BOT yazindua sarafu ya tsh 50,000

Benki kuu ya Tanzania BOT imezindua sarafu mpya ya Tsh 50,000/= iliyotengenezwa kwa madini ya fedha ambayo itauzwa katika mabenki kwa ajili ya shamrashamra za miaka 50 ya uhuru je wachumi mliobobea mnalionaje hili na hali ya uchumi wetu ulivyo kwa sasa je ni nani atakubali yaani ununue sarafu ya kufungia chumbani khaaaa!!!!! source tbc jambo leo saa 1 asbh.

Kama ni sarafu ya fedha basi hii itakuwa na thamani tajwa, mara nyingi sarafu kama hizi za "commemoration" huwa ni "collectors items" na uzoefu unaonesha kuwa kila miaka ikienda zinazidi thamani na si kupunguwa. Najitayarisha kununuwa.
 
Sarafu kwa jina jingine ni noti?
mm hawa wamelewa nn?? natmai sarafu ni coin kwa kimombo au??? lakini ni lazima tusali pia tumuombe mola wetu, huu ni uchuro kwetu, tanzania ata kuitaja maana mdomo unaunda, hii itapelekea kufikilia kuwa na sarafu ya elfu amsini?? tumekwisha, au awa jamaa wanatulia timing ili ikibidi waiingize katika mzunguko (circulation), lakini viongozi wetu waliofikilia ivi na kuilete hii taarifa wana laana na wana roho mbaya sana, wameuvuruga uchumi ambako kwa sasa tuna inflation ya kutisha wana tubip kwa sarafu ya elf50??lazima watanzania tuwe serious na hizi habari kwani hii serikali iko serious kwa jinsi uchumi wetu unavyoelekea tutakuwa kama nchi ya zimbambwe ambapo tutakuwa na noti ata ya trilion 500
 
Benki kuu ya Tanzania BOT imezindua sarafu mpya ya Tsh 50,000/= iliyotengenezwa kwa madini ya fedha ambayo itauzwa katika mabenki kwa ajili ya shamrashamra za miaka 50 ya uhuru je wachumi mliobobea mnalionaje hili na hali ya uchumi wetu ulivyo kwa sasa je ni nani atakubali yaani ununue sarafu ya kufungia chumbani khaaaa!!!!! source tbc jambo leo saa 1 asbh.
ipo kazi mwaka huu!Pesa za maandalizi ya miaka 50 hazijatosha nini?
 
humu janvini kuna watu wanachangia kiushabiki tu, ni bora kama hujui chochote ukae kimya.

- hicho mnacho kiongelea si kigeni kabisa katika mataifa mengine, kama kuna wafuatiliaji wazuri wa mambo ya kimataifa watagundua hicho si kitu kigeni.
- nchi nying sana duniani zinapo azimisha miaka either 25, 50 au 100 huwa na sherehe mbalimbali na kila taasisi ya hizo nchi huja na staili yake ya kuazimisha miaka kadhaa. Na moja wapo huwa ni benk kuu za hizo nchi.

- mnacho pigie kelele sikioni mara o tutakuwa kama zimbabwe mara matrafiki,

- wakuu ni kwamba bot wamejalibu kuiba hii aidia kutoka mataifa mengine ambayo yameisha wahi kuadhimisha miaka yao ya uhuru.

- Mf
ano philipine wakati wanaadhimisha miaka yao nazani ilikuwa 50 au 75 nimesahau kidogo, wao benki kuu yao ilitengeneza not yenye ukubwa wa yale mabango ya barabarani, na hiyo ilitumika kwa siku hiyo pekee yake baada ya hiyo siku kupita, ilibidi waliozipokea wazipeleke benk kuu.
Na si philipine pikee, kuna nchi nyingi zimewahi kutoa pesa ya ajabu maalumu kwa ajili ya kusherekea kitu fulani

turudu huku kwetu, hiyo koin, inaweza kuwa imetengenezwa maalumu kwa ajili ya kutumika siku hiyo tu. Yaani ukibahatika kuipata utaweza nunua bidhaa dukani lakini baada ya siku hiyo walio zipokea watalazimika kwenda kuzichenji benk ili wapewe pesa za kawaida.

na huwa hazitengenezwi nyingi na ni wachache hubahatika kuzitumia, na wanatengeneza kidogo kwa sababu, zitakuwepo kwenye mzunguko kwa siku moja tu. Hao wachache wano bahatika kuzitumia ndo huwakilisha hao walio kosa. Unaweza kuta zitatolewa jumla kuu yake zikawa na thamani ya milioni hata 20. Na zinaweza sambazwa kila wilaya labda koin kadhaa ili wilaya zote zipate watu wakuzitumia kwa siku hiyo.

Akili za kuazima changanya na zako!
Hivi unaposema ni utaratibu wa kawaida na unatumika katika mataifa mengine, so what?...
BRODA UNALINGANISHAJE TANZANIA NA PHILIPINES?...unalinganisha mbingu na ardhi?.....

Hiyo noti itasaidia vipi kusogeza maisha ya Mtz?....Mbona hatuigi mambo ya maendeleo kama ya hapa jirani tu Rwanda?
Kwanini tunaiga vitu vya kuzalisha fedha ya ghafla inayoenda mifukoni mwa watu?

Cha msingi ilikuwa tujilinganishe na nchi zilizopata uhuru mwaka 1961 + or - miaka 5!...je maendeleo yetu yanalinganaje, Kilimo chetu kinasonga mbele, viwanda nk!

Siku ya 9 December inatakiwa kila mtu akae nyumbani kwake akilia machozi na kujiuliza kwanini tupo hapa tulipo, na baadaye aibuke na means za kusaidia kuinua nchi...
Ni maoni binafsi!

Huu ni mji wa Makathi, mji wa kibiashara wa Philipines, ambapo niliyemquote hapo juu anataka tuwaige!....my gosh!
 
Kama wamezindua hiyo inamaana inatumika au ni kwa ajili ya maonyesho tuu?? Huko ni kushuka kwa uchumi vibaya sana angalau ingekuwa ya 20,000/= lakini from 10,000/= to 50,000/= shilingi itakuwa thamani imeshuka sana

Chonde chonde jamani. Hiyo sarafu SI PESA itakayoingia kwenye mzunguko. Ni sarafu ya Sh 50,000 iliyotengenezwa kwa madini ya fedha na itauzwa kama vile pete, mkufu, bangili, heleni au vyovyote utakavyopenda kiita. Zimetengenezwa sarafu 5,000 tu na kila moja itauzwa kwa TSh 50,000.00
 
Kama ni sarafu ya fedha basi hii itakuwa na thamani tajwa, mara nyingi sarafu kama hizi za "commemoration" huwa ni "collectors items" na uzoefu unaonesha kuwa kila miaka ikienda zinazidi thamani na si kupunguwa. Najitayarisha kununuwa.
Fursa hii ya kuinunua fedha hiyo na kujiongezea fedha inawezekana kwa Watanzania kiasi gani, kama si wajanja wachache?
Unainadi sherehe kuwa ni Miaka 50 ya uhuru wa Tz bara, lakini unafanya mambo ya kuwanufaisha wenye fedha ili waongeze akiba zao!...cant easily figure out and finally buy this!
 
mliochangia mada wengi mmeipotosha wengine wameamua kuwa ni noti na itaingia kwenye mzunguko ishu yangu ilikuwa ni jee katika hali ya mdororo wa uchumi wetu na huku kila mtanzania aahh sehemu kubwa ya watz wakilia njaa na ukata wa fedha leo hii watu wanaibuka na ishu ya kutengeneza sarafu kwa ajili ya kuiuza ni nani atamudu kuinunua aache shida zake lukuki zinazohitaji hela ni sahihi kweli nadhani badala ya kutengeneza hizo sarafu ni heri BOT ingetumia gharama hizo kununulia japo dawa na kusambaza kwenye hospitali hata tatu tu za wilaya ingesaidia saaaaaannnaaaa!!!kuliko hizi sanaa
 
Chonde chonde jamani. Hiyo sarafu SI PESA itakayoingia kwenye mzunguko. Ni sarafu ya Sh 50,000 iliyotengenezwa kwa madini ya fedha na itauzwa kama vile pete, mkufu, bangili, heleni au vyovyote utakavyopenda kiita. Zimetengenezwa sarafu 5,000 tu na kila moja itauzwa kwa TSh 50,000.00
Sasa ukitaka kugombana na watu ulizia gharama iliyotumika kuzitengeneza hizo coins 5000, utakutana na Version II ya twin towers !
 
Yawezekana hii picha ikawa na ukweli eeh?

NTAKUFA.jpg
 
Hivi sarafu ni note au coin?????!!
Jamani, eleweni thread!

Hii noti ni just ceremonial denomination, na haitaingia kwenye mzunguko wa fedha!

Ila kitendo cha kutengeneza sarafu hii mimi nakiita ulevi tu, maana ni kuchezea rasilimali za nchi, na kutafuta means zote za kujiongezea kipato 'kichafu' kwa baadhi ya maofisa wa BoT!..

Sarafu hiyo itasaidia nini!

Eti kwaajili ya kusherekea niaka 50 ya UHURU,, uhuru wa nani?, nani yuko huru?, nani ameshauri upumbafu huu, na nchi inayosherekea uhuru huu ni ipi, kuna Tanganyika hapa?, Wakoloni weusi wameenda wapi!, ....my hairs!

Ni wangapi(percentage-wise) ya waTanzania watakuwa na uwezo wa kuinunua fedha hiyo kwa purpose ya kuiweka mchagoni kama pambo?

Lakini watangulizi wetu walishasema kuwa dalili ya mvua ni mawingu!...ukiona inatengenezwa sarafu ya denomination hiyo ujue kuwa hiyo idea ndiyo iliyopo vichwani mwa maafisa hawa, na believe me or not, this note is on the pipeline, and soon or later you will test its bitterness!

Shenzi kabisa!
 
humu janvini kuna watu wanachangia kiushabiki tu, ni bora kama hujui chochote ukae kimya.

- hicho mnacho kiongelea si kigeni kabisa katika mataifa mengine, kama kuna wafuatiliaji wazuri wa mambo ya kimataifa watagundua hicho si kitu kigeni.
- nchi nying sana duniani zinapo azimisha miaka either 25, 50 au 100 huwa na sherehe mbalimbali na kila taasisi ya hizo nchi huja na staili yake ya kuazimisha miaka kadhaa. Na moja wapo huwa ni benk kuu za hizo nchi.

- mnacho pigie kelele sikioni mara o tutakuwa kama zimbabwe mara matrafiki,

- wakuu ni kwamba bot wamejalibu kuiba hii aidia kutoka mataifa mengine ambayo yameisha wahi kuadhimisha miaka yao ya uhuru.

- Mf
ano philipine wakati wanaadhimisha miaka yao nazani ilikuwa 50 au 75 nimesahau kidogo, wao benki kuu yao ilitengeneza not yenye ukubwa wa yale mabango ya barabarani, na hiyo ilitumika kwa siku hiyo pekee yake baada ya hiyo siku kupita, ilibidi waliozipokea wazipeleke benk kuu.
Na si philipine pikee, kuna nchi nyingi zimewahi kutoa pesa ya ajabu maalumu kwa ajili ya kusherekea kitu fulani

turudu huku kwetu, hiyo koin, inaweza kuwa imetengenezwa maalumu kwa ajili ya kutumika siku hiyo tu. Yaani ukibahatika kuipata utaweza nunua bidhaa dukani lakini baada ya siku hiyo walio zipokea watalazimika kwenda kuzichenji benk ili wapewe pesa za kawaida.

na huwa hazitengenezwi nyingi na ni wachache hubahatika kuzitumia, na wanatengeneza kidogo kwa sababu, zitakuwepo kwenye mzunguko kwa siku moja tu. Hao wachache wano bahatika kuzitumia ndo huwakilisha hao walio kosa. Unaweza kuta zitatolewa jumla kuu yake zikawa na thamani ya milioni hata 20. Na zinaweza sambazwa kila wilaya labda koin kadhaa ili wilaya zote zipate watu wakuzitumia kwa siku hiyo.

Ili iweje?
 
Fursa hii ya kuinunua fedha hiyo na kujiongezea fedha inawezekana kwa Watanzania kiasi gani, kama si wajanja wachache?
Unainadi sherehe kuwa ni Miaka 50 ya uhuru wa Tz bara, lakini unafanya mambo ya kuwanufaisha wenye fedha ili waongeze akiba zao!...cant easily figure out and finally buy this!

Hizi ni kwa ma "collectors" au "hobby" hii huitwa "numismatic" na si kwa kila mtu na ndo maana hizo huwa "limited" na sarafu kama hizi huwa haziingizwi kwenye mzunguko wa fedha.

Tatizo laki ni ilmu na ilmu haipatikani kwenye kuta nne tu.

Hata wenye fedha wengi huwa hawazinunui hizi kwa sababu si "hobby" yao, na si sarafu tu hutolewa stempu, tshirts, khanga, vitenge, "key chains" na vitu vingi vinavyoweza kukumbusha baadae "occasion" hiyo. Na hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kutoa sarafu za "commemoration" (kumbukumbu). Funguka kidogo.
 
Back
Top Bottom