alimanusura atuingize ziwani kwani kulikuwa inanyesha mvua nyingi sana hapo Bukoba.

Kweli siusahau uwanja huo

By the way vipi Nsenene?
 
Naomba nijaribu kurejelea mambo flani machache na ksho ntarudi hapa kutoa maelezo ya sehemu ya2 ya habari hii na mwisho ntatakiwa kutoa msimamo wangu kulingana na nilyoyaona

Kuna ishu ya uwekezaji katka utalii ikiwa ni pamoja na hotel na vivutio vngne kama walvyoongelea baadhi ya wadau humu ndani,nachokiona ni kmoja kwamba kama unaplan ya kuwekeza nakushauri nenda,kwann?kimsingi biashara haijachanganya sana lakini kuna dalili za kuchanganya mda si mrefu,uwepo wa vyombo vya habari na kujengwa kwa stand mpya ya mabasi kutachochea biashara ukizingatia ni nchi4 zitakutana pale na tofauti na ilvyokuwa mwanzo stand ndogo ikawa haina na uwezo wa kuingiza magari mengi na bado haikuwa ya kisasa

Kwahyo wekeni vitu na vyuo naona vimeanza naamini kwa baadae vijana watatapakaa na pesa itaweza kuzunguka vya kutosha na kufanya biashara kuwa ya uhakika sana,ndugu zangu tukutane kesho kwenye sehemu ya 2 na ya mwisho ya taharifa hii

Alamsiki,Mungu awabariki nyote!
 
inasemekana mwaka juzi 2010 (sijui kabla ya hapo) zilitoka pesa za kuukarabati kwa kiwango cha lami lakini kama unavyojua 'uongozi wa juu' ukapeleka hela kwingine.
Kwa hiyo uliishia hii hatua ambayo bado inasabaisha vumbi wakati wa jua na matope wakati wa mvua kwa hiyo kufanya uwanja huu usiaminike kwa muda wote wa saa 24.
Hizi picha pia ni nyakati ambazo muweka uzi huu alikuwepo.
bk ap 1.jpg

bk ap.jpg
Ulivyotaja hicho kiwanja cha ndege umenikumbusha mbali sana. Kwani wakti mmoja nikiwa wizara ya fedha muungano nilisafiri kutumia ndege ya Jeshi la wananchi kutoka Dar nikiwa naenda Bukoba kikazi. nakumbuka rubani alikuwa Meja Lwena na ndege ilikuwa HS. hakika katika kutua alimanusura atuingize ziwani kwani kulikuwa inanyesha mvua nyingi sana hapo Bukoba.

Kweli siusahau uwanja huo

By the way vipi Nsenene?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom