BOT yazindua sarafu ya tsh 50,000

Elfu Hamsini niiweke mapambo???!!!!???
NI mlo wa siku ngapi kwa mTZ wa kawaida??
NI bia ngapi au crate ngapi za serengeti kwani??
NI mifuko mingapi ya cement,nimalizie kibanda changu??
ETI niweke mapambo, viongozi wetu hawa kweli wametuchoka!!!!
 
:poa:poa:poa:juggle::juggle::juggle::nerd::nerd::nerd:
 
Benki kuu ya Tanzania BOT imezindua sarafu mpya ya Tsh 50,000/= iliyotengenezwa kwa madini ya fedha ambayo itauzwa katika mabenki kwa ajili ya shamrashamra za miaka 50 ya uhuru je wachumi mliobobea mnalionaje hili na hali ya uchumi wetu ulivyo kwa sasa je ni nani atakubali yaani ununue sarafu ya kufungia chumbani khaaaa!!!!! source tbc jambo leo saa 1 asbh.
Benki Kuu yatoa sarafu ya 50,000/-
02/01/2014 | Posted by Mwandishi Wetu | Kitaifamoto | 0 comments | 15 views
Gavana wa BoT, Profesa Benno NduluBENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema jana kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.

Kwa mujibu wa Gavana, kutolewa kwa sarafu hiyo kunakwenda sambamba na utaratibu wa Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya matukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na kimataifa.

“Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi huongezeka na kuwa na faida zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa Ndulu.

Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000 katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.

“Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi kupitia matawi yake,” alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji zitatolewa na benki hizo.
1964-2014. Benki Kuu yatoa sarafu ya 50,000/-
02/01/2014 | Posted by Mwandishi Wetu | Kitaifamoto | 0 comments | 15 views

ndulu_1.jpg
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema jana kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.
Kwa mujibu wa Gavana, kutolewa kwa sarafu hiyo kunakwenda sambamba na utaratibu wa Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya matukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na kimataifa.
“Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi huongezeka na kuwa na faida zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa Ndulu.
Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000 katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.
“Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi kupitia matawi yake,” alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji zitatolewa na benki hizo.
Katika sarafu hiyo, upande wa mbele unaonyesha sura ya hayati Sheikh Abeid Aman Karume na maandishi yanayosomeka: ‘Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi’. Upande mwingine wa sarafu unaonyesha nembo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, maandishi yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya Mapinduzi”, thamani ya sarafu na miaka 1964-2014.
 
hiyo noti ni ya kumbukumbu tu haiwezwi kuingizwa kwenye mzunguko:llama:
 
Hizi ni kwa ma "collectors" au "hobby" hii huitwa "numismatic" na si kwa kila mtu na ndo maana hizo huwa "limited" na sarafu kama hizi huwa haziingizwi kwenye mzunguko wa fedha.

Tatizo laki ni ilmu na ilmu haipatikani kwenye kuta nne tu.

Hata wenye fedha wengi huwa hawazinunui hizi kwa sababu si "hobby" yao, na si sarafu tu hutolewa stempu, tshirts, khanga, vitenge, "key chains" na vitu vingi vinavyoweza kukumbusha baadae "occasion" hiyo. Na hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kutoa sarafu za "commemoration" (kumbukumbu). Funguka kidogo.

BoT inaleta hobby katika kipindi hiki!!????
Hobby ya watu 3000 ni kitu cha kufanywa na BoT kabisa???!!!!
Mapinduzi ya nchi yatumike kutekeleza hobby ya watu 3000????!!!

"Ama kweli kama umekosa mkate kula keki"
 
Miaka hamsini ya uhuru tuna uchumi mbovu kiasi hiki!
Tunasababu ya kusherehekea?Mi naona ni mianya ya watu flani kujitengenezea kipato.ISITISHWE.
Watanzania tunapaswa kufunga na kusali kwa miaka hii 50 baada ya uhuru maana tuna hali dhoof bin taaban
 
BoT inaleta hobby katika kipindi hiki!!????
Hobby ya watu 3000 ni kitu cha kufanywa na BoT kabisa???!!!!
Mapinduzi ya nchi yatumike kutekeleza hobby ya watu 3000????!!!

"Ama kweli kama umekosa mkate kula keki"

Tatizo lenu kubwa ni ujinga mliojazwa shule mlizosoma, watu wanaenda shule kupata ilmu, wenzangu naona mlikwenda kusomea ujinga.
 
Tatizo lenu kubwa ni ujinga mliojazwa shule mlizosoma, watu wanaenda shule kupata ilmu, wenzangu naona mlikwenda kusomea ujinga.

Wewe si ndio umesema kuwa nazo ni hobby sasa BoT watengeneze vitu vya hobby za watu wachache wakati tuna shida lukuki za kiuchumi!!!!!!!!

Hii ndio ilmu sio??!!!!!!

"kweli kujua kwingi mbele giza"
 
Wewe si ndio umesema kuwa nazo ni hobby sasa BoT watengeneze vitu vya hobby za watu wachache wakati tuna shida lukuki za kiuchumi!!!!!!!!

Hii ndio ilmu sio??!!!!!!

"kweli kujua kwingi mbele giza"

Hizo shida za kiuchumi zilikuwa tatizo wakati wa Nyerere, alikuwa hajuwi namna ya kuzitaua. Sasa hivi muarubaini wake Kikwete anaujuwa vilivyo na toka ameshika 2005 tunachanja mbuga, uchumi unakuwa mwaka hadi mwaka. Upo hapo ulipo?

Ukimsikia mtu analia sana shida za kiuchumi ujuwe huyo ni mlevi au mivu wa kutupwa. Wanakuja Wachina kutoka kwao huko wanauza karanga tu na wanatoka, wewe unaelia shida za uchumi unafanya nini? sana sana mda mrefu unaupoteza vilabu vya pombe na starehe.
 
Hao wachina unaowsifia faiza fox .wanabiashara zingine nyuma ya pazia hizi karanga ni zuga tu. ukitaka kuprove maneno yangu rejea matukio kadhaa ya mwaka jana walikamatwa na unga wengine na meno ya tembo.mnawasifia kuwa wanajua biashara huku tembo wanafinish.
 
Back
Top Bottom