Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Born Again Pagan: The Big Ideas And...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Feb 6, 2007.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Feb 6, 2007
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 974
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 18
  The Big Ideas and Dialogues
  Copyright: Born Again Pagan, 2007-02-05

  CCM ruling political party
  Where is the big idea
  For the big dialogue
  Where is the engaging conversation
  Halting and containing ujamaa
  The essence for equality and cooperation? Read on: http://mjengwa.blogspot.com
   
 2. S

  Sumaku Senior Member

  #2
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ( inatoka kwanzajamii.com)  BAP: Shule ya Bwiru Sekondari (Wavulana) 1959-1964 (1)
  Msomaji mpendwa, Mjengwa alikidhi ombi la kutupatia angalau picha za Shule ya Sekondari Bwiru (Wavulana), Mwanza. Baadhi ya wasomaji wamechangia maoni yao, ikiwa ni pamoja na kunitaka nichangie ya Shule ya Sekondari Bwiru (Wavulana) wakati wa enzi yetu (1960-63).
  Niruhusu nikidhi , pia, ombi hilo, kwa kuchangia mfululizo wa makala tano.
  Nitachangia leo, kama ifuatavyo: ujumbe mfupi, kwa ujumla; baadhi ya waliofuzu hapo Shule ya Sekondari Bwiru (Wavulana); kuwakimbia wa-Sabato (Ikizu Middle School) huko East Lake Province (wakati huo); na wanafunzi wenzetu wakatazwa kuandika Mtihani wa Darasa la 8, ikiwa ni pamoja na kujitayarisha kwangu kujiunga na Bwiru (Wavulana).
  Ujumbe
  Sisi wengine tulipata bahati kubwa sana ya kulipiwa gharama zote za masomo toka sekondari hadi kuhitimu digrii za uzamili (doctoral level) na serikali yetu na/au skolashipu za wafadhili (binafsi, mashirika yasiyo ya serikali au serikali za nje): Tulilipiwa taaluma, afya/bima ya maisha, chakula/vinywaji, malazi, sare za shule, mablanketi/shulea na taulo, sabuni na karatasi za ******, usafiri (hata daraja la pili –meli/tren/basi la relwe), na kadhalika.
  Mfumo huo wa elimu umebadilika; eti, tunakwenda na wakati! U-binafsi umejikita kiasi cha kusaliti taifa letu. Kuna matatizo makubwa leo hii kwa watoto wa walalahoi wanapojaribu kutafuta elimu, maarifa na hekima ya kuishi zaidi ya maisha ya kukidhi mahitaji yao ya lazima; kwani wanyama nao hukidhi mahitaji hayo ya lazima. Binadamu inambidi kutafuta/kupata chakula cha ubongo/akili.
  Baadhi yetu yafaa turudi nyuma kutafukari bahati hiyo tuliyopata. Turudi nyuma na kuanza kujenga na kuimarisha vyama vya alumna (alumni associations). Alumna hivyo huchangia sana maendeleo ya shule walizohitimu wana-alumna (majengo na vifaa). La sivyo, tuliopata bahati hiyo tutakuwa tunalisaliti taifa letu.
  Tuliopata bahati hiyo inatubidi daima tujifananishe na nyuki “wafanyakazi” wa mzingani warukao kutafuta asali na nekta. Hao nyuki wasiporudisha asali na nekta hiyo mzingani, wanaweza kabisa kuua uhai wa kundi zima la nyuki mzingani.
  Rais Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliona maono ya umuhimu huo. Alitoa wosia wa mfano wa kijiji kitoacho chakula kwa baadhi wana-kijiji wake ili wapate nguvu za kwenda kuhemea na kurudisha chakula kijijini.
  Sambamba na jukumu la kusaidia shule tulizohitimu, kupitia alumna, sera za taifa hazina budi kuwekeza katika kile tukiitacho, “human development index” chenye vigezo muhimu vya kuendeleza elimu itakayoweza kukidhi Tanzania ya karne hii. Na hakuna la maana zaidi ya kuwekeza katika mafunzo na maslahi ya walimu, wanafunzi, vifaa – ikiwa ni pamoja na majengo vitabu na taaluma.
  Katika hili la kukuza “human development index” tusijenge matabaka, kwa kujigamba eti uchu wa u-binafsi ndio injini ya kuharakisha maendeleo! Tulichangia kulaani, kupambana na kushinda vita dhidi ya apaatedi (apartheid) huko Afrika Kusini. Kwa nini leo tunaijenga na tunaikaribisha apaatedi yetu wenyewe kupitia mlango wa nyuma (au wa mbele kwa wazi) katika mfumo wa elimu?
  Kwa wale ambao bado mpo shuleni, chuchumilieni elimu kwa nguvu zenu na uwezo wenu wote. Hamjui Tanzania na ulimwengu wa usoni vimewaandalia nini. Kwahiyo, msife moyo, vijana; dunia ya leo na kesho ni yenu.
  Kufuatia ujumbe huo, unakaribishwa “on an excursionary travelogue” hapo Bwiru (Wavulana) ya wakati wangu (1960-63).
  Wahitimu Bwiru (Wavulana)
  Nitataja tu baadhi ya majina “maarufu” (majina mengine unaweza kuongezea) tangu mwaka 1959 hadi 1964. Nimetumia ki-sifa cha “maarufu” (for solely descriptive pedestal of recognition, appreciation and acknowledgment) nikijikita katika yale waliyoyafanya watajwa huku nikizingatia kwa makini kutowakweza wahusika. Kuna wengine waliotangulia (ama kujiunga baada ya wakati-tajwa) ambao wanastahili ki-sifa nilichotumia, pia.
  Baadhi ya watajwa wameishatuacha (“wametangulia mbele ya haki”); wapumzike kwa amani. Wengine wamestaafu; na, huenda, nimechanganya miaka.
  Mosi, Shule ya Sekondari ya Bwiru (Wavulana) imechangia, kwa kiasi fulani, katika kujenga Tanzania ya leo:
  Mwaka 1959: Charles Musama Nyirabu (BoT). Charles alihitimu mwaka 1959 kabla sijajiunga na Bwiru (Wavulana). Kwa kuwa nimemtaja hapo juu, nimeweka picha yake:
  Charles Musama Nyirabu
  Mwaka 1960: Joseph Sinde Warioba (m-Diplomasia/m-Bunge/Waziri Mkuu/Jaji), Walter Scott Bgoya (m-Diplomasia/Mkurugenzi TPH/Mkuu wa Mkuki-Nyota), Wenceslaus Kilama (Prof./Daktari), Jackson Ng’ombe (Mekaniko Injinia-Relwe), Mark Lwiza (Elekroniki Injinia), Alex Ruhaga Murasi (Mkuu wa Shule/Chuo/Mkurugenzi Wizara), Adoniah Baluhi na Francis Lazaro Bomani.
  Joseph Sinde Warioba Walter Scott Bgoya
  Mwaka 1961: Nimrod Tito Lugoe (Mwanasheria/m-Diplomasia/Usalama wa Taifa-Ikulu/Mkuu wa Wilaya/Balozi/Mkuu wa Mkoa), Joshua W. Opanga (m-Diplomasia/Balozi), Asaph Abraham Maradufu (Prof. Sayansi), William Mahalu (Prof./Daktari) na Kisia Almasi (Elektroniki Injinia).
  William Mahalu (Kofi ya Kijivu Kushoto Nyuma ya ma-Yaya)
  Joshua W. Opanga Nimrod Tito Lugoe
  Mwaka 1962: Silas Mayunga (Afisa Jeshi/Mkuu wa Mkoa/Balozi), Ali Hussein Magomasi (m-Diplomasia) na Ng’ombe (Daktari) - mdogo wa Jackson Ng’ombe.
  Silas Mayunga (Katikati)
  Mwaka 1963 (Mwaka Wangu): Donasian Mwita (Mwanasheria/Kabidhi Wasihi/Jaji), Christopher Mbotte Nyirabu (Katibu Mkuu Wizara/Mkurugenzi-Mazingira Ziwa Victoria), Born Again Pagan (Media Ecologist/Adj. Prof.), Adamu Marwa (East African Airways/Ikulu/m-Diplomasia/Balozi) na Ernest Nyanda (Afisa Biashara/m-Bunge/Waziri).
  Kidollah Makani BAP (Born Again Pagan) Ernest Kisumo Nyanda
  Wengineo: Chorwa Mgonche Wambura na Paul Shigi (ma-Afisa Jeshi), Zakayo Igenge (Daktari), Philip Mussa (Mwalimu/Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwiru-Wavulana), Amos Petro Dabana (Mwlimu/Mkufunzi/Usalama wa Taifa-Ikulu), Kidollah Makani (Bima) na John Magembe Williams Nyagiro (Mwalimu/Afisa Mitihani Afrika Mashariki/Afisa Wizara Kilimo).
  Mwaka 1964: Brendire Moronda (TANU), Raphael Isaro Chacha na Daudi Ngw’ananogu (ma-Afisa Jeshi), John Mynah (Elektroniki Injinia), Kaseselo (Daktari) na Kassim Juma Maharage Mwawado (m-Diplomasi/Balozi).
  Mwaka 1965: Issa Omar (Elekroniki Injinia/m-Diplomasia Benki-Dunia/Mfanyabiashara) na Said Mecki Sadiki (Mkuu wa Mkoa).
  Omari Issa Said Mecki Sadiki (Kaunda)
  Mwaka 1964: Josephia Fanuel Muindi (Prof./Daktari-Saratini).
  Josephia Muindi
  Kuwakimbia wa-Sabato
  Pili, niliingia Bwiru mwaka 1960 nikiwa ni mwanafunzi peke yangu kutoka Ikizu Middle School ya wa-Sabato, kama nilivyotaja mapema. Ikizu ndio ilikuwa Middle School peke yake kwa wa-Sabato nchini ikichukuwa jumla ya wanafunzi 45 tu kutoka mashule yenye Darasa la 6: Bwasi Majita, Kibumaye Tarime, Suji Pare na Njombe. Wanafunzi kutoka Heru Juu, Kasulu, walijiunga kutoka Darasa la 4.
  Sijui ni wanafunzi wangapi walioanza Darasa la 1 katika shule za wa-Sabato ambao hawakupata nafasi ya kuingia hapo Ikizu Middle School!
  Wanafunzi wenzangu tisa na mimi tuligoma kujiunga na Bugema Missionary College, Uganda - sekondari moja tu ya wa-Sabato kwa Afrika Mashariki nzima. Tulitaka kujiunga na shule za sekondari za serikali. Shule/Misheni ya wa-Sabato Ikizu haikupenda tutengane na wa-Sabato! Wagomaji ndio tulikuwa tunaongoza darasani, academically.
  Wavulana: Israeli H. Magessa, Mispar Zakaria Munema, James Zefania Maserele, Eliakim Sando, Jeremiah Nyainchowa, John Maduhu na mimi. Wasichana; Maza Maduhu, Drusilla Samson Karilo na Lois Ezekiel Majura.
  Hedimasta Mundy kutoka Bwiru (Wavulana) alikuja kutufanyia interview. Waliomfahamu Bwana Mundy walikuwa wakitueleza kuwa ni Mkuu wa Shule machachari. Alikuwa na macho makubwa na akikutazama, ni kama alikuwa anaangalia endapo kichwa chako kilikuwa na ubungo kweli.
