BREAKING NEWS:Hiace yaanguka Kolandoto-Shinyanga na kuua mtu mmoja papohapo

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722
Ni mida hii,ilikuwa inatokea Mwadui kuelekea Shinyanga mjini,zaidi ya majeruhi 15 wamekimbizwa hapo Kolandoto Hoaspital kwa matibabu,marehemu alikuwa ni mwalimu katika Shule ya Msingi Songwa,jirani na mgodi wa almasi wa Mwadui.(na za gari na jina la marehemu baadaye kidogo)

Poleni wafiwa na Mungu awajalie majeruhi wapone haraka.

RIP Mwalimu.


UPDATES:

Ajali imetokea kwenye ile kona ya barabara ya vumbi itokayo Kolandoto Hospital kuingia bara kuu ya rami(Mwanza-Shinyanga) na ni kwamba Hiace hiyo imegongwa na Lori kubwa wakati ikiingia main road.

Mpaka sasa imethibitika majeruhi wengine 6 wamefariki Dunia miongoni mwao ni wanafunzi wa Shybush Sekondari.Na pia duru ambazo hazijathibitishwa bado zinaarifu kuwa kuwa majeruhi waliokimbizwa hospital wamefariki Dunia isipokuwa dereva na abiria wengine 4 wanaendelea kuhudumiwa na pia hali zao zinaelezwa kuwa ni mbaya sana.

Tutaendelea kupeana updates zaidi.
 
Ni mida hii,ilikuwa inatokea Mwadui kuelekea Shinyanga mjini,zaidi ya majeruhi 15 wamekimbizwa hapo Kolandoto Hoaspital kwa matibabu,marehemu alikuwa ni mwalimu katika Shule ya Msingi Songwa,jirani na mgodi wa almasi wa Mwadui.(na za gari na jina la marehemu baadaye kidogo)


RIP Mwalimu.

Mkuu tupe updates zaidi.
Mbona nimesikia waliokufa ni pamoja na wanafunzi wanne wa Shy Bush? Au wamefia hospital?
 
Mkuu,

Taarifa za Uhakika watu 17 wamefariki baada ya FUSO kugongana na gari la abiria maeneo ya Kolandoto. Waathiriwa takribani 10 wa vijiji kuzunguka Maganzo wamefariki akiwemo Mke wa Diwani wa zamani kata ya Songwa Hayati Daniel Nyang'inja wa Maganzo.
 
Poleni wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu kwenu,Mungu awasamehe dhambi marehemu wote na awalaze mahali pema peponi.Amina
 
Jamani poleni sana watanzania kwa janga hili ambalo lingeweza kuzuilika,jamani madereva wetu tuzidi kuwa makini.
Bwana ametoa nae ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
Back
Top Bottom