BOT yadai "Hatujalipa Mabilioni Kisiasa!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Kama kuna Jamhuri inayojua kufuja fedha na rasilimali bila kutumia akili ama kwa makusudi, ni jamhuri ya Tanzania.

Serikali iliona ulazima kutumia fedha nyingi kiasi hiki eti kutoa fidia bila uhakiki au uthibitisho. Kila kitu kilifanywa kwa hisia na kufuata mkumbo.

Maswali nililouliza wakati hii Stimuli ilipoanzishwa nayauliza tena na nyongeza! Zaidi ni kuonyesha wazi kuwa kama tuliweza chapisha fedha eti kunusuru ajira za watu 42000 wa sekta binafsi, lakini leo hii tunakataa kuongea kima cha chini tukidai hatuna fedha ni upunguani wa hali ya juu.

Maswali yangu kwa Ndulu na Rais wake Kikwete ni haya:
  1. Fidia hizi zilitolewa kama misaada, mikopo au sadaka? Je ni masharti gani yaliambatanishwa na fidia hizi?
  2. Kama fidia ilikuwa ni msaada wa kugawia mtu fedha kama sadaka, je ni uthibitisho gani kuwa makampuni haya yalipata hasara kwa ajili ya mtikisiko wa mwaka mmoja? Je miaka mingine waliyopata faida ya ziada hawakuwa na limbikizo la mtaji na faida la kutosha ili kumudu kupungua kwa mapato?
  3. Je makampuni haya, yamekuwa yakiliingizia Taifa mapato ya kiasi gani na kodi wanayoilipa ni kiasi gani?
  4. Je fedha hizi za misaada zitaonekana vipi katika mizania (balance sheet) ya makampuni haya na je zitakatwa kodi?
  5. Kwa nini Serikali ilipotenga fungu hili, halikuliweka kama mikopo na kuweka ulazima wa kulipwa na kuhakikiwa kwa fidia hii itakayoonyesha makampuni haya yakitumia hizo fedha kuongeza uzalishaji?
  6. Kwa nini Serikali haikutumia fedha hizi kuboresha miundo mbinu au kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza bidhaa kamili (process industry) ili kupunguza tabia ya Tanzania kupoteza thamani ya mazao yake kwa kwenda kwa madalali? Mfano kama Pamba inalimwa Mwanza, na mkulima anaiuza kwa Ushirika nao unapelekwa kwenye jineri kwa uchambuzi kisha kupeleka nyuzi ulaya, kwa nin Serikali haikutumia nafasi hii kuimarisha uchambuzi wa Pamba kutoka utengenezaji wa nyuzi na pamba iliyochambuliwa na kuwa vitambaa na nguo kamili ili kuongezea Taifa pato na hata kuongeza ajira?
Naomba wasaidizi wa Ndulu na Kikwete mtoke mekoni na mje kujibu maswali yangu!

Kama mtadai eti hata Marekani walitoa Stimuli, nitawapasha hivi, Stimuli ya Marekani haikugawiwa kama peremende, ilikuwa ni mikopo kwa Mabenki ambayo yaliwekewa masharti magumu na muda maalumu wa kurudisha mtaji(mkopo), na serikali ikapunguza kodi za mapato kwa wananchi wake wenye mishahara na kipato fulani na mwisho Serikali ikatumia fedha hizo hizo kwa kuamsha shughuli za uzalishaji mali kwa kutenga fungu maalumu lililolipia gharama za uzalishaji mali huo ambao ni nje ya bajeti ya kawaida ya matumizi!

BoT: Hatujalipa mabilioni kisiasa Send to a friend Monday, 10 May 2010 17:25
Na Ramadhan Semtawa
BENKI Kuu (BoT) imechukizwa na taarifa kuwa Sh1.7 trilioni zilizotengwa kwa ajili ya kunusuru zimegawiwa kwa malengo ya kisiasa na kufafanua kuwa asilimia 80 ya fedha hizo zimetumika kuziba pengo la makusanyo ya mapato.
Tayari kumekuwa na taarifa zinazotaja wamiliki wa baadhi ya makampuni, hasa ya pamba, kuwa wamejipatia fedha nyingi kutoka kwenye tengo hilo na wanajipanga kuzitumia katika shughuli za kisiasa, huku uchaguzi mkuu ukizidi kukaribia.
Lakini Gavana Ndulu jana alilazimika kuzungumzia tena suala hilo akisema kuwa madai hayo ni ya upotoshaji.
Kwa mujibu wa Profesa Ndulu, asilimia kubwa ya fedha hizo hazikuwa kwa makampuni bali kuziba pengo la mapato ambalo lilitokana na kuanguka kwa makusanyo yaliyotokana na mtikisiko wa uchumi wa dunia.
"Asilimia 80 ya hizi fedha ni kwa ajili ya kuziba pengo la mapato ambalo lilijitokeza baada ya mtikisiko wa uchumi, sasa kusema kuna watu wamelipwa mabilioni kisiasa bila kustahili ni uongo," alifafanua gavana Ndulu.
Alisema makampuni yaliyolipwa yalifanyiwa tathimini ya kina kutokana na athari walizopata kuthibitisha kama zilitokana kweli na mtikisiko wa kiuchumi wa dunia.
"Kila tulichofanya kilikwenda hatua kwa hatua, sasa kusema kuna fedha zimelipwa kisiasa kwa makampuni ambayo hayakustahili hizo taarifa sijui zina ukweli upi, ripoti zetu tumekabidhi kwa kamati za Bunge," alisisitiza.
Gavana Ndulu aliweka bayana kwamba BoT imejiridhisha kwa kila hatua kwani mchakato mzima umekuwa ukifanyika kitalaamu kwa kuhusisha watu mbalimbali wenye uwezo.
Mkuu huyo wa taasisi kuu ya fedha ya nchi ambaye aliongoza Kikosi Kazi cha kuangalia athari za mtikisiko huo, alisema kiasi hicho cha asilimia 80 kilitumika kuziba mapengo ya fedha ikiwemo za kigeni kutokana na kuzorota sekta za utalii.
Aliongeza kwamba mazao mengine ya ndani kama karafuu, pamba na chai yalichambuliwa kwa makini kubaini nani alistahili kupata nini na kwa sababu zipi hasa.
Akiongea na gazeti dada la Mwananchi la The Citizen mwishoni mwa mwaka jana, Gavana Ndulu alisema kuwa fedha hizo hazikutengwa kwa ajili ya makampuni wala mabenki na kwamba serikali ilitenga kiasi cha Sh825 bilioni kwa ajili ya kuziba mapengo katika makusanyo ya fedha na kwamba kwa wakati huo ni Sh600 bilioni tu zilizokuwa zimegawiwa kwa serikali.
Katika siku za karibuni kumeibuka taarifa mbalimbali ambazo zinaeleza baadhi ya wanasiasa walitumia ujanja kujipatia kiasi kikubwa cha fedha wasichostahili ambazo sasa wanazitumia kwa kampeni za chini kwa chini katika nafasi za ubunge.
Baadhi ya wakuu wa makampuni (majina tunayo) waliopo kanda ya ziwa wanatajwa kunufaika na mpango huo na sasa wanajiandaa kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali hasa ubunge.
Mwaka jana serikali ilitangaza kutumia sh 1.7 trilioni kwa ajili ya kunusuru nchi na mtikisiko wa uchumi ambao tayari mawimbi yake yalisababisha watu 42,000 kupoteza ajira, kupungua fedha na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI).
 
PDidy,

TUlikuwa na fedha za kutosha kuiboresha mfumo a Reli ili usafirishaji uendelee bila matatizo. Tulikuwa na fedha za kutosha kuboresha mfumo wa umeme na maji ili uzalishaji uendelee na Serikali iwe na uhakika wa mapato.

Lakini pesa tumewapa Maandazi Tour Company na Changudoa Motel kisa eti watalii kutoka Ugagagigikoko walishindwa kupanda ungo!

Viwanda kila siku vinashidwa kufanya kazi kutokana na ukosefu wa umeme na maji na wanashindwa kusafirisha bidhaa kisa TRL mataruma yamepata pancha lakini hatuoni umuhimu wa kuwekeza kwenye miundo mbinu itakayo hakikisha kuna uzalishaji mali!
 
Tshs. 1.7 TRILLION kunusuru uchumi zinatoka serikalini, Tshs 1.5 BILLION kunusuru reli zinaombwa kwa Gaddafi.....walahiiiiiii tumelogwa
 
Back
Top Bottom