  Lakini walimu wetu waliotukazania, kwa siri kubwa, tujiunge na shule za sekondari za serikali, Lamech Mulinga Lima na Ibrahim Mujinja Andrea Fundi, walitutayarisha kwa hiyo “interview” na kututia moyo wa kutomwogopa Bwana Mundy.
  Baada ya interview yangu, Bwana Mundy alinihakikishia kuwa angependa nijiunge na shule yake. Aliniuliza kama kuna mwanafunzi yotote niliyemfahamu hapo shuleni kwake. Nilimjibu kuwa kulikuwepo akina Salmon Fanuel Ngereja, Zablon Matome, Asaph Abrahim Maradufu, Nimrod Tito Lugoe na Augustine Nyambhibho (wanafunzi waliokuwa wakitokea sehemu za kwetu na wengine jamaa zangu).
  Tulioamua kujiunga na sekondari za serikali tulisumbuliwa sana. Kanisani, Pasto Raphael Megera alituita jina la “waasi”. Wakati wa ibada Jumamosi, tuliombewa kwa Mungu atubadilishe msimamo wetu.
  Shule/Misheni iliposhindwa kutubadili msimamo wetu, tulipewa jaribio la mwisho: Tulilazimishwa kila mmoja kwenda nyumbani (Majita, Ukerewe, Tarime na Usukuma) ili kupata vibali kutoka kwa wazazi/walezi wetu, na huku tumebakiza majuma mawili tu ya kufunga shule!
  Wengine hatukuwa na nauli ya kutupeleka nyumbani kwa sababu tulitaka kutumia hiyo nauli wakati wa kufunga shule. Kwa bahati nzuri, kwa siri kubwa, walimu niliowataja hapo juu walikuwa tayari kutukopesha nauli za kutupeleka nyumbani ili tupate vibali vya kwenda shule za serikali kutoka kwa wazazi/walezi wetu. Kama tungekataa, ungekuwa ni ushahidi wa kukiuka msimamo wetu!
  Asubuhi moja, tulijitayarisha kupanda basi la United Bus Company kutupelekwa hapo Nyamuswa kusubiri mabasi yaendayo Mwanza na Ukerewe au kuendelea na basi hilo hadi Musoma kupata mabasi ya kupeleka wengine Mugango/Majita na Tarime. Wote tulirudi na vibali vya kwenda shule za serikali.
  Vibali hivyo vilitonesha kidonda. Tulipoteza muda mwingi wa prep (kujisomea jioni) tukikutana na viongozi wa shule, tukihubiriwa na tukiombewa na huku wenzetu wakijisomea. Tulifukuzwa na Headmaster kutohudhuria darasa lake la Somo la Maarifa kwa kutuita aingiapo darasani, “Travellers, out! Ikatubidi kuanza kufundishana.
  Njama hizo zilidhamiria tupoteze muda wa kujisomea ili tushindwe Mtihani wa Mwisho! Zaidi, Shule/Misheni ilikuwa ikitafuta visingizio vya kutufukuza.
  Lakini wapi! Tulijua kuwa Shule/Misheni haingeweza kutufukuza. Na kama ingethubutu kutufukuza, walimu waliokuwa upande wetu kwa siri walitudokezea kuwa walikuwa tayari kutuombea nafasi katika shule za seikali ili tuweze kumaliza Darasa la 8. Tukawa na vichwa vigumu, kama chuma cha pua! Tukajitia moyo na kaulimbiu yetu, “Hawatuwezi!”
  Wakuu wa shule wakawaacha wanafunzi wenzangu na kuanza kuniandama mimi binafsi ili nikubali kwenda huko Bugema. Shule/Misheni ilikuwa na imani kubwa kwangu; nilikuwa nafanya vizuri sana darasani. Ili kuweza kuniteka, Shule/Misheni ilimtumia “heavy-weight” wa ushawishi, Mwalimu Elisha Okeyo.
  Wakati wa alasiri yote ya Jumamosi moja (wakati wenzangu wamekwenda nje kuhubiri neno la Mungu) Mwalimu Elisha Okeyo alinichukua kwa matembezi. Tuliangua machungwa kutoka kwenye mti wa chungwa aliokuwa ameununua kwa Mzee mmoja wa kanisa. Mimi nilijaza mifuko ya kaputura yangu.
  Tulitembea kuelekea kwenye rambo la maji, tukifuata kijito kilichokauka, hadi kwenye miamba penye kivuli tukapumzika.
  Mwalimu Elisha Okeyo alinikazania kwa maombi nibadilishe msimamo wangu. Alinieleza jinsi ambayo Mungu angenisaidia kuweza kupata pesa za karo kwa kuuza vitabu, kama Missionary Colporteur.
  Imani yangu ilikuwa si kubwa kiasi cha kuhamisha huo mlima wa kero uliokuwa mbele yangu (Matayo 17:19-21). Nilikataa kujirusha chini, pia; sikuona Malaika wa kunidaka (Matayo 4:5-6), pengine, shauri ya imani yangu duni!
  Matokeo yake: Nikamgomea!
  Wanafunzi Wakatazwa Kuandika Mtihani wa Kumaliza Darasa la 8
  LY (Last Year) wa mwaka huo tulijiandaa kuandika Mtihani wa Mwisho. Siku ya kuandika Mtihani huo ikafika. Mwangalizi alikuwa ni Mwalimu m-Amerika kutoka Bumangi Middle School (Mennonite).
  Tulipokuwa tayari kuingia ndani ya Chumba cha Mtihani (Mess Hall), Mwangalizi huo alitoa taarifa ifuatayo:
  “I have good and bad news. The good news: On behalf of the Department of Education, allow me to take this opportunity to congratulate Ikizu Middle School on succeeding to sustain the number of pupils who entered Standard 7. It is very encouraging to note that all those pupils have finished Standard 8.”
  Kabla hajamaliza, Mkuu wa Shule/Misheni Principal Beavon (m-Amerika), Hedimasta Lukius Mkobe na sisi wanafunzi tulianza kupiga makofi kujipongeza kwa sifa hiyo. Mara mwangalizi aliendelea:
  “However, the bad news is that only those pupils who have elected to join Government Secondary Schools are allowed to sit for the Examination.”
  Mwangalizi huyo alizidi kueleza kuwa agizo hilo lilizingatia hoja kwamba kwa kuwa wa-Sabato hawakupenda kupeleka wanafunzi wao katika shule za serikali, hivyo basi, hakukuwa na “relevancy” kwa wanafuzi wao kuandika Mtihani wa Serikali.
  Mkuu wa Shule/Misheni, Hedimasta na wanafunzi wenzetu waliokatazwa kuandika Mtihani wa Mwisho walibaki wameduwaa, kana kwamba huyo Mwangalizi alikuwa akitania!
  Mara Mwangalizi alianza kusoma majina ya watahiniwa kumi tu, ambao tuliruhusiwa kujipanga mstari wetu na kuingia ndani ya Chumba cha Mtihani (Mess Hall) ili kuanza kuandika Mtihani wa Mwisho. Wenzetu waliambiwa wangeandika Mtihani wa kwenda Bugema, ambao ungetolewa na Shule!
  Mwangalizi aliwaamuru wanafunzi wengine watawanyike.
  Wanafunzi wenzetu karibu wafanye fujo hapo shuleni! Kwa sababu Shule haikuwa na Mtihani wa kuwatahini kuonyesha kuwa wameamaliza Darasa la 8 (isipokuwa wa somo la Biblia). Siku iliyofuata, wakajikuta wanafanya maswali ya Mtihani tuliokuwa tumefanya jana yake, ambao tayari walikuwa wameishauona . Nafikiri wengine walifanya vizuri. The rest is a sad history ya udanganyifu!
  Hatukuelewa kabisa endapo amri ya kuwakataza wanafunzi wenzetu wasiandike Mtihani wa Mwisho ilikuwa imetoka Dar es Salaam au ulikuwa ni uamuzi tu wa Mkuu wa Elimu wa Mkoa (East Lake Province), Miss Mary Edith Hancock (Mama Nyang’oko, kama alivyojulikana kote Mkoani).
  Wengi wetu tulimfahamu Mama Nyang’oko akiwa ni Mkaguzi wa Shule za Primari Wilaya ya South Mara (Musoma) akipenda mavazi ya ki-“safari” ya tai nyeusi, koti, sketi ya khaki na stokingi, ungefikiri alikuwa ni mwanamume, kasoro ya sketi. Mama Nyang’oko alikuwa na ujeuri wake! Alikuwa na machachari kweli! Alikuwa na tabia ya ku“harrass” walimu wazembe mbele ya wanafunzi kiasi cha yeye kushika chaki na kufundisha!
  Baadaye, Mama Nyang’oko alipandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Elimu. Alichukia sana kuona wanafunzi wanakataliwa kwenda shule za serikali kwa sababu tu ya dini kwa sababu Serikali ya Madaraka ilikuwa tayari imeondoa ubaguzi wa rangi na dini mashuleni katika mfumo wake wa elimu nchini.
  Baada ya Mtihani huo na mkasa uliotokea. Tuliagana kuelekeza nyumbani kwa machozi yaliyokaushwa tu kwa kutakiana kila la heri maishani kwa faraja ya methali ya “milima haikutani; binadamu hukutana.” Wengine tulijua kuwa huo ndio, pengine, ungekuwa ni mwisho wa kukutana!
  Nilipokea barua ya kuchaguliwa kujiunga na Bwiru (Wavulana) na kutakiwa kujitayarishwa kwenda Musoma kupata waranti ya meli kwa safari yangu kwenda Mwanza. Hapo mjini Musoma nilikutana na wanafunzi wengine waliokuwa wakienda St. Michael na St. George Iringa (Mkwawa ya baadaye) ambao walikuwa wakipewa waranti za Daraja la Pili (kwa usafiri wa meli/trenibasi-Relwe) na sisi wengine tulipewa waranti za Daraja la Tatu! Tumetoka mbali; the rest is history!
  Baadaye, nilibaini kuwa ni wawili tu tuliochaguliwa kwenda sekondari: Mispar Zakaria Munema (Ifunda Technical School) – alihitimu na kujiunga na Tanesco iliyompeleka Uingereza kusomea mambo ya umeme - na mimi Bwiru Sekondari (Wavulana). Baadaye, wenzetu wengine wawili nao walipata kujiunga na sekondari: Israeli H. Magessa (Musoma Alliance Secondary School) – ambaye tulikutana tena hapo Mlimani (1966) na James Zefania Maserele (Dar es Salaam Technical School) - alihitimu na kujiunga na Shirika la Posta.
  Dada zetu Drusilla Karilo na Lois Majura walipata kazi katika Hospitali ya Serikali, mjini Musoma. Dada Maza Maduhu (mrembo wa darasa letu) alipotelea sijui wapi huko kwao Mwagala au Ntusu, Usukumani!
  Labda, DaMija anaweza kulifuatilia hili la dada Maza Maduhu.
  Itaendelea…
  E-mail: [email protected]
  CHANZO: Kwanzajamii.com
   
