BP yasimamishwa, bosi wake kushitakiwa

Sijaona kama kafungiwa, jumla auze kwa wengine, rejareja wauze kwa kununua kwa wengine! Just another paradox.
 
Nini maana ya kusimamisha? Nahisi ban inaninyemelea. Ngoja nikae kimya kwanza niangalie upepo unaelekea wapi.
Wakati umechoka kwa kazi, una kizunguzungu kwa kuzunguka sana kutafuta petrol na hatimaye umefika nyumbani kupumzika unakutana na utundu huu, aisee CD nimecheka nahisi nimetumia energy nyingi sana... duh
 
Ewura wamefungia Kampun ya BP kuuza rejareja. Mi naishangaa serikali inawafungi afu inaruhusu wauze yaliyoko kwenye stoke mi nilitegemea hawauzi na yaliyopo either yaharibike au yataifishwe kwan BP ni wahujum uchumi na wamewatesa wananchi. Nawasilisha wadau maoni yenu kuhusu hili.
 
FRIDAY, AUGUST 12, 2011

Sixth Floor, Harbourview Towers, Samora AvenueP O Box 72175, Dar Es Salaam, Tanzania
TEL: (+255-22) 2123850; 2123853; 2123854; 2123856; FAX: (+255-22) 2123180
E-mail: info@ewura.go.tz Website: http//www.ewura.go.tz

TAARIFA KWA UMMA JUU YA KUSISITISHA KWA LESENI YA BIASHARA YA JUMLA KWA KAMPUNI YA BP (T) LTD KWA MATUFA YA PETROLI, DIZELI NA TAA NA KUTOA ONYO KALI KWA KAMPUNI ZA ENGEN PETROLEUM (T) LTD, OILCOM (T) LTD NA CAMEL OIL (T) LTD

UTANGULIZI
Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 22 Juni 2011 Serikali, kupitia kwa Waziri wa Fedha na Uchumi wakati akihitimisha Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, ilitoa maagizo kwa EWURA kuchukua hatua mbalimbali zitakazochangia kupunguza bei za mafuta kwa utaja maeneo mengi kama ifuatavyo (tunanukuu):
(a) Ukokotoaji wa thamani ya shilingi kwa kuioanisha na Dola ya Marekani (yaani Exchange rate);
(b) Kuondoa au kupunguza wigo wa asilimia 7.5 ambayo makampuni yaliruhusiwa kuwekwa ili kufidia baadhi ya gharama;
(c) kupitia upya misingi ya ukokotoaji wa viwango vya tozo mbalimbali za taasisi za Umma kwa lengo la kubakia na tozo stahili na kwa viwango stahili bila kuathiri majukumu ya udhibiti ma usimamizi yanayofanywa na Taasisi hizo;
(d) kupunguza tozo za kampuni za mafuta ikiwa ni pamoja na gharama za kibenki (yaani Financing Charges); na
(e) Upotevu wa mafuta yanayosafirishwa kwenye meli na gharama ya ukaguzi (yaani inspection fee).
(mwisho wa kunukuu).
Aidha, mnamo tarehe 4 Julai 2011, EWURA ilianza mchakato kwa kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari kuhusu mchakato wa kupunguza bei za mafuta. Pia EWURA iliandaa dokezo (discussuon paper) lililokuwa na vipengele mbalimbali ambavyo vitapunguzwa na kusambazwa kwa wadau mbalimbali wakiwemo wauzaji wa mafuta hapa nchini.
Wadau mbalimbali walichangia dokezo hilo na kuwasilisha EWURA kwa maandishi na hatimaye mchakato wa utengenezaji wa Kanuni mpya ambayo imepunguza bei za mafuta ulihitimishwa kwa kuitisha Mkutano wa TAFTISHI uliofanyika Julai 22, 2011 katika Ukumbi wa Karimjee

USHIRIKISHAJI WADAU
Mchakato wa kupata maoni ya wadau (taftishi) ulianza tarehe 04 Julai 2011 na kukamilika tarehe 26 Julai 2011. Kwa kawaida, mchakato huu ungechukua siku 81 lakini kutokana na unyeti wa suala hili, Mamlaka ililazimika kuufupisha hadi siku 23. Wadau walioshirikishwa katika taftishi hiyo ni pamoja na kampuni za mafuta, Baraza la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na EWURA (Consumer Consultative Council), Baraza la Ushauri la Serikali, Taasisi za Umma kama vile TRA, TBS, WMA, TPDC, TPA, SUMATRA, na TIPER.
MATOKEO BAADA Maoni mbalimbali ya wadau yalipokelewa na kuchambuliwa na timu ya wataalam kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na Uchumi, Shirika la Maendeleo ya Mfuta Tanzania (TPDC), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na EWURA na katika mfumo mzima wa kufanikisha utayarishaji wa kanuni hii mpya, wadau wote walifahamishwa katika mchakato huu kuwa bei mpya zitatolewa tarehe 1 Agosti 2011.

YA KUTANGAZ BEI MPYA

Baada ya kutangaza bei mpya zilizoanza Agosti 3, 2011 kampuni zilianza mgomo baridi wa kutouza mafuta kutoka kwenye magahala yake. Hata hivyo mgomo huo haukufahamika sana kutokana na kutokea wakati kukiwa na siku za mapumziko ya muda mrefu yaani taari 6 hadi tarehe 8 Agosti 2011.

Baada ya kugundua hilo, Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA ilikaa Agosti 9, 2011 na kutoa AGIZO LA KISHERIA (ORDER) kwa kampuni nne ambazo zilionekana ndizo kinara wa mgomo husika. Kampuni hizo ni BP (T) Ltd, Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd.

Agizo hilo la kisheria lilizitaka kampuni hizotajwa kutekeleza yafuatayo;
(a) Waanze kuuza mafuta mara moja baada ya kupata agizo la kisheria kutoka EWURA
(b) Waache mara moja vitendo vyovyote vinavyozuia uuzwaji wa mafuta
(c) Watoe maelezo kwa maandishi katika muda wa saa 24 kwa kuvunja Sheria ya Petroli ya mwaka 2008 kifungu 24 (1).
Baada ya agizo kutolewa tarehe 9 Agosti 2011, kesho yake kampuni zote zilianza kuuza mafuta kwenye maghala ambapo siku ya kwanza tarehe 10, Agosti 2011 ziliuzwa lita 8,535,700 kutoka kwenye maghala .
Hata hivyo, pamoja na kuuzwa kwa mafuta kwa wingi, bado BP (T) Ltd alionekana kukahidi amri halali ya EWURA kwa kuzingatia Sheria ya Petroli ya mwaka 2008, kifungu 24 (1) kwa kutouzaa mafuta kwenye vituo vyake vyote.

HATUA ZINAZOCHUKULIWA

Baada ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, Bodi ya Wakurugenzi imekutana leo na kuamua yafuatayo:
a) Kuziandikia ONYO KALI kampuni za Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd kuwaonya kutorudia tabia walioionesha ambayo ni kinyume na Sheria za Tanzania na kuwaagiza wauze mafuta kwa watu wote bila ubaguzi. Amri hii itafuatiliwa kwa ujirani na ikibainika wamekiuka hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao mara moja
b) Kusitisha leseni ya biashara kwa BP (T) Ltd kwa MIEZI MITATU KUANZIA LEO kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na Taa.

c) BP (T) Ltd ataruhusiwa kuendelea kuuza mafuta ya ndege kutokana na ukweli kwamba EWURA haidhibiti bei za mafuta ya ndege ambao ndio msingi wa mgomo kwa wafanyabiashara ya mafuta.
d) Pia BP (T) Ltd ataruhusiwa kuuza mafuta yake yote ya petroli, dizeli na taa yaliyopo kwenye maghala yake kwa wafanyabiashara wengine wa jumla kama wanataka kwa usimamizi wa EWURA ili kuzuia kutoharibika kwa mafuta hayo katika kipindi hicho cha miezi mitatu ambapo hataruhusiwa kufanya biashara ya mafuta ya jumla.
e) Hata hivyo, vituo vyote vya rejareja (Petrol Stations) vya vyenye nembo ya BP vitaruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua mafuta kwa wafanyabiashara wengine wa jumla na si kwa BP.
f) Pia Bodi ya Wakurugenzi imeeagiza Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa BP (T) Ltd kufikishwa Mahakamani kwa kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Jinai (DPP).

USIMAMIZI WA MAFUTA

a) Kuanzia sasa EWURA itaendelea kuangalia mfumo mzima wa mafuta yanayoingia bandarini.
b) Pia EWURA itaendelea kufuatilia bei zinazouzwa kwenye vituo kama zinafanana na zile zilizotangazwa.

IMESAINIWA
Haruna Masebu
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI (EWURA)
 
CHANGA LA MACHO HILO BP WANAMPANGO WAKUONDOKA BONGO

BP Ceases Its Country Operations

It is end of an era for BP Tanzania, ..........
The decision is likely to affect Tanzania's petroleum marketing industry ......... Until recently, BP Tanzania has had a 35 per cent market share in both the retail and service stations and about 70 per cent in aviation. In Zanzibar it has been controlling the aviation fuel market by about 100 per cent....

Hapo kwenye blue !!!!

Ninachokisoma hapa inaonekana BP walishajitoa ktk biashara ya petroli, diesel na kerosine.
Inaonekana wala hawakugoma ... isipokuwa hawakuwa na stock kwa sababu they no longer traded in these commodities.

Sasa these goons from EWURA wamechunguza na wamecomfirm kuwa BP hawana kitu cha kuuza, sasa how do they get some mileage out of this??? Na kuonyesha kwamba serikali imefanya uamuzi mgumu??
Wameamua watunge stori na kudanganya Watanzania... I will bet my tshs 500/= on this scenario !!!

The catch word ktk hiyo report ni ... "until recently...."
 
Kiongozi Halisi:

Huu uamuzi umejaa "utata"!

Unaweza "kusitisha leseni" halafu ukaruhusu kuendelea "kuuza mafuta ya ndege" na "..kwa vituo vya rejareja vyenye nembo ya BP"?

yaani we hacha tu hapa ewura wanataka tuamini wamechukua hatua hahahahah
ina maana hivyo vituo vyenye NEMBO sio sehemu ya BP hayo mafuta ya jumla wanayosema BP itawauzia wauzaji wa jumla
wengine ni miezi mingapi (i mean ni stock kubwa kiasi gani)?
Hawa wamepiga BAN hewa by the time stock ya mafuta ya BP inakwisha kwenye hizo depot muda wa BAN umekwisha by the way vituo vyao vya mafuta bado viko wazi

upuuzi huu sijui utaisha lini
wananikumbusha uswahili mtoto anakutukana matusi ya NGUO NA KUKUDHALILISHA unakwenda kusema kwa mama yake
mama anatoka na kanga na kuanza kumchapa mtoto na upindo wa kanga huku mtoto ana cheka na wewe unaangalia adhabu inayotolea
ukilalamika unaambiwa babu weee kube mimba miezi tisa sio mchezo, sasa ndio haya
 
mmmmh! kulia nataka, kutukana nataka, kunyamaza najitwisha zigo rohoni, sasa daaah! i wish ningekuwa arusha jana walau nijifariji kwa kuona nyomi la pipooos.
 
d) Pia BP (T) Ltd ataruhusiwa kuuza mafuta yake yote ya petroli, dizeli na taa yaliyopo kwenye maghala yake kwa wafanyabiashara wengine wa jumla kama wanataka kwa usimamizi wa EWURA ili kuzuia kutoharibika kwa mafuta hayo katika kipindi hicho cha miezi mitatu ambapo hataruhusiwa kufanya biashara ya mafuta ya jumla.

e) Hata hivyo, vituo vyote vya rejareja (Petrol Stations) vya vyenye nembo ya BP vitaruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua mafuta kwa wafanyabiashara wengine wa jumla na si kwa BP.
.
Kwa kifupi BP atakua anauza/anahifadhi/anahamisha kwa Mshirika wake tuseme Engen,
Kisha Engen anamsaidia BP kumuuzia mafuta kwa vituo vyake vyenye nembo ya BP,
Kisha watu wanampa Ngeleja Credit kwa hili suala,
Ukichanganya na mitambo feki iliyotokea Mombasa na huu umeme wa kudanganyishiwa kwa muda Bajeti inapita kwa kishindo.
Halafu kichapo kinarudi palepale!!
Wajinga ndio tuliwao, hatuna Jinsi, ndio tushazaliwa Danganyika
 
Hakika hiyo ni danganya toto na ni ufisadi huo,serikali ina hisa BP asilimia 49 wameifungia leseni makampuni mengine ambayo serikali haina hisa haijaguswa hata moja,huo ni mpango mkubwa wa kuiba mali za wananchi.
 
HATUA ZINAZOCHUKULIWA

Baada ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, Bodi ya Wakurugenzi imekutana leo na kuamua yafuatayo:

a) Kuziandikia ONYO KALI kampuni za Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd kuwaonya kutorudia tabia walioionesha ambayo ni kinyume na Sheria za Tanzania na kuwaagiza wauze mafuta kwa watu wote bila ubaguzi. Amri hii itafuatiliwa kwa ujirani na ikibainika wamekiuka hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao mara moja

b) Kusitisha leseni ya biashara kwa BP (T) Ltd kwa MIEZI MITATU KUANZIA LEO kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na Taa.

c) BP (T) Ltd ataruhusiwa kuendelea kuuza mafuta ya ndege kutokana na ukweli kwamba EWURA haidhibiti bei za mafuta ya ndege ambao ndio msingi wa mgomo kwa wafanyabiashara ya mafuta.

d) Pia BP (T) Ltd ataruhusiwa kuuza mafuta yake yote ya petroli, dizeli na taa yaliyopo kwenye maghala yake kwa wafanyabiashara wengine wa jumla kama wanataka kwa usimamizi wa EWURA ili kuzuia kutoharibika kwa mafuta hayo katika kipindi hicho cha miezi mitatu ambapo hataruhusiwa kufanya biashara ya mafuta ya jumla.

e) Hata hivyo, vituo vyote vya rejareja (Petrol Stations) vya vyenye nembo ya BP vitaruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua mafuta kwa wafanyabiashara wengine wa jumla na si kwa BP.

f) Pia Bodi ya Wakurugenzi imeeagiza Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa BP (T) Ltd kufikishwa Mahakamani kwa kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Jinai (DPP).

USIMAMIZI WA MAFUTA

a) Kuanzia sasa EWURA itaendelea kuangalia mfumo mzima wa mafuta yanayoingia bandarini.

b) Pia EWURA itaendelea kufuatilia bei zinazouzwa kwenye vituo kama zinafanana na zile zilizotangazwa.

inakupasa kuwa juha kuamini hizi pumba za ewura.

BP pulls out of Tanzania - UPI.com
 
Kwa icho kipengele namba nne et vituo vyenye nembo ya bp waendelee kuuza mafuta ila wasiyanunue toka kwa Bp wenyewe.hapo mwenye kufikir anajua kabisa 2naibiwa
 
hawa magamba zero kabisa. yaani bp ilivyojitoa hawakutangaza; sasa magamba wamelikoroga wanaanza kututangazia wameifungia bp? wadanganyika amkeni jamani.
 
HATUA ZINAZOCHUKULIWA

Baada ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, Bodi ya Wakurugenzi imekutana leo na kuamua yafuatayo:

a) Kuziandikia ONYO KALI kampuni za Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd kuwaonya kutorudia tabia walioionesha ambayo ni kinyume na Sheria za Tanzania na kuwaagiza wauze mafuta kwa watu wote bila ubaguzi. Amri hii itafuatiliwa kwa ujirani na ikibainika wamekiuka hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao mara moja

b) Kusitisha leseni ya biashara kwa BP (T) Ltd kwa MIEZI MITATU KUANZIA LEO kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na Taa.

c) BP (T) Ltd ataruhusiwa kuendelea kuuza mafuta ya ndege kutokana na ukweli kwamba EWURA haidhibiti bei za mafuta ya ndege ambao ndio msingi wa mgomo kwa wafanyabiashara ya mafuta.

d) Pia BP (T) Ltd ataruhusiwa kuuza mafuta yake yote ya petroli, dizeli na taa yaliyopo kwenye maghala yake kwa wafanyabiashara wengine wa jumla kama wanataka kwa usimamizi wa EWURA ili kuzuia kutoharibika kwa mafuta hayo katika kipindi hicho cha miezi mitatu ambapo hataruhusiwa kufanya biashara ya mafuta ya jumla.

e) Hata hivyo, vituo vyote vya rejareja (Petrol Stations) vya vyenye nembo ya BP vitaruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua mafuta kwa wafanyabiashara wengine wa jumla na si kwa BP.

f) Pia Bodi ya Wakurugenzi imeeagiza Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa BP (T) Ltd kufikishwa Mahakamani kwa kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Jinai (DPP).

USIMAMIZI WA MAFUTA

a) Kuanzia sasa EWURA itaendelea kuangalia mfumo mzima wa mafuta yanayoingia bandarini.

b) Pia EWURA itaendelea kufuatilia bei zinazouzwa kwenye vituo kama zinafanana na zile zilizotangazwa.

Mbona kipengele (d) na (e) vinajichanganyaaa?
 
1. Leseni ya BP imefungwa kwa muda, imesitishwa. lakini, ikumbukwe kwamba kwa kuwa EWURA anabanwa kisheria pia kuhakikisha service providers wanakuwa financially viable, ndiyo maana wameruhusu hii stock iliyopo iweze kuuzwa (maana mafuta yakikaa miezi mitatu yanaweza kubadilika ubora wake, kwa mujibu wa ninachokisikia kwa wataalamu) na ikumbukwe kwamba 2. mafuta yaliyopo BP takwimu zake anazo regulator, na ndiyo maana atakapotaka kuuza itabidi awa consult EWURA.

2. JET A1 bei yake hairatibiwi na EWURA, kwa mujibu wa sheria, na ndiyo maana hawa jamaa hawajihushsi nayo.

3. Si kweli kwamba kila kituo chenye nembo ya BP kinamilikiwa na BP, wakuu, (mfano Mwanamboka, na BP Sinza) na ndiyo maana imewekwa wazi vile vituo vinaweza kuuza tu mafuta hayo ila si kununua toka BP.

4. Adhabu hii ina maana BP akiuza stock yake iliyopo sasa, hatafanya biashara mitaani kwa miezi mitatu, na tusijidanganye kuwa stock yake ilikuwa ya kutosha biashara ya miezi mitatu.

5. The way forward ni BP kukata rufaa Fair Competition Tribunal, Baraza la Ushindani wa Haki, ambako kesi nzima inaweza kuangalia upya.

6. Kwa kuwa BP walishiriki kwenye kile kinachoonekana cartel na makampuni mengine, huko yawezekana wakakutana na kesi mpya dhidi yao ambayo EWURA tayari imeshaforward malalamiko.

hakuna haja ya kushabikia bila kujaribu kutafsiri haya...tumieni website ya EWURA kwa maelezo zaidi ya mechanism ya maamuzi.
 
