BRELA Ipanguliwe

kaka vita vimehamia Twitter

Nyalandu wakati yuko Dubai ilibidi kwa afute watu waliokuwa wanamwandama juua ya BRELA

Mbaya zaidi watu wanawasemea kwa nchi wahisani wanaotoa pesa za kuendesha vyombo kama Brela & Co

lakini ile siri ya JF na Mawalla advocates na Brela ni nzito sana

mwenye macho haambiwi ona
 
Mzee Mwanakijiji, mabadiliko mengi yameisha tokea Brella sasa sio idara tena ni walala wa serikali unaojitegemea.

Tatizo ni watu kutofuata sheria, taratibu na kanuni. Brella inaendesha mambo yake yote kwa kufuata Company Law Cap 212 au 312 ambayo tumeirithi kutoka kwa Waingereza.

Sheria hiyo inatoa fursa kwa majina ya wamiliki na kiwango cha umiliki wao kuwasilishwa Brella pamoja na articles of association na memorandum of the company.

Majina hayo ya wamiliki hupewa kinga iitwayo "corporate veil" na kampuni inasimama "as a person". Hivyo majina ya wamiliki sio public domain!.

Ndio maana hata kukitokea kesi mahakamani, kampuni inasimama kama kampuni japo wenye resiponsibility ya kutekeleza maamuzi ya mahakama ni wamiliki kupitia menejimenti zao!.

Ili kuwajua wamiliki, lazima uombe kibali cha mahakama ku lift ile corporate veil in case kuna kitendo chochote cha jinai kwa sababu company haiwezi kutenda jinai, wanaotenda jinai ni watu na hapa ndipo wamiliki hushitakiwa kama kwenye kesi za EPA.

Ili kufungua account bank, sio lazima kuwa na registration ya Brella kwani makampuni kibao tuu ya offshore yana accounts hapa hayana wafanyakazi na hawalipi kodi hata senti moja!.

Kusajili wafanyakazi wako NSSF sio lazima kuwa na usajili wa brella ndio maana wafanyakazi kibao wa mashirika ya kimataifa na ofisi za ubalozi, wanalipwa super salaries na wanawasilisha makato NSSF lakini hawalipi kodi hata senti moja!.

Sheria za nchi ziko wazi kila mtu lazima alipe kodi na anatakiwa awe na tin number, watu kibao hawana tin number, na wenye nazo hawaonyeshi real income zao hivyo hawalipi kodi!.

TRA wameanzisha mashine za EFD zinazotumia GPRS hivyo tangu unapopeleka tax invoice, TRA wanaiona, unapolipwa TRA wanaiona hivyo kiwango chako cha kodi kinaonekana wazi, lakini wajanja wa mujini wameshaingia kwenye system ya TRA, unafanya transactions zote, TRA wanaona, mpaka tax receipt ya fedha zako za kodi ulizolipa zinaonekana kwenye mtandao wa TRA lakini hakuna kilicho ingia!.

Tatizo letu kubwa ni compliance ya sheria na track down mechanisim hatuna!.

Jiji la Geneva public transport ni bure wakati wa mikutano mikubwa, baada ya mkutano hutakiwa kulipa kwa kujinunulia tiketi kwenye mashine. Niliover stay na kuendelea kutolipa nikijifanya mkutano unaendelea, nilikuwa booked mara mbili jamaa wakamulika tuu passport yangu na kunishauri nikalipe na faini at my own time!. Nikajua ni kama bongo tuu, watanipatia wapi?. Unashikwa na kosa unaambiwa nenda kalipe faini at your own time!. Siku naondoka zangu kurudi bongo, kufika passport control desk, nashanga mbona wanachelewa kuicheki passport yangu, kumbe jamaa wametoa print out ya zile mara mbili nilizokuwa booked, jamaa wakanitaka nionyeshe risiti nyingine zozote nilizowahi kukata, sikuwa nazo!, ikapigwa hesabu ya two trips per day tangu siku ya kuisha mkutano mpaka ile nakuja kuondoka, ikaja bili ya ajabu plus fine, hakuna majadiliano, kalipe ndipo uje uwe cleared!. Hapa hatuna any track down mechanisim ndio maana watu hatulipi kodi kunakoifanya serikali yetu kuwa omba omba!.

Mwalimu alisema, "corrupt government haikusanyi kodi", hii ndio serikali yetu!.
 
Pasco issue ya Brela sio kodi

kuna zito zaidi ambalo limeenda all the way to the top echelons of the Government of Tanzania

btw:

hivi unajua kuwa watu stad 7 wanafanya kazi pale?
 
Mwanakijiji,
Umewahi ku deal na BRELA? Labda wenye experience na hapo mahali waseme. Kwa maoni yangu BRELA inahitaji documents nyingi mno kusajili.
Ndio maana nimeshangaa ilikuwaje Norconsult wakaendesha biashara bila kuwa na usajili wa BRELA?
Nenda bank kufungua account ya company, moja ya documents ni pamoja na registration ya BRELA, na documents nyingine kibao. Sasa hata kwenye bank Norconsult wakapeta tu, hapo kweli utasema tatizo ni sheria?
Kuhusu Mkapa, sheria zilizopo zinatosha kabisa kumfikisha Mkapa mahakamani kama will ya viongozi wetu itakuwepo.
Tatizo la TZ sheria zina sura, zinaangalia nani mtenda kosa. Kwa sheria hizo hizo ingetakiwa polisi wawe na mamlaka ya mwisho na sio kusubiri JK anasema nini.
Ndio maana mimi siamini kabisa kwamba tatizo ni sheria, sheria zilizopo zinatosha hasa, sanasana ni marekebisho ya hapa na pale. Watanzania ndio tunatakiwa kubadilika na kuanza kuuza maadili ya kazi kwa pesa.
Nadhani tatizo ni usimamizi wa sheria na sheria zenyewe.

Sheria zetu zina loopholes nyingi. Mathalani, kama sheria inataka mtu asiruhusiwe kuwa na account bila uthibitisho wa BRELA hapo tatizo ni usimamizi wa sheria katika benki na pia sheria yenyewe kwasababu haielezi mabenki yatachukuliwa hatua gani yakikiuka, na kama ipo basi haisimamiwi na wanaopaswa kusimamia hizo sheria zifanye kazi.

Tatizo la nchi yetu mifumo ya kazi haitegemeani. Kwanini BRELA, Benki, NSSF, PPF wasiwe na mfumo unaohakiki kuwa uthibitisho wa kampuni X umefanywa na kuidhinishwa na Ndugu Z? Faili likipotea ni rahisi ku-trace nani yupo nyuma ya mpango mzima.

Kuna kitu muhimu sana huwa hatukiongelei, yaani usalama wa taifa. Nakumbuka miaka ya 70,80 mtu aliyeingia nchini atajulikana tu hata kama atajificha Naliendele kijijini. Siku hizi siyo tu wanaingia bali pia wanapata passport, ardhi,mikopo ya elimu n.k.

Unajua kuna mambo ya Takukuru na mengine ni ya usalama wa taifa. Sijui kama usalama wa taifa wa leo una maana ile ile tulioijua wengine au ni kuongoza misafara ya viongozi!
 
Back
Top Bottom