 3. S

  Sumaku Senior Member

  #3
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  ( Sehemu ya tatu iko kule kwanzajamii.com)

  22 February 2010 164 views 2 Comments
  Alikotokea Profesa Born Again Pagan na Wenzake:
  Bwiru Sekondari (Wavulana) 1960-1963 (2)
  Msomaji mpendwa, katika makala iliyopita, nilianza na ujumbe mfupi, kwa ujumla; niliwataja baadhi tu ya wanafunzi waliofuzu hapo Shule ya Sekondari Bwiru (Wavulana) – 1959-1964 (kwa bahati mbaya, kutokana na hitilafu za ki-teknolojia, picha hazikuweza kutokea).
  Nilionyesha jinsi nilivyowakimbia wa-Sabato wangu hapo Ikizu Middle School, Musoma, East Lake Province (wakati huo); na jinsi wanafunzi wenzetu walivyokatazwa kuandika Mtihani wa Darasa la 8, ikiwa ni pamoja na kujitayarisha kwangu kujiunga na Bwiru (Wavulana).
  Makala iliyopita imechochea msululu wa barua pepe! Kuna walioniomba nieleze maisha yangu ya nyuma yalikuwaje nikikua kabla ya kujiunga na Primary na Ikizu Middle School.
  Hili ni ombi mwafaka sana tukizingatia nafasi ya familia; jamii kijijini; na viongozi wa dini; na shule (uduni wa elimu waliyokuwa nao walimu, uhaba wa vitabu na vifaa muhimu, ufundishaji pamoja na adhabu zake) katika kulea watoto wawe na maadili bora, na ni wapi tulikuwa tunapata vielelezo (au mifano ya kuigwa mithili ya ruwaza na tarakibu), yaani, role models wetu katika mazingira yenye uhaba wa “vya usasa”.
  Wasomaji wawili tofauti walionilitea barua pepe changamoto wakinitaka niandike kitabu juu ya hayo maisha ya wakati huo.
  Wote walioniomba, lau, kama wangebaini kuwa yote hayo nilikuwa nimeyaandikia hadithi katika kitabu kimoja, The Daunting Quadruple Influences: Growing Up Without Shoes in Emajita, Musoma, Tanganyika, Under Traditionalism, Seventh-day Adventism, Colonialism and Nationalism (PublishAmerica, Baltimore, 2004)!
  Ingawa maelezo ya kitabu hiki yapo online, bahati mbaya hakipatikani! Kutokana na sababu maalumu, sikupenda kitabu hiki kiuzwe; nilikitoa kwenye “circulation”. Sasa kitabu chenyewe kinayatarishwa upya na kimeendelezwa kuwa “vitabu” vitatu:
  1. The Daunting Quadruple Influences – Vol. 1: Transitory Spaces - Growing Up Without Shoes in Emajita, Musoma, Tanganyika, Under Traditionalism/Indigenism and Colonialism – juu ya ujadi na ukoloni kupitwa na wakati.
  2. The Daunting Quadruple Influences – Vol. 2: Anticipatory Spaces - Growing Up Without Shoes in Emajita, Musoma, Tanganyika, Under Seventh-day Adventism and Nationalism – juu ya mategemeo ya u-Kristo na uhuru katika kurithi ufalme wa mbinguni na kujenga maisha mapya ya u-taifa, vikifuatana (“respectively”).
  3. The Portrait of a Socialist Youth: Maturing Under Socialism-Aspiring Tanzania – juu ya ujana katika muktadha wa Ujamaa.
  “Vitabu” hivi vitatu vikichapishwa, vitaelezea maisha yangu toka utoto hadi upevuki (“infancy, childhood, adolescence, youth and maturity”) kati ya mwaka 1945 na 1975.
  Leo nitaendelea kueleza tabia ya ma-“Seniors” Kunyanyasa ma-“Juniors”; na mchakato au mkakati wa uhuru wa kuabudu.
  Wanafunzi wa Darasa la 8 waliokuwa bado kubatizwa walitakiwa wabatizwe kabla ya Mtihani wa Mwisho; nilikuwa mmojawapo wa hao wanafunzi. Tuliitwa kutahiniwa kwa mahojiano na Pasto Raphael Chacha Megera tayari kwa ubatizo.
  Nakumbuka Pasto Raphael Megera aliponiuliza endapo nilikuwa tayari kubatizwa, nilimjibu hapana. Pasto Megera aliniuliza, “Unasema hujawa tayari kubatizwa, je, Yesu akija kesho wewe utakuwa upande gani”?
  Bila hata kufikiria matokeo ya jibu langu, nilimjibu mara moja, “Yesu haji kesho”!
  Pasto Megera alinitazama kwa kukata tamaa. Hakuweza kuniuliza swali lingine. Alitoa amri nimwite mwanafunzi mwenzangu mwingine aje naye ahojiwe.
  Ni mwanafunzi mmoja tu kati ya kumi tuliokuwa tumeamua kujiunga na shule sa sekondari za serikali alikuwa tayari amebatizwa (Israeli H. Magessa), na alikuwa amebatizwa Bwasi kabla ya kujiunga na Ikizu. Wengine tisa tulikataa kubatizwa; tukaitwa, “waasi”! Baadaye, nilibatizwa nikiwa Darasa la 14 Tabora (Wavulana).
  Nilikataa kata kwenda Bugema Missionary College, Uganda - sekondari moja tu ya wa-Sabato Afrika Mashariki nzima. Nilijua wazi kuwa wazazi wangu wasingeweza kumudu karo ya shule huko Bugema!
  Mwalimu Elisha Okeyo, mmoja wa viongozi wa shule, katika mazungumzo yaliyochukua alasiri nzima ya Jumamosi moja, alinihakikishia kuwa ningeweza kumudu karo ya shule kwa kuuza vitabu vitabu vya dini (“a missionary colporteur”).
  Alinitolea mfano wa mwanafunzi mmoja (Gideon Enock Katondo) wa kutoka huko kwetu Majita aliyekuwa anatumia likizo lake (akisafiri kwa treni kati ya Kampala na Mombasa) akiuza vitabu vya dini kuweza kumudu karo ya shule hapo Bugema Missionary College.
  Imani yangu ilikuwa si kubwa kiasi cha kuhamisha huo mlima wa kero uliokuwa mbele yangu (Matayo 17:19-21). Nilikataa kujirusha chini, pia; sikuona Malaika wa kunidaka (Matayo 4:5-6), pengine, shauri ya imani yangu duni! The rest is history.
  Leo hii nayatafukari maneno na wosia wa Mwalimu Elisha Okeyo, kulingana na nyimbo nyingi za Injili na Taarab zenye maneno kuwa mpaji ni Mungu; Inshallah tutaowana; Mungu akitaka kukuruzuku, hakuletei barua; mlango wa Mungu u wazi; bora tumtegemee Mungu (Jalali) kunyoosha mambo yetu; kazi ya Mungu haiingiliwi; na lililopangwa na Mungu haliepukwi, kwa hiyo, tukubali majaaliwa, kwa upande mmoja.
  Hayo ni maneno na injili nzito; kuyaelezea, nawaachia wenye kuyafahamu zaidi!
  Lakini, kwa upande mwingine, kama m-Kristu, pia naamini kuwa (kwa kuasi amri ya Mungu) Adamu na Hawa waliambiwa kutumia akili yao kufukua fukua aridhini (na kufanya mambo mengineyo) ili wajipatie chochote cha kusetri uhai wao - huku wakingojea paradiso mpya (a new paradisiacal return re-conquered).
  Kusema kweli, wa-Sabato hapo Ikizu sio kuwa hawakupenda mwaka wetu tu ndio tusiende shule za serikali. Ilikuwa ni sheria kwa wanafunzi wao (eti, kutokana na kuchaguliwa/kukubaliwa kujiunga na Ikizu Middle School) kumaanisha kuwa wazazi/walezi wa wanafunzi hao walitiliana mkataba na Shule kwa watoto wao kuendelea tu na masomo ya juu katika mashule ya wa-Sabato!
  Kwa mfano, kulikuwa na wanafunzi wawili waliopata First Class (Territorial Standard Eight – 1956): Matogolo alikuwa akitokea huko Usukumani na mwingine alikuwa Nyatarangwa akitokea Kisiwa cha Ukara. Lakini hawakuweza kwenda Bugema kwa sababu wazazi wao walikuwa ni masikini sana. Matogolo na Nyatarangwa walikatazwa wasiende shule za serikali, albeit.
  Kuna wanafunzi wengine waliokatazwa kwenda shule za serikali na wakaenda huko Bugema (Uganda) na baadaye kuikimbia Bugema na kurudi Tanganyika kusoma katika shule za serikali, kwa mfano, mwanafunzi Nimrod Masoma Tito Lugoe.
  Hapo badaye, wanafunzi wengine (kwa mfano, Nimrod Elineema Ezekiel Mkono na Pedael Mufungo Silas Meli Mujaya) iliwabidi waendelee na masomo ya sekondari hapo Bugema na kumaliza darasa la 12. Lakini walirudi Tanzania kusoma ma-Marasa ya 13 -14 na kuendelea Chuo Kikuu.
  Ingekuwa Ikizu ni shule ya serikali, Matogolo na Nyatarangwa, pengine, wangejiunga bila kupingwa huko Tabora (Wavulana). Matogolo na Nyatarangwa walijiunga na Ikizu mwaka 1957 katika mpango, ambao ulikufa, wa kuanzisha sekondari hapo Ikizu.
  Najua Nyatarangwa hakukata tama! Alijisomesha kupitia masomo kwa njia ya posta (British Tutorial College) - yenye ofisi hapo Nairobi na Dar es Salaam. Nilipokuwa ninamaliza hapo Mlimani (1970), Nyatarangwa alikuwa amejikongoja hadi kuingia Chuo Kikuu (mwaka wake wa kwanza)!
  Popote pale ulipo, Nyatarangwa (mwana-Ukara), hongera sana kwa kuwa kielelezo (au mfano ya kuigwa mithili ya ruwaza na tarakibu - yaani, kwa Kiingereza, role models, katika mazingira magumu, kama ya hapo Kisiwani Ukara, pamoja na mikitadha ya historia ya kudhalilisha na kudhulumu utu na maisha ya wananchi wa hicho Kisiwa!
  Shule za Serikali: Ma-“Seniors” Kunyanyasa ma-“Juniors”
  Niliingia Bwiru na donda la kukimbia elimu ya wa-Sabato. Lakini sikuwakimbia wa-Sabato!
  Darasa la 9 letu hapo Bwiru lilifungua mitaala miwili – A na B, kutokana na maono na uongozi wa Julius Kambarage Nyerere na TANU kuendeleza elimu ya sekondari nchini.
  Ma-Kaka wa Bwiru (Wavulana), kama zilivyokuwa tabia ya shule nyingi za serikali (Middle na Sekondari) kulikuwa na tabia ya ma-“Seniors” kudhulumu utu na uanafunzi wa wadogo zao (ma-“Juniors”): kufagiliwa sehemu zao, kufagia Senior Recreation Room, kuoshewa masahani, na kadhalika.
  Bwiru (Wavulana) ilikuwa ya matabaka makubwa mawili tofauti na Ikizu Middle Scholl ambapo wanafunzi wote tulikuwa sawa. Hapo Bwiru (Wavulana) kulikuwa na matabaka ya ma-Bwana Wadogo (ma-“Juniors”) wa Darasa la 9-10 na ma-Bwana Wakubwa (ma-“Seniors”) wa Darasa la 11-12. Ma-Bwana Wakubwa (ma-Kaka zetu) walikuwa na Senior Recreation Room yao haikuingiwa na ma-Bwana Wadogo (ma-“Juniors”), labda wawe wanafahamiana na hao ma-Kaka zetu.
  Siku moja, baadhi ya ma-Kaka zetu wa kutoka Musoma (Zablon Matome na Salmon Fanuel Ngereja) walitukaribisha (baadhi ya wadodgo zao) kuingia “Senior Recreation Room”.
  Kuingia tu “Senior Recreation Room”, tukadakwa na “Senior” mmoja, “Nyie wa-Bwana Wadogo, ni nani aliyewapa rukusa kuingia humu? Hamjui kuwa hii ni ‘Senior Recreation Room’? Mtafagia chumba hiki kwa juma zima!”
  Ma-Kaka zetu haowaliotukaribisha waliingilia kati, “Hao ni wadogo zetu.”
  Tulipona kufagia “Senior Recreation Room” kwa juma!
  Baadaye, tulimtambua huyo “Senior” kuwa aliitwa Adoniah Baluhi, kijana mmoja wa ki-Sukuma mwenye tabia ya kuwachachafya ma-“Juniors”. Wakuu wa Shule nao hawakuingilia kati kudhibiti tabia hiyo ya udhalimu.
  Kutokana na kunyanyaswa, kudhalilishwa na kudhulumiwa huko, ma-“Juniors” walipohitimu na kuwa ma-“Seniors”, walijibu mapigo, na wakati mwingine, kwa kisasi!
  Kwa kawaida, hapo Bwiru (na katika sekondari nyingi nchini), Darasa la 9 huwa linaongoza kwa nidhamu na unadhifu. Wanafunzi huingia Darasa la 9 wametayarishwa na wazazi/walezi wao sawa sawa kwa kununuliwa karibu kila kifaa upya.
  Hapo Bwiru (Wavulana), kwa sababu ya umri mdogo, wanafunzi wa Darasa la 9 walikuwa wanaonyesha “nidhamu ya woga” mara nyingi mbele ya ma-Kaka zao wa ma-Darasa 11 na 12 waliokuwa na ka-tabia ka kuwanyanyasa, kuwadhalilisha na kuwadhulumu wadogo zao.
  Darasa la 10 huwa ndilo la wanafunzi wakorofi! Pengine, ni kwa sababu ya kujikomboa kutokana na nyanyaso, udhalimu na dhuluma wakiwa Darasa la 9. Nidhamu nzuri huwa inarudi Darassa la 11. Wanafunzi wanakuwa “serious” kwa masomo.
  Darasa la 12 huwa linajumlisha wakorofi (wanaoona hawana mwisho mzuri, ki-masomo) na wenye nidhamu (wanaoona kuwa kuna uwezekano wa kufanya vizuri, ki-masomo), licha ya kujiona kana kwamba hawana uwajibikaji; Lys, after all!