Poor Africa. Every person is political oriented not business oriented. And so we are poor. And so we take poor government decisions as tough decisions. And so all international companies are flying out. Shell gone, BP gone, Caltex gone, Agip gone, Esso gone. And so we are left with corrupt and unethical oil companies. Name it GAPCO, Moil, Oilcom, Camel Oil, Lake Oil. And all these are owned by immoral, corrupt and unethical segregative races of Asia. And name them Indians and Arabs.
BP is an ethical oriented company that cannot deny government decisions if they are genuine and legal. In this saga government is the problem not BP. If a company bought tones of fuel in higher prices with higher taxes who is going to recover losses raising from low price sales. Poor tanzania government is putting business down to please frustruated citizens who cannot think.
 
1. Leseni ya bp imefungwa kwa muda, imesitishwa. Lakini, ikumbukwe kwamba kwa kuwa ewura anabanwa kisheria pia kuhakikisha service providers wanakuwa financially viable, ndiyo maana wameruhusu hii stock iliyopo iweze kuuzwa (maana mafuta yakikaa miezi mitatu yanaweza kubadilika ubora wake, kwa mujibu wa ninachokisikia kwa wataalamu) na ikumbukwe kwamba 2. Mafuta yaliyopo bp takwimu zake anazo regulator, na ndiyo maana atakapotaka kuuza itabidi awa consult ewura.

2. Jet a1 bei yake hairatibiwi na ewura, kwa mujibu wa sheria, na ndiyo maana hawa jamaa hawajihushsi nayo.

3. Si kweli kwamba kila kituo chenye nembo ya bp kinamilikiwa na bp, wakuu, (mfano mwanamboka, na bp sinza) na ndiyo maana imewekwa wazi vile vituo vinaweza kuuza tu mafuta hayo ila si kununua toka bp.

4. Adhabu hii ina maana bp akiuza stock yake iliyopo sasa, hatafanya biashara mitaani kwa miezi mitatu, na tusijidanganye kuwa stock yake ilikuwa ya kutosha biashara ya miezi mitatu.

5. The way forward ni bp kukata rufaa fair competition tribunal, baraza la ushindani wa haki, ambako kesi nzima inaweza kuangalia upya.

6. Kwa kuwa bp walishiriki kwenye kile kinachoonekana cartel na makampuni mengine, huko yawezekana wakakutana na kesi mpya dhidi yao ambayo ewura tayari imeshaforward malalamiko.

Hakuna haja ya kushabikia bila kujaribu kutafsiri haya...tumieni website ya ewura kwa maelezo zaidi ya mechanism ya maamuzi.

mkuu ila kumbuka kwamba bp wako kwenye mpango wa kuondoka kabisa tanzania na ndo starategies yao hiyo. Bp wana miaka mingi kuliko kampuni yoyote ile hapa tanzania na hawawezi hata siku moja kuigomea serikali.

Tatizo wa tz ujuha unatusumbua sana tunaaminshwa kwamba bp ndo wabaya kumbe sivyo
 
Komandoo, haihitaji masters kujua walichokifanya BP. Kama uko Tanzania, umeona vituo vya BP vikifanya biashara toka siku ile walipopewa amri na EWURA wafungue biashara waliyoombea leseni? wakati wengine walilazimika kufungua, wao mpaka leo wamegoma. Hilo ndilo kosa ambalo mwenye leseni ameamua kuwaadhibia.

Kwa siku tatu, wameamua kuuza lita za petroli 48,000 tu, tena wamepeleka migodini. Bila shaka wanakijua walichoamua, lakini hata kama wanafunga biashara, wanaadhibiwa kwa kosa la leo na wala hawaadhibiwi kwa namna nyingine. Na hata utetezi wao ulikuwa very flimsy...ni kama vile hawajali.
 
Back
Top Bottom