Boss anataka kunitenganisha na mke wangu

hengo

JF-Expert Member
Jun 6, 2011
402
50
Jamani niko mbioni kutafuta mke mwingine baadaya shemeji yenu kukataliwa na boss wake kuja kuja kuishi na mimi.
Ni takribani miaka miwili sasa tangu nifunge ndoa takatifu na shemeji/wifi yenu,lakini kulingana na mazingira ya kazi nimekuwa nikiishi mbali na mke wangu na tunakutana mara moja moja kama wanafunzi na shemeji/wifi yenu.Hii yeto inatokana na ukiritimba pamoja na urasimu ninaofanyiwa na boss huyu, ambaye ni Afisa Elimu katika Wilaya ya Bahi.Angekuwa mwanaume ningesema anamtaka mke wangu,bahati nzuri ni mwanamke.

Hata hivyo nashindwa kuelewa mama huyu ana mpango gani na maisha ya ndoa yangu,eti anadai hawezi kumpa uhamisha hadi wilaya yake itakapo kuwa na walimu wa kutosha! kwa hakika bado wapo viongozi wasio tambua wala kuamini kuwa Dunia huzunguka Jua

Naomba ushauri na muongozo wa kisheria kwenu kuhusu vigezo vya mtumishi kuhama kumfuata mwenza wake.
 
kaka sikufichi hili swala la uhamisho kwa waalim hasa kwenda kwenye majiji ni gumu sana hata kama umeoa au kuolewa. mkeo kafanya kzi muda wa mika miwili anasubiri nini huko bahi? mwambie atafute chuo aapply kisha aende masomoni mkoa uliopo.

istoshe nenda katafuti kitabu cha taratibu na sheria za umma ukisome kisha ukomae na kudai haki yako ya mkeo kufanya kazi mkoa na hata wilaya uliyopo. ukihofu tu imekula kwako.
 
kama unajiweza changeni aende chuo....
la atafute shule za private inayolipa vizuri...
au tafuta connection wizarani ulobby ahame....
au la aache afungue biashara aachane na ualimu....
 
Ongea na Afisa Elimu katika wilaya uliyopo kama kuna nafasi ambayo mke wako anaweza kuja kujaza au kama kuna mwalimu ambaye wanaweza kubadilishana. Ukishakuwa na uhakika huo mke wako aombe moja kwa moja TAMISEMI uhamisho. Huyo Afisa Elimu anayebana atapewa amri na taarifa ya uhamisho, hatakuwa mfanya maamuzi.
 
Zamani ili mwalimu apate uhamisho kirahisi walikuwa wanafoji vyeti vya ndoa.....wanavipeleka wilayani uhamisho unafanyika faster!! sasa wewe una ndoa halali unazubaa nini?? nenda kwa REO, kama DEO anakuzengua!!
 
duuuu! labda ukamuone yule muheshimiwa mbunge wa Bahi,,,lakini ujipange kabla ya kumuona si unajua anapenda nini
 
Jamani niko mbioni kutafuta mke mwingine baadaya shemeji yenu kukataliwa na boss wake kuja kuja kuishi na mimi.
Ni takribani miaka miwili sasa tangu nifunge ndoa takatifu na shemeji/wifi yenu,lakini kulingana na mazingira ya kazi nimekuwa nikiishi mbali na mke wangu na tunakutana mara moja moja kama wanafunzi na shemeji/wifi yenu.Hii yeto inatokana na ukiritimba pamoja na urasimu ninaofanyiwa na boss huyu, ambaye ni Afisa Elimu katika Wilaya ya Bahi.Angekuwa mwanaume ningesema anamtaka mke wangu,bahati nzuri ni mwanamke.

Hata hivyo nashindwa kuelewa mama huyu ana mpango gani na maisha ya ndoa yangu,eti anadai hawezi kumpa uhamisha hadi wilaya yake itakapo kuwa na walimu wa kutosha! kwa hakika bado wapo viongozi wasio tambua wala kuamini kuwa Dunia huzunguka Jua

Naomba ushauri na muongozo wa kisheria kwenu kuhusu vigezo vya mtumishi kuhama kumfuata mwenza wake.

Hapo penye nyekundu sijapaelewa kabisa, yaani unatafuta mwanamke mwingine wa kuoa kisa mkeo halali wa ndoa kanyimwa uhamisho? Au unatafuta uhalali wa kuwa na wake wawili? Huyo utakayemuoa tena akipata uhamisho utaoa tena?? Na hata ukimapata mwingine anayefanya kazi na wewe na then wewe mwenyewe ukapewa uhamisho, huko uendako utaoa tena??

Kwanini usifikirie kumtafutia ajira nyingine maeneo ya wewe unakoishi badala ya kufikiria kuoa tena? Kwa nini usimtafutie hata kazi za kujiajiri mwenyewe ili awe karibu yako na kuacha kunyanyaswa na mabosi?
Siamini na sintaamini kabisa kuwa kuoa mke mwingine kunaweza kuwa suluhu ya tatizo lako, acha kabisa!
 
Ndo maana watu wengine wana matatizo yasiyoisha.Lakini kwanini unataka kuoa badala ya kufight?Kwanza nina hasira ngoja kwanza nije!
 
Jamani niko mbioni kutafuta mke mwingine baadaya shemeji yenu kukataliwa na boss wake kuja kuja kuishi na mimi.
Ni takribani miaka miwili sasa tangu nifunge ndoa takatifu na shemeji/wifi yenu,lakini kulingana na mazingira ya kazi nimekuwa nikiishi mbali na mke wangu na tunakutana mara moja moja kama wanafunzi na shemeji/wifi yenu.Hii yeto inatokana na ukiritimba pamoja na urasimu ninaofanyiwa na boss huyu, ambaye ni Afisa Elimu katika Wilaya ya Bahi.Angekuwa mwanaume ningesema anamtaka mke wangu,bahati nzuri ni mwanamke.

Hata hivyo nashindwa kuelewa mama huyu ana mpango gani na maisha ya ndoa yangu,eti anadai hawezi kumpa uhamisha hadi wilaya yake itakapo kuwa na walimu wa kutosha! kwa hakika bado wapo viongozi wasio tambua wala kuamini kuwa Dunia huzunguka Jua

Naomba ushauri na muongozo wa kisheria kwenu kuhusu vigezo vya mtumishi kuhama kumfuata mwenza wake.

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaa kama enzi ukitoka bweni
 
[[I]Jamani niko mbioni kutafuta mke mwingine baadaya shemeji yenu kukataliwa na boss wake kuja kuja kuishi na mimi.
Ni takribani miaka miwili sasa tangu nifunge ndoa takatifu na shemeji/wifi yenu,lakini kulingana na mazingira ya kazi nimekuwa nikiishi mbali na mke wangu na tunakutana mara moja moja kama wanafunzi na shemeji/wifi yenu.Hii yeto inatokana na ukiritimba pamoja na urasimu ninaofanyiwa na boss huyu, ambaye ni Afisa Elimu katika Wilaya ya Bahi.Angekuwa mwanaume ningesema anamtaka mke wangu,bahati nzuri ni mwanamke.

Hata hivyo nashindwa kuelewa mama huyu ana mpango gani na maisha ya ndoa yangu,eti anadai hawezi kumpa uhamisha hadi wilaya yake itakapo kuwa na walimu wa kutosha! kwa hakika bado wapo viongozi wasio tambua wala kuamini kuwa Dunia huzunguka Jua

Naomba ushauri na muongozo wa kisheria kwenu kuhusu vigezo vya mtumishi kuhama kumfuata mwenza wake.[/
I]]
Unachelewesha kupata watoto, hama wewe na wewe ni mwenza wake sheria haipendekezi wanawake tu ndiyo wawafuate waume zao, hata wewe waweza kumfuata pia.
Ila pima hali ya hewa isije kwenda kwako kukakuletea matatizo zaidi maishani mwako :A S 465::A S 465::eek2::eek2:
 
Hengo kuwa makini sana wewe, eti angekuwa mwanaume huyo afisa elimu ndio ungekuwa na wasi wasi. Unaonaje nikikuambia kuwa mimi nimeongea na huyo afisa elimu akuambie hivyo ili my wife wangu wako asiamishwe na mimi Ndukidi niendelee kufaidi, ukitilia maanani ni kama mke wangu kwani tangu uoe hujakaa nae hata zaidi ya miezi miwili!!
Sasa kwakuwa mimi ninakukubali wewe ndugu yangu, nakushauri uchukue hatua!!!:yawn::yawn::yawn:
 
kama mkeo angeona hiki ulichoandika?upo matatani mkuu,siamini kama unamaanisha hivyo..lob atahama tu kaka,pesa ndio kila kitu sasa.
 
Back
Top Bottom