  Hayo ya nidhamu ndio niliweza kujifunza hapo Bwiru na, baadaye, wakati wa miaka yangu miwili ya Ualimu Shule ya Sekondari Ufundi, Moshi, kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu Mlimani, kama Mhadhiri Msaidizi.
  Uhuru wa Kuabudu
  Hapo Bwiru (Wavulana), nilikutana na wanafunzi wengine wa-Sabato: Salmon Fanuel Ngereja (jamaa yangu) na Francis Lazaro Bomani (Darasa la 12); Asaph Abraham Maradufu (jamaa yangu) na Nimrod Masoma Tito Lugoe - aliyekuwa mbele yangu hapo Bwasi Central School, Majita, Musoma (Darasa la 11); na Silas Mayunga, Edward Raphael na Augustine Joctan Nyambibho - jamaa yangu (Darasa la 10).
  Darasa la 9 nilikuwa na wa-Sabato wafuatao: Zakayo Igenge, Joel Majinge Mabhibha (aliyetoka shule za serikali za Bukima Native Authority Primary School - karibu na nyumbani kwetu - na Kasoma N.A. Middle Schoo) na Isaac Chitama - tuliyekutana Darasa la 4 na kuachana Darasa la 6 hapo Bwasi Central School, pia.
  Hapo Bwasi Central School (Darasa la 6), Isaac Chitama hakuchaguliwa kwenda Ikizu kwa sababu walezi wake hawakuwa wa-Sabato; yeye alikuwa hajabatizwa. Hata hivyo, alifanikiwa kwenda Ukerewe Kisiwani alikomalizia Darasa la 8 hapo Bukongo Middle School ya serikali.
  Kama nilivyokwisha kueleza, kutokana na maono mazuri na uongozi bora wa Julius Kambarage Nyerere, Serikali ya Madaraka ilikuwa tayari imetoa ubaguzi wa rangi na dini katika mfumo wa elimu, ikiwa ni pamoja na kuzingatia uhuru wa kuabudu/kusali. Katika shule za serikali tulijumuika bila kujali dini au rangi (ingawa wa-Hindi na wa-Ulaya walipenda kujitenga-tenga).
  Hakuna mwanafunzi “Taifa jipya la Tanganyika-tegemewa” ambaye alibaguliwa!
  Chache zifuatazo hazilengi kukaribisha malumbano yenye kujaa “subjective” maoni! Lakini wakati mwingine nashangaa sana nisikiapo ndugu zetu wa-Islamu wakilalamika kuwa Julius Kambarage Nyerere alipendelea wa-Kristo na alitaka Tanganyika (na baadaye) Tanzania itawaliwe ki-Katoliki!
  Malalamiko, kama hayo, yanapamba kurasa za muongozo wa uchaguzi uliotayarishwa na SHURA YA MAIMAMU TANZANIA (KAMATI KUU YA SIASA) - UCHAGUZI MKUU 2010 - WARAKA KWA MAIMAMU TANZANIA.
  Zaidi, mengi ya malalmiko hayo yako sambamba na yale yaliyopamba, pia, kurasa za maandishi mengi ya Mohammed Said juu ya wa-Isalamu na makakati wa mapambano ya uhuru. Sana sana, yale Mohammed Said aliyoandika katika kitabu chake, The Life and Times of Abdulwahid Sykes - 1924-1968: The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika (London: Minerva Press 1998).
  Wa-jameni, Nyerere katuondolea ubaguzi mashuleni (rangi na dini) hata kabla ya Tanganyika kujitawala!
  Lakini huko kwetu Majita, wa-Sabato hawakupenda kupeleka watoto wao katika shule za serikali kwa sababu ya kufanyakazi siku ya Jumamosi, walimu kuvuta sigara, kunywa pombe, kucheza dansi na mambo mengineyo. wa-Sabato walikuwa na ubaguzi wa kutaka watoto wa wa-Sabato ndio tu waendelee na elimu ya juu.
  Wa-Islamu nao hawakupenda watoto wao kujumuika na kushiriki katika shule za serikali (na dini nyingine) kwani tabia nyinginezo waliziona kuwa ni haramu, kwa mifano, kula nyama ya nguruwe na kula nyama isiyochinjwa na m-Islamu, na kadhalika. Watoto wa-Islamu walibakia kusoma ”madarasa” na kukariri kwa ki-Arabu maelezo ya dini.
  Unyonge wa kutojua maelezo ya dini (Biblia na Kurani) katika lugha zetu ulikuwa ni tatizo kubwa. Kwa mfano, watoto wa-Katoliki walikariri maelezo ya dini kwa ki-Latini - hadi hapo Biblia ya Kiswahili ilipokubaliwa kutumika katika Kanisa katoliki na kuwakomboa wengi kutokana na unyonge wa kutojua au kutoelewa lugha ngumu ya ki-Latini. Na hii pia ilihusu maelezo ya dini kutoka ki-Arabu kwenda Kiswahili!
  Hebu tuedelee na ka-hadithi ketu…Wanafunzi wa-Sabato tulidai haki ya kuabudu/kusali siku ya Jumamosi - tulidai kwa sababu tuliamini haki haiombwi! Wakati huo wa-Sabato hawakuwa hawajajenga kanisa lao. Walitumia Ukumbi wa Jamii wa Kanisa Katoliki hapo Bugando, licha ya uhasama wa ki-dini kati ya Kanisa Katoliki na Sabato. Baadaye, walijenga kanisa lao hapo Mlimani, Kirumba.
  Mapumziko kwa wa-Sabato siku ya Jumamosi yaliingiliana na ratiba ya shule. Jumamosi ilikuwa ni siku ya kufanya usafi wa mabweni, madarasa na mazingira tayari kwa ukaguzi siku hiyo. Wa-Sabato tulikuwa hatukushiriki. Hivyo, baadhi ya wanafunzi wenzetu walianza kulalamika kuwa tulikuwa tunapendelewa (the sacred cows).
  Ili kulegeza mvutano, tulikuwa tumekubaliana na wanafunzi wengine kutufanyia kazi siku ya Jumamosi na sisi kuwafanyia zamu zao kwa siku nyingine za juma. Muafaka huo, ambao haukuwa rasmi, haukuzua utata wowote.
  Mvutano ulijitokeza baina ya Wakuu wa Shule na kundi la wanafunzi wa-Sabato. Utata ulikuja wakati wa mashindano (riadha na soka) siku ya Jumamosi baina ya shule za mjini Mwanza na vitongoji vyake:
  Butimba Teachers Training College (Serikali), Nyegezi Seminary College na Nsumba Secondary School (Katoliki), Lake Secondary School (Wa-Hindu) na Mwanza Secondary School (Aga Khan). Na mara moja kwa mwaka, wanafunzi wa Tabora (Wavulana) walikuwa wakija kushindana na Bwiru Wavulana (soka na hockey) mwishoni mwa juma.
  Kati ya kundi la wanafunzi wa-Sabato walikuwa ni wanariadha mahiri (Nimrod Tito Lugoe na Reuben Matango) na wanasoka ma-golikipa hodari (Francis Lazaro Bomani na Silas Mayunga).
  Kutoshiriki kwa wanafunzi wa-Sabato kulidororesha hadhi ya shule katika riadha na soka kiasi cha kumuudhi Mkuu wa Shule (Bwana Mull, m-Skoti m-Uingereza, ambaye kwa kawaida alikuwa mpole sana na “very fatherly”)!
  Siku moja, yeye na Msaidizi wake Bwana A.R. Thompson (m-Uingereza), machachari, mfupi, mwenye matege, na mcheza soka/hockey/rugby) walituita wa-Sabato wote ofisini.
  Bwana Thompson alianza kwa kuibua kero ya wanafunzi wa-Sabato kutoshiriki katika usafi siku ya Jumamosi, kabla ya Mkuu wa Shule kutaja lililokuwa likiikera shule zaidi.
  Tukamjibu Bwana A.R. Thompson kuwa tunalipia siku hiyo kwa ku-“swap” na wenzetu.
  Bwana Mull alitamka wazi kuwa baadhi yetu tulikuwa tumetoka Middle Schools za wa-Sabato kwa sababu tulitaka kuendelea na elimu ya sekondari katika shule za serikali. Na kwamba tulijua wazi sheria na kanuni za serikali kufanyakazi siku ya Jumamosi.
  Alitoa hoja kali akimsakama Nimrod Tito Lugoe kwamba alikuwa amekimbia kutoka Bugema Missionary College, Uganda, alipokuwa Darasa la 10, kwa sababu hakupenda kile huyo Mkuu wa Shule alichokiita, “eti, kutii dini ya Sabato”. Hakuona sababu kwa nini Nimrod naye alikataa kufanyakazi siku ya Jumamosi.
  Huku akitusifia kuwa baadhi yetu tulikuwa tunang’aa hapo shuleni, “academically”, Bwana Mull hakutaka tujitetee. Alitegemea tukubali kutii sheria, kanuni na maagizo ya serikali katika kuendesha shule za serikali nchini. La sivyo, alikuwa tayari kutufukuza na kuturudisha katika shule hiyo ya wa-Sabato huko Uganda.
  Tulimwomba Mkuu wa Shule huyo atupe muda wa kutafakari waliyotuambia.
  Nilianza kutetemeka kwa tishio la kufukuzwa. Nilitetemeka sana kwa sababu nilikumbuka kisa kilichonitoa Ikizu cha kuitwa “muasi” wakati nilipokataa kujiunga na Bugema Missionary College, Uganda.
  Nilijuta endapo kweli Bwana Mull angetufukuza! Nilijuta kujiona nikirudi mbele ya macho ya wazazi wangu, eti nimefukuzwa shule! Sijui ningewaambia kitu gani!
  Hadithi ya Biblia ya Mzee Yona ilinizonga akilini (Yona 1:17). Nilijiona nipo karibu kumezwa na samaki mkubwa ambaye angenitapika hapo ufukoni Ninawi (Bugema) ambapo ningekaribishwa kwa mikono miwili!
  Hata hivyo, tulijua kuwa Bwana Mull asingeweza kutufukuza kwa sababu ya dini. Hapo jirani, kulikuwa na Bwiru (Wasichana) yenye Darasa la 5 hadi 12. Kutufukuza kungefungulia “kopo la minyoo” kwa shule nyinginezo za Mkoa wa Mwanza, na mikoa yote nchini.
  Baada ya siku tatu tulikutana na Mkuu wa Shule tena. Tulimjibu kuwa ni lazima tutii dini yetu.
  Bwana Mull hakuwa na la kusema. Alitishia kutushitaki mbele ya Mkuu wa Mkoa (Elimu) kwas kupeleka mzozo wetu mbele ya Mkuu wa Mkoa (Elimu) ambaye alishindwa kuuutatua, pia. Ikabidi aupeleke mbele ya Waziri wa Elimu, Dar es Salaam.
  Uamuzi na hatua ya kupeleka mzozo wetu Dar es Salaam vilizidi kutuvimbisha vichwa na kupata uhakika kuwa tusingefukuzwa!
  Huko Dar es Salaam, Waziri wa Elimu naye akashindwa kuamua. Kwani tatizo halikuwa la Wizara ya Elimu tu; kulikuwa na wa-Sabato wafanyakazi katika wizara nyingine, pia. Mzozo wetu ukajikita na kujipamba ki-taifa.
  Kati ya ma-Waziri tulikuwa na m-Sabato m-Bunge/Waziri Paulo Lazaro Bomani. Kabineti haikutaka kukiuka Katiba ya Nchi. Ikaamua kutoa uhuru wa kuabudu kwa wa-Sabato siku ya Jumamosi ambapo wafanyakazi wa-Sabato walitakiwa kulipa saa za Jumamosi siku ya Jumapili.
  Bunge likaridhia msimamo wa uhuru wa kuabudu si kwa wa-Sabato tu kupumzika siku ya Jumamosi bali pia kwa wa-Islamu nao walipewa ruhusa siku ya Ijumaa kwenda Ibada na kutakiwa na kuhitajiwa kulipia saa za Ibada ya siku ya Ijumaa.
  Hapo Bwiru (Wavulana), tulikubaliwa kupumzika Sabato na kwenda kanisani siku ya Jumamosi. Tulimpata pia Pasto wa kuja kutufundisha dini siku ya Jumanne, kama yalivyokuwa madhehebu mengine.
  Kwa bahati nzuri, Pasto m-Sabato aliyeletwa hapo Mwanza, Pasto Lukius Mkobe (m-Nata wa kutoka Mkoa wa East LakeProvincce) alikuwa ni yule yule Hedimasta wangu aliyekuwa akitufukuza kutoka Somo la Maarifa alilofundisha wakati wa mwaka wa mwisho hapo Ikizu Middle School!
  Pasto Lukius Mkobe alifurahi kuona wanafunzi wake wa zamani: Nimrod Tito Lugoe, Isa Chitama na mimi – alikuwa ametufundisha katika madarasa ya nyuma hapo Majita Bwasi Central School; na Nimrod na mimi hapo Ikizu Middle School.
  Hapo Bwiru (Wavulana) tulitakiwa kulipa saa za Jumamosi kwa kusafisha madirisha ya vioo vya madarasa na maabara ya sayansi siku ya Jumatano alasiri (hatukuwa na masomo ya alasiri siku hiyo).
  Hata hivyo, Bwana Mull (Mkuu wa Shule) hakupendezwa na uamuzi huo. Katika kufafanua uamuzi huo, aliweka vikwazo vingine (rules and regulations). Wanafunzi wa-Sabato tulitakiwa kumaliza “homework” zote tulizopewa kufanya wakati wa wikiendi. La sivyo, endapo kama angepokea kutoka kwa walimu malalamiko yeyote ya kutomaliza au kutofanya “homework” hizo, basi mwanafunzi mtuhumiwa angefukuzwa shuleni, mara moja!
  Hakuna mwanafunzi yeyote m-Sabato aliyefukuzwa kwa kushindwa kutimiza wajibu wa “homewoork”!
  Tutaendelea kuona ya Masomo na Burudani hapo Bwiru (Wavulana).
  E-mail: [email protected]
  CHANZO: KWANZAJAMII
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana kwa ajilin ya kupenda Elimu na kama unaweza anzisha Alumina yenu huko huko katika shule yenu ya Bwiru itakuwa vizuri sana katika kuchangia elimu ya shule yenu
   
