Bosi wa mashuhushu wanaomlinda Obama alivyojiuzulu ni darasa kwa Idara yetu ya Usalama wa Taifa

Atupe Mfano wa nchi ambako secret service huitwa bungeni na kuhojiwa!,unaweza kuhoji kuhusu secret service wakati si moja wao??
 
Ameshaorodhesha Marekani hapo juu,wao wanamwita kwenye baraza la Seneti.
 
Naendelea kushangazwa Na yanotukia Tanzania, tembo wanakufa, twiga wanapanda ndege, epa, Richmond, escrow, mabehewa, makontena nk, hadi haya yote yanatukia hii taasisi ilikuwa likizo?? Au vipi
 
Idara ya usalama wa taifa wa tz ndio imara na shupavu na namba moja kwa Africa ikifuatiwa na SA.

Kuhusu kuhoji utendaj kazi wa idara hii me nadhani ni uendawazimu, Tiss ipo imara na Salama nchini ya mkurugenz wake Mh Othman na vijana wake.

Wakati mwingine tusijifanye much know kwa mambo msioyajua.
 
Idara imara ni ile iliyojengwa katika misisngi ya kukosolewa.
Idara ya usalama wa taifa wa tz ndio imara na shupavu na namba moja kwa Africa ikifuatiwa na SA.

Kuhusu kuhoji utendaj kazi wa idara hii me nadhani ni uendawazimu, Tiss ipo imara na Salama nchini ya mkurugenz wake Mh Othman na vijana wake.

Wakati mwingine tusijifanye much know kwa mambo msioyajua.
 
Bado mtoa Mada haja nishawishi kuona kuwa TISS inahitaji marekebisho ya kimfumo na ili kidhibitisha kuwa idara yetu iko imara angalia matukio ya RAIS wetu, kama ingelikuwa imelala sidhani kama angepata fursa ya kutumbua haya majipu.
 
Kama mtu mwenye uelewa kiasi kuhusu utendaji kazi wa Idara yetu ya Usalama wa Taifa, nimekuwa 'nikipiga kelele' mara kwa mara kuhusu haja ya mageuzi ndani ya taasisi hiyo nyeti. Kwa bahati mbaya sio tu kelele hizo ni vigumu kueleweka kwa Watanzania wengi, uwezekano wa kusikilizwa ni mdogo hasa ikizingatiwa kuwa asili ya taasisi hiyo ni kutekeleza majukumu yake kwa siri, na kama hiyo haitoshi, mara nyingi wahusika wa taaluma hiyo inayopaswa kuhusisha matumizi ya hali ya juu ya akili, hawapendi kusikia ushauri wa 'walio nje' kama akina sie.

Mageuzi ninayoyapigia kelele ni ya kimfumo. Kubwa zaidi ni haja ya uwepo wa mazingira ya uwajibikaji pale watu wanapoboronga. Moja ya dhana zinazotawala fani ya ushushushu ni ile isemayo 'kushamiri kwa matishio ya usalama katika nchi husika ni dalili kuwa taasisi ya ushushushu katika nchi husika ina mapungufu.' Sasa huhitaji uelewa wa fani hiyo kutambua kushamiri kwa matishio kadhaa ya usalama katika Tanzania yetu, kubwa zaidi likiwa ufisadi.

Labda waweza kujiuliza, iweje ufisadi uwe tishio la usalama? Jibu jepesi ni kwamba ufisadi unatoa fursa kwa maadui wa ndani na nje wa taifa kutimiza azma zao kwa urahisi. Kwa mfano, laiti kukiwa na ufisadi kwenye mipaka ambapo wahusika wanaruhusu kirahisi tu wageni kuingia nchini pasi kuzingatia taratibu zilizopo, ni rahisi kwa magaidi kutumia mwanya huo.

Ufisadi unaweza kutuletea tapeli la kimataifa kuwekeza kwenye maeneo yanayofahamika kiusalama kama 'vituo muhimu' (vital installations) kama vile viwanja vya ndege na bandarini.

