Bukoba hawajui hata mgao wa umeme/giza ukoje, wananchi wanasema tunazusha

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Kuna baadhi ya mikoa hapa nchini hususan Kagera hasahasa Bukoba hapa mjini, Kyaka Bunazi, Karagwe hawajui kabisaaa kama kuna tatizo la umeme nchini. Wanapoona magazeti yanaandika kuhusu mgao wao wanashangaa akusema eti ni Tanzania wanayoijua wao au nyingine. Nawaomba wawapigie simu ndugu zao walioko mikoani kwingine wawaeleze mziki ulivyo. Bukoba hapo na maeneo wanayoyataja wanapata umeme kutoka Uganda ambao kukatika ni mara chache sana. Waganda wako kibiashara zaidi kiasi kwamba kwao hutokea ukakatika lakini wanaouuza Tanzania haukatiki. Nisaidieni kuwaelezea jinsi ambavyo watu wanaoishi kwa kuuza ice cream hawana kazi sasa hivi, wale wauza maji hawana kazi, na mambo mengine kibao. Wanaofanya kazi viwanda vya samaki hapa wao kila siku wako job, mashine za kusaga wao wako job kila siku, waulizeni wa Shinyanga huko wawaeleze. Waandishi wa habari na sisi vijana wanaharakati hatuzushi. Nchi ina hali mbaya msidanganywe na Geografia iliyowabeba. Mwingine anadiliki kusema eti "kweli wapinzani hamna dogo, mbona umeme hapa una miezi karibia 8 haujakatika hata kufikia muda nusu saa?" ni kweli lakini Tanzania sio Bukoba tu, wananchi kwingine wanatabu bana! CCM wengine watatumia kutoelewa kwa wananchi waseme wapinzani wazushi, kisa kelele za umeme wakati hawajaona umekatika. Wasiofikiri wataamini. Mwenye kuamisha kiwanda akilete huku azalishe na sio siasa za kuwadanganya watu kuwa nchi nzima ina umeme.
 
Mojawapo ya njia nzuri ya kutatua tatizo la umeme ni kuwa na vyanzo vya kuzalisha vinavyojitegemea tofauti katika maeneo mbalimbali bila kulazimika kuunganishwa kwenye grid ya taifa. Mfano watu wa kigoma, mtwara na kagera.
 
pamoja na kuwa na umeme nimegundua itu kimoja nachi ni kuwa hawana hata radio wala tv.....kazi kunywa lubisi tu

Ahahahahahaahhahahahaha, radio ipo ya Kagasheki bana, loh!! umeua mwanaaaaaaaaaaaaaa
 
Ta Muganyizi,

Mushanage Waitu? Vipi Lubisi hapo Kanazi?
r

tehetehetehetehetehetehetehetehete Lubisi ya kumwaga umeme mwingi sana huku yaaani balaaa. Mie naona kila mkoa uzalishe wa kwake. Mikoa ambayo haina vyanzo vya kuzalisha isaidiwe na ile ya jirani kuliko kuwa na li- grid la Taifa ambalo kila siku ni wizi mtupu
 
Ni kweli nimetoka huko juma lililopita-RC anasema kwao mgao wa umeme ni vocabulary!
 
kweli bukoba pombe watu simlikuwa mnamuona tibaigana pombe mtu hivyo sishangaii hata kusikia hivyo.
 
Inaonekana kwao kuwe na umeme kusiwe na umeme sawa as am told ni ya 19 kimaendeleo tanzania wakiwa na pato la tshs 483158 kwa mwaka na kati ya hecta 1.5milioni ni laki sita tuu ndo zatumika kumbuka iyo ni arable land.
Jamani wahaya kazaneni migombani ili mpate uinua mkoa wenu kama wachaga wanakazana kwenye kahawa
 
Ta muganyizi, hapa bunazi kama tupo ulaya kwakeli, actually umeme uku kukatika n wakati wa service, wanapo fanya service wanakata kwa masaa mawili tu, then tunaendelea kula mema ya nchi. nawashauri nyote mliopo kwenye mgao wa umeme muhamie bukoba kwa muda.
 
pamoja na kuwa na umeme nimegundua itu kimoja nachi ni kuwa hawana hata radio wala tv.....kazi kunywa lubisi tu
We shika adabu yako tuombe radhi wana Bk bukoba kuna vituo viwili vya redio navyo ni KasibnteFm na Radio vision fm na zote zin coverage mkoa mzima achilia mbali RFA na Radio one,tatizo wanasema NGUO YA KUAZIMA...! Wana Bk umeme tumeazimwa ni muhimu tukaunganishwa na gridi ya taifa.
 
Kwa nini unafungua mada mpya wakati kuna mada za umeme hapa jamani ? Haya ungalisemea kule kupunguza utitiri wa mada hapa ndugu yangu .Duh haya
 
Back
Top Bottom