Breking Newz: Mswada wa sheria ya Katiba mpya kufutwa!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,244
OFISI ya Bunge imesema kuna uwezekano wa kubadilishwa au kufutwa kabisa kwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011, endapo itaonekana kuna sababu za msingi.Hayo yamebainishwa katika taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Ushirikiano wa Kimataifa ya Ofisi ya Bunge.

“Muswada huo, ambao Bunge liliupitishwa baada ya kuusoma kwa mara ya tatu, ambao unasubiri kuwa sheria baada ya Rais kutia saini na kuwa sheria utaendelea kusimamiwa na kutekelezwa kama sheria nyingine yoyote ambayo utekelezwaji wake unaweza kusababisha mtizamo tofauti na hivyo kupelekea kufanyiwa marekebisho endapo itaonekana kuwa ipo sababu ya kufanya hivyo na mbunge yeyote, kamati au Serikali,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza:

“Kwa hiyo endapo sababu zitaonekana kuwa za msingi, basi* kubadilishwa au kufutwa wote na Bunge. Kwa hiyo kwa taratibu za uendeshaji, Bunge haikuwepo sababu ya msingi kuzuia muswada huo usisomwe kwa mara ya pili na pia hapakuwa na kanuni zozote, zilizozuia usisomwe kwa mara ya pili kwa kuwa ulikidhi mahitaji yote kikanuni.”

Ilisema baada ya kusomwa kwa mara ya kwanza Bungeni, wananchi hupata fursa ya kushiriki kutunga sheria ama kwa kushiriki wao wenyewe kutoa maoni au kupitia wabunge ambao ndiyo wawakilishi wao.

“Wakati wa kujadili muswada huu mara baada ya kusomwa kwa mara ya pili na kabla haujasomwa kwa mara ya tatu, wabunge walikuwa na nafasi ya kuwasilisha mawazo yao kwa kuchangia,” ilieleza taarifa hiyo.

Imeeleza kuwa baadhi ya wabunge walitekeleza demokrasia hiyo kwa kuwasilisha mapendekezo yao pamoja na jedwali la mabadiliko.

Taarifa hiyo ya Bunge ambayo imekuja huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wakiongozwa na chama kikuu cha upinzani cha Chadema na na wanaharakati chini ya Jukwaa la Katiba, ilifafanua kuwa muswada huo ulilenga kuweka chombo ambacho kitafanya kazi ya kuchukua maoni ya wananchi ili kuyapeleka katika Bunge la Katiba ambalo litakuwa na nafasi ya uwakilishi wa kila mtu katika jamii.

Pia imesema muswada huo ni kama mingine iliyopitishwa na Bunge na unaweka utaratibu wa kuwafikia wananchi, kuwasikiliza na kupata utashi wao juu ya mapendekezo ya kuandika Katiba Mpya ili kila Mtanzania aweze kushirikishwa.

“Lakini muswada wenyewe hauhitaji ushiriki wa moja kwa moja wa wananchi isipokuwa kupitia kwa wawakilishi wao; wabunge, walipitisha kwa kauli moja kuwa Sheria na siyo Katiba kama inavyoelezwa na baadhi ya wadau.”

“Bunge limeuchambua Muswada wa Sheria na kuupitisha kuwa sheria na siyo muswada wa kubadilisha katiba. Katiba sasa haitobadilishwa, bali itaandikwa upya na Serikali iliyopo madarakani kwa sasa na Bunge lake.”
 
Dhubuti! hapa lao moja, hapa wanajaribu kupunguza presha kutoka kwa wanaoupinga. Watu tukikaa kimyaa lazima waupitishe hata kama hauna maslahi mbeleni wakati mimi nawewe pengine tutakuwa tuliyashaoza. Hapa ni kula nao sahani moja hadi kieleweke.
 
Kwangu mimi hii sio breaking news kwa sababu hata wakati umepitishwa, bunge lilitoa kauli hizo hizo.
Mi naona tusubiri mawasilianao kati ya CHADEMA na Ikuku yatatoka na jibu lipi.
 
Kwahiyo bunge letu linazidiwa hoja na watu waliyo nje na kama ndivyo hawa wabunge tunawalipa mamilioni ya kazi gani kama wanashindwa kuona mambo muhimu ya kimsingi na kuamua kuupitisha kwa asilimia 100..hongera CDM make mmejiweka kando ktk kupitisha ushenzi huu ila Ole wao ccm na cuf walioupitisha muswada huu wa kusadikika

VIVA CHADEMA,sauti yenu ni sauti ya umma
 
Kama ukifutwa kwanza waupeleke kwa hao hao wabunge walioupitisha ili waufute wenyewe. Pili, warudishe pesa yote ya posho waliochukua wakati wakiwa kwenye vikao vya kupitisha mswada bomu. Otherwise, tutakuwa tunachezewa hapa. Watu wanakula posho kwa kupitisha miswada ambayo haina tija kwa taifa.
 
Kwahiyo bunge letu linazidiwa hoja na watu waliyo nje na kama ndivyo hawa wabunge tunawalipa mamilioni ya kazi gani kama wanashindwa kuona mambo muhimu ya kimsingi na kuamua kuupitisha kwa asilimia 100..hongera CDM make mmejiweka kando ktk kupitisha ushenzi huu ila Ole wao ccm na cuf walioupitisha muswada huu wa kusadikika

VIVA CHADEMA,sauti yenu ni sauti ya umma
mkuu hawa ni wanandoa,itakua ajabu mume na mke wapishane kauri.hicho ndicho kiapo chao cha ndoa kwamba nitakupenda kwa shida na raha.
Sasa kazi wanayo wanacho kifanya ni kama mchezo wa draft kuangalia timing jinsi gani ya kula kete,na sisi hatuliki ng'o!
 
mkuu hawa ni wanandoa,itakua ajabu mume na mke wapishane kauri.hicho ndicho kiapo chao cha ndoa kwamba nitakupenda kwa shida na raha.
Sasa kazi wanayo wanacho kifanya ni kama mchezo wa draft kuangalia timing jinsi gani ya kula kete,na sisi hatuliki ng'o!

Mkuu umeifanya lanchi yangu murua!!!!!!!!!!!
 
JB ni kama kuna message umeileta ikiwa imefichwa ktk heading? Tupe source ya heading basi, ya content umetoa!
 
Walichokifanya Serikali ya Ccm pamoja na wabunge wao ni kitu ambacho awakielewi, zaidi ya kusema ndio
kwa kupitisha mswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba. Maana ya mabadiliko ya Katiba ni kuendana na
mfumo wa wakati tulionao wa vyama vingi, na ndio sababu yakuhitajika marekebisho ya Katiba ya zamani,
maalum kumuondolea na kumpunguzia madaraka makubwa aliyonayo Rais. Na kuweka mchakato mzima
wa kuunda Katiba mpya mikononi mwa Wananchi. Sisi Wananchi pamoja na CDM. tunafikiri, tunajua na
tunalielewa ilo, Kutokana na kauli waliyotoa Bunge yenye kigeugeu, inaonyesha kuwa Serikali ya Ccm na
Wabunge wake akili zao zinaanza kuwarudia.
 
Naomba watanzania wafahamishwe mswaada utakaporudishwa kwa wananchi tutajadili nini, na itakapotungwa sheria tujadili nini? , kuhusu katiba plz ufafanuzi
 
Watz tumeshazoea kuburuzwa ila safari hii wamekutaniza wamekabwa kila Idara mpaka penaliti bado imekabwa kazi kwao
 
Hivi kulikua na sababu gani ya kuupitisha kama unaweza kufutwa kirahisi hivyo? Ila nakubali inaweza kutokea kama JB asemavyo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom