BoT Saga Unfolding: Meghji says I was duped by governor Ballali

Hili suala haliwezi likamgusa Balali pekee yake, kuna kitu kikubwa kimejificha hapa na Namshauri JK katika ile timu ya IGP, AG na CAG aliyoiunda kufuatilia ufisadi huu aweke pia watu huru kama viongozi wa dini na muipuaji wa scandal hii Dr Slaa ndipo tutakuwa na Imani otherwise tunahisi kuna vitu vinataka kufichwa hapa maana hii kitu inagusa watu wazito na matumbo yao na ndio wafadhili wakuu wa CCM na wanaojitokeza kuchangia harambee zinazosimamiwa na Mh.JK kwa kumwaga mamilioni.

This is terrible, Tume huru iundwe indelee pale alipoishia Ernest& Young
Kweli kabisa, nakuunga mkono kwa hili, mbona kwenye madini kambandika Zitto, na hapa amweke Slaa, au...

Je hujuwi system ni nini?
 
So tangia kipindi hicho kwanini alichelewa kuchukua hatua za kum fire Balali wakati alishuhudia kabisa kuwa alidanganywa? Hapa Balali atatupiwa kila kitu. Wana JF bado tuna kazi nzito. Alichoongeza Bi Meghji ni upuuzi mtupu na hakupaswa kuongea upuuzi huu mbele ya jamii yetu ya wasomi.
Hii inadhihirisha kwamba KIAPO CHA WAHESHIMIWA MAWAZIRI HUWA NI MAANDALIZI YA KUHUJUMU UCHUMI WA NCHI "Wanasema... Sitatoa siri za Baraza la Mawaziri....." SIRI IPI HIYO? Kuna uwazi hapo? Huyu Zakia ni kigeu geu sana wa kauli zake. Huko Bungeni walikuwa wakimpinga Dr Slaa wakati akijua yale yanayosemwa na Dr Slaa ni ya kweli huo sio unafiki??? Hatufai JK angeanza na huyo huyo maana hakuwa makini katika kitengo chake.
 
Bubu bwana na wewe kujua kusema tuu unaogopa kusema yote?
Huyu mama siyo kigeu geu tuu ni kwamba sasa hivi anatapa tapa. Anajaribu kumtwika mzigo wote Balali ili yeye aonekane yuko clean. Si unajua mfa maji haachi kutapa tapa? Mwaacheni aendelee kutapa tapa tutazidi kujua mengi.

Huyu mama 100% naamini alijua ni fedha za nini na ndio maana alisign hii kusema alidanganywa ni yeye anataka kudanganya watanzania bado sijashawishika kabisa kama kweli yeye alisign tuu bila kujua.
 
Yaani huyu mama kwa kiburi alichonacho bado anaendelea kutufanya mazezeta...masikini wadanganyika!!
 
Mwaka wa shetani kweli kwa sisiemu.
Mbona Mramba tulishamlalamikia siku nyingi sana?
Huyu alikuwa mchafu tangu akiwa mkuu wa mkoa wa Mbeya miaka ya hiyo! Nashangaa wengine ndio mnamuona leo kwamba kachafuka kwa ufisadi.
 
Yaani kutokana na short story iliyo andikwa kwenye Nipashe, i can connect dots and ask for Zakia resignation soon. Meghji kama waziri mkuu ana kila haki ya kuuliza na kuchunguza kabla ajatia saini kwenye document yoyote.

Kwanza yeye Zakia na office yake walifanya uchunguzi wa aina gani kuhusu KAGODA and national security? What is the corelation between those two? If Zakia believed that there was a scum inside BoT why didn't she rise a red flag? Kwa nini alisubiri mpaka Dr Slaa kuleta habari public? Hata baada ya Slaa kuja public kwa nini alikuwa akipanga kwamba tuhuma ni uzushi?

Unajua hapa CCM wanataka kucheza kiini macho, kwamba sababu Balali hayupo then kila kosa akandamizwe nalo yeye.Yeye kama Zakia alifanya nini kuchunguza hilo? Mimi nadhani huyu mama anatakiwa kuwa amejiuzuru tangu JK alipotoa speech yake.

Sababu za kujiuzuru ni chache tuu, Poor leadership skills and luck of communication with in her organization. What i believe is, she shows luckiness and poor judgement, and that disqualify her to run as a leader in that particular sector.

Go back kwenye maandamano, i have questions kwa wote hawa wanaotaka andamana. kwanza what did JK accomplished concern this particular issue at this moment? Balali resign prior to all this YOUR FIRED scum, nothing has been solved yet. `No case has been filed to this moment, no one is at the justice hand and Balali is steel runing loose. Now tell me, where does this chear leaders got the strength to wine that JK is the winner. We all loosers here, Balali disappered, we don't know who own Kagoda and defenetly who owned other 20 companies. Who need to stand on the trial court and face the justice?

While this people are acting nuts, neither of them questioned Lowassa (JK home boy and allie). He once said Balali is clean, now can he eat is words? What does he stand now compare to then? So can we call him flip flopper? How about miss judgemental scunky? Or you need PhD like Dr Slaa to figure out inside BoT there is big and fat stealing activities going on?

To JK, when will the report go public? How much does the building real cost? How about BMW and Yona with Kiwira Mining? How about other alligations that went public 2007 summer, when are we going to get answers? What you told us is 5% of the story we want the other 95%.
 
Unampa pongezi Juha mkuu ?
Unajua we are missing a point hapa .CCM wanawapiga bao watanzania kwa kuwa wamefa jua very serious issues wanazipeleka ki shabiki.So wakiingia mtaani mtaanza kulumbana na magazeti yao yataandika sana then issue inakufa .Nasema Hongera sana sana JF .nasema ukweli kama si michango ya wana JF kumsaidia Lowasa na kuja na data hapa nakwambia wangaliweza kuandamana .Lakini sasa majuha wachache wanaanza kupatwa na akili.
 
Hivi Meghji kuwa ni mtu wa Mkoa upi na kwa nini hajawahi kuomba kura za wana jimbo ila anapewa kwa kuteuliwa Ubunge wa Bure na kila akipewa Ubunge wa bure bado uwaziri hakosi ? Amekuwa maliasili na Utalii naamini uozo huko utakuwa mkubwa zaidi.She give hazina ili kuficha ukweli wa kujichotea pesa kwa ajili ya Kampeni . Nakubaliana na Phillimon kwa asilimia kubwa .Balali hajaiba .
Huyu mama kwa habari za mitaani, sijui zina ukweli kiasi gani, nadhani ametoka kusini mashariki ya tanzania, kama si Rufiji ni Kilwa au Mtwara na akaolewa zanzibar, sasa sijui alihamia zanzibar kabla au baada ya kuolewa
 
siri imefichuka. kumbe kuna hela waziri anasaini tu bila kujiridhisha kwa sababu ni kwa ajili ya masuala nyeti ya usalama wa taifa? Haulizi hata kwa mkubwa wake wa kazi?

Kwa hiyo deep green, et al ndio imetoka hiyo...waziri mzima unadanganywa kama mtoto?

ndio maana kumbe hata maliasili alipokuwepo huyu mama palikuwa na rushwa za kutisha namna hiyo.

Ama kweli ndege mjanja....huyu mama kwisha kazi. nadhani alifikiri hizo hela zilikuwa zinakwenda kwa rostam> alipogundua sivyo akaandika barua kwa wakaguzi, kama ni kweli. ama kweli za wezi ni arobaini. tutawasikia wengi mwaka huu.

Yaani huyu mama kwa kiburi alichonacho bado anaendelea kutufanya mazezeta...masikini wadanganyika!!

All of the above contributions prove her dishonesty,incompitence,crookedness,and to crown it all, ARROGANCE
 
Nimesoma hii habari ya huyu mama Thisday na mpaka machozi yamenitoka.

Please Mr. President, sack her as quick as possible. She is lying, she is incompetent, and she participated in stealing our money. She should be ashamed of herself. She should go now!

I am gobsmacked by her revelation, no way, she should go now!
 
Chama Cha Majuha(CCM), hivi walitaka kupongezana nini badala ya kuwapongeza wale waliowaita waongo na maadui wa taifa kwa kuweka ufisadi huu hadharani? Unafiki mtupu. Hongera Kikwete kwa kuwabaini wanafiki.

Asha
Hiki chama sasa kinazidisha vioja,Wameshasahau kabisa jinsi walivyo ongozwa na kile kibabu(Kingunge) kuwashambulia Dr Slaa na mashujaa wenzake kuwa wanasema uongo.
Sasa leo JK kafanya yale waliyomtaka afanye, CCM wanampongeza kwa maandamano.Hii ni aibu,aibu,aibu.
 
Waungwana nakumbuka kuna tetesi zilivuma kipindi cha nyuma kuwa mmiliki wa KAGODA ni Rostam Aziz na huyu jamaa ana uhusiano wa karibu/ndani sana na huyu mama. Naona kama ni sahihi basi huu mchezo mchafu wa kujichotea 40b atakuwa anaufahamu na alihusika moja kwa moja na asisingizie kudanganywa na Balali. Awajibishwe hata kama alidanganywa kwani kukubali kudanganywa ni uzembe mkubwa pia.
 
Tanzania!, Tanzania!

1. Maneno haya ya Balalli kwa Zakhia(kama ni kweli) yameweka wazi kwamba fedha ziliolewa kwa 'matumizi nyeti ya serikali'- na kwa kuwa Balalli aliyesema akiwa kifua mbele- inaashiria kwamba kuna fungu lilikuwa kwa 'matumizi nyeti ya serikali ya wakati huo'(soma: kwa ajili ya Mkapa na wenzake kugharamia uchaguzi uliomwingiza Kikwete madarakani) lakini pia hapo hapo Baadhi ya wale waliomo kwenye "Orodha ya Mafisadi" wakatumia mwanya huo kujichotea fedha kwa ajili ya 'matumbo' yao binafsi. Hivyo, Balalli ataje waliomtuma- na aliowakabidhi! Sijui kwanini waziri wa fedha wa wakati huo na Katibu Mkuu wake wasichukuliwe hatua kabla hata ya Gavana wa Fedha bwana Balalli? Sijui kwa nini katika mazingira haya bado tunaendelea kuambiwa Mzee Mkapa aachwe apumzike!

2. Bi Zakhia Meghji anapaswa kujiuzulu mara moja- mtu akikudanganya, ukiwa na uwezo wa kujua kudanganywa huko, lakini ukakubali kudanganyika- wewe ni sehemu ya uongo huo- ama kwa kuwa mmoja wa waongo hao au kwa ujinga wa kuukubali uongo huo!. Waziri wa Fedha ni cheo kikubwa sana, unapokubali Gavana wa Fedha akwambie matumizi haya ni SIRI ya serikali, wewe kama mtunza siri ukashindwa kuhoji ni siri gani hiyo; wewe hujui kazi yako! Upaswa kujiuzulu mara moja. Kuna uwezekano mkubwa Bi Zakhia Meghji anaendelea kuwadanganya watanzania; inawezekana kabisa Balalli alimwambia wazi ni matumizi gani hayo nyeti yaliyofanywa na awamu iliyopita ndio maana akakubali kuisaini ile barua. Sasa kwa kuwa Balalli anaelekea 'kunyongwa' ni lazima Bi Zakhia na wengine wamkane mara tatu kabla jogoo halijawika.

Wasichojua Bi Zakhia na Wenzake ni kwamba watu wachache wanaweza kudanganyika kwa muda mchache lakini si watu wote wakati wote. Kazi kwako Rais Kikwete, kijua ndio hiki- usipouanika, utautwanga mbichi.

Natoweka

JJ

Kwanza mimi ndiye niliichokoza hii mada katika ile thread ya "Balali kafara" nilianza kwa kusema leo kutakua na jambo na baadaye nikalisema jambo lenyewe, kwa hiyo najua kwa undani mno jambo hili.

