Bravo JK kuwatolea nje Balozi shoga wa Uingereza!

Jambo kubwa hapa ni kushikamana tumsifu Mh kikwete kama kweli kaukataa ushoga,
lakini Busara itumike tena kwa makini kabisa ilii Ktk KATIBA MPYA ITAMKWE WAZI NO USHOGA
hapa ndipo tutakapo piga bao Mh kikwete RUHUSU katiba ipitiwe na wadau wote ONDOA usa
nii katika mambo mazito ili Tujenge nchi.......
 
Nilikuwa nasikiliza redio moja ya hapa jijini mchana huu na kati ya mambo yaliyojiri ni utambulisho wa Balozi mmoja mgeni wa Uingereza ambaye nchi yake ilimteua ili aje awe Balozi hapa kwetu.

Balozi huyo shoga kaoa mwanaume mwenziwe. Mambo ya nje kuona hii ni issue hot ilimpelekea JK suala hili na kulingana na Waziri Membe JK alistushwa na kutamka "Yallahi toba!!!' Baadaye akakataa katakata kumpokea Balozi huyo.

Nampongeza JK kwa hilo, limetudhalilisha sana swala la huyu David Cameron kutaka kutushutisha ushoga wao nchi za Dunia ya Tatu

Source :East Africa Radio-Zembwela na Baruti

huyu huyu jk wetu ninayemjua au...??

kama ni kweli hii imetokea, jk atarudi kukanusha na kudai alipewa misleading taarifa na wasaidizi wake...... subirini.
 
Tunajua Serikali yetu haina dini. Je, Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasemaje kuhusu hayo mambo?
 
Nilikuwa nasikiliza redio moja ya hapa jijini mchana huu na kati ya mambo yaliyojiri ni utambulisho wa Balozi mmoja mgeni wa Uingereza ambaye nchi yake ilimteua ili aje awe Balozi hapa kwetu.

Balozi huyo shoga kaoa mwanaume mwenziwe. Mambo ya nje kuona hii ni issue hot ilimpelekea JK suala hili na kulingana na Waziri Membe JK alistushwa na kutamka "Yallahi toba!!!' Baadaye akakataa katakata kumpokea Balozi huyo.

Nampongeza JK kwa hilo, limetudhalilisha sana swala la huyu David Cameron kutaka kutushutisha ushoga wao nchi za Dunia ya Tatu

Source :East Africa Radio-Zembwela na Baruti
Hili suala jk hastahili kupongezwa maana aliapa kuilinda na kuitetea katiba ya jamhuri ya muungano ambayo inakataza ndoa ya jinsia moja. Hivi unaweza kumsifia shehe kuvaa kanzu msikitini wakati ni vazi la kiislamu?
 
Natamani kuona katuni muafaka ya swala hili kwenye gazeti.... sijui itafananaje
 
Balozi wa Uingereza Tanzania ni mwanamke. Hii habari labda ya uongo? Huyo Balozi JK alikataa kuonana naye au amemfukuza nchini?
 
Tobaa! Haki ya kwenda kinyume cha maumbile!!!!!?? Cameroon aachwe na ngawila zake nasi tubaki na utu wetu...kwani msaada lazima uingereza tu! mbona bado kuna wafadhili wengi na wa maana kuliko hao.

Achana na dependency syndrome wewe *****, kwani ni lazima tuwategemee hao unaowaita wafadhili; sisi tunaweza kubana mianya tunayonyonywa na mafisadi na kupata fedha za kutosha kujiendeleza!! Bandari ya Dar es salaam pekee ikiendeshwa kwa ufanisi inaweza kututoa kimasomaso!!Tatizo liko kwa mkweree na genge lake ndio wanaturudisha nyuma.
 
Hili swala ni la kifedhuli kabisa. Kwanza ni dharau kwa nchi ya Uingereza kuliambia bara zima la Afrika upuuzi kama huu.
Walitakiwa wakati anasema haya wajumbe wote kutoka Afrika watoke nje ya mkutano. Hapa wanatuonyesha kuwa bado wanatutawala kimawazo au nini haswa?

Japokuwa sijakaa huko UK, lakini siamini kama nusu ya wananchi wa Uingereza wanaunga mkono ushoga.
Hakuna kitu kibaya kama misaada hapa duniani.
Inabidi kweli tusimame imara. Ukiona haya yanaaza ujue kuna agenda ya siri wanayo hawa wazungu. Walahi watakuja kutuletea madawa huku wageuze watoto wetu mashoga! Hapa inahitajika kufikiri kwa haraka sana.
 
Balozi wa Uingereza Tanzania ni mwanamke. Hii habari labda ya uongo? Huyo Balozi JK alikataa kuonana naye au amemfukuza nchini?

Hata me naona kama ya uongo sababu huyo balozi mwenyewe hata hatajwi jina na awasemi kaja lini! Kama kuna mtu anamjua heb wekeni jina lake hapa
 
Sioni sababu ya kuendeleza mjadala usiokuwa na tija yoyote wakati tunayo mambo mengi ya msingi. Issue ya kukataa balozi ni jambo la kawaida. Nashangaa mambo ambayo yalipaswa kubakia Wizarani na Ikulu yanaletwa kwetu. Huu ni uswahili na kutafuta cheap popularity. Kama anaweza ropoka hayo,ni mangapi anaropoka bar na kwa marafiki zake.
 
Nsubiri Salva ajitokeze kukanusha taarifa hizi lakini mpaka sasa naona kimya.....atuambie Membe alimaanishi nini kutoa taarifa zisizo na ukweli, taarifa ambazo ni za uongo zilizotolewa na waziri wa mambo ya nje zinazomhusisha rais wa nchi....
Inabidi ufafanuzi utolewe haraka kabla ya aibu ya kutengeneza hadithi ili ku-gain credi haijatutokea.
 
habari hii haina ukweli wowote nimefwatilia kama cameron aliteua mabalozi nimekuta hamna kitu...mada nyingine tuchangie kwa kuangalia watoa mada...
 
hahahaaaaaah Kikwete aliwahi kusema hawezi kukaa hapa kujenga nchi na kula nasi mihogo, yeye anapanda ndege kwenda kuhemea ili sisi Watu wake tuendelee kufaidi , hahaaaah sasa Mpango mzima kubinuana na kubinjuana ...!
Kikwete hana kiburi wala uwezo wa kuwakatalia wazungu mahitaji yao.

Bangi za kilosa utazijua tu. Sasa wewe unaambiwa kamkataa halafu unasema hana ubavu, wa kufanya nini?
 
Kwa mara ya kwanza JK atatoa maamuzi ya kiume
Kafanya hivyo kulipa kisasi maana walikuwa wametoka kupunguza msaada wao ktk budget kwa 30%. Kama wasingempunguzia msaada angekauka kau!. Ukitaka kujua kuwa ushoga haumkeri kikwete jiulize mbona hatujasikia kuna shoga kachukuliwa hatua yoyote, wakati wako chungu nzima hapa nchini na wengine wanajitangaza kabisa.
 
Back
Top Bottom