Bosi wa Airtel aingia nchini, akutana na JK na akataa kupigwa picha

KICHAKA

Member
Jun 17, 2009
58
9
Unajua nimeshangaa sana kusikia watu wanalalamikia picha ya Al Adaiwi tu, lakini bosi huyo ameingia juzi na kukutana na wafanyakazi wa Airtel kisha kwa JK na hawakumpiga picha. Hivi sisi watanzania tulikuwa na shida gani na Al adawi na waandishi mbona huyu bosi hamkumpiga picha?
 
Jaribu kuhusianisha matokeo sio matukio. Wote wawili sawa wamekuja tanzania, je matokeo (impacts) yake yanafanana?
 
kichaka bana.......sasa apigwe picha ili iweje?....watanzania wanadeal na mwizi wao sio mtu aliyekuja zake kwa shughuli zake.....au ili mradi utoe thread?
 
kama kuna ushahidi ana "agenda" za kuhujumu uchumi au kuumiza wa nanchi kwa njia moja au nyengine basi itabidi tumjue mapema n ataifa tujihadhari
 
kichaka bana.......sasa apigwe picha ili iweje?....watanzania wanadeal na mwizi wao sio mtu aliyekuja zake kwa shughuli zake.....au ili mradi utoe thread?

Unajua nyie watu hapa hamtaki kuunganisha dot! Tangu ilipokuwa Celtel ilikuwa ya umma na imeuzwa matra kadhaa na kuna nchi wakati ikiwa Zain waligoma isinunuliwe na Airtel hivyo huyu jamaa picha yake kukosekana ni sawa na Al Adawi! Lakini waandishi kama mnayo si muweke hapa ama naye aliwanyang'anya kamera?
 
Unajua nimeshangaa sana kusikia watu wanalalamikia picha ya Al Adaiwi tu, lakini bosi huyo ameingia juzi na kukutana na wafanyakazi wa Airtel kisha kwa JK na hawakumpiga picha. Hivi sisi watanzania tulikuwa na shida gani na Al adawi na waandishi mbona huyu bosi hamkumpiga picha?

kimsingi kuna watanzania wenzetu wakati mwingine wanamawazo ya kishamba sana! hata mimi nimebahatika kumuona huyo bosi wa airtel kwa harakaharaka ni mtu ambaye hana muda kabisa wa kufanya mambo ya kuuza sura, hana muda wa kujitangaza maana kinachotakiwa ni kuona biashara yake inasonga mbele, yeye anajitangaza kupitia kampuni yake. kwa mfano hizo picha za AL Adawi baada ya kuziona imetusaidia nini?
kwa wale wasiofahamu Bosi huyo wa airtel alikuwa akiongozwa na escot ya polisi pamoja na pikipiki moja ya trafiki.
 
jamaa anahusishwa na ukwepaji wa kodi kwa makampuni yake ndo maana anakua anabadilsha majina sijui zain,seltel,n.k.
 
Unajua nimeshangaa sana kusikia watu wanalalamikia picha ya Al Adaiwi tu, lakini bosi huyo ameingia juzi na kukutana na wafanyakazi wa Airtel kisha kwa JK na hawakumpiga picha. Hivi sisi watanzania tulikuwa na shida gani na Al adawi na waandishi mbona huyu bosi hamkumpiga picha?

Kwa wenzetu Mfanyabishara wa kigeni Upokelewa na Wafanyabiashara Wenzake,kwa Tanzania Mfanyabiashara wa kigeni upokelewa na Rais(kuadi wa ufisadi).
 
kichaka bana.......sasa apigwe picha ili iweje?....watanzania wanadeal na mwizi wao sio mtu aliyekuja zake kwa shughuli zake.....au ili mradi utoe thread?

Preta mpenzi,

Al adawi si mwizi ila siasa ndio inataka kufanya aonekane mwizi! Tatzi letu kuna watu sio kama hawajasoma na hawajui sheria za mikataba! wanafahamu ila pengine wao ndio wezi wanaochonga deal huwezi kufuta mkataba ulioutumikia more than two years na imebaki miezi mitatu bila kuangalia impacts zake.

Au ile issue ya uwakala wa sumatra uliofutiwa mkataba december ilihali mkataba unaisha january! unataka kuniambia hawa wanaovunja mikataba hawajui wanachokifanya? hawana washauri?

Al adawi na kampuni yake ya dowans wamewachaji Tanesco kapasiti chaji ya mil 152 kwa siku na kuiuzia Tanesco uniti moja ya umeme kwa senti 4.50 ya kimarekani

IPTL wanawachaji Tanesko kapasiti chaji 300 mil kwa siku na wanauza unit moja ya umeme kwa Tanesco senti 17 ya kimarekani.

Ukiangalia hapo utajua kuna siasa inachezwa wala huhitaji uwe na phd mpenzi.... we kula ugali wako na matembele waache wenyewe wajipange for 2015......................
 
Pointeless thread, kampuni mmoja ipo kwenye kashfa nzito na "bossi" hajulikani nyingine inafanya biashara zake kwa uwazi kabisa na haina kashfa as far as we know.
Kama unataka kuona picha yake nenda website ya Airtel.
Airtel Management Board
 
Unajua nyie watu hapa hamtaki kuunganisha dot! Tangu ilipokuwa Celtel ilikuwa ya umma na imeuzwa matra kadhaa na kuna nchi wakati ikiwa Zain waligoma isinunuliwe na Airtel hivyo huyu jamaa picha yake kukosekana ni sawa na Al Adawi! Lakini waandishi kama mnayo si muweke hapa ama naye aliwanyang'anya kamera?
Kichaka hebu tuambie imekuwaje si ya umma now?
 
HEKO JF KWA KUMBUKUMBU HIZI, JAPO MASIKIO YALIZIBWA ILA SASA UHALISIA U WAZI, AISE OGOPA MUDA, TEKINOLOJIA NA UELEWA.
Kiukweli, kuifungia JAMIIFORUM isiwe hewani utakuwa umefanya kosa kubwa sana. Ni eneo pekee unaweza pata data za watu na maoni yao kwa kipindi kilichopita bila shida.
 
Back
Top Bottom