Breaking News: Muhimbili Waharibu tena.!

mchemsho

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
3,212
867
Habari za kuaminika ni Kwamba hospitali ya Taifa muhimbili Imetoa Mpya nyingine kwa kuwakabidhi wafiwa maiti ya Muhindi badala ya Mswahili mwenzao. Maiti hiyo iligundulika kuwa siyo yenyewe baada ya kufikishwa Tanga eneo la Mkanyageni ambapo mazishi yalikuwa yafanyike leo saa 7 mchana, baada ya kugundua hilo imebidi maiti huyo muhindi asafirishwe kurudishwa dar, pia ile familia ya kihindi ambayo maiti wao alichukuliwa inasemekana wako njiani kwenda tanga kumrudisha maiti asiyekuwa wao ili wapewe maiti wao. Chanzo kikubwa cha mkanganyiko huo inasemekana ni majina ambapo maiti wa kihindi anaitwa "luke" na mwingine aitwa "lukeman" sina hakika kama majina yanaandikwa hivyo. Nawasilisha.
 
pole yao. tuwekee na chanzo cha habari. je hilo tukio limetokea lini?
 
Pole zao sana!
Ina maana hawakufungua kujiridhisha kabla ya kuondoka?...waliochukua walikuwa watu wa mshahara nini?
 
Makosa ya kiutendaji hayo. Hapo kosa sio la MNH bali la ndugu wa Tanga ambao walitumwa kuja kumtambua marehemu na kumchukua, kwa nini walichukua maiti ambayo siyo ya ndugu yao ?
 
Muhimbili hawajaharibu hapo unawapakazia. Ndugu waliotakiwa kutambua ndio wamehariba.
 
Hiki kichekesho hao jamaa huyo maiti hawakumsafisha walibeba tu
 
Sina hakika kama habari ni ya kweli. Kiutaratibu hata kama wametayarishiwa mwili kwa kulipia, hawekwi kwenye sanduku hadi nduguze wawepo. Sasa ina maana walipeleka sanduku wakaacha hapo wakapitia paseli yao? Wangezika tu huyo muhindi akawakilisha!
 
Unapoenda mochwale zoezi la kutambua mwili wa marehemu ndo huwa la kwanza kabla jamaa hajaanza kuushughulikia kama kuuosha,kuupanga kwa geneza ,kuupiga pamba etc
So ndugu walaumiwe na si MNH
 
Makosa ya kiutendaji hayo. Hapo kosa sio la MNH bali la ndugu wa Tanga ambao walitumwa kuja kumtambua marehemu na kumchukua, kwa nini walichukua maiti ambayo siyo ya ndugu yao ?

wanaogopa kuangalia mwili wa marehemu
 
Makosa ya kiutendaji hayo. Hapo kosa sio la MNH bali la ndugu wa Tanga ambao walitumwa kuja kumtambua marehemu na kumchukua, kwa nini walichukua maiti ambayo siyo ya ndugu yao ?

inasemekana baada ya ku verify yule mfanyakazi wa mochwali alichanganya lebo za majina kwa kuwa majina yanafanana kiasi
 
hii taarifa haiko sahihi kuna uwalakini ...

mkuu nlikuwa na mishe mkanyageni nimefika hadi msibani, nimeongea na mwenykti wa kijiji cha mkanyageni kadhibitisha hili tukio
 
Na hao watoaji wa 'mzigo' hawakuona tatizo lolote kukabidhi maiti ya kihindi kwa Waswahili watupu. Si bure, kuna jambo hapo!
 
Muhimbili mnawaonea tu hapo wakulaumiwa ni hao wabebe mzigo bila kukagua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom