BSS Majaji wanatukana na wameapa na kumpitisha mariamu

mambo ni hovyo kabisa hawa wasichana rita ,salama na miss j wameonekana ni wajinga kabisa na mashindano yameharibika kabisa hayana maana kabisa

Mie nadhani umefika wakati sasa wa kutenganisha waandaaji wa shindano na majaji. Waandaaji wao wawe kazi yao ni kushughulikia na masuala ya maandalizi na utawala , na majaji wawe ni watu tofauti kabisa ambao hawahusiani na waandaaji
 
Kwa ujumla Master "J" amewakosea Watanzania wote kwa ujumla. Kitendo cha kutuita wabongo washamba hiki hakikubaliki hata kidogo. He owes us an apology!
 
Hivi madam Rita Ana elimu kiwango gani. She is too lousy and unprofessional
 
Watu wengi sana wamelaani kinachoendelea mwenye BSS, mliopata fursa ya kuangalia hiyo kitu mtupe issue kwa ufupi sie tulio mbali...
 
Makampuni yanayosponsor BSS kama yanataka kutunza heshima zao kwa wananchi ni lazima wahakikishe kuwa kanuni za mashindano zilizokubaliwa zinafuatwa pamoja na kuthibiti wao wenyewe jinsi kura zinazopigwa kwa njia ya SMS zinavyojumlishwa; kwani nahisi safari hii hawa jamaa wameiga mtindo wa kuchakachua na wamefanya hivyo na kumpata mshindi ambae kwa maoni yangu hakustahili!! Kuna umuhimu pia kuwa na judges wenye hadhi na heshima kwa umma unaokuwa ukumbini na wale wanaoangalia toka majumbani kupitia luninga kwani lugha walizotumia baadhi ya majaji safari hii hazikuwa za kistaarabu.
 
Hakuna ninachoweza kufananisha na Tusker fame ya kenya. Nilipoanza kuangalia sikurudi kuangalia hii bss. Yaani hakuna viwango kabisa? Na kwa kweli si kweli kwamba Tanzania hakuna viwango hapana hawa waendesha mashindano ndio hawana viwango. utapigaje playback bwana? hizo instrument zao wanaza compose mara nyingi zimewapoteza contestant wao na wakaonekana kama viwango vyao ni vidogo. Mimi niliacha siku nyingi kuangalia. Hivi matokeo ilikuwaje?
 
....,.. kwani nahisi safari hii hawa jamaa wameiga mtindo wa kuchakachua na wamefanya hivyo na kumpata mshindi ambae kwa maoni yangu hakustahili!! .........

Kwa maoni yako unestahili ni wewe au ndugu yako yupo pale?
 
Master J amewakosea watanzania kwa kuwatukana na kuwaita eti ni WASHAMBA kwa kuwa aliona watu wanamshangilia sana mzungu Joseph Payne kuliko wengine.

Kama kawaida yake Master J huwa hajiamini na kuwa miaka yote hatimaye anafuatisha kile anachotaka Salama Jabir.
Salama alisema toka mwanzo kuwa hayupo kwenye boti wala basi la mzungu, na hatimaye Master J kama kawaida yake akamuiga.

Walimkandia sana mzungu siku ile ya mwisho ili kumkatisha tamaa, wakati alifanya vizuri.

BSS imekuwa ni usanii mtupu sasa, wanapanga mshindi, na wasiowataka wanawahujumu.

Kwaheri BSS, hatutaonana tena; na karibu TPF (Tusker Project fame)
 
Back
Top Bottom