 5. Waberoya

  Waberoya JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 7,955
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 83
  Sumaku, Objective ya hii habari ni nini? input yake, can you summarise ambao hatujaziona hizo zilizotangulia?

  pia jaribu kuweka paragraph, usi-CnP kama mimi.
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  Feb 27, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,985
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimeshindwa kuisoma yote
   
 7. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 5,953
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 63
  Mimi pia nimesoma Bwiru boys , shule ile sitaisahahu maana tulikuwa tunawekewa mafuta ya taa ktk maharage, kitu kingine tulikuwa na upinzani wa asili na Nsumba.

  Nikirudi ktk habari , basi nimeshindwa kuimaliza wala sijaelewa anaongelea nini, maana nime i scrol ikiwa ndefu na mpangilio hauna mvuto.
   
 8. S

  Sumaku Senior Member

  #8
  Mar 6, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ( Part 1,2,na 3 zinapatikana kwanzajamii.com)  Shukrani zangu za dhati kwa wasomaji wote wanaoniletea e-mails zao kuhusu hadithi hii inayoendelea.
  Stori, kama hii niandikayo, inatufanya tukumbushane mada (themes) sawa lakini kwa miaka na michakato tofauti. Kuna wengi wapendao sana kujua ya mazingira, raha, taabu na mambo mengine yaliyotokea zamani. Kwa mfano, msomaji mmoja amenitaka nitoe maelezo binafsi ya marehemu mzazi wake aliyewahi naye kupita hapo Bwiru (Wavulana), endapo nilimfahamu,
  Msomaji mwingine, akitoa mfano wa shule ya Tabora (Wavulana) mwaka 2000: uchafu wa vyoo, ukosefu wa maji na uhaba wa nafasi ya kulala wanafunzi (kiasi cha wanafunzi wengine kulala sakafuni), alitaka kujua endapo nimewahi kuitembelea shule ya Bwiru (Wavulana) hivi majuzi ili kupima hali yake ilivyo. Pengine ni vizuri kuipima Bwiru (Wavulana) katika muktadha wa sasa kuliko kutumia “macho” ya mwaka 1960-63!
  Wakati wetu hatukuwa na msongamano, kama mfano huo wa Tabora (Wavulana) kwa baadhi ya wanafunzi kuweka magodoro sakafuni mabwenini! Kwa mifano, kutokana na mwaka wetu kuanza mitaala miwili, “Senior Recreation Room” ilifutwa na kufanywa Library tukiwa darsa la 10. Wakati huo huo, Mess Hall mpya ilianza kujengwa na Mess Halls za zamani moja ikabadlishwa kuwa Library na nyingine pembeni ikawa Geography Room.
  Baadaye, ili kukidhi nafasi kwa ma-Darasa 12-A na 12-B jengo jeupe lilijengwa (ingawa liliezekwa kwa vigae vya “asbestos”), ambalo tuliliita, “White House”.
  Shule zote za Bwiru (Msingi, Kati na Sekondari) zilikuwa na mashini yake ya kuvuta. Hata hivyo, hapo Bwiru (Wavulana) mazingira ya vyoo hayakuwa mazuri kwa sababu ya kungoja matanki ya maji ya kuvuta (“cistern”) yajae”. Na wakati wa “heavy traffick”, mifereji iliziba; na wakati mwingine maji machafu yalijaa na kufurika siku kadhaa kabla ya kuwasili kwa gari la kufyonza uchafu (cesspit emptier) huo. Mazingira ya shule yalinukwa kwa harufu mabaya. Gari lilimwaga uchafu huo popote hapo milimani!
  Inafaa sana izingatiwe kuwa niyaandikayo sana sana ni ya kati ya mwaka 1960 na kumalizikia mwaka 1963 hapo Bwiru (Wavulana) – sizungumzii kwa ujumla ya shule zote za serikali. Hata ya miaka ya nyuma au baadaye hapo Bwiru (Wavulana) ni “outside the scope” ya hadithi hii; nawaachia wengine wayaandike, wakitaka. Ila katika hadithi itakayofuata nitamalizia na ya Tabora (Wavulana) ya wakati wangu.
  Ingawa sijaenda Bwiru (Wavulana) kwa muda mrefu, katika kuandika hadithi hii, simaanishi kuwa enzi zetu tuliishi katika “paradisiacal” mazingira. La hasha! Pamoja na mapungufu ya Bwiru (Wavulana), kama hadithi hii itakavyozidi kuelezea hapo baadaye, tulikazana sana tufaulu na kufuzu.
  Wakati huo, shule ilikuwa haishindani na mazingira mengine ya “vya usasa” katika kuleta mabadiliko maishani. Pengine hili linahitaji mada tofauti, na niliwahi kulizungumzia katika mfululizo wa maandishi yangu juu ya Kuporomoka kwa Maadili Mema kwa Vijana Wetu (gazeti la KwanzaJamii lililokufa).
  Msomaji, ni matumani yangu kuwa waendelea kufurahia “excursionary travelogue” hapo Bwiru (Wavulana) ya wakati wangu (1960-63). Leo tutaendelea kuangalia mambo matano: Mosi, dereva, wapishi na mlinzi wetu wa usiku. Pili, ya “The Oliver Twist School” - mgomo wa tatu nilioshiriki. Mgomo wa kwanza ulikuwa ni hapo Ikizu Middle School wakati wanafunzi kumi tulipogoma kuendelea na masomo ya sekondari katika shule za wa-Sabato. Mgomo wa pili ulikuw nilikataa kubatizwa. Tatu, harakati za kudhibiti siasa na uchumi hapo Mwanza. Nne, mwanafunzi wa Bwiru (Wavulana) alivyoshinda Brooke Bond Tea Literary Competition na kutembelea Uingereza kwa muda wa mwezi mmoja. Tano, Bwiru (Wavulana) daima itamkumbuka Mwalimu Frank Mitchell.
  Katika orodha yetu, tulimalizia na nambari kumi.
  Kumi na moja, kidogo, nisimulie ya dereva, wapishi na mlinzi wetu wa usiku. Bwiru (Wavulana) ilikuwa na dereva wetu mashuhuri, Bwana Manugwa, ambaye tulimpenda kwa umahiri wa kuendesha ki-gari chetu kidogo kizee cha “van” (rangi ya kijani – kama yalivyokuwa magari yote ya serikali) kilichokuwa wazi, kabla ya shule kuletewa lori kubwa, kama walilokuwa nalo Bwiru (Wasichana). Dereva Manungwa hakuwa mtanashati, kama alivyokuwa mwenzake, Adam wa Bwiru, wa Bwiru (Wasichana).
  Dereva Manugwa alitupeleka kwenye vituo vya mabasi, bandari ya meli na stesheni ya treni wakati wa kwenda likizo au kutuchukua kutoka likizoni; kupeleka wagonjwa Hospitalini; kupeleka wachezaji michezoni na kwenye makomangano mjini Mwanza na vitongoji vyake.
  Wakati mwingine dereva Manugwa alipuuzia alama za trafiki na sheria zake bila kukamatwa. Nafikiri, aliujua uzembe wa ma-Afisa wa Trafik, kwa upande mmoja. Alipuuzia pia kutokana na gari hilo kubeba wanafunzi wa shule ya serikali, kwa upande mwingine. Dereva Manungwa alikuwa akihatarisha maisha yetu. lkini hatukujali!
  kwa mfano, kama kulikuwa na gari lingine mbele, hasa la Bwiru (Wasichana), tulimchokoza, “Potea Manungwa”! Aliweza kupotea kwa mwendo wa kasi na kuyaacha magari mengine mavumbini huko kwenye barabara ya Bwiru mlimani na ya lami – Makongoro Road (Kiwanja cha Ndege-Mwanza Mjini) au Tabora Road kuelekea sehemu za Butimba TTC, Nyegezi Seminary, Rosary College na Nsumba Sekondari.
  Tulikuwa na wapishi kama wanne hivi – maarufu walikuwa wazee Ndege na Reli. Wapishi wote walikuwa wanywa gongo na “mapuya” sana. Licha ya ulevi huo, walikuwa ni “very fatherly.” Na mara nyingine walikuwa wakilala katika stoo ya vyakula ili wasichelewe kuandaa ujiwa asubuhi.
  Mwenye machachari na ukali alikuwa ni mlinzi wetu wa usiku – mzee m-Kuria, mnywa gongo kama maji! Tulimpachika jina la “Kukuru Kakara”, kaulimbiu aliyopenda sana kuitumia wakati akiwa kazini. wakati wa kuzima taa (“lights out”), alisika akiungunguruma saa nne za usiku, “Kukuru kakara, saa ya kurara sasa!”
  Wakati mwingine “Kukuru Kakara” alipenda kufukuza wanafunzi waliokuwa wamezoea kuamka kwa siri usiku saa tisa na nusu hivi kujisomea madarasani kwa mwanga wa vibatari/vikoroboi, hususan wakati wa mtihani ukaribiapo.
  “The Oliver Twist School”
  Kumi na mbili, kulikuwa na “Bwiru” nyingi: toka Darasa la 1 hadi 12 (wavulana na wasichana). Mtoto aliyezaliwa hapo Bwiru aliweza kumaliza Darasa la 12 akingali katika mazingira ya Bwiru.
  Mwaka 1962, moja ya hizo “Bwiru” - Bwiru (Wavulana) - tuligomea chakula. Gazeti la Kiingereza (The Tanganyika Standard) lilituhurumia na kuandika habari za mgomo huo kwa kichwa cha habari, “The Oliver Twist School’, kuufananisha na hadithi ya Oliver Twist iliyoandikwa na Charles Dinkens – juu ya mustakabali wa watoto yatima na masikini walivyokinyanyaswa, kuchapwa viboko na kuteswa katika mazingira magumu ya mapinduzi viwandani huko Uingereza.
  Katika hadithi hiyo, huku akitetemeka na kushikilia bakuli lake la chakula, mtoto Oliver alimwendea Mkuu wa Shule kuomba aongezewe chakula: “Please, sir, I want some more.”
  Tuliandaa mgomo kwa sababu kiasi cha chakula - uji, ugali na maharage, nyama, samaki na wali (“kitee”) na “la juu” (mafuta ya mawese) - tulichokuwa tumezoea kukipata kilianza kupungua sana. Uongozi wa shule haukutuarifu kwa nini kulikuwa na uhaba wa chakula; hivyo, tukagoma, mithili ya Oliver, “Please, sir, we want some more.”
  Nafikiri sababu ya kupunguka kiasi cha chakula ilitokana na kuongezeka kwa mitaala miwili miwili tangu Darasa la 9 (1960) bila kuongeza mapesa. Kwani sio Bwiru (Wavulana) tu iliyogoma mwaka huo; shule za sekondari nyingine (Old Moshi na Tosamaganga) nazo ziligoma, kama sikukosea.
  Ma-Prefekti wa zamu siku hiyo ya mgomo, ambamo kila mwanafunzi alishiriki, walikuwa kutoka Speke House: Silas Mayunga na Msaidizi wake Ali Hussein Magomasi. Badala ya kwenda mstarini kukaguliwa (kabla ya kuingia madarasani), tulielekea upande mwingine karibu na Mess Hall na wengine kupotea milimani. Mwalimu wa Zamu aliduwaa tu kutuona tunazila ukaguzi, kabla ya Hedi Prefekti Pamba Masyole (m-Kerewe) kumtaarifu juu ya mgomo.
  Mkuu wa Shule A.R. Thompson, aliyeshika nafasi ya Bwana Mull, alitaarifiwa na kuitisha mkutano wa walimu mara moja. Kuona walimu wanajifungia mkutanoni, tulianza kutembea kuelekea mjini ili kutoa kilio chetu mbele ya Mkuu wa Mkoa (Elimu).
  Baada ya mwendo wa kama nusu saa hivi, walimu wa-Matumbi wawili (Venables B. Mtabi na Methuselah Kishosha) walitufuata ndani ya gari dogo aina ya Popular la Mwalimu m-Amerika Frank Mitchell. Walitupita; na mara wakasimama. (Nitasimulia msaada wa baadaye wa Mwalimu Frank Mitchellkwa shule yake hiyo ya zamani mwishoni).
  Mwalimu Methuselah Kishosha alitusihi turudi shuleni kuyazungumza. Ubishi ukawaka moto. Kitambo, Hedi Prefekti akatusihi tuwatii hao walimu wetu wa-Matumbi. Tukarudi shuleni.
  Kurudi shuleni, tuliambiwa kukaa hapo shuleni bila kufanya fujo bila kubaini kuwa Mkuu wa alikuwa ameishamwarifu Mkuu wa Mkoa (Elimu), ambaye alimpa maagizo ya kuturudisha shuleni hadi tusikie kutoka kwa Waziri wa Elimu (Waziri Solomon Nkya Eliufoo, MP) na Kamishina wa Elimu (Bwana Dunstan Omari), Dar es Salaam!
  Mara ujumbe ukafika. Akizingatia kuwa huo mgomo haukumlenga yeye (Bwana Thompson, kama Mkuu wa Shule) bali ulilenga serikali yetu huru, Mkuu wa Shule aliitisha mkutano na kutamka maneno makali, mithili ya mbogo mkali, kama ifuatavyo:
  “You have decided to go against your own government. The warning message from your government is that you will all be sent home; and home you will go, immediately! Your warrants are being prepared. Go and pack your belongings ready to go home!”
  Huo ujumbe haukuingia vizuri ndani ya masikio ya baadhi yetu na kusababisha Mkuu wa Shule kurudia kwa ukali:
  “Disperse to your dorms to pack up your belongings! After packing, you must all come to the Office for your return travel warrants to your respective homes! The school is closed until the start of the next term!”
  Tulitawanyika kama vifaranga kwa unyonge mkubwa! Tulikuwa tumebakiza mwezi mmoja wa kumaliza nusu muhula wa shule. Tulipewa hizo “return travel warrants” na kujipa moyo kuwa wote tutarudishwa.
  Kwa kawaida sisi kutoka Mkoa wa Mara tulikuwa tukisafiri kwa meli - wakati huo meli mpya kabisa ya MV Victoria. Lakini siku hiyo sisi kutoka Mkoa wa Mara tulisafirishwa kwa njia ya basi la kampuni ya Tanganyika Bus Services hadi mjini Musoma, na hapo baadaye, kujipakia kwa mabasi yaliyotupeleka hadi nyumbani kwetu. Na wa kuelekea sehemu za Kwimba na Shinyanga walikuwa wakisafiri kwa treni. Siku hiyo walipelekwa kwenye stesheni kupanda treni lililokuwa lisafiri siku hiyo, na hapo baadaye wapande mabasi hadi majumbani kwao.
  Wazazi wangu walishangaa kuniona nimewahi kuja nyumbani. Kabla ya kuniuliza kisa cha kuwahi, nilidakia kuwaambia kisa chenyewe. Kumbe walikuwa tayari wamepata habari kupitia redio juu ya kufukuzwa kwetu.
  Kwa ukali, Mama alinijibu, “Tulikupeleka Bwiru kusoma; sio kugoma”!
  Nilikaa hapo nyumbani kwa mapumziko marefu ya miezi miwili (“likizo ya kufukuzwa”) na kurudi shuleni kumalizia muhula uliobakia na mwisho wa mwaka. Chakula kili-“improve” sana baada ya huo mgomo!
  Kumi na tatu, mwaka ulioanza, m-Matumbi wa kwanza Bwana Venables B. Mtabi alichaguliwa kuwa Mkuu wa Shule badala ya Bwana A.R. Thompson aliyepewa uhamisho kwenda Makao Makuu ya Wizara ya Elimu, ambako alishughulikia suala la kutunga muhtasari wa kufundisha Historia (Mafunzo ya Ualimu).
  (Tulimkuta Bwana A.R. Thompson mwaka 1966 Institute of Education, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akifundisha jinsi ya kufundisha Somo la Historia kabla ya kufunga virago vyake na kurudi kwao Uingereza.)
  Kumi na nne, niliona michezo ya maajabu ya sarakasi kwa mara ya kwanza hapo Mwanza (1960). Kundi la Circo Brasil lilikuja kutumbuiza hapo kwenye sehemu ya Kirumba (Uwanja wa Mpira wa sasa): mapikipiki ya kasi ndani ya tufe la chuma, temb waigizaji, na kadhalika. Kila mara Circo Brasil iliwatumbuiza watazamaji kwa nyimbo mbalimbali. Wimbo uliotia fora ulikuwa ni ule wa Marina (fungua Youtube uusikie).
  Kumi na tano, Mwanza ilivuma wakati huo, ki-siasa na ki-uchumi. Sana sana, ki-siasa kati ya Tanganyika African National Union (TANU) ya Julius Kambarage Nyerere (siasa za utaifa wa Mseto) na African National Congress (ANC) ya Zuberi Mwinshehe Manga Mtemvu na mzee mmoja kwa jina Saidi Chamwenyewe (siasa za u-taifa wa Mwafrika), ambao walikuja kwa nyakati tofauti kuhutumbia wananchi wa mji wa Mwanza hapo kwenye Uwanja wa Kirumba; na siasa kali za u-Temi kujiunga na siasa mpya au hapana wakati wa-Koloni wakiwa na njama zao za kuunda Temi kubwa kupitia sera ya kuwa na Paramount Chief huko u-Sukumani, kama walivyofanya huko u-Chaggani.
  Zaidi, ushirikiano kati ya siasa na vyama vya ushirika na jinsi TANU ilivyopiku wanachama wa Chama cha Ushirika cha Victoria Federation of Cooperative Unions (VFCU) - vyote vikajikuta vinakabiliana na adui mmoja (kisiasa na ki-uchumi); kuzuka kwa chama kingine cha siasa kilichoanza kama cha ushirika kupambana na VFCU; siasa kali za TANU huko Geita zilizoleteleza FFU kuingilia kati, mbali ya woga wa “Mau Mau” mpya; na siasa za mfumo wa ui-ubaguzi (“tripartite system”): wa-Ulaya (thamani 3); wa-Hindi (thamani 2) na wa-Matumbi (thamani 1).
  Hakuna utafiti wenye kuelezea mchakato huo wa siasa na uchumi kama wa G. Andrew Maquire, ambaye alifanya utafiti huo tukiwa Darasa la 10 na kuwahi kututembelea kwa mwaliko wa Mwalimu Bob Amos, m-Amerika mwenzake. Baadaye, Bwana Maguire aliandika utafiti huo kama kitabu, Towards Uhuru in Tanganyika: The Politics of Participation (Cambridge University Press, 1969).
  Ki-uchumi (retai trade – dukawalla), Mwanza ilikuwa ya wa-Hindi, kwa mifano, familia za Patel, Chopra na wengineo. Familia ya Chopra ilikoga na kuranda barabara za Mwanza kwa magari mawili ya fahari aina ya Royce-Rolls pamoja na moja la Mzungu wa Schumann’s Garage. Wengi wa wa-Hindi matajiri wa Tanganyika ya wakati huo walijiunga na TANU na kukisaidia kwa mapesa: Chopra na Patel (wa Mwanza), Amir Habib Jamal, Mahmoud Rattansey, Karimjee Jivanjee, Sophia Mustafa, Alnoor Kassam, Sir Chande (wa Tanga/Dar es Salaam), na familia nyinginezo.
  Mwanza ilikuwa pia ya wa-Ulaya wa migodi wakitokea Shinyanga, Geita na Kiabakari/Buhemba, Musoma. Wengine walifanya kazi East African Common Services Organisation iliyokuwa na Makao Makuu ya Utafiti wa Tiba, hasa kichocho (schistosomiasis).
  Nakumbuka wanafunzi kutoka sehemu za Usukumani wa Middle School na hapo shuleni kwetu walipimwa na kukutwa na kichocho. Walichaguliwa kupewa tiba-tafiti kwa kudungwa sindano. Matokeo yake wakaugua hoi kwa muda wa siku mbili hivi, hadi shule ikasimamisha tiba-tafiti hiyo!
  Wa-Ulaya waliishi hapo Capri Point, Bwiru Hills na sehemu ya Isamilo. Kulikuwa na vilima vya Pisii na Disii; nyumba zao zilijengwa hapo vileleni.
  Kumi na sita, wakati huo kusikia kuwa mtu kapigwa bunduki na kufa lilikuwa ni tukio la kutisha sana. Hata hivyo, mwaka 1960 huko sehemu za Malampaka, askari koplo mmoja wa Relwe mwendwazimu aliua watu watatu kwa bunduki ya Askari Jela wa wakati huo.
  Askari wa FFU wa West Lake, Mwanza, East Lake, Arusha na Western Province walijipanga kumsaka mtuhumiwa, Ambale Sichenga - m-Luhya wa Kenya – askari wa Relwe. Wakati huo Askari Polisi wa Relwe walikuwa wa Afrika Mashariki – waliweza kupelekwa kufanya kazi popote Afrika Mashariki.
  Shule ilitahadharishwa na kuomba kutoa habari mara moja kwa Polisi endapo mtuhumiwa angeonekana. Alionekana kajificha mstuni huko Malampaka; mapambano yakawaka moto. Mtuhumiwa alikamatwa baada ya kuishiwa risasi. Hofu ikaisha! Koplo Ambale Sichenga alihukumiwa kunyongwa.
  Brooke Bond Tea Literary Competition
  Kumi na saba, kila mwaka, Kampuni ya Chai nchini (Tanganyika Brooke Bond Tea Company) ilikuwa ikitayarisha mashindano ya kuandika insha kwa Kiingereza kwa Darasa la 11. Na kampuni–dada za Brooke Bond Tea nchini Kenya, Uganda na Zanzibar nazo zilikuwa zikitayarisha mashindano ya namna hiyo. Mshindi kutoka kila nchi alikuwa akipewa zawadi, zikiwa ni pamoja na safari ya kwenda Uingereza kwa utalii wa mwezi mmoja akiandamana na Mwalimu-Msindikizaji kutoka shuleni kwake.
  Mwaka wetu (Darasa la 11) tuliambiwa kuandika insha yenye kichwa, “The Importance of Drinking Tea” (yenye maneno yasiyopungua 500). Insha zetu zilisahihishwa kwanza hapo shuleni. Insha ya Kidollah Makani ilipata ushindi wa kwanza. Kidollah alizidi kuinoa kazi yake; na shule iliwasilisha insha-nolewa mbele ya Tanganyika Brooke Bond Tea Company na kushinda zawadi ya kwanza nchini Tanganyika mwaka huo.
  Ushindi wa Kiodollah Makani ukawa ni wa Darasa la 11 - Mwaka 1962 Bwiru (Wavulana)! Ushindi kwa Bwiru (Wavulana) Mwaka 1962! Ushindi kwa Mkoa wa Mwanza Mwaka 1962! Kwa muda wa miaka mingi, Tabora (Wavulana) ndio ilikuwa inaongoza kwa ushindi.
  Kidollah Makani na Mwalimu wa Hesabu Venables B. Mtabi (Mkuu wa Shule Msaidizi) waliongozana hadi Uingereza na kurudi kutusimulia ya safari yao.
  Bwiru (Wavulana) Daima Itamkumbuka Frank Mitchell
  Napenda kuhitimisha kwa mchango wa Mwalimu Frank Mitchell kwa Bwiru (Wavulana), shule yake ya zamani. Nilipofika hapa Amerika (1975), nilijitahidi kuwatafuta hao walimu wetu wa-Amerika waliotufundisha enzi hizo hapo Bwiru (Wavulana). Wawili walikuwa ni wa kundi la “Teachers of East Africa” : Bob Amos na Frank Mitchel. Wengine walikuwa ni wa kundi la US Peace-Corps: Bruce Levine, Berkowitz na wengineo.
  Nilifanikiwa kuwasiliana na kukutana na mwalimu wangu wa zamani, Frank Mitchell (aliyekuwa Mwalimu Biolojia). Alikuwa akifundisha hapo Ohio State University. Mwalimu Frank alifurahi sana kukutana nami. Tulibadilishana ya maisha ikiwa ni pamoja na kumtaarifu kuwa mmoja wa wanafunzi wake (Mwalimu Phillip Mussa) ndiye alikuwa Mkuu wa Shule. Mwalimu Frank aliahidi kuitembelea shule yake hiyo ya zamani.
  Zaidi, tulijadili jinsi ya kuisaidia Bwiru (Wavulana) kwa kuipatia vifaa vya komputa na kuiunganisha shule yetu hiyo ya zamani kwa Internet. Niliwasiliana na (na kupata ushirikiano wa) Mkuu wa Shule Mwalimu Phillip Mussa (tuliyekuwa naye darasa moja) kumweleza juu ya ka-projekti hako na jinsi ya kukafanikisha kwa kuingiza vifaa vya komputa bila ushuru.
  Kutokana na habari kutoka kwa Frank, mpango huo ulifanikiwa mwaka 2005 wakati alipotembelea shule yake hiyo ya zamani na kutoa zawadi za komputa na “internet connection” kwa Mkuu wa Shule - wakati huo, Mr. Elia Kissuu. Lakini sijui sasa mambo yakoje!)
  Picha zifuatazo (zinapatikana http://www.tea-a.org/ - angalia upande wa Schools/Tanzania) ni kutokana na juhudi za kukutana kwangu na Mwalimu Frank Mitchell:
  Bwiru Boys: Mr. Frank Internet Cafe
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Mipangoni: Frank na Hedimasta Elia Kissuu
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Ujenzi wa Mapokezi ya Internet (Communication Tower)
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Mwalimu Frank Mitchell anabadilishana mawaidha na baadhi ya wananchi
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Wanafunzi wanafundishana ujuzi wa Internet
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Mwalimu gwiji anakagua baadhi ya kumputa zilizotolewa zawadi tayari kwa kazi
  Asante sana Mwalimu Frank Mitchell!
  Msomaji mpendwa, karibu tunafikia mwisho wa safari. “Leg” yetu ya mwisho itaangalia ya “utoto” – wakati mwingine wanafunzi tunatenda vi-ji-mambo vya ajabu ajabu tu, kama watoto wadogo; mwenzetu alivyopata skolashipu kusomea u-Daktari Algeria; Mtihanii wa Cambridge School Certificate “Ordinary Level” wa Kumaliza Darasa la 12 na uteuzi wa kuingia Darasa la 13 bila majibu kutoka Cambridge; na ya kujiunga na kuhitimu Tabora (Wavulana), kwa kifupi tu.
  E-mail: [email protected]
  CHANZO: Kwanzajamii.com
   
