Baraza la Mawaziri Limevunjwa! (2008)

Hapo kikwete umecheza. Sasa panga timu yenye akili. Pili, punguza idadi ya mawaziri. Hatutaki kusikia mawaziri 60!! It is too expensive for poor country like tanzania to maintain, 60 ministers!!! Napendekeza baraza jipya liwe na mawaziri wasiozidi 15!!
 
lakini pia ninaongezea kwenye list yangu watu kama kingunge ngomable mwiru...mhm mama hawa ghasia wanaweza shindania that post na rostam aziz
 
halafuuu n wat abt our magariz bin shangingiz zilizokua na namba za w na nw??si zibaki na namba tuu wakija wengine wapewe as naona tayari kuna mazingaombwe yanafanywa watabaki nayo hao sitini while it is not takiwad to b done that way as ni gari za ofisi
 
kama nilivyosema juzi kuwa LOLOTE LITAKALOTOKEA LINA BARAKA ZA KIKWETE.....ALISHAAMUA KUMTOSA RAFIKI YAKE..

DURU ZINASEMA KUWA UHUSIANO WAO ULIKUWA UMELEGA SANA....NA HII KWA KIASI KIKUBWA INATOKANA NA AMBITION ZA URAIS ZA BAADHI YA WATU...NA PIA KUNA BAADHI YA WASHAURI WA RAIS [MARAFIKI]..WALIKUWA HAWAFURAHISHWI NA UTENDAJI WA PM KUMU OVERSHDOW JK.....

KUNA WALIOKUWA WAKIMPAKAZIA KWA JK KUWA HAFUATI MAAGIZO YAKE..BALI ANAJIFANYIA KAZI KWA UTARATIBU ANAOUTAKA YEYE....

VIONGOZI WENGI WANAPENDA KUWA NA WASAIDIZI DOWN LOW...KAMA WOTE NI MAARUFU KITAKACHOTOKEA NDIO KAMA HIKI CHA JK NA LOWASSA KUVUNJA UBIA RASMI......MKAPA ALIWEZA KUDUMU NA SUMAYE KWA SABABU AINA YA UTENDAJI WAKE ULIKUWA NI WA KUPOKEA MAAGIZO KAMA KAWAWA....

MNAWEZA KUONA MAWAZIRI WAKUU AGRESSIVE KAMA SOKOINE WALIVYOISHIA...HATA MTU KAMA MALECELA ILIKUWAJE!!!

LOWASSA ANA MAKOSA LAKINI LAZIMA MJUE KUANGUKA KWA LOWASSA NDIOO MWANZO WA KUMOMONYOKA KWA NGUVU ZA KISIASA ZA KIKWETE ...NA WATANZANIA WASIWE NA MATARAJIO MAKUBWA KUWA BAADA YA LOWASSA KUONDOKA SASA KILA KITU KITAKUWA SAWA NA MAISHA BORA YANAKUJA...LA HASHA!!!
 
Siku ya nyani kufa miti yote huteleza. Atakayechaguliwa ni lazima awe safi vinginevyo tutakuwa tunafanya mchezo wa kuigiza tunasubiri hilo jina na wabunge waendeleze kazi waliyotumwa na wawakilishi wao wanaowalipa marupurupu.

....."wabunge waendeleze kazi waliyotumwa........"

Hapo ndipo palipo na ufunguo wa kila matatizo makubwa yanayotukabili sasa. Labda safari hii wataanza kuwajibika kwa wananchi. Tusubiri.
 
JK anapiga mabao ya visigino ambapo mashabiki hawatarajii yeye hapo hapo shaaaaaaaa!!!!!!
JK ni msanii aliye qualify anahitaji tuzo ktk hilo
2010 JK atapita kwa 90%.
 
Kwanza nawashukuru wana JF kwa michango yenu mingi mnayo itoa hapa kijiweni. nashukuru kwa kuamua kutumia muda wenu mwingi kutafuta habari na kuzileta hapa JF.
Pia nawashukuru kwa kuendeleza moto wa mapambano ya kuwakatilia mbali Mahabithi Mafisadi wakubwa ndani na nje ya serikali.

Wana Jf mmefanya kazi kubwa sana kutoa elimu ya uhakika na kutoa mfano wa namna ya kushikia bango uoza wa viongozi wa serikali na vyama vya kisiasa.
Naomba moto huu wa kwenda kinyume na maovu ya watendaji wa serikali undelee na udumu daima.
Juhudi zenu za kutumia uwanja huu wa Kisasa kabisa katika kufikisha ujumbe wa Mageuzi ya kweli Tanzania zimefanikiwa vyema na zimeonyesha wazi kwamba hakuna tatizo linalo shindikana kutolewa mwafaka pale wananchi wenye uchungu na nchi ya wakiwa na nia thabiti ya kulikomesha.
Ninaamini kabisa kwamba kijiwe hiki kitatoa wabunge wengi sana endapo tu wana JF walio wengi watakwenda sambamba na maneno yao na mawazo yao na kuyageuza vitendo halisi katika uwanja wa siasa.
Vita hii ndo kwanza imeanza tu, kuna mengi yanakuja yanayo hitaji busara kuu.
Ikumbukwe kwamba ushindi si kushika namba moja tu ni pamoja na kupambana kwa nguvu zote hadi kieleweke.
Mahabithi hawa wenye Roho za kifisadi watajaribu kufa na watu wengine ili ionekane ni kifo cha wengi, naomba tusiwape nafasi hiyo kwa kuichua maovu yao yote.
Mahabithi hawa watajaribu kuFight back ili kudhoofisha nguvu za wanamapambano na wana mageuzi wa kizazi hiki, jaribio hilo likitokea ni lazima wafikishwe mahakamni.
Nawaombeni wana JF mtumie busara zenu kuangalia nyendo zote za watu hawa nje na ndani ya Tanzania ili kamwe wasipate nafasi ya kuharibu taratibu na mipangilio ya kuwang'oa katika juhudi zao za kutaka kujijengea ngome zisizoshambulika.

Kumbukeni hata Ibilisi alipo fukuzwa Mbinguni hakunyang'anywa nguvu zake. Anazo zote hadi hivi niandikapo walaka huu.
Ukimwendea Ibili bila kufuata utaratibu wa kiroho atakupa maumivu ya mwanakoma.

Naomba Mungu awabariki wana JF wote wenye nia njema na kuwapa neema zote katika mawazo yenu katika ndoto zenu na katika mapito yenu yote.

Nawaombea kwa Mungu ili akwajaze hekima kuu ili muweze kupambana na tufani ya mageuzi haya ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini Tanzania.

Mungu yuko upande wetu, tumwogope nani?

Kwako MH Lowassa.
Mimi binafsi nimekuwa mpiganaji mkubwa nikipiga kelele juu ya Uhabithi wako.

Mungu amekulipa uovu wako, si haki kabisa kumlaumu Dr Mwakyembe wakulaumu ni dhamira yako chafu ya kupenda kutajirika bila kufanya kazi, na zaidi kutajirika huku ukiweka nchi katika lindi kuu la umasikini wa kujitakia.
Unaifilisi na kuiangamiza kwa hila na chuki nchi ambayo imekulea hadi umeota mvi ukiwa kijana.
Wewe na Wazebaki wenzako ni lazima mahali penu patoweke kabisa, libakie jivu tu juu ya mahali hapo
MH sana Mamvi hatimaye umevuna ulichopanda. Ulipanda bangi ili utuvutishe Mungu mkubwa umevuna bangi na sasa inabidi uivute mwenyewe na mashoga zako.
Bangi hailiwi kama mchicha bangi inavutwa katika msokoto. Nakuombea uvutaji mwema, angalie tu usiwape wanao hiyo misokoto.
Mungu akipenda nitakuja kukusalimu na kukujulia hali ukiwa Keko na kibaka chako kwenye mfuko wa shati.
Hii ni katika kukuonyesha kwamba kama unajua maana yake kimbilia ughaibuni.

Buriani ya kisiasa MH Lowassa.
 
Jamani mimi naona sasa Tanzania Mwamko unakuja, na mambo yanabadilika!! Haya mambo ndiyo tulikuwa unayasubiri tukiwa wavumilivu....Ama kweli mvumilivu, hula mbivu!

Huyu Lowasa sio tu ajiuzulu uwaziri, avuliwe ubunge wake pia... maana kama amefanya haya madhambi yasosemeka, sasa tunamsubirisha nini???? Huyu anatakiwa awekwe chini ya ulinzi kabisa, na maswahiba wake woooote wafuatie nyuma! Jamani nchi nyingine watu kama hawa huwa hawaachiwi hivi hivi!

As for the next PM....JK had better think really good before appointing any FISADI!!!
 
Sasa Rubani wa ile "NDEGE INAYOPAA" amepoteza fahamu ikiwa angani,nani ataishusha?
 
Ninampenda kuipongeza tume teule iliyopewa jukumu hili zito la richmond kwa kuja na ripoti yenye upambanuo yakinifu. Nimepata muda wa kuipitia ripoti yote, na bila kusita inaonesha dhahiri kwamba kiutendaji na kiuwajibikaji Tanzania bado tuna safari ndefu sana. Tanzania si nchi masikini hata kidogo bali hatuna uongozi bora.

Mwisho napenda kuwapongeza wabunge wetu kwa ushujaa wa pamoja walioanza kutuonesha wa kutetea masilahi ya wananchi. Endeleeni na msimamo huo huo na sisi wananchi tutakuwa pamoja nanyi muda wote.
 
Kama alivyo tayari kuwasamehe mafisadi watakaojitokeza, wakikiri ubadhilifu na kurudisha mali, nami nitamsamehe Kikwete akiweza kuwaadhibu wahusika wote bila kumungalia nyani usoni. Nitashindwa kumsamehe kama wahujumu kama Rostam Aziz na wengine hawatafilisiwa mara na kupewa masaa ya kuondoka Tz. Keko wawafungulie vibaka na kukarabati vyumba kwa wateja wapya.

Nitashangaa kama atawarudisha watu kama NW David Msuya alodanganya kuhusu elimu yake kwa kudai ana Shahada ya falsafa (PhD). Nikimsikia Meghji labda iwe mahakani kwenye kesi ya magogo kugeuza nchi jangwa. Mzee pesa mbili naye vivyo hivyo.

Sidhani kama ajira za kindugu BOT zinahitaji tume nyingine.
Kisingov
 
Neema neema, neema imefunguliwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!! vigeregere na vifijo jamani, mwanga umeanza kuonekana! na tukomae hadi mwanga mwangavu upatikane!! God bless us!
 
Hapo kikwete umecheza. Sasa panga timu yenye akili. Pili, punguza idadi ya mawaziri. Hatutaki kusikia mawaziri 60!! It is too expensive for poor country like tanzania to maintain, 60 ministers!!! Napendekeza baraza jipya liwe na mawaziri wasiozidi 15!!

Naelekea Kufikiri vilevile Jk anapaswa kuwaapisha mawaziri wake wapya kwa kuzingatia Amri kuu 10 za Siasa Tz:
1.Usiwe mwongo kama Karamangi.
2.Usiwe Mwizi kama balali.
3.Usiwe Mbishi kama Zitto.
4.Usiwe mbabe kama Sitta.
5.Usihukumu kama Mudhihiri.
6.Usiue kama Ditto.
7.Usidandiye hoja kama Mrema.
8.Ipende Nchi yako kama Slaa.
9.Usiwe na makelele kama Makamba.
10.Usipende hela kama lowwasa.
 
Back
Top Bottom