BoT Saga Unfolding: Ballali ni Kafara

Mr Mikael

Hilo swala la Watanzania(waafrika) wakiwa na watu weupe hasa ulaya na Marekani hua wanafanya vizuri mnoo mie bado najiuliza hua nini haswa ? lakini huyo huyo ukimchanganya nyumbani ndiyo mborongaji mzuri

Hii si ki elimu tu hata ukianglia mpira wa mguu waafrika wanapochezea timu zao za ulaya wakichanganyikana na wazungu hua wanacheza vizuri mnoo lakini hao hao wakija kwenye timu yao ya taifa unaona kiwango kipo chini mnoooooo.

Mie hua wakati mwingine nafikiri wenda waafrika hua tunakitu kidogo tuna kimiss tunapokua wenyewe na ikitokea ukachanganyikana na mzugu hiyo weekness wenda mzungu hua ana i overcome na tunafanya vizuri.

Now you are talking,
Ni kweli kabisa watu wengi wa Afrika hasa watanzania, ukiwaweka na watu wanaofuata taratibu za kazi, na wanaofuata maadili ya kazi huwa wanafanya kazi vizuri sana. Na wanasifiwa kwa kuwa innovative, creative na hard working. Lakini sababu hakuna sababu ya kujiuliza kwanini wakiwa Tanzania hawasaidii.
Kwa sababu kwanza sytem yetu hapa imejaa uswahili, ubabashaji, ufisadi, uvivu, majungu na uozo mwingi. Hata ukimleta leo mweupe, wa njano, wa bluu, mwekundu au mweusi kutoka sehemu nyingine yoyote,ili afanikiwe itabidi aingie na afit kwenye system ya uozo. This is how things work here.
Kwa mnaofanya kazi serikali mnajua ninachosema, know how will take you know where in Tanzania. Know who, fitna na ushirikina ndio msingi wa mafanikio(binafsi), Tanzania hakuna kitu kinachoitwa maslahi ya taifa au maslahi ya umma, neno hilo linatumika kwa jili ya kulinda maslahi ya watu fulani. That is straight and simple.
Ukiangalia issue ya BOT utajiuliza why the hell nifanye kazi kwa bidii wakati pesa wanakula wengine kiulaini, kwa hiyo mwenye akili timamu inabidi na wewe uingie kwenye system hiyo ili uwe sehemu yao!
 
...hata mjaribu spin kiasi gani huyu ni fisadi tuu na anastahili kushtakiwa maana yeye ndio alikuwa mkuu wa BOT ambapo wizi ulitokea,hana huruma kabisa huyu kuibia au kuachia wizi mkubwa kiasi kile kwa nchi maskini kama yetu,na wala hatuhitaji story yake kuwataja mafisadi wenzake maana tukimpeleka mahakamani atawataja tuu na nina uhakika report original inajua ni kina nani wezi,hatuwezi kumaliza kesi kwa kumtegemea Balali apone na wala sio factor kwenye hii prosecution kama kweli itakuja maana naye ni mwizi tuu,kama kapewa sumu pole lakini isiwe tabu
 
Wale kina Lukaza nao wametajwa na ukiangalia ni kweli pesa walipozitoa ghafla hazijulikani na sijui kwanini bado wako mtaani,tungeanza nao na kama prosecution ni nzuri wangesema uchafu wote,lakini kama mnavyojua tumejaza vilaza na wasio na maadili msitegemee chochote hapo na hii kesi imekwisha ndio maana nasema muungwana is one of the worst na ni mswahili tuu wa kulinda mafisadi
 
...hata mjaribu spin kiasi gani huyu ni fisadi tuu na anastahili kushtakiwa maana yeye ndio alikuwa mkuu wa BOT ambapo wizi ulitokea,hana huruma kabisa huyu kuibia au kuachia wizi mkubwa kiasi kile kwa nchi maskini kama yetu,na wala hatuhitaji story yake kuwataja mafisadi wenzake maana tukimpeleka mahakamani atawataja tuu na nina uhakika report original inajua ni kina nani wezi,hatuwezi kumaliza kesi kwa kumtegemea Balali apone na wala sio factor kwenye hii prosecution kama kweli itakuja maana naye ni mwizi tuu,kama kapewa sumu pole lakini isiwe tabu

Koba,

Mkuu umesema kweli kweli hapa, spinning imekuwa kubwa. Ballali ni fisadi sawa na hao wengine tu na hakuna cha sumu wala nini. Kama anaumwa ni magonjwa mengine, hili la sumu ni kujaribu kutuhamisha kutoka kwenye ufisadi kwenda kwenye conspiracy theories.

Ballali is in a big hole, he should stop digging it further, and he needs to come clean ASAP.

Tutamwamini Ballali aliyejaribu hata kuita waandishi wa habari na kusema watu wanawaonea wivu huku anajua fika wamechota pesa? Unahitaji data gani toka kwa mtu kama huyo?
 
Mimi nadhani hakuna anayebisha kwamba Balali ni fisadi, hii ni kweli na haina mjadala. Lakini kutolewa kafara ina maana viongozi waliamua lawama zote zimwangukie, wakati nao walihusika. Sasa yeye kaona kama nazama naenda na wengine. Ndiyo maana mimi naona hii stori ya sumu inawezekana (it is not that far fetched) lakini ni vitu viwili tofauti. Hii ya sumu hata ikiwa kweli haiondoi ukweli kuwa Balali ni fisadi na ni lazima arudi kujibu mashtaka na arudishe mali alizochukua la sivyo afilisiwe!
 
Hakuna cha sumu wala nini huyu ni fisadi tu na hao wenzie soon wata surface... waswahili wanasema "ushirika wa wanga haudumu"
 
Hakuna cha sumu wala nini huyu ni fisadi tu na hao wenzie soon wata surface... waswahili wanasema "ushirika wa wanga haudumu"
 
Mtanzania,
Kuna sababu halali kwa Balali kukaa kimya. Kufikia wiki ya kwanza ya Desemba alikuwa hawezi kuzungumza. Hata wakati RO amekwenda kumwona alikuwa bado ni mtu wa kugeuzwa kitandani. It is just a few weeks now that he's talking and the first priority is to get his health back. That is why in my previous threads nimesema tuendelee kumwombea kwa Mwenyezi Mungu. He needs the prayers and he needs to get his energy back. Baada ya hapo, who knows?
 
Jasusi,

Nimekuelewa mkuu na sitaandika tena juu ya Ballali mpaka baada ya ukweli zaidi kufahamika.
 
Quote: Halisi
Ballali atabebeshwa kila balaa ... kuanzia kesho tutasikia mengi
Keil
kesho kuna nini mkuu?

Utasikia kwamba Ballali ndiye alipotosha kila jambo
 
Quote: Jasusi
Mtanzania,
Kuna sababu halali kwa Balali kukaa kimya. Kufikia wiki ya kwanza ya Desemba alikuwa hawezi kuzungumza. Hata wakati RO amekwenda kumwona alikuwa bado ni mtu wa kugeuzwa kitandani. It is just a few weeks now that he's talking and the first priority is to get his health back. That is why in my previous threads nimesema tuendelee kumwombea kwa Mwenyezi Mungu. He needs the prayers and he needs to get his energy back. Baada ya hapo, who knows?

Ni habari njema kwa wote wenye ubinadamu. Ndio maana Waislamu wanafahamu hadithi ya Mtume Muhamad (SAW) kumtembelea adui yake mkubwa alipokua mgonjwa. maadili ya kibinadamu katika dini na mila zote ni kuheshimu wagonjwa na walioaga dunia. Ni kwa MASLAHI ya Taifa kwa Ballali kuwa mzima na kumwaga UKWELI hadharani bila woga maana dunia sasa imebadilika hakuna jambo la kuogopa, kwani kama wangetaka yaishe wangekubali kujiuzulu kwake na kama wana kesi wangeendelea nayo na si kujifanya hawajui kama ni mgonjwa
 
Tatizo lilopo tanzania na afrika wa ujumla ni kwamba,wasomi hawatumiki na kama wakitumika wanatumika kwa maslahi ya kisiasa. Watu kama Balali na profile zao,walipokuja bot walikuwa na malengo mazuri tu na wenye nia ya dhati na nchi yao,tatizo linakuja pale ambapo yuleyule aliyekuteua na chama chake wanataka kushinda uchaguzi na ndio wanakuwa wa kwanza kukushawishi uwape hela kinyume na taratibu,watafanya hivyo mara mbili tatu,baadaye na yeye na yeye anaona bullshit potelea kokote wacha kila mtu afe na zake, wenzetu wanasema you are eating and we are eating too. Dawa ni kutenganisha siasa na utendaji/utaalamu
 
Wandugu mimi nina wazo. Hivi hatuwezi kufikisha hii issue kwenye media za kimataifa kama BBC, CNN, FOX, SKY ili waweze kufuatilia hiki kilio cha watanzania??? Hawa jamaa wanaweza kumtrace alipo na kufanya mahojiano naye huyu dalali!! Tumechoka sasa, kila siku tunapiga kelele tu hapa, kila mtu na lake. Tunataka tusikie haya majambo kupitia media za kimataifa. Mwenye uwezo wa ku-influence hili atusaidie. Tutaendelea kubaki gizani mpaka lini???
 
Misumari ya kumgongelea Balali kwenye msalaba wa Ufisadi inazidi kuchongwa.. siyo tu atawambwa kama wale vyura wa somo la biolojia kwenye karatasi, Balali atakuwa ndiyo shetani mwenye mapembe wa ufisadi nchini.. Wakati wanamgongelea misumari hiyo mashetani yenyewe yatakuwa yamekaa pembeni na kushangilia!
 
mie kusema kweli namsapoti aliyetoa wazo la international medias zitumike japo tupate kuona ka mahojiano ka balali na medias tujue zipi mbivu na zipi mbichi...
alipatikana osama akafanyiwa mahojiano ndio sembuse balali??
 
Huo ni udikteta sasa! Sina haja ya kuwa na data zaidi ya nilizosema,na sijakataa kitu.Nani hapa alikuja na death certificate inyoonyesha cause of death ku proove their point? Hizi ndio data,kama za yule mrusi wa Polonium.

Hata mimi naweza kuzua tu kuwa mjomba wangu alilogwa na shemeji yake,sasa hio utiita ni data kwa sababu aliye kufa ni mjomba wangu na mimi ndio niliyosema?
Huwezi kumwambia mtu akae pembeni simply because u do not agree with what he says,what i sed is my opinion,si sikutegemea kuwa kila mtu atakubalina na mimi,na ndio maana tunakuwa na mijadala,na wengi tumejifunza mambo mengi sana humu.Mimi nimetoa mifano ya watu wote 'waliouawa' sikusema mtu yeyote ni muongo.Kama hii ni JF na wewe una data,basi lete death certificate zinazoonyesha sababu za vifo hivyo,hizo ndio dataz! Zilizobaki ni speculations tu ambazo 90% ya watu humu wanatoa,and theres nothing wrong with that.
Lakini hii biashara ya kupigana mikwara eti mtu akae pembeni kama hana dataz ni mambo ya kizamani,na pia ita deter watu ambao maybe they have something to say,lakini wanajua kuna watu kama wewe watawaambia wakae pembeni.
This is a free society,if what i say is crap to u then treat it like so,lakini i'm sure kuna mwingine ataona sio crap..or rather dont read whatever that has been posted by Zanaki,lakini ujue pia kuwa i have the same rights in here as u do
....mimi na wewe ni members tu,none of us owns this forum.

You have my full support on this one!
 
Misumari ya kumgongelea Balali kwenye msalaba wa Ufisadi inazidi kuchongwa.. siyo tu atawambwa kama wale vyura wa somo la biolojia kwenye karatasi, Balali atakuwa ndiyo shetani mwenye mapembe wa ufisadi nchini.. Wakati wanamgongelea misumari hiyo mashetani yenyewe yatakuwa yamekaa pembeni na kushangilia!
__________________

Hivi kwanini hatuko kama wenzetu wa Kenya na mataifa mengine duniani? Hivi hakuna Watanzania Wazalendo ndani ya BoT, CRDB, NBC, Exim Bank, Stanbic, Standard Chartered ambao watatusaidia kuweka wazi mbali ya makampuni 22 yaliyoorodheshwa na IKULU watuambia ni kina nani waliochukua fedha kutoka benki zao? Kwa kuanzia kwa wale waliopo CRDB Holand, walioko NBC Samora watupe data za Kagoda na makampuni mengine yaliyochota fedha za EPA na nyinginezo
 
Back
Top Bottom