Bukoba Mjini si salama tena ?,Majambazi wakiwa SMG waua 2,polisi wafika baada saa 1

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
Lilipotokea tukio hili ni Km kama mbili hivi kutoka kituo kikuu cha Polisi cha Mkoa huo na polsi walifika kunako tukio saa 2 usiku


MAJAMBAZI watano wote wakiwa na silaha mbalimmbali ikiwemo bunduki ya (SMG) siku ya jumamosi iliyopita majira ya saa moja na nusu jioni,walizingira kituo kimoja cha mafuta kilichopo kata ya Kagondo mjini Bukoba mkoani Kagera nakuua watu wawili kwa kuwapiga risasi na kukimbia kusikojulikana.

Majambazi hao ambao waliingia kituo cha kuuzia mafuta kijulikanacho kwa jina la ‘Mwendo wa Saa'huku wakijifanya wanahitaji huduma ya mafuta ya diseli wakiwa wameshikilia kidumu tupu cha lita tano,na kumkuta mfanyakazi wa kituo hicho akiwa ameisha kabidhi mauzo kwa mwajili wake.

Kwa mujibu wa mfanyakazi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Jamira Abdul(38)tukio hilo lilitokea wakati yeye akiondoka kurudi nyumbani kwake mara baada ya kumkabidhi mkurugenzi wa kituo hicho Nassor Ahmed(57) maarufu kwa jina la Mabruuk,ambaye aliuawa mara baada ya kupigwa risasi.

Jamira alisema kuwa baada ya watu hao(Majambazi)kuuliza mafuta ya diseli,yeye aliwajibu kuwa kituo hicho hakihudumii mafuta ya diseli zaidi ya petrol tu,ndipo mmoja wa majambazi alimkaba na kumnyanganya simu na mkoba wake huku wenzake wakianza kurusha risasi hewani na kumpiga risasi mlinzi aliyejulikana kwa jina moja Adriano aliyekuwa lindo na kumuua papo hapo.

"Nilishutushwa na tukio hilo na kukimbilia kusikojulikana,huku risasi zikiendelea kumiminwa ofisini kwa mkurugenzi…"alieleza mfanyakazi huyo.

Habari zaidi kutoka ndani ya familia ya marehemu Mabruuk,zinasema marehemu alifariki mara baada ya kufikishwa hospitali ya mkoa Kagera,alipokuwa amekimbizwa ili kupatiwa huduma mara baada ya kupigwa risasi moja ya kifuani,wakati alipokuwa akitoka ofisini kuangalia ni nini kilichokuwa kikiendelea nje ya ofisi yake.

Mmoja wa familia ya marehemu Salum Mawingu,alisema mbali na mauaji hayo ya kutisha,majambazi hao walimpiga mwendesha pikipiki mmoja aliyekuwa amefika kituoni hapo kupata huduma ya mafuta na kumuacha amezirahi,huku bunduki ya mlinzi wa kampuni ya Passific ikivunjwa vunjwa na majambazi hao.

Mawingu alisema mpaka sasa hakuna taarifa kamili iliyokuwa imejulikana kujua ni kiasi gani cha fedha kilichochukuliwa na majambazi hao,japo amekiri kuwa fedha nyingi imechukuliwa kutokana na kituo hicho kuwa ni moja ya vituo vinavyotoa huduma ya kuuza mafuta kwa wingi.

Kutokana na tukio hilo,baadhi ya wakazi mjini hapa wamelaani tukio hilo na kutupa lawama kwa jeshi la polisi kwa kukaa kuwinda waendesha pikipiki tu huku majambazi wakitawala mitaani.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Henry Salewi,alipoulizwa juu ya tukio hilo alielekeza kuwa yeye hayupo ndani ya mkoa ,hivyo taarifa zitolewe na kaimu wake ambaye naye alijibu kuwa bado anaendelea na likizo,japo taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo zimethibitisha tukio hilo kutokea na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi.
 
Back
Top Bottom