Sasa tukichukulia mfano wa ufisadi, sio tu umeshamiri vya kutosha lakini ndo wazidi kuongezeka. Kuna wanaojiuliza je TISS (Idara yetu ya Usalama wa Taifa) ipo likizo ndefu, wahusika wapo katika usingizi fofofo au kazi imewashinda? Mie sina jibu la moja kwa moja lakini nadhani tatizo la TISS ni la kimfumo zaidi kuliko kiutendaji, japo utendaji wao nao una walakini.

Lakini kabla ya kuingia kwa undani katika mada hii, nirejee kwenye kichwa cha habari. Majuzi, mkuu wa taasisi yenye jukumu la ulinzi wa viongozi wakuu wa Marekani, Secret Service, Bi Julia Pierson alilazimika kujiuzulu wadhifa huo baada ya mtu mmoja kuingia uzio wa Ikulu ya nchi hiyo na kutishia usalama wa Rais Barack Obama. Kwa wenzetu tukio hilo lilikuwa na uzito mkubwa sana, na lilitawala sana katika vyombo vya habari.
Hata hivyo, kwa vile wenzetu wanaendesha mambo kwa uwazi, mwanamama huyo aliitwa mbele ya kamati moja ya bunge la juu la nchi hiyo na kupewa fursa ya kuieleza, ambapo watunga sheria waliafikiana kwamba anapaswa kujiuzulu.
Julia+Pierson+Testifies+House+Committee+yFaGpsh9L0yx.jpg
gty_barack_obama_secret_service_jt_120416_wmain.jpg

Tukirejea huko nyumbani, ukweli usiopingika ni kwamba licha ya vikwazo vya kimfumo vinavyoikabili TISS, ksingizio cha 'taasisi hii yafanya kazi kwa siri na hakuna anayepaswa kuhoji' kinatoa fursa kwa wazembe kupata kinga katika utendaji wao mbovu. Ndio, kazi za TISS ni za siri lakini so far usiri huo haujafanikiwa kuwawezesha kukabiliana ipasavyo na matishio ya kiusalama, la wazi likiwa ni ufisadi.

Miongoni mwa mapendekezo yangu (yapo mengi) kuhusu haja ya mageuzi ni kama ifuatavyo.

Kwanza, uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu unapaswa kufanywa kwa uwazi zaidi, ikiwezekana kuidhinishwa na Bunge. Hiyo itazuia uwezekano wa Rais kumpatia wadhifa huo mtu yeyote yule bila kuzingatia uadilifu na uwezo wake kikazi. Kwa kumpa Rais 'blank cheque' ni rahisi kwake kumchagua mtu wake, au mshkaji wake kwa minajili ya kumlinda au kuwa kibaraka wake badala ya kulitumikia taifa kiufanisi.
IMG_0470.JPG
Pili, ni muhimu TISS kama taasisi iwajibike kwa umma, na si kwa Rais pekee (maana huyo Waziri Katika Ofisi ya Rais mwenye jukumu la kuisimamia TISS anakwazwa na mazingira yalivyo, sambamba na 'uoga' wa kawaida). Ifike mahali, watendaji wakuu wa TISS waweze kuitwa Bungeni, kwa mfano, kuhojiwa kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu taasisi hiyo.

Kiutendaji, ni muhimu kwa taasisi hiyo kupewa uhuru wa kioperesheni utakaoiwezesha kuondokana na hali iliyopo sasa ambapo kwa kiasi kikubwa imekuwa kama tawi la usalama la chama tawala. Sambamba na hilo ni haja ya kuitengenezea mazingira yatayoiwezesha kuhakikisha mapendekezo yake kwa Rais yanafanyiwa kazi hata pale Rais anapoyapuuza. Ikumbukwe kuwa licha ya Rais kuwa 'mkuu halisi wa TISS,' yeye bado ni mwananchi kama wananchi wengine ambao TISS inawajibika kuhakikisha sio tu usalama wao bali hawawi tishio kwa usalama huo. Rais anapopuuza ushauri unaotishia usalama wa taifa basi TISS ijengewe mazingira ya kuhakikisha kuwa ushauri wake unafanyiwa kazi.

Nimalizie kwa kutumaini kuwa 'kelele' hizi zitasikika kwa wahusika. Tujifunze kwa wenzetu waliotatutangulia na wahusika wasione aibu kusikia ushauri wa wenye uelewa hata kama wapo nje ya 'uwanja wa mapambano.'
Makala hii imeandikwa na ndugu Evarist Chahali.
With no shadow of doubt, I support you. My reasons being.
1. To maintain checks and balances in the three arms of the gvt.
2. To keep up with public interest. Scholars from various parts of the world ( like US ) have proposed to add the media in the list of pillars of states. This is because of the far reaching implications that the media posses nowadays, information sharing has become a global trait. I think it's about time that everyone realise that we're living in the 21stC, public interest should be of paramount importance.
 
Kama mtu mwenye uelewa kiasi kuhusu utendaji kazi wa Idara yetu ya Usalama wa Taifa, nimekuwa 'nikipiga kelele' mara kwa mara kuhusu haja ya mageuzi ndani ya taasisi hiyo nyeti. Kwa bahati mbaya sio tu kelele hizo ni vigumu kueleweka kwa Watanzania wengi, uwezekano wa kusikilizwa ni mdogo hasa ikizingatiwa kuwa asili ya taasisi hiyo ni kutekeleza majukumu yake kwa siri, na kama hiyo haitoshi, mara nyingi wahusika wa taaluma hiyo inayopaswa kuhusisha matumizi ya hali ya juu ya akili, hawapendi kusikia ushauri wa 'walio nje' kama akina sie.

Mageuzi ninayoyapigia kelele ni ya kimfumo. Kubwa zaidi ni haja ya uwepo wa mazingira ya uwajibikaji pale watu wanapoboronga. Moja ya dhana zinazotawala fani ya ushushushu ni ile isemayo 'kushamiri kwa matishio ya usalama katika nchi husika ni dalili kuwa taasisi ya ushushushu katika nchi husika ina mapungufu.' Sasa huhitaji uelewa wa fani hiyo kutambua kushamiri kwa matishio kadhaa ya usalama katika Tanzania yetu, kubwa zaidi likiwa ufisadi.

Labda waweza kujiuliza, iweje ufisadi uwe tishio la usalama? Jibu jepesi ni kwamba ufisadi unatoa fursa kwa maadui wa ndani na nje wa taifa kutimiza azma zao kwa urahisi. Kwa mfano, laiti kukiwa na ufisadi kwenye mipaka ambapo wahusika wanaruhusu kirahisi tu wageni kuingia nchini pasi kuzingatia taratibu zilizopo, ni rahisi kwa magaidi kutumia mwanya huo.

Ufisadi unaweza kutuletea tapeli la kimataifa kuwekeza kwenye maeneo yanayofahamika kiusalama kama 'vituo muhimu' (vital installations) kama vile viwanja vya ndege na bandarini.

Sasa tukichukulia mfano wa ufisadi, sio tu umeshamiri vya kutosha lakini ndo wazidi kuongezeka. Kuna wanaojiuliza je TISS (Idara yetu ya Usalama wa Taifa) ipo likizo ndefu, wahusika wapo katika usingizi fofofo au kazi imewashinda? Mie sina jibu la moja kwa moja lakini nadhani tatizo la TISS ni la kimfumo zaidi kuliko kiutendaji, japo utendaji wao nao una walakini.

Lakini kabla ya kuingia kwa undani katika mada hii, nirejee kwenye kichwa cha habari. Majuzi, mkuu wa taasisi yenye jukumu la ulinzi wa viongozi wakuu wa Marekani, Secret Service, Bi Julia Pierson alilazimika kujiuzulu wadhifa huo baada ya mtu mmoja kuingia uzio wa Ikulu ya nchi hiyo na kutishia usalama wa Rais Barack Obama. Kwa wenzetu tukio hilo lilikuwa na uzito mkubwa sana, na lilitawala sana katika vyombo vya habari.
Hata hivyo, kwa vile wenzetu wanaendesha mambo kwa uwazi, mwanamama huyo aliitwa mbele ya kamati moja ya bunge la juu la nchi hiyo na kupewa fursa ya kuieleza, ambapo watunga sheria waliafikiana kwamba anapaswa kujiuzulu.
Julia+Pierson+Testifies+House+Committee+yFaGpsh9L0yx.jpg
gty_barack_obama_secret_service_jt_120416_wmain.jpg

Tukirejea huko nyumbani, ukweli usiopingika ni kwamba licha ya vikwazo vya kimfumo vinavyoikabili TISS, ksingizio cha 'taasisi hii yafanya kazi kwa siri na hakuna anayepaswa kuhoji' kinatoa fursa kwa wazembe kupata kinga katika utendaji wao mbovu. Ndio, kazi za TISS ni za siri lakini so far usiri huo haujafanikiwa kuwawezesha kukabiliana ipasavyo na matishio ya kiusalama, la wazi likiwa ni ufisadi.

Miongoni mwa mapendekezo yangu (yapo mengi) kuhusu haja ya mageuzi ni kama ifuatavyo.

Kwanza, uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu unapaswa kufanywa kwa uwazi zaidi, ikiwezekana kuidhinishwa na Bunge. Hiyo itazuia uwezekano wa Rais kumpatia wadhifa huo mtu yeyote yule bila kuzingatia uadilifu na uwezo wake kikazi. Kwa kumpa Rais 'blank cheque' ni rahisi kwake kumchagua mtu wake, au mshkaji wake kwa minajili ya kumlinda au kuwa kibaraka wake badala ya kulitumikia taifa kiufanisi.
IMG_0470.JPG
Pili, ni muhimu TISS kama taasisi iwajibike kwa umma, na si kwa Rais pekee (maana huyo Waziri Katika Ofisi ya Rais mwenye jukumu la kuisimamia TISS anakwazwa na mazingira yalivyo, sambamba na 'uoga' wa kawaida). Ifike mahali, watendaji wakuu wa TISS waweze kuitwa Bungeni, kwa mfano, kuhojiwa kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu taasisi hiyo.

Kiutendaji, ni muhimu kwa taasisi hiyo kupewa uhuru wa kioperesheni utakaoiwezesha kuondokana na hali iliyopo sasa ambapo kwa kiasi kikubwa imekuwa kama tawi la usalama la chama tawala. Sambamba na hilo ni haja ya kuitengenezea mazingira yatayoiwezesha kuhakikisha mapendekezo yake kwa Rais yanafanyiwa kazi hata pale Rais anapoyapuuza. Ikumbukwe kuwa licha ya Rais kuwa 'mkuu halisi wa TISS,' yeye bado ni mwananchi kama wananchi wengine ambao TISS inawajibika kuhakikisha sio tu usalama wao bali hawawi tishio kwa usalama huo. Rais anapopuuza ushauri unaotishia usalama wa taifa basi TISS ijengewe mazingira ya kuhakikisha kuwa ushauri wake unafanyiwa kazi.

Nimalizie kwa kutumaini kuwa 'kelele' hizi zitasikika kwa wahusika. Tujifunze kwa wenzetu waliotatutangulia na wahusika wasione aibu kusikia ushauri wa wenye uelewa hata kama wapo nje ya 'uwanja wa mapambano.'
Makala hii imeandikwa na ndugu Evarist Chahali.
Makala ndefuuu... hivi majukumu ya TISS unayajua? Unajua failures na successes za TISS tangu enzi za Mwalimu hadi karne hii ya kidijitali??? Kwahiyo kwakua wa Marekani kajiuzulu, na huku kwetu pia wajiuzulu? Kwani wa marekani anatoka mbinguni au unawaona ni noble sana? mbona nasikia wanahangaika kuja [kuomba] taarifa ukanda huu.... wa afrika if wao wana uwezo zaidi???? Then jingine.. naomba nifafanulie, hivi kumbe TISS ipo chini ya Waziri, Waziri gani vile??? Tufahamishe ndugu.
 
Mifumo yetu yote. Inaiga huko ughaibuni. Tiss waige pia usa.kwa sana. Hata wanajeshi wetu wamewahi kujifunza mbinu china,urusi,cuba nk. Tiss nao wawe walinda usalama wa taifa. Uchumi ukiwemo.....nawapa hongera ila wazidishe uzalendo kwa nchi.

Umeongelea "mifumo" halafu ukaongelea "mbinu".

Inaonesha wazi huelewi hiyo "mifumo" ni ipi na wala hilo neno lina maana ipi.

Kuna sita sita? Nne mbili? tatu tatu? Au?

Wacheni kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Ukiona mtu anaelezea jambo halafu akataja "mfumo" au even worse akataja "mifumo" ujuwe huyo ni kilaza asiyeelewa anachokiandika bali anaandika na yeye awe yumo yumo tu.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Hivi bado hamjamuelewa tu mleta mada?

"Tatizo" ni jina la mkuu wa TISS. Same father same mother na "tatizo" la mkuu wa NSSF.

Same father same mother na "tatizo" la Rais wa awamu iliyopita.

Kwa kigezo hicho hata awe malaika katika utendaji uliotukuka basi atakuwa ni shetani tu na kwa kigezo hicho hicho basi hata awe shetani fisadi basi kwa watu kama mleta mada huyo atakuwa ni malaika tu.

Asiye na macho haambiwi tazama.
 
kwakweliusalama wa taifa naona kuna baadhi ya vitu wamelala,wote tumeshuhudia matukio makubwa ya ugaidi yanayotokea nchi jirani lakini naona kama hawajifunzi kitu mfano magaidi walioshambulia mall za kenya walitumia simu ambazo hazijasajiliwa lakini huku kwetu makampuni ya simu ni yamehalalishwa kuruhusu hizo namba mpaka ukienda kwenye mihamala kuna gharama za kutuma au kupokea pesa kwa simu ambazo hazijasajiliwa wao wana uwezo wa kuishinikiza serikali ikafuta ujinga huu
 
H
Hivi bado hamjamuelewa tu mleta mada?

"Tatizo" ni jina la mkuu wa TISS. Same father same mother na "tatizo" la mkuu wa NSSF.

Same father same mother na "tatizo" la Rais wa awamu iliyopita.

Kwa kigezo hicho hata awe malaika katika utendaji uliotukuka basi atakuwa ni shetani tu na kwa kigezo hicho hicho basi hata awe shetani fisadi basi kwa watu kama mleta mada huyo atakuwa ni malaika tu.

Asiye na macho haambiwi tazama.
Awa jamaa zako ulowataja ndo walomuharibu jk kwa udini wao
 
I second idea ya kuwa hawa jamaa uteuzi wao upitishwe na bunge na pia incase of anyting aweze itwa kwa bunge kutoa maelezo
 
Wenzetu wanajua nini maana ya usalama wa rais hivyo inapotokea tukio ka hilo huwa wanajiona ni aibu kubwa na fedheha! Kwa tasisi nyeti ka hiyo
 
TISS nadhani wao hawana tatizo,tatizo sio Taasisi huru ingekuwa inajitegemea ingekuwa mbali,ingekuwa inawajibika kwa bunge ingekuwa safi sana,ila inawatendaji wengi wenye uwelidi mkubwa sana,ata hayo majipu yanayolipuka wao wanamchango mkubwa sana,nadhani kuu zaidi iwe huru kufanya mambo yake Bila kuingiliwa na watu
 
TISS sio wezi kama chombo ila mfanyakazi kuwa mwizi ni tabia yake na mawazo yake
 
Sijui mfumo wao wa kutoa ajira,ila nilisikia zamani kuwa wanafuatilia watu tangu shule na kuwarecruit ambapo maajenti wakubwa walikuwa ni walimu,
ila miaka hii mtoto wa mjomba ,wa dada na kila ndugu ndiyonhuingizwa huko,
wapo wengine wanaona ujiko kujitambulisha kwa kuonyesha vitambulisho vyekundu vyenye ngao na wengine kukunjua mashati kuonyesha silaha.
sasa najiuliza mtunkama huyo habari atazipataje?maana ameshajulikana!
wafunzwe maadili sana

bahati nzuri wahusika wakuu Nifah, UncleBen na Mussolin5 wamo humu humu hivyo ngoja na wao sasa waje waitetee hii hoja yako japo nakubaliana na wewe kwa 100% zote kwani hata hao majamaa tajwa hapo hunipiga mno mkwara na kuna siku mmoja wapo nilibishana nae humu akanitolea bastola nikawa kila niki type tu naiona. nilinywea mwenyewe mkuu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom