Budget 2010 hii hapa

Bajeti hii sio kwa ajili ya watanzania , ila ni kwa ajili ya wenye nchi,

1. Pikipiki zimeongezewa kodi, ile hali huu ni usafiri wa kawaida kwa walalahoi wa nchi hii. Badala yake makampuni ya madini yamesamehewa kulipa ushuru wa mafuta kwa ajili ya migodi yao.
2. Matumizi ya serikali yameongezeka sana ukilinganisha na bajeti ya mwaka jana ambayo imeongezeka kwa 1.8 trilioni.
3.Mazao ya biashara kama pamba, kahawa, katani na chai --yameachwa pembezoni kabisa , ila faraja inaweza ikawa ni kwa wakulima wa korosho.
4.Wavuvi wote hawapo wala vifaa vyao havijapunguziwa ushuru ili walau waweze kutumia nyavu halali badala ya kutumia chandarua , kitu ambacho kinapoteza mazalio ya samaki .
5.Leo imekuwa 11 Trilion, ila ukweli ni kuwa hizo ukilinganisha na kuporomoka kwa shilingi yetu ukiangalia na mwaka jana utaona kuwa hakuna nyongeza kwani mwaka jana ilikuwa 9 trilion ,leo tunasema tumeongeza kwa 18% , ila hali shingi imeanguka ukilinganisha na dola kwa zaidi ya 26% , hivyo hakuna kilichoongezeka.
6.Mfumko wa bei ambao sasa tumeambiwa umeshuka kutoka 12.4% na umefikia 10.2% , hakuna mkakati wowote wa kuhakikisha kuwa mfumko huu unapungua , kwani kati ya vitu vikubwa ambavyo vinasababisha mfumko wa bei ni matumizi ya kaya kwa ajili ya chakula, kila kaya zaidi ya 55% ya kipato ni kwa ajili ya matumizi ya chakula , sasa kama tungetaka kupunguza mfumko wa bei basi tungewekeza kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula.

Hii sio bajeti yetu , ni ya kwao..
 
Nilikuwa naangalia bajeti na kwa haraka haraka naona mapungufu yafuatayo:
  • No comparatives - naamini wanaotengeneza hii budget ni wahasibu waliobobea ningelitegemea kuwe na comparatives za kila item inayosomeka kwenye bajeti
  • Borrowings - ningelitegemea kuwe na habari zaidi kwenye madeni, je ni madeni gani nchi inayo kutoka kwa nani na kwa masharti yapi (interest rates, security of these loans, movement in each loan item during the year, etc)
  • Pia kungelikuwa na majedwali zaidi kuliko hizi blah blah za mheshimiwa spika sijui nini.. naamini habari ya pesa inaeleweka zaidi ikiwekwa kwenye charts, graphs, etc.
Je na hii ya kupunguza 1% kwenye kodi inamaanisha nini?? Halafu gharama za maisha unaongeza kwa zaidi ya 30% (vinywaji, usafiri - gharama za upkeep ya magari imepanda,etc)
 
Watanzania wapo ICU tayari - Mgonjwa wa akiwa ICU huwa hana maumivu kuzidi wala kupungua!

BTW: Hotuba ndiyo inasomwa sasa hivi Bungeni (kwa Kiswahili): hilo toleo la Kiingereza lilitolewa asubuhi na Ofisi ya Bunge kwa ajili ya Diplomats hasa hasa

Hotuba ya Kiswahili lugha yetu ya taifa HII HAPA. WE BOFYA TU
 
Buget hii bado naichambua nitaweka uchambuzi wangu ikimaliza. Ilaanayeishi kijijini kaumia-ila atapata tishirt-vitenge na kanaga bila kusahau kofia na burudani soon!!
 
Buget hii bado naichambua nitaweka uchambuzi wangu ikimaliza. Ilaanayeishi kijijini kaumia-ila atapata tishirt-vitenge na kanaga bila kusahau kofia na burudani soon!!


Sisi longolongo na siasa nyingi zimezidi sana , linganisheni ya TZ na ya Kenya ndio mtaona . Kenya wao wamepanga Trilioni 18 za kibongo na kila shilingi unaiona inaenda kufanya nini hata kama ni kununua pikipiki kwa ajili ya wahudumu wa afya vijijini zinaonekana , za kwetu huwezi jua ni za kazi gani hata usome mpaka bajeti ijayo..
 
Je hakuna fedha zinazobaki mwisho wa mwaka wa fedha (Carried forward fund)? mbona hili halizungumziwi?
 
Code:
Wafanyakazi wamepigwa 'changa la macho'. Kupuguza kiwango cha kodi kutoka 15% mpaka 14% is a big joke! Technically ameowaongezea wafanyakazi shilingi 2,600 tu!
Code:

Acha mambo ya KISENGENYAJI wewe.....ulitaka wafanyakazi waongezewe milioni moja moja?
 
Acha mambo ya KISENGENYAJI wewe...
Kwani nimemsengenya nani? Ki vipi?

....ulitaka wafanyakazi waongezewe milioni moja moja?
Hapana! Najua serikali ya CCM haina uwezo wa kulipa hata sh 315,000 kwa watumishi wake!...sembuse hiyo milioni? Lakini kama walikuwa wanakusudia kupunguza kodi basi angalau ingalikuwa kutoka 15% to 10% ikiwa na pamoja na kurekebisha zile tax bands za chini ili zisitozwe kodi ili wenye vipato vidogo wasitozwe kodi.
 
Kuna habari zilizoandikwa na gazeti moja zikieleza, "Serikali imefanya maamuzi magumu kadhaa kwa lengo la kudhibiti matumizi makubwa" katika bajeti ya mwaka huu.

Wakati huo huo, serikali inahalalisha matumizi ya bilioni, sijui ngapi, kuleta Timu ya Mpira ya Brazil kutupakiza "opium" kwa muda wa dakika 90!

Ni nchi mbili tu zilizolipia hiyo timu kuja Afrika na kurudi: Zimbabwe na Tanzania.
 
Please any body answer my question above, niliuliza je hakuna fedha za matumizi ya kawaida (reccurent expenditure) zinazobaki mwisho wa mwaka wa fedha? na kama zipo where are they accounted for. nilitegemea kama zipo, ziwe vyanzo vya mapato kwa ajili ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha. Kwa maana hiyo kiasi kingetajwa bungeni.
 
Back
Top Bottom