Breaking News-Mafuriko Mwanza Uwanja wa ndege wafungwa!

Mkubwa PakaJimmy kama ulibahatika kupata nakala ya The Guardian ya jana jumapili (japo yaliyoandikwa yanajulikana kwa wengi) ni lazima uone uchungu sana na kujiuliza ni nini hasa serikari yetu inafikiria kama kweli ipo!
Wanasema km 1 ya lami inajengwa kwa 800-1000m, kwa hesabu hiyo uwanja ulio busy kama wa Mwanza haukupaswa kuwa na matatizo kama haya. Angalia uwanja wa Bukoba, inasemekana pesa ilikuwa diverted ukaishia nusu na wenyewe unategemea 'kudra za mwenyezi Mungu'! Na juzi tulisikia ajali iliyotokea Arusha (arumeru) sababu ya matatizo ya uwanja!
Mbaya hii.
Miundombinu ya Mwanza ina tatizo la kudumu la kutuamisha maji, na hii ndiyo iliyopelekea hata ndege ya Atcl ku'skid-off na kuharibika vibaya mwaka jana. Mamlaka husika inatakiwa kuvalia njuga suala hili, hasa kwa kutotanguliza maslahi binafsi kwenye kandarasi za ujenzi wa miundombinu.
 
Kweli kwenye msafara wa mamba na kenge wamo, suala CHADEMA linaingiaje tena humu? Poleni watu wa Mwanza, lakini kwa namna ambavyo kama nchi hatuna utaratibu wa kujihami na majanga lolote linaweza kutokea, ukiona watu tunaanza kusema Mungu apishe mbali, ujue uwezo wa kufikiri umefika kikomo.
 
Back
Top Bottom