Boss anataka kunitenganisha na mke wangu

Jamani niko mbioni kutafuta mke mwingine baadaya shemeji yenu kukataliwa na boss wake kuja kuja kuishi na mimi.
Ni takribani miaka miwili sasa tangu nifunge ndoa takatifu na shemeji/wifi yenu,lakini kulingana na mazingira ya kazi nimekuwa nikiishi mbali na mke wangu na tunakutana mara moja moja kama wanafunzi na shemeji/wifi yenu.Hii yeto inatokana na ukiritimba pamoja na urasimu ninaofanyiwa na boss huyu, ambaye ni Afisa Elimu katika Wilaya ya Bahi.Angekuwa mwanaume ningesema anamtaka mke wangu,bahati nzuri ni mwanamke.

Hata hivyo nashindwa kuelewa mama huyu ana mpango gani na maisha ya ndoa yangu,eti anadai hawezi kumpa uhamisha hadi wilaya yake itakapo kuwa na walimu wa kutosha! kwa hakika bado wapo viongozi wasio tambua wala kuamini kuwa Dunia huzunguka Jua

Naomba ushauri na muongozo wa kisheria kwenu kuhusu vigezo vya mtumishi kuhama kumfuata mwenza wake.

kuna vitu viwili mbele ya shemeji yetu, naomba umfikishie maswali haya ninayokuuliza. jibu atakalokupa ndio litakalokufanya uamue ndoa ivunjike au la.
1. kati ya kazi na ndoa kwake muhimu nini?- hapa jibu kama ni kazi basi mwulize swali hili la pili. lakini kama jibu lake kuwa ndoa ni muhimu basi aandike barua ya kuacha kazi
2. yupo tayari kuacha kazi ili aje atafute kazi ya ualimu hapo ulipo wewe?
 
jamani niko mbioni kutafuta mke mwingine baadaya shemeji yenu kukataliwa na boss wake kuja kuja kuishi na mimi.
ni takribani miaka miwili sasa tangu nifunge ndoa takatifu na shemeji/wifi yenu,lakini kulingana na mazingira ya kazi nimekuwa nikiishi mbali na mke wangu na tunakutana mara moja moja kama wanafunzi na shemeji/wifi yenu.hii yeto inatokana na ukiritimba pamoja na urasimu ninaofanyiwa na boss huyu, ambaye ni afisa elimu katika wilaya ya bahi.angekuwa mwanaume ningesema anamtaka mke wangu,bahati nzuri ni mwanamke.

Hata hivyo nashindwa kuelewa mama huyu ana mpango gani na maisha ya ndoa yangu,eti anadai hawezi kumpa uhamisha hadi wilaya yake itakapo kuwa na walimu wa kutosha! Kwa hakika bado wapo viongozi wasio tambua wala kuamini kuwa dunia huzunguka jua

naomba ushauri na muongozo wa kisheria kwenu kuhusu vigezo vya mtumishi kuhama kumfuata mwenza wake.

mwambie hiviiii...! Kama anategemea na anasubiria eti kuna siku walimu watatosha katika wilaya yake basi atakuwa ni mvivu wa kufikiri, maana hata ulaya na marekani bado wanalia na upungufu wa walimu sembuse wilaya ya bahi...!

Hakuna siku walimu watatosha hapo bahi, singida wala tanzania hii, aache urasimu na ukiritimba wa kizamani huyo, aache uvivu wa kufikiri....!
 
Mwambie mkeo aandike barua kwa katibu mkuu wizara ya elimu aambatanishe na barua ambazo aliwahi kuandika huyo afisa elimu akabana kisha ahoji afisa elimu anampango gn na ndoa yake hasa kipindi hichi cha majanga kama ukimwi,yaani kwa issue km hiyo hakuna majadiliano ni kupewa tu uamisho sema maafisa elimu na wakuu wa shule huwa wananyanyasa walimu wasiyojua,yeye mwambie ampandie wizarani.
 
Mkuu endeleeni tu kutumia hekima na busara ili amhamishe mkeo. Nijuavyo hakuna sheria inayomlazimisha amuhamishe. Kinachofanyikaga ni privilege tu but not your right
 
Mbona kama tayari unachakufanya...KUOA MKE MWINGINE! Hahahaaa umenichekesha. Ni kama unakijisababu cha kuamua kuoa. Cha mno jitahidi upate mwalimu wa kubadilishana naye. Hapo mzizi wa fitna utaisha. Huwa wanaweka hadi matangazo kwenye mbao za matangazo ili hilo lifanyike. Hope you'll succeed!
 
Mkuu umenipandisha mzuka,sasa nitamfuata gia mpya.asante sana
 
Mwaka uliopita miezi kama hii niliomba ushauri kaama huu hapa jukwaani.Michango na ushauri wa watu ulifanya by Novemba ya mwaka huohuo nipate uhamisho wa kuwa jirani na familia yangu...... Mnaomshauri aende Wizara ya elimu mnampotosha siku hizi Walimu wote wa Msingi na Sekondari mambo yao yanashughulikwa na TAMISEMI, Vyuo vya Ualimu na Ukaguzi ndio wanashughulikiwa na MOEVT. Mkuu hengo achana na DEO (Afisa Elimu) tafuta kwanza nafasi unakotaka ahamie ukipata mshauri aandike barua kwa Katibu Mkuu TAMISEMI akiambatanisha na barua ya nafasi aliyopata halafu aende kwa Mkurugenzi wa Bahi amweleze uhalisia na viambatanisho muhimu ni vyeti vya ndoa, kitambulisho cha kazi (chako kama ushahidi wa eneo unalofanyia kazi) na barua yako ya ajira. Uhamisho wa Walimu hufanyika mara mbili kwa mwaka (June na Desemba) na bila shaka atapata tu. Ukiwa na swali zaidi ni PM nikuongezee maarifa zaidi
 
Last edited by a moderator:
Jamani niko mbioni kutafuta mke mwingine baadaya shemeji yenu kukataliwa na boss wake kuja kuja kuishi na mimi.
Ni takribani miaka miwili sasa tangu nifunge ndoa takatifu na shemeji/wifi yenu,lakini kulingana na mazingira ya kazi nimekuwa nikiishi mbali na mke wangu na tunakutana mara moja moja kama wanafunzi na shemeji/wifi yenu.Hii yeto inatokana na ukiritimba pamoja na urasimu ninaofanyiwa na boss huyu, ambaye ni Afisa Elimu katika Wilaya ya Bahi.Angekuwa mwanaume ningesema anamtaka mke wangu,bahati nzuri ni mwanamke.

Hata hivyo nashindwa kuelewa mama huyu ana mpango gani na maisha ya ndoa yangu,eti anadai hawezi kumpa uhamisha hadi wilaya yake itakapo kuwa na walimu wa kutosha! kwa hakika bado wapo viongozi wasio tambua wala kuamini kuwa Dunia huzunguka Jua

Naomba ushauri na muongozo wa kisheria kwenu kuhusu vigezo vya mtumishi kuhama kumfuata mwenza wake.

NI wakati wa haki sawa sasa! Hivyo mwanamke hawezi kumtaka mkeo?
 
pole sana kaka,
ila kwa utaratibu wa sasa, ndoa sio kigezo cha kuhamishwa. hamna sheria utakayoegamia. kama wadau walivyoshauri; uombe huo uhamisho kwa hekima maana ni favour, wewe uhame umfuate au mmoja wenu aache kazi kumfuata mwenzie.au atafute mtu wa kubadilishana nae
 
Wasiliana na sekta husika but vp huyo mwanamke mnavyokutana ..mnaelewa kama mwanzo au amebadilika usije ukamhukumu bila kosa baadaye ukaja kujuta chunguza kwanza ujue kweli kabla ya kufanya maamuzi hayo.
 
Mwaka uliopita miezi kama hii niliomba ushauri kaama huu hapa jukwaani.Michango na ushauri wa watu ulifanya by Novemba ya mwaka huohuo nipate uhamisho wa kuwa jirani na familia yangu...... Mnaomshauri aende Wizara ya elimu mnampotosha siku hizi Walimu wote wa Msingi na Sekondari mambo yao yanashughulikwa na TAMISEMI, Vyuo vya Ualimu na Ukaguzi ndio wanashughulikiwa na MOEVT. Mkuu
hengo achana na DEO (Afisa Elimu) tafuta kwanza nafasi unakotaka ahamie ukipata mshauri aandike barua kwa Katibu Mkuu TAMISEMI akiambatanisha na barua ya nafasi aliyopata halafu aende kwa Mkurugenzi wa Bahi amweleze uhalisia na viambatanisho muhimu ni vyeti vya ndoa, kitambulisho cha kazi (chako kama ushahidi wa eneo unalofanyia kazi) na barua yako ya ajira. Uhamisho wa Walimu hufanyika mara mbili kwa mwaka (June na Desemba) na bila shaka atapata tu. Ukiwa na swali zaidi ni PM nikuongezee maarifa zaidi
Mkuu ushauri wako unaendele kuzaa matunda Gerrad ushauri wa ko unaendele kuzaa matunda, niko kwenye hatua za mwisho kisha nisubiri Desemba - Januari kwa utekelezaji.Napenda kukushukuru sana kwa mara nyingine kwa ushauri na kunitia moyo.Naomba tuendelee kuhabarishana.Ni kweli information is power
 
Jamani niko mbioni kutafuta mke mwingine baadaya shemeji yenu kukataliwa na boss wake kuja kuja kuishi na mimi.
Ni takribani miaka miwili sasa tangu nifunge ndoa takatifu na shemeji/wifi yenu,lakini kulingana na mazingira ya kazi nimekuwa nikiishi mbali na mke wangu na tunakutana mara moja moja kama wanafunzi na shemeji/wifi yenu.Hii yeto inatokana na ukiritimba pamoja na urasimu ninaofanyiwa na boss huyu, ambaye ni Afisa Elimu katika Wilaya ya Bahi.Angekuwa mwanaume ningesema anamtaka mke wangu,bahati nzuri ni mwanamke.

Hata hivyo nashindwa kuelewa mama huyu ana mpango gani na maisha ya ndoa yangu,eti anadai hawezi kumpa uhamisha hadi wilaya yake itakapo kuwa na walimu wa kutosha! kwa hakika bado wapo viongozi wasio tambua wala kuamini kuwa Dunia huzunguka Jua

Naomba ushauri na muongozo wa kisheria kwenu kuhusu vigezo vya mtumishi kuhama kumfuata mwenza wake.
hengo tatizo lako litaisha pale utakapotambua kuwa serikali siyo mwajiri pekee kwa sasa. Shule za binafsi ziko nyingi, mishahara sehemu nyingine inazidi hiyo ya serikalini kama mkeo anathamini ndoa yake si aomba kazi shule za binafsi. Huenda mkeo alihitaji tuu cheti kwamba ameolewa lakini moyoni mwake haumo na maisha yanaendelea bila uwepo wako karibu naye
 
Last edited by a moderator:
Napata wasiwasi kujua au kuamini kama kweli unampenda mkeo, maneno yako kama yanaashiria tayari una kimada au anasubiria jibu...Kiushauri sio rahisi sana hao watu kukubali kutoa uhamisho kwani wilaya kama Bahi wengi wanapangiwa wanaingia mitini ndio maana aliajiriwa analindwa na mabosi wake....Cha kufanya jaribu kufanya UTANZANIA uongee vizuri na huyo mama kwani wengi wamefanikiwa kwa kudumisha huo Utanzania, ila ukiendelea kulalamika hope miaka michache ijayo utarudi jamvini kuomba ushauri na namna ya kuachana na vimada ili urudiane ma mkeo kama kweli unampenda.....All the best
 
Mkuu ushauri wako unaendele kuzaa matunda Gerrad ushauri wa ko unaendele kuzaa matunda, niko kwenye hatua za mwisho kisha nisubiri Desemba - Januari kwa utekelezaji.Napenda kukushukuru sana kwa mara nyingine kwa ushauri na kunitia moyo.Naomba tuendelee kuhabarishana.Ni kweli information is power
Nimefurahi sana kusikia habari hizi. Napokea shukrani zako lakini nakupongeza pia kwa kutokata tamaa na kufuata ushauri. Sisi ni binadamu hapa duniani tunapita tu. Hakuna gharama yoyote kumshauri binadamu mwenzio na akafanikiwa badala yake unabarikiwa zaidi na zaidi. Nakuombea sana Mkuu ili shetani asiingilie kwenye hatua hizi za mwisho na wale jamaa wa TAMISEMI amini usiamini hawana tatizo kama umeweka attachments zote na umepata nafasi. Kila la heri Mkuu hengo
 
Last edited by a moderator:
hengo tatizo lako litaisha pale utakapotambua kuwa serikali siyo mwajiri pekee kwa sasa. Shule za binafsi ziko nyingi, mishahara sehemu nyingine inazidi hiyo ya serikalini kama mkeo anathamini ndoa yake si aomba kazi shule za binafsi. Huenda mkeo alihitaji tuu cheti kwamba ameolewa lakini moyoni mwake haumo na maisha yanaendelea bila uwepo wako karibu naye
Kama Mkewe ni Mwalimu wa Msingi, ziko shule ngapi za Private za msingi hapa Tanzania? Kwa Mwanamke ni vyema apiganie abaki serikalini ili apate pia muda wa kulea watoto, huko private awaachie wanaume
 
Back
Top Bottom