BSS vs Tusker Project Fame

HATA MIMI NASHANGAA ila mwanzo mgumu.....

Watanzania huwa tunalea uzembe kwa visingizio vya "mwanzo mgumu." Hawa wameanza lini bwana? Tusker wameanza lini? Madam Ritha ataimprove vipi ikiwa mind yake ni kusema "Una macho mazuri, umependeza."? Wao wanachofanya ni kukusanya pesa tu za sms na wadhamini. Jamani Watnzania tuache kuchukulia mambo kirahisi kwa visingizio vya "Mwanzo mgumu."
 
Watanzania huwa tunalea uzembe kwa visingizio vya "mwanzo mgumu." Hawa wameanza lini bwana? Tusker wameanza lini? Madam Ritha ataimprove vipi ikiwa mind yake ni kusema "Una macho mazuri, umependeza."? Wao wanachofanya ni kukusanya pesa tu za sms na wadhamini. Jamani Watnzania tuache kuchukulia mambo kirahisi kwa visingizio vya "Mwanzo mgumu."
sipati picha wakimualika jaji Ian japo kwa siku moja
 
Hakuna cha mwanzo wala nini jamaa wa BSS hawako siriasi kabisa wako kibiashara zaidi.

Tumeni msg kuchagua makapi mnawachangia pesa za kutumbua na familia zao. Hivi mtu kama rita anaujua mziki kweli? wanajua kuwa watanzania ni majuha ndio maana...........
 
Asante sana mtu aliyaanzisha mada hii sasa kinachotakiwa ni kushauri na kumwambia ukweli rita mwenyewe,ni kweli anachofanya ni kujipatia pesa yeye kama yeye nothing else usanii tu,thanks God sijawahi kujichosha hata siku moja kupiga kura kwa sababu ni upuuzi mtupu,jamani wale wajuaji wa muziki wamsaidie mawazo huyu dada lakini kama yuko kibiashara sidhani kama watapewa nafasi ya kutoa maoni yao na yakafanyiwa kazi,hakika hatuko siriasi hata kidogo,inaboa sana
 
Kwa upande wangu naona BSS ingekuwa na majaji wazuri na makini ingekuwa bora ila sipendezwi kabisa na majaji waliopo naona kama vile wako pale kishikaji zaidi na sio kama wako kazini. na kwa Upande wa washiriki naona kama wastragle sana wenyewe maana wanapojajiwa hawaambiwi weekness yao iko wapi zaidi ya kuambiwa mara umependeza, au unaboa au unaimba nyimbo za marehemu na mengineyo yafananayo sasa huo sioni kama niujaji au ni kumkatisha mtu tamaa.

Ila TPF iko juu kwa kweli na pia hawana upendeleo unaona kabisa mtu anapewa hukumu ya haki.
 
Kwa hili nimefurahi sana watu kuona kile ambacho mm nimekiona. BSS hawana lolote. sisemi kuwa hawawezi la hasha, ila wako kibiashara zaidi na kwa sisi mambo haya yako all most every where. Tukitafuta warembo wetu tunakuwa na uamuzi au waamuzi wepesi wasio na ujuzi wa kufanya uamuzi sahihi matokeo tukishindana nje ya nchi tinakuwa wasindikizaji na watia aibu wakubwa. Ukienda kwenye mpira mambo ni hayo hayo, Ridha hali na hiyo. Wanachofanya BSS ni kutengeneza hela which is not bad lakini hawawasaidii wasanii wetu kufika viwango kwa sababu na wenyewe hawajui. Washauriwe wenyewe kwanza wakasome muziki au wawatafute wataalamu wa muziki. When you watch TPF you `ll like it
 
achaneni na mambo haya, kwa sasa tujadili uchaguzi hadi mwezi ujao ndo mambo ya bsss yatakuja. OK!
 
choice za participants sio nzuri kwa BSS kutokana na kutokua na judges wazuri wanaojua mziki, mtu anakua top 8 lakini hajui kuimba u wonder amefikaje huko...katika washiriki waliopo wote 8 ni mmoja tu unayeweza sema anajaribu kuimba, wengine wanapiga kelele tu, watanzania ni mabingwa wa kufanya mambo kwa mazoea, hawajali viwango..
 
Bss hakuna anaye jua kuimba,imejaa wapiga kelele tuu.

Ni dhambi kuilinganisha BSS NA TPF.
 
BSS bado sanaaa kwa TPF. TPF wapo serious with wat they are doing. BSS mhhh
 
Rita kavurugwa na Mzee Machache kummwaga na ghafla kumzalisha Kei Lyynn Mapacha. So Ritta hajui nini anafanya kwa stess hizo anagongwa na kina Ali kiba, Z Anto
 
Back
Top Bottom