 9. S

  Sumaku Senior Member

  #9
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ( Part 1, 2, 3 na 4 kwenye kwanzajamii.com)


  Msomaji mpendwa, tulianza na ujumbe mfupi kuhusu elimu nchini uliotilia mkazo kwa wanafunzi wahitimu kuanzisha na kuendeleza huduma za alumna kwenye mashule yao popote pale nchini (msingi, kati, sekondari na chuo cha juu); na kuwataja baadhi tu ya wanafunzi waliofuzu hapo Shule ya Sekondari Bwiru (Wavulana) miaka ya 1959 hadi 1964. (Picha zao hazikutokea; bado nafikiria, ki-ufundi, namna ya kuweza kufanikiwa kuzitundika.)
  Zaidi, jinsi nilielezea jinsi nilivyowakimbia wa-Sabato (Ikizu Middle School of Seventh-day Adventists -SDA), Musoma, East Lake Province (wakati huo); wanafunzi wenzetu walivyozuiliwa kuandika Mtihani wa Darasa la 8 hapo Ikizu Middle School mwaka 1959; kujiunga kwangu na Bwiru (Wavulana); mchakato au mkakati wa uhuru wa kuabudu hapo shuleni; ya masomo na “debating societies”, kwa kifupi tu; na burudani - hafla za densi, “makombora”, “wakamba”, “mauno”, “milongo”, na kadhalika.
  Pia, tuliendelea kuyaona ya mgomo wa tatu nilioshiriki (mgomo wa kwanza ulikuwa ni kukataa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule za wa-Sabato na wa pili ulikuwa ni kukataa kubatizwa hapo Ikizu Middle School); dereva, wapishi na mlinzi wetu wa usiku hapo Bwiru (Wavulana); ya “The Oliver Twist School” - mgomo wa tatu nilioshiriki; harakati za kudhibiti siasa na uchumi hapo Mwanza; mwanafunzi wa Bwiru (Wavulana) alivyoshinda Brooke Bond Tea Literary Competition na kutembelea Uingereza kwa muda wa mwezi mmoja; na Bwiru (Wavulana) daima itamkumbuka m-Amerika Mwalimu Frank Mitchell.
  Pengine, wengine watauliza kwa nini nmemchagua Mwalimu Frank Mitchell? Kila baada ya Jumapili mbili, Mwalimu Frank Mitchell alikuwa anatuwezesha kuona picha za sinema alizokuwa akiagiza kutoka Goldwin-Mayers, Nairobi; alileta vitabu (vya picha) vya ziada kwa ajili ya somo lake la Baiolojia nah ii ilituwezesha sana kuelewa somo hilo; na mara nyingi, alitukaribisha kunywa soda na biskutii hapo nyumbani kwake.
  Zaidi, alitujaza ndani ya ki-gari (Popular) chake wikiendi tukitoka mjini ili tusichelewe “roll-call” shuleni. Ki-gari chenyewe kilichokuwa hakina “starter”. Kilihitaji kusukumwa au kuegeshwa kwenye mteremeko na kudhibitiwa kwa “handbrake” ili ikiondolewa, kinajisukuma mbele na kuanza “kuwaka”, tayari kwa mwendo. Mwisho, Mwalimu Frank Mitchell alituzawadisha baadhi yetu tuliofuzu mwaka 1963 kila mmoja Kamuzi ya Kiingereza.
  Kutokana na mapenzi yake kwa Bwiru (Wavulana), Mwalimu Frank Mitchell alijitolea kuitikia mwito wangu wa kutaka kuisaidia shule yetu hiyo ya zamani kwa kuweka Intenet hapo shuleni. Baada ya mazungumzo yetu, Mwalimu Frank Mitchell aliniomba nimwachie huo mradi na yeye atajaribu awezavyo kuhakikisha kuwa Bwiru (Wavulana) inapata Intenet.
  ————–
  Msomaji mpendwa, mambo manne yafuatayo leo yanatufikisha mwishoni mwa safari yetu, ambayo kweli imekuwa “an excursionary travelogue” hapo Bwiru (Wavulana) ya wakati wangu (1960-63):
  Mosi, ya “utoto” – wakati mwingine wanafunzi tunatenda vijimambo vya ajabu ajabu tu, kama watoto wadogo. Pili, mwezetu alivyopata skolashipu kusoma Algeria. Tatu, Mtihani wa Cambridge Kumaliza Darasa la 12 (Cambridge School Certificate “Ordinary Level”) na uteuzi Darasa la 13 kabla ya majibu kutoka Cambridge. Nne, kujiunga kwangu na Tabora School (Wavulana), kwa kifupi.
  Kwenye orodha ya matukio, tulimalizia nambari kumi na sita.
  Ya “Utoto”
  Kumi na saba, Bwiru (wavulana) ilikuwa na visa vyake vya “utoto”. Kwa mfano, tukiwa Darasa la 12 baadhi yetu tuliwachukia ma-Prefekti tuliowaona kuwa ni wakali na wenye kujikomba kwa Walimu: Reuben Matango (Hedi Prefekti) na Isaac Chitama (Msaidizi aliyekuwa pia Prefekti wa Grant House). Ma-Prefekti walikuwa waliteuliwa na walimu. Walitekeleza matakwa ya walimu zaidi kuliko ya wanafunzi wenzao.
  John Williams, Hussein Bakari Mbaruku, Charles Mashala, Joel Mabhibha, Mathew Henge, Adamu Marwa, Amos Petro Dabana na mimi tuliazimia kuwakomoa kwa kuwaadhibu kwa mlo siku moja. Siku hiyo ilipofika, baadhi yetu tulikuwa ni ma-“Orderlies” wa kugawa chakula. Tulijua sahani na mabakuli ya Reuben Matango na Isaac Chitama. Tuliwawekea ukoko tu wa ugali wa mahindi tuliobandua na mchuzi wa maharage bila maharage ndani!
  Reuben na Isaac walijua ni nani walifanya kitendo hicho cha chuki. Wakatushitaki kwa Wakuu wa Shule (Hedmasta Mtabi na Msaidizi wake Mwalimu Kishosha). Tuliitwa mbele ya Wakuu wa Shule kujitetea.
  Tulipoingia tu Ofisini, Wakuu hao walishangaa sana kutuona. Kisa: Hawakufikiria kuwa wanafunzi kama sisi tungeweza kupanga na kutekelza njama za chuki na katili. Tulikuwa ni baadhi ya wanafunzi wenye nidhamu nzuri hapo shuleni! Zaidi, tulikuwa tukiongoza darasani – wote tulikuwa Darasa la 12-A!
  Msaidizi wa Mkuu wa Shule, Mwalimu Methusellah Kishosha alitukaripia, “Waone hawa! Kwanza, baadhi yenu tumeishawateua kuingia Darasa la 13. Mnataka kujiharibia?”
  Mkuu wa Shule Mwalimu Mtabi alidakia, “Tokeni mbele yetu mara moja! Nendeni mkawaombe msamaha Matango na Chitama!
  Tulienda kuwaomba msamaha hao ma-Prefekti kwa shingo upande. Yakaisha.
  Mwezetu Apata Skolashipu Kusoma Algeria
  Kumi na nane, kabla ya mwisho wa mwaka, serikali ya Tanganyika ilipewa skolarashipu 10 na serikali ya Algeria ya Rais Ben Bella ili kuwawezesha wanafunzi kusomea u-Daktari. Kutoka Bwiru yetu Zakayo M. Igenge alichaguliwa. Hatukulalamika; Zakayo alistahili tuzo hiyo.
  Zakayo alikuwa anapenda sana Masomo ya Sayansi, hususan, Kemia na Baiolojia. Tulikuwa tukimtania kuwa anaweza kukariri chapta zote za kitabu cha Kemia kilichokuwa kimeandikwa na mtaalamu Mee)! Wengine mnakumbuka The Table of Elements!. Zakayo Igenge alikariri hiyo orodha karibu yote!
  Zakayo alikuwa na tabia ya kuamka kila usiku saa tisa na nusu hivi ili kuanza kujisomea kwa ki-koroboi chake. Kila mara alifukuzwa na mlinzi wetu wa usiku, mzee Kukuru Kakara. Lakini wengine tulikuwa tunapenda sana kuendelea kuukata huo usingizi bila kuvutwa na huko kujisomea!
  Tulimuaga Zakayo M. Igenge na kumtakia kila heri huko uhaibuni Algeria.
  Kwa bahati mbaya, mwaka 1965 Ben Bella alipinduliwa ki-jeshi na Jenerali Houari Boumedienne. Wanafunzi wote wa Tanganyika wakarudishwa nyumbani. Kwa kuwa wengi walikuwa hawakumaliza Darasa la 12, iliwabidi warudie darasa hilo!
  Nipohitimu haopo Mlimani mwaka 1970, Zakayo M. Igenge alikuwa, nafikiri mwaka wa pili hapo Muhimbili, akichukua masomo ya u-Daktar. Alifanikiwa kufaulu u-Daktari na leo hii ni Mkuu wa Idara ya Emergency Medicine hapo Hospitali ya Bugando, Mwanza (fungua: http://www.bugandomedicalcentre.go.tz/emergency.htm), kama picha hiyo hapa chini inavyoonyesha akiwa kazini:
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Dk. Zakayo M. Igenge akiwa kazini
  Mtihani na Uteuzi Darasa la 13 Kabla ya Majibu Kutoka Cambridge
  Kumi na tisa, wakati ulifika wa kuandika Cambridge School Certificate “Ordinary Level” mwezi wa Novemba. Tukiwa katikati ya kumaliza mtihani, siku moja asubuhi Mwangalizi wa mtihani Mwalimu Bob Amos (m-Amerika) aliwahi kuja katika Chumba cha Mtihani a kutuarifu kuwa siku hiyo hangeweza kusimamia Mtihani.
  Tulibakia na mshangao mkubwa wa kutaka kujua kulikoni. Tulifikiria, pengine, katimuliwa. Lakini alitueleza kuwa ilikuwa ni kutokana na kuomboleza kifo cha Rais wake (John F. Kennedy) aliyepigwa risasi huko Dallas, Texas.
  Pia, wakati ulifika wa kutaka kujua ni nani walioteuliwa mapema kuingia Darasa la 13. Kilamwanafunzi akawa anaitwa mbele ya Mkuu wa Shule na Msaidizi wake aliyekuwa aki-“double” kama “Careers Master” wetu.
  Ikafika zamu yangu. Kuingia tu, “Careers Master” wetu aliniuliza, kwa utani, “Na wewe unakuja hapa kufanya nini?”
  Kabla ya kumjibu, akaongezea, “Kwanza, tueleze unataka kufanya nini baada ya Darasa la 12?”
  Nikawajibu, “Sana sana, ninataka kuwa rubani wa ndege. Kwahiyo, ninataka kujiunga na East African Airways Corporation. Pili, kama uchaguzi huu wa kwanza hautafaulu, ninataka kuingia Jeshi la TR (Tanganyika Rifles).
  Akaniuliza, kwa mshangao mkubwa, “Rubani wa ndege, kwa nini? Utawezaje kuingia Jeshi na huku bado ni mtoto mdogo!? Tumekuchagua kwenda Tabora School. Kwaheri!”
  Wanafunzi tuliokuwa tunatoka Mkoa wa Mara (Christopher Mbotte Nyirabu, Donatian Mwita, Thomas Kiboko, Adamu Marwa, Reuben Matango na Chorwa Mgonche Wambura) tulitaka kujiunga na Tanganyika Rifles. Lakini ni Chorwa Mgonche Wambura tu aliyejiunga na Jeshi (Kikosi cha Maji). Wengine tulikataliwa ili tuweze kuendelea na High School.
  Baada ya mkutano huo, ilibainika ni akina nani waliochaguliwa: Kidollah Makani (Kahororo Secondari), John Williams, Mathew Henge na Hussein Bakari Mbaruku (Mkwawa), Charles Mashala na Amos Dabana Petro (Minaki), Christopher Nyirabu, Donatian Mwita na mimi (Tabora).
  Baadhi ya wanafunzi wenzetu wa darsa la 12-A hawakupendezwa na uteuzi huo kwa sababu mmoja wa kutoka Darasa la 12-B hakustahili kabisa kuchaguliwa. Waliuona uteuzi huo kuwa wa upendeleo kwa kuwaacha wengi wa wanafunzi waliostahili na kumchagua huyo mwenzetu.
  Baada ya matokeo ya kutoka Cambridge, wanafunzi wenzetu wengine nao walichaguliwa kuingia High School: Thomas Kiboko (Tosamaganga), Sylivester Lugangiza Chanilla (Mkwawa) na Adamu Marwa (Aga Khan Dar). Walobaki, walijiunga penginepo kufanyakazi.
  Kwa machozi, tuliagana na tuliiaga Bwiru (Wavulana) na mzingira yake, ambayo kwa muda wa miaka minne ilikuwa ni “temporal space” huku baadhi yetu tukijua kuwa mlango wa Darasa la 13 ulikuwa wazi tayari kutupokea; na tulikuwa tunakwenda shule gani. Tulijihakikishia kuwa ya Mungu mengi na milima haikutani lakini binadamu hukutana. Lakini hatukujua endapo kweli tutakutana wapi na lini. Kuagana huko kulinikumbusha jinsi tulivyoagana tulipomaliza Ikizu Middle School.
  “Incidentally”, tuliojiunga na Darasa la 13, tulikutana tena Mlimani, isipokuwa Charles Mashala (alijiunga na Mwadui Diamond Company), Mathew Henge (alijiunga na Usalama wa Taifa), Sylvester Lugangiza Chanilla (alijiunga na BoT) na Hussein Bakari Mbaruku (alijiunga na Barclays Bank).
  Ya Tabora School kwa Ufupi
  Mjengwa alidokeza juu ya maisha yangu hapo Tabora (Wavulana). Nitaendeleza kwa kifupi tu.
  Ishirini, tulijiunga na Tabora (Wavulana) wakati wa maasi ya Jeshi la Tanganyika Rifles (TR)! Baada ya muda mfupi, kati ya ma-Afisa wa Jeshi la Wananchi la Ulinzi walioletwa hapo Tabora Barracks (Mirambo ya sasa) walikuwa ni Silas Mayunga – tuliyekuwa naye hapo Bwiru (wavulana) - ambaye alikuwa amemaliza mafunzo yake huko Israel na afisa mwenzake Mahende. Ma-Afisa hao walitufanya tujione si wageni sana hapo mjini Tabora, mji wa Kiko Kids na Unyanyembe (Tabora) Jazz Band!
  Tulipofika tu Tabora, tulikuta wanafunzi kutoka Bwiru (Wavulana) wakitafutwa sana na Walimu waliokuwa wakifundisha Somo la Kiingereza. Walidhani kuwa Kidollah Makani, aliyeshinda insha ya Kiingereza ya Brooke Bond Tea Company, angejiunga na Tabora (Wavulana) – shule ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ikitoa washindi wa mashindano hayo.
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Kidollah Makani
  Tulimwambia mmoja wa Walimu hao kuwa mwenzetu Kidollah Makani alichaguliwa kwenda Kahororo High School, Bukoba. Mwalimu huyo alibaki na mshangao mkubwa. Walimu hao walitaka wakutane naye kumshauri ki-taaluma achukue Principal ya Kiingereza. Kulikuwa na tetesi kuwa shule ilijaribu kumhamisha Kidollah Makani aje hapo Tabora (Wavulana) lakini haikuwezekana.
  Zaidi, tulikuta sifa nzuri zikivuma za kaka zetu kutoka Bwiru (Wavulana) waliotutangulia hapo Tabora (Wavulana): Joseph Warioba, Nimrod Lugoe, Asaph Maradufu, Joshua Opanga na William Mahalu. Hiyo ilikuwa ni changamoto kali kwetu jinsi ya kuvaa viatu walivyoacha.
  Tulishangaa kuona kuwa mwaka uliotutangulia haukutoa hata mwanafunzi mmoja kwenda Tabora Boys School! Natumaini mwaka huo hawakufanya vizuri.
  Na wakati tunajiunga na Mlimani, hakukuwa na mwanafunzi wa Bwiru wa mwaka uliotutangulia, isipokuwa mmoja tu William Ng’ombe aliyekuwa hapo Muhimbili akichukua u-Daktari! Wanafunzi wengine wawili, Ali Hussein Magomasi (Australia) na Mansur yahya Hussein – mdogo wa mnajimu Yahya Hussein (u-Rusi) walipata skolashipu, kama nilivyoonyesha.
  Ishirini na moja, baadhi ya wanafunzi wenzetu walikouwa mbele yetu Darasa la 14 walikuwa:
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Emmanuel Asajile Mwambulukutu Mwalimu/DDD)/Director of Manpower and Administration- Ikulu/RDD/Mwenyekiti RTC/Mawziri Mdogo-Wizara kadhaa/Katibu Msaidizi (TANU Lumumba Makao Makuu)/m-Bunge/Mjumbe wa TANU-NEC/Balozi.
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  George H. Alliy - Mwenyekiti na Mkuu wa TANconsult Ltd.
  Wengine wachache walikuwa ni akina Grant Mwakatundu, Mwambungu (jina la kwanza limenitoka), W.K. Parmena, Dr. Mhango (jina la kwanza limenitoka), Elisha (jina la pili limenitoka) na Meshack Maganga - Mkuu wa Shule ya Uandishi Habari.
  Ishirini na mbili, nilikutana na wanafunzi wenzangu wa-Sabato: Keto Mshigeni (Prof./Vice Chancellor kaigaruki University) aliyekuwa pia Bweni la Biscoe na mimi na Alphaxad Genya. Zaidi, kutoka Tabora (Wasichana) alikuwa ni dada yetu Hulda Stanley (Hulda Stanley Kibacha - baadaye m-Bunge wa Afrika Mashariki). Wote tulibatizwa Jumamosi moja hapo Kazima Dam!
  Wanafunzi wa mwaka wangu wengine walikuwa ni Peter C.T. Mayeye, Godfrey L. Kamukala, Augustine Ramadhani (Jaji Mkuu), Wilfred Mlay (Prof. Vice-President World Vision), Abel G.M. Ishumi (Prof. Elimu), Samuel Maselle (Prof./u-Daktari/Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Madawa wa Binaadamu), Idris Ali Mtulia (Prof./u-Daktari/m-Bunge), Bakari Lembariti (Prof./u-Daktari/Vice-Chancellor MUHAS), Bakari Ali Mbano (Prof./Wildlife Mweka), Mwandu (Daktari) na Michael Mhairwa (Agriculture/Businessman.
  Zaidi, James Kateka (m-Diplomasia/Balozi/Jaji wa Mataifa) na Augustine Ramadhani (Jaji Mkuu), Ali S.K. Mchumo (Mwanasheria/Balozi/Mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa), Martin Dewasi (Civil Enginner/Mkurugenzi TANconsult), Abdallah Ngororo (Mwanahabari/Katibu Mkuu-Wizara), Majebele (jina la kwanza limenikimbia), Mohammed Mfaume, Samuel Amolo, Archibald Kapote Mwakasungula (M-Malawi) na kijana mwingine m-Malawi – jina limenitoka) na Kagansha (jina la kwanza limenikimbia).
  Kagansha aliacha shule kutokana na ulevi wa “mapuya’ na kusakamwa na Hedimasta Partner. Kagansha aliyapenda “mapuya’ kiasi cha kubeba galoni imejaa hadi bwenini (Williams House). Siku moja, Kagansha laishitakiwa kwa Mkuu wa Shule Partner.
  kagansha aliingia ofisini.
  Kagansha alishindwa kujieleza vizuri. Ghafla, Bwana Partner alimfukuza kutoka ofisini mwake, “Get out of my office! You smell liquor, after all!”
  Kagansha alirudi bwenini na kufunga mizigo yake na kutuaga kwaheri. Baada ya muda alikuja hapo shuleni na akatwambia kuwa aliamua kujiunga na Jeshi.
  Wanafunzi tulichanganyika:
  Mosi, waliochukua Pure Mathematics, Applied Mathematics na Fizikia. Hao walijiunga kuchukua Uinjinia (Mechanica, Civil au Electrical) huko Nairobi University.
  Pili, waliochukua Kemia, Baiolojia na Jiografia. Kati yao walijiunga kuchukua Ualimu Dar es Salaam.
  Tatu, waliochukua Kemia, Baiolojia na Fiziki. Hawa walijiunga na Makerere na Dar es Salaam kuchukua u-Daktari. World Affairs/British Constitutution, African History na Jiografia. Wengi walipenda kuchukua Sheria Dar es Salaam, Ualimu au Digrii ya kawaida.
  Nne, wengine walichukua World Affairs/British Constitutution, African History na Kiingereza. Hao pia walipenda kuchukua Sheria.
  Tano, World Affairs/British Constitutution, African History na Jiografia. Hao walipenda kuchukua Digrii ya kawaida au Ualimu.
  Lakini cha ajabu ni kwamba tulipokwenda Mlimani watoto wa wakubwa na vigogo na waliokuwa marafiki zao hawakuchukua kozi ya ualimu. Na hata baadhi ya wale waliokuwa wamechaguliwa kuchukua kozi hiyo walibadilisha baada ya kufukuzwa na kurudishwa kutokana na Mgomo wa Oktoba, 1966. Ni watoto wa ma-Waziri wawili tu walioendelea na Kozi ya Ualimu: Said Muhaji (Waziri Mdogo – Elimu) na Waziri Steven Mhando (Mambo ya nNchi za Nje). Watoto wa wakubwa/vigogo hawachukui Ualimu!
  Msomaji, kuna picha chache za wenzangu wa Tabora (Boys) – 1964-1965, kama zifuatavyo:
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Prof. Samuel Maselle (mwenye mkoba mkononi) - Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Madawa wa Binaadamu
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  (Kushoto yako) Prof. Keto Mshigeni - Vice Chancellor – Kaigaruki University.
  (Kulia yako) Prof. Idris Ali Mtulia - Daktari/m-Bunge
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  (Kushoto yako) James L. Kateka - Jaji – The Hague UN Tribunal.
  (Kulia yako) Abdallah Ngororo (RIP) - Journalist/Permanent Secretary
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  (Kushoto) Prof. Wilfred Mlay - World Vision International Vice President.
  (Kulia yako) Godfrey L. Kamukala - Director General Tanzania National Environment Management Council/Senior Technical Advisor, Rwanda Environment Management Authority
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden. Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  (Kushoto yako) Augustine Ramadhani - Jaji Mkuu.
  (Kulia yako) Martin L. Dewasi - Director/Injinia TANconsult
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden. Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  (Kushoto yako) Ali S.K. Mchumo (Mwanasheria/Balozi/Mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa).
  (Kulia yako) Bakari Lembariti (Prof./u-Daktari/Vice-Chancellor MUHAS)
  Tabora (Wavulana) ilikuwa na mfumo wa kuchagua ki-demokrasia ma-Prefekti. Wanafunzi wenyewe waliwapigia kura wagombea. Lakini wakati mwingine, Mwalimu wa Nyumba (House Master0 aliweza kutumia kura yake ya veto kumkataa aliyechaguliwa, kama ilivyotokea hapo Biscoe House. Hapo Bwiru (Wavulana) walimu ndio walikuwa wakituchagulia ma-Prefekti. Wanafunzi tulikuwa tukichagua tu ma-Monita wa ma-Darasa.
  Hedi Prefekti wetu alikuwa ni Mwakasege (jina la kwanza limenitoka) akisaidiana na Martin Dewasi. Ma-Prefekti wa Nyumba walikuwa ni James L. Kateka, Samuel Maselle, Abdallah Ngororo, Christopher Mbotte Nyirabu, Mwandu, Munuo (hawa wawili majina yao ya kwanza yamenitoka), Augustine Ramadhani na mimi.
  Augustine Ramadhani na mimi tulikuwa ni ma-Prefekti wa Biscoe House. Ma-House Monita wetu walikuwa ni Kinyaga Msuya (Meja Jenerali) na Henry Clemens Orawia (Mkuu wa Wilaya), ambao walikuwa Darasa la 12 na akina Rajabu Bakari Mbano (ambaye anon wa Tue Jan 26, 07:43:00 PM EAT:mjengwablogspot.com) alitaka kusikia machache juu yake, Charles Mwandambo, James Mukoyogo (Daktari), Moses Maira (Wakili), Juma Kapuya (Prof./m-Bunge/Waziri) na Philipo Bwatondi (Prof.).
  Wakati tunaingia Darasa ala 14, wanafunzi wengine kutoka Bwiru (Wavulana) walikuja kujiunga na Tabora (Wavulana): Nathanael Mahunda (Mwanasheria na m-Diplomasia), Kalimiro Malagila (Mwanasheria), John Mynah (Electroniki Injinia) na Crispo Gunje (Injinia wa Ndege).
  Sana sana, hapo Tabora (Wavulana) ilikuwa eti ni “aibu kubwa” kwa wanafunzi wavulana wa ma-Darasa la 13 na 14 kunywa uji (au kwa ki-Jaluo, “nyuka”!) Tabia ambayo sisi wa kutoka nje tulianza kuiponda!
  Na hapo (Tabora Wasichana kulikuwa na dada zetu waliokuwa wametoka pia Bwiru Girls: Dinah Kanywa na Ester Nutting – ambao walikuwa na wenzao akina Getrude Makanza (Waziri/Balozi/Mbunge), Christine Kalua, Ngurukulu, Mboni Cheka (ex-M-Bunge), Estella “Shapiro” Amri, Blandina Mhando na Hulda Stanley (ex-m-Bunge EALA) – kwa kutaja wachache tu.
  Baada ya kuzizoea Tabora Boys/Girls, sikuona “fundamental” tofauti kubwa sana na shule za Bwiru Boys/Girls. Mazoea yakawa ni maendelezo ya burudani (hafla za densi, makomangano, na mabadilishano ya “makombora” (missiles), kuongozana (“processions” au kwa kifupi, “pros”) na wasichana kwenda na kutoka mjini siku ya Jumapili na kujificha kwenye busitani za machungwa, mapera na maembe (orchids).
  Wanafunzi wa Darasa la 9 na Darasa la 13 kutoka mashule mengine kutoka nje tuliitwa kwa jina la akina “mugya” au “the un-initiated into Taboraism)! Tofauti kubwa iliyojitokeza ilikuwa ni tabaka kati ya wanafunzi wa Darasa la 9-12 ma-“Juniors”, kwa upande mmoja, na wa Darasa la 13-14 (ma-“Seniors”), kwa upande mwingine.
  Ishirini na moja, mwaka 1965 serikali ilitaka kuanzisha shule ya Shinyanga Sekondari (Biashara) ikisaidiana na Mgodi wa Almasi (Williamson Diamond Company). Lakini kutokana na kuchelewa ujenzi wake, wanafunzi waliokuwa waanze Darasa la 13 iliwabidi waletwe hapo Tabora kwetu. Kuletwa kwa wanafunzi hao kiliniunganisha na wanafunzi niliowafahamu miaka ya nyuma: Elineema Ezekiel Mkono (Nimrod Mkono) na Pedael Mufungo Meli (Mufungo Mujaya).
  Ishirini na mbili, mwaka huo huo, Tanzania ilikuwa tayari kuanza mfumo wa chama kimoja, muