BoT na Ushindi wa kishindo wa JK: Mambo hadharani

Mwiba,
mbona unajichoresha hivyo,jua kwanza taratibu za kibenk zinavyofanya kazi au kama hujui basi uliza iliuelekezwe.hapa ni sehemu ya kuelimishana na kufundishana pia.mwisho tafuta mwalimu wa kukufundisha kuandika.
 
duh.. sikugundua hiyo aliyopost shorty ni kucopy toka nakala ya pdf ambayo niliitengeneza na tayari imeshapostiwa hapa.
 
ubadhilifu huo wahusiana vipi na ushindi wa kishindo wa JK?? ni kweli kuna hujuma nyingi dhidi ya uchumi wa Inji hii umefanyika kipindi cha awamu iliyopita. ni vizuri tukazungumzia kwa uyakinifu kuliko kupeleka pasipohusika "misplacing attention of the matter".

Hivi huyo JK ni kipi cha ajabu sana alichofanya????? kwamba Balali kaiba BOT mlitaka keshoye akamatwe aswekwe ndani??
Bulyamhulu wanaiba dhahabu, usiku uleule afunge mgodi???
RA mwizi, palepale avunje urafiki, amfukuze ccm,wanainji igunga wamnyang'anye ubunge. Kaiba wapi,lini! hamna jibu, ooh tajiri, muirani, kanunua flana na kofia ccm! achaa! acheni utoto!!

Hivi tukiwa na rais kama huyo, akaamka asubuhi akasema funga JF tutampongeza??? mbona ndio staili ya rais tumtakaye???

Rais si kila kitu ktk innji, kuna taasisi na mifumo ya utendaji kiutawala.

ooh! samahani nimetoka nje ya mada, KWELI WATU WAMEIBA ILA NI KUJIDANGANYA KUSEMA ETI ZIMECHANGIA USHINDI WA KISHINDO WA JK, mnyonge mnyongeni hakiye mpeni!! JK alipendwa na wapiga kura wengi, kama atavurunda, ni swala jingine,

WAKATABAHU

Kuna watu sijui wanakula nini kabla ya kulog in hapa na kuanza kuandika! yaani Bokasa imebidi tu nianze kucheka jinsi mishipa ilivyokutoka kujaribu kutetea huu ufisadi ambao uko wazi kabisa
 
WaBongo sasa wanaweza kukodiwa kuandika habari feki,zote nimezisoma kuhusu hii mada na zinaonekana ni copy and paste from origino,sasa kule kwenye sahihi ndio kindende maana wameogopa kuziiga ,ikiwa kutazuka patashika watajwa wanaweza kuzikana kwamba hazitokani na ridhaa yao tofauti na ile ya mkataba sahihi zilikuwepo.

Ndio maana wakati mwingine sishangai kuwa kuna watu walifukuzwa kanisani kwa kusema kuwa dunia iko duara na sio flat. Huyu mwiba hana tofauti kabisa na waliokuwa tayari kufa ili tafsiri ya dunia iendelee kubaki flat.

Kama haya mambo ni kweli basi toeni ronyo za hundi zilizotumika,sio minamba na kuwazuga wananchi ,unajua upinzani utafanya kazi kweli kweli kuwasilimisha watu ili kukiasi chama cha mapinduzi kwani dau hili wanalotaka kuvukia linaonekana hakuna kitakachokuwa zaidi ya proper ganda ,wakati ndizi zimekwisha kuliwa halafu unawakuwa watu wa vijijini huko wao ndio waumini halisi wa CCM ,ibada yao ni ile ile ya CCM ndio baba na CCM ndio Mama huna lugha ya kuwasimulia wakakufuata.

Wewe unataka nani akufanyie home work kisha wewe usome. Hizi pesa ni zako pia hivyo nawewe unaweza kufanya utafiti kujua hili sio kusubiri kila kitu ufanyiwe.

Na huu muungano wa Upinzani ni unafiki mtupu ,unaokwenda na wakati hawa hawa si ndio waliwawekea pingamizi wabunge sijui wawakilishi wa CUF kule Pemba .sasa hapa si kuna uzinguaji tu.

Oh hoooo,

kumbe issue hapa ni chuki zako dhidi ya upinzani na wala sio wizi wa mabilioni ya pesa za watanzania wakati mama na watoto wakifa vijijini kwa magonjwa yanayotibika!
 
Kuna watu sijui wanakula nini kabla ya kulog in hapa na kuanza kuandika! yaani Bokasa imebidi tu nianze kucheka jinsi mishipa ilivyokutoka kujaribu kutetea huu ufisadi ambao uko wazi kabisa

Mwafrika wa Kike issue si ufisadi!!! soma vizuri post yangu!! Huwa nakereka sana MTU KUTUMIA UONGO KUELEZA UKWELI, MBAYA ZAIDI UKWELI WENYEWE UKIHUSU KITU NYETI!!! kwenye issue siriaz tutumie ukweli, kueleza kweli ili tupate ukweli. ni hivyo tu mupenzi!!!
 
Mwafrika wa Kike issue si ufisadi!!! soma vizuri post yangu!! Huwa nakereka sana MTU KUTUMIA UONGO KUELEZA UKWELI, MBAYA ZAIDI UKWELI WENYEWE UKIHUSU KITU NYETI!!! kwenye issue siriaz tutumie ukweli, kueleza kweli ili tupate ukweli. ni hivyo tu mupenzi!!!

Nimesoma tena na sijaona kitu hata kimoja ulichosema kuwa ni cha uongo! unaonaje kama ukisema kuwa check namba fulani, au account fulani ya benki hapo ni ya uongo?
 
Mfrk wa kike

Hivi wamtumikia nani?

Inji au chama?

Toa kwanza mifano ya kipi ni cha uongo kwenye report, check, account number, majina ya makampuni, au the whole thing?

kisha ndio upate jibu kuwa pesa zinazoibiwa hapa sio za chadema wala tlp bali za watanzania wootee!
 
Mwafrika wa K! sina hakika kama tatizo huna uwezo wa kuelewa au hutaki kuelewa, kwa mbali napata hisia kuwa la pili ni sahihi zaidi.

Hoja niliyopost haitofautiani sana na ya mkandara ambayo pia ulipinga! hata nilipokuomba upitie tena post yangu hukuelewa!!

Zingatia hili "ISSUE SI KUWA HAKUNA UFISADI, nilichosema ni kuwa TUWE MAKINI KUELEZEA WALIOTENDA UFISADI NA WALIOFAIDIKA! Kukurupuka kuwa pesa zimetumika ktk kampeni ya JK twaweza kupelekwa kusiko!! kwa mtazamo dhaifu waweza kujiona u-mkereketwa wa inji hii ila ukweli ni kuwa unapindisha ukweli na pengine ni nyezo ya kuficha ufisadi halisi! Yawezekana wahusika mojakwamoja au umepandikizwa fikra hizo na hivyo watumika bila kujua.

Mkandara aliuliza, ufisadi ulifanyika kipindi cha BWM vipi tukimbilie kumkaba koo JK?? tena yajulikana kuwa JK hakuwa chaguo la BWM. Ielewweke vizuri hapa kuwa hoja yangu haitoi uwezekano wa kuwa JK nae alishiriki ktk ufusadi huo lakini pia yawezekana mafisadi waliokuwa sehemu ya mamlaka ya utawala uliopita walijichotea pesa hizo ili waondoke wakiwa fresh! Isitoshe kampeni za uchaguzi zilianza kipindi cha mchakato wa kutafuta mgombea wa CCM ambapo watu zaidi ya 10 wengi kama si wote wakiwa ktk nafasi kubwa serikalini.

Mwafrika wa kike! twendeni kwa ufasaha ktk jambo hili nyeti! ufisadi uliotokea BoT ni mkubwa na una madhira makubwa sana ktk Taifa hili masikini!! TUJARIBU KUWEKA KWELI KTK UKWELI TUJUE KWELI TUPARE HERI.

Bado naamini kukimbilia kwenye majibu (ambayo hayana uyakini) ni mbinu za mafisadi au vibaraka wao kuficha majibu ya kweli!!!
 
Je yawezekana kuwa pesa hizo ziliishia mikononi mwa wajanja wachache na walitumia heka heka za uchaguzi kama distraction? Maana mwanamingaombwe mahiri lazima awe na distraction anapofanya ile grand illusion...
 
Back
Top Bottom