Kwanza tuwe wa kweli na turudi nyuma na kuangalia kumbukumbu. Hii vita ya mafisadi ni ngumu sana na kwamba inashirikisha watu wengi upande wa kupigana na upande wa mafisadi. Hebu tujiulize Meghji yuko upande gani? na anapambana na kina nani?

Kwa taarifa yenu ni kwamba kwa muda mrefu sana (karibu miaka miwili) Meghji hana mahusiano mazuri na RA na EL. Sababu hasa ya ugomvi wao haijawekwa wazi lakini Kagoda ni moja ya sababu.

Tutakumbuka kwamba Meghji alitoa tangazo katika gazeti la Daily News kuhusu kuagiza special audit kwa akaunti ya EPA pale BoT. uamuzi huo ulitokana na kukerwa na jinsi Ballali alivyokubali kusukumwa na EL na RA kumuingiza mkenge kwa barua hiyo kudai kwamba hizo fedha zimekwenda katika masuala ya ulinzi na usalama. Kwa bahati kumbe mafisadi hawakua wamewasiliana na Mgonja (maana ni mwenzao pia)kwa kua alikua nje ya nchi na waliamini biashara imekwisha baada ya Meghji kusaini hiyo barua. jambo lililowashangaza ni pale Mgonja alipokuja akaulizwa kama kawaida tu kuhusu hayo malipo na kwa kuwa alikua Katibu Mkuu chini ya Mramba, alisema Kagoda haina uhusiano na mambo ya serikali na akamwambia Meghji ni nani wanahusika na Kagoda. Siku tatu tu baada ya barua ya kwanza kuwasilishwa kwa wakaguzi, Meghji akaandika barua ya kuifuta ile ya mwanzo na pia kwa kuwasiliana tena na Ballali ambaye alikubali pia kusukumwa na watu, akiwamo Mkapa.

Baada ya Meghji kuwasiliana na JK, aliandaa barua hiyo na kuiwasisha kwa wakaguzi na hapohapo kufanya mawasiliano na vyombo vya kimataifa na kupata baraka zote. Hatua hiyo ya KIJASIRI ndio iliyomjengea uadui mkubwa na RA na EL na kwa kweli amini musiamini hawa watu hawaivi kabisa.

Hebu tujiulize, waandishi wa habari wakati ule walikua wakiandika BoT kwa angle ya twin tower, Mwananchi Gold, Import Support na Credit Guarantee Scheme waliyopewa Kagera Sugar, kashfa ambazo Mkapa alihusika nazo zote.

Baadaye ndipo Dr Slaa, June, 2007 akapata data za uhakika na kuzimwaga hadharani na ndipo mambo yakawa moto. Kwa wanaomjua Meghji alikiri mara kadhaa kuwapo kwa tatizo japo alisisitiza kwamba watu wasubiri uchunguzi, ambao ndio sasa JK ameutumia kuanza kuwashughulikia watu japo bado kuna vigogo zaidi ya 30 ambao wametajwa kwa majina katika ripoti hiyo.

pamoja na itikadi zetu za kisiasa na mengineyo, TUSIKUBALI KAMWE KUTUMIKA na kina RA na EL
 
Hivi kwanini wahusika wote ambao wanajulikana wasikamatwe, badala ya kuangalia Meghji? Kwa mfano Meghji akijizulu nani atakua Waziri wa fedha? Wanasema Karamagi ndiye anafaa kuwa Waziri wa Fedha, au Abdalah Kigoda mwenye taaluma ya uhasibu ili kuweka mtu ambaye si mtandao na hasa wakihofia Karamagi kuchafuliwa na Buzwagi. Atakapokuja Waziri mwingine kazi itakua imekwisha? je, wahusika wataendelea kupeta kama anavyopeta Manji na mapesa ya import support? kama wanavyopeta kina Supperdol na bilioni 65 za BoT (guaranteed by GOV)?
 
Waungwana,

Mimi naona hapa JF tuende hatua moja zaidi, kwa jumla tuandike barua kwenye magazeti yote muhimu na kuomba Meghji awe sacked mara moja.

Tusiishie kusema hapa lazima tuongeze pressure. JF ni kubwa na inawakilisha Watanzania wengi sana tena wasomi. Lets act together for the betterment of our motherland.

Waandishi wa maana kama akina Mwanakijiji wanaweza kutusaidia kuandika lakini ili iwe na nguvu inabidi isambazwe kama imetumwa na JF na tutume copies kila sehemu, hasa huko wanakoshinda wakiomba pesa kama omba omba huku wanaiba pesa hizo hizo bila hata aibu.

Wakati umefika wa kuanza kuwafunga kengere ili kila mtu awaone na kuwasikia kwamba ni mafisadi hasa.
 
Kwanza mimi ndiye niliichokoza hii mada katika ile thread ya "Balali kafara" nilianza kwa kusema leo kutakua na jambo na baadaye nikalisema jambo lenyewe, kwa hiyo najua kwa undani mno jambo hili.

Kwanza tuwe wa kweli na turudi nyuma na kuangalia kumbukumbu. Hii vita ya mafisadi ni ngumu sana na kwamba inashirikisha watu wengi upande wa kupigana na upande wa mafisadi. Hebu tujiulize Meghji yuko upande gani? na anapambana na kina nani?

Kwa taarifa yenu ni kwamba kwa muda mrefu sana (karibu miaka miwili) Meghji hana mahusiano mazuri na RA na EL. Sababu hasa ya ugomvi wao haijawekwa wazi lakini Kagoda ni moja ya sababu.
Tutakumbuka kwamba Meghji alitoa tangazo katika gazeti la Daily News kuhusu kuagiza special audit kwa akaunti ya EPA pale BoT. uamuzi huo ulitokana na kukerwa na jinsi Ballali alivyokubali kusukumwa na EL na RA kumuingiza mkenge kwa barua hiyo kudai kwamba hizo fedha zimekwenda katika masuala ya ulinzi na usalama. Kwa bahati kumbe mafisadi hawakua wamewasiliana na Mgonja (maana ni mwenzao pia)kwa kua alikua nje ya nchi na waliamini biashara imekwisha baada ya Meghji kusaini hiyo barua. jambo lililowashangaza ni pale Mgonja alipokuja akaulizwa kama kawaida tu kuhusu hayo malipo na kwa kuwa alikua Katibu Mkuu chini ya Mramba, alisema Kagoda haina uhusiano na mambo ya serikali na akamwambia Meghji ni nani wanahusika na Kagoda. Siku tatu tu baada ya barua ya kwanza kuwasilishwa kwa wakaguzi, Meghji akaandika barua ya kuifuta ile ya mwanzo na pia kwa kuwasiliana tena na Ballali ambaye alikubali pia kusukumwa na watu, akiwamo Mkapa.

Baada ya Meghji kuwasiliana na JK, aliandaa barua hiyo na kuiwasisha kwa wakaguzi na hapohapo kufanya mawasiliano na vyombo vya kimataifa na kupata baraka zote. Hatua hiyo ya KIJASIRI ndio iliyomjengea uadui mkubwa na RA na EL na kwa kweli amini musiamini hawa watu hawaivi kabisa.
Hebu tujiulize, waandishi wa habari wakati ule walikua wakiandika BoT kwa angle ya twin tower, Mwananchi Gold, Import Support na Credit Guarantee Scheme waliyopewa Kagera Sugar, kashfa ambazo Mkapa alihusika nazo zote.

Baadaye ndipo Dr Slaa, June, 2007 akapata data za uhakika na kuzimwaga hadharani na ndipo mambo yakawa moto. Kwa wanaomjua Meghji alikiri mara kadhaa kuwapo kwa tatizo japo alisisitiza kwamba watu wasubiri uchunguzi, ambao ndio sasa JK ameutumia kuanza kuwashughulikia watu japo bado kuna vigogo zaidi ya 30 ambao wametajwa kwa majina katika ripoti hiyo.

pamoja na itikadi zetu za kisiasa na mengineyo, TUSIKUBALI KAMWE KUTUMIKA na kina RA na EL

Sasa aliyetumika hapa si yeye ZM au ni nani? Suala la yeye kununiana na kina RA na EL kwangu mimi ali hold water! Aliweka sahihi fedha zetu zikaliwa...period! SHE WAS SUPPOSED TO BE MORE CAREFUL!
Inawezekana alianza kwa ujasiri lakini hakukimaliza kwa ujasiri bali kwa woga.
ALL IN ALL SHE IS RESPONSIBLE WHETHER ALIKATIWA MSHIKO AU LA!
 
Mkuu Halisi,

Hata kama kila ulichoandika ni kweli bado huyu mama kaingusha nchi yake, katusaliti wananchi wake, kaiingizia nchi yake hasara kubwa.

Alijua toka mwanzo kabisa na wala kulikuwa hakuna hata sababu ya kuwaita wakaguzi wa nje.

Inatakiwa tuanzie kwenye kichwa chake, baada ya hapo ndio awataje wote waliomfikisha hapo alipo.

Sitatoa hata chozi moja akiwa sacked, in fact ninaomba awe sacked hata dakika hii.

Serikali ikiendelea kuwakumbatia watu kama, wasije wakalamika watu wakichukua madaraka mikononi mwao na kuanza kuwashughulikia hawa watu. Hawana tofauti na vibaka wanaochomwa moto barabarani.

Lazima tuwe tayari kulinda mali zetu. Huyu mama inabidi aende, I don't care who will be a finance minister. Ukimweka hata chekea atafaa kuliko hawa majambazi.

Nchi ina wasomi wengi tu wanaoweza kufanya hizo kazi, watu ambao wako tayari kuheshimu imani kubwa wanayopewa na wananchi na sio kuanza kuiabuse.

Sina imani ya hata asilimia moja na huyu mama, inabidi aende na maji!
 
Naounga mkono wale wote waliosema kwamba ni lazima Meghji akubali responsibility. Cha kushangaza ni kwamba bado kaachwa kuwa waziri. Mimi niliongea na diplomats mwaka 2006 February nasikia mkutano wake wa kwanza na wafadhili didn't go down well, maana mama alikuwa gizani kabisaa. Lugha aliyotumia ilikuwa ni ya kitoto na alionekana wazi kuwa hakuwa competent. Nikaulizwa na hawa diplomats kwa nini JK ambaye waliamini alikuwa very competent amemweka. Nikawaambia wazi that hii ni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanamtandao watakula vizuri maana yule mama zaidi ya kula nao, pia ni zero, kwa hiyo watachota sana. Madiplomat wote wakanianglia kama sina akili nzuri wakacheka wakijua it's a joke! Kumbe!
 
Mtanzania,

Kama aliyoyaandika Halisi yana ukweli (na kutokana na jinsi ninavyomfahamu Halisi nina uhakika yana ukweli kwa 100%)! Sioni kama kumtosa Meghji peke yake litakuwa ni suluhisho la ujambazi wa fedha za umma. Tatizo haswa liko kwa watu 2, EL na RA. Je, JK yuko tayari kuwatosa hao jamaa? Kama akiwatosa basi mimi nitafanya sherehe kubwa sana na kuanzia hapo ninawahakikishia wana JF kwamba hakuna mtu atamchekea JK hasa ikizingatiwa role ya EL na RA kwenye swala zima la JK kuwa mkuu wa kaya.

Kama Meghji akitoswa peke yake kwa kosa la kudanganywa pasipo kufanya uchunguzi, na akina EL na RA wakabaki, basi mchezo wa kuchota utadumu katika miaka yote 10 ya utawala wa JK. Hivi JK hajiamini kwamba alichaguliwa na wananchi? Kwanini anawaogopa au anawakumbatia hao mafisadi wawili ambao tangu aingie madarakani wamekuwa wakimsababishia utawala wake kuonekana wa kisanii?

Mzee Halisi - Hii issue sasa ninaiona kwamba iko complicated na ni ngumu sana na hasa BWM anapoonekana kuwa na mkono kwenye hizi deals za BoT. JK alishasema BWM asiguswe, kwa mwendo huo JK hataweza kuondoa shina la ufisadi Tanzania, bali atakuwa anaondoa vile vitawi vidogo na yale makubwa anayaacha yakichanua.
 
Back
Top Bottom