Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,918
- 31,160
BRIC ni mjumuiko wa mataifa ya Brazil,Russia,India na China ambayo kwa pamoja yako katika stage ya uchumi unaokuwa kwa haraka sana [Advanced economic development] pia nchi hizi ujulikana kama Big 4.Inatarajiwa ifikapo 2027 uchumi wa BRIC utakuwa mkubwa kuliko ule wa G 7 [USA,Japan,Canada,France,UK,Italy & German].South Afrika yenye idadi ya watu 50 milion imejumuishwa ingawa idadi ya watu wake ni ndogo mno kulinganisha na mataifa ya China,India,Brazil au Russia na kuifanya jumuiya ijulikane BRICS.BRICS pia zinataka mageuzi katika shirika la fedha dunia IMF linalotawaliwa na mataifa ya magharibi.