Baraza la Mawaziri Limevunjwa! (2008)

Dodoma si shwari kabisa. Nimekuta madereva Dodoma hotel wakibandua vibao vya namba za Uwaziri na kuweka STK.... wamekua wadogo hawaongei.

JK alisema, "Nimepokea kwa masikitiko makubwa barua za mawaziri watatu, kati yao limo la Waziri Mkuu. Nimekubali barua zao na kwa kuwa Waziri Mkuu ndiye, ambaye tulishauriana naye kuwateua nyote hapa, kwa hiyo mkataba kati yetu umemalizika leo. Kwa hiyo nitakapotangaza wale ambao sitawaita wasiseme nimewaacha, kwa kuwa nimewacha wote. Wengine tutawaita kuendelea kushirikiana."

Baada ya hapo, kila Waziri alimwambia dereva kubadili namba za W na NW kuwa STK.... Wote niliokutana naye hakuna aliyekua tayari kuzungumza lolote. Hali INATISHA na kumejaa maofisa Usalama kutoka mikoa tofauti na hapa ni "Man 2 man" kwa wale wanaohofiwa kuweza kuleta madhara. Ni kama MAPINDUZI VILE
 
Kama hii issue yote hakuwa na personal interest kuwachafua watu basi Kikwete anakuwa maarufu next to Nyerere katika historia ya nchi hii.
 
Itakuwa bora akipunguza ukubwa wa Baraza, aidha achague watu wenye nia ya kweli ya kwenda na kauli mbiu yake iliyompatia ushindi wa kishindo.
Zaidi anapaswa kuona kujua kuwa mamilioni ya Watanzania wanamtizama yeye na bado wana imani kubwa kwake, hivyo karata zake safari hii azipange vizuri...
 
Why MEMBE?? Amefanya kitu gani cha ajabu au cha muhimu kwa Tanzania? This guy seems like the most inefficient minister ambaye anabebwa na JK kwa ajili ya urafiki wao wa siku nyingi. Hatutaki PM mpya awe swahiba mwingine wa muungwana, tunataka mtu mchapakazi na asiye na unafiki.
 
Masatu,
Macho yangu yana makengeza au manake juu pale naona pameandikwa "...where we dare to talk openly" au kuna limit?

Khah Khah! Mafuchila kwani hata Takukuru walisema mkataba wa Richmond ulikuwa safi na shindanishi, tuliyaona jana sina haja ya kuyarudia!
 
Membe alimchomea Hans Kitime kwa nani? nadhani Kitine alijichomea mwenyewe kama alivyojichomea Lowassa, asisingiziwe mtu mwingine.
 
Hapo CCM ndipo ninapowapenda
Grafu lao lilikua limeshuka mpaka karibu na ziro saizi hakika wameripandisha balaa.
Bush akija nikusifia tu kwenda mbele na mataifa yote ya afrika kuambiwa wajifunze toka kwa Kikwete.
Kikwete Aminia unajua kucheza vizuri na wabongo TEN OVER TEN
 
Mambo ya kutabiri jina la PM sasa hivi hayatufai chochote, nina uhakika JK alishaamua siku nyingi kuhusu PM mpya.
 
Siku ya nyani kufa miti yote huteleza. Atakayechaguliwa ni lazima awe safi vinginevyo tutakuwa tunafanya mchezo wa kuigiza tunasubiri hilo jina na wabunge waendeleze kazi waliyotumwa na wawakilishi wao wanaowalipa marupurupu.
 
mie sintoshangaa Rostam Aziz akiwa Pm mpyaaa heheeee...

mayb mr President might go for a lady Pm ajiongezee umaarufu na kurudisha baraza la mawaziri wachache kuongeza mboga chumvi ikolee vyema kuwadanganya wananchi vyema 2010!!!
 
Kama chess JK analijua! Umeona alivyomwahi swahiba wake na kumshangaza na "check mate" katika saa asiyoitarajia kabisa?
 
Kama chess JK analijua! Umeona alivyomwahi swahiba wake na kumshangaza na "check mate" katika saa asiyoitarajia kabisa?

Politics balaa, yaani EL leo kashakuwa kimeo, hakuna mtu anayetaka kujiweka karibu yake.
 
Kama hii issue yote hakuwa na personal interest kuwachafua watu basi Kikwete anakuwa maarufu next to Nyerere katika historia ya nchi hii.

Bahati yetu ilivyo nzuri; haitatulazimu kuendelea kuandika kwa mate, wino uko njiani. Tuvute subira tu kidogo.
 
Kama hii issue yote hakuwa na personal interest kuwachafua watu basi Kikwete anakuwa maarufu next to Nyerere katika historia ya nchi hii.

...lakini umeme bado hatujapata na hakuna yeyote aliyechukua pesa zetu amerudisha,afanye kazi na ndio tulitaka hivi wakati anachaguliwa sio kuwaacha mafia watuibie
 
Back
Top Bottom