Bracket kumshitaki msanii chipukizi wa Uganda kwa kuiba wimbo wao

Kabota

Member
Aug 15, 2009
63
10
Wanamuziki wa kundi la Bracket la Nigeria Ozioko Nwachukwu a.k.a Vast na Ali Obumneme wamepanga kumshitaki msanii anayechipukia kwa kasi nchini Uganda, Ray wa Big Tym Crew kwa kuwaibia wimbo (Kukiuka sheria za haki miliki)


Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, wimbo wa Ray uitwao Kasenyanku, ambao unahit kinoma nchini Uganda ni kopi ya wimbo wao.


Wasanii hao walikuwa wanangalia video kwenye mtandao wa Youtube na kama bahati tu wakaiona video hiyo na walipousikiliza wakasikia unasound kila kitu kama wimbo wao uitwao Me & You.

Clink link hapo chini kwa taarifa zaidi na kusikiliza nyimbo hizo


DAILY ENTERTAINMENT TAKE AWAY: Bracket kumshitaki msanii chipukizi wa Uganda kwa kuiba wimbo wao
 
Ni kweli sio habari njema kwake. Lakini yeye anadai kuwa alipewa go ahead na XMALEYA!
 
Back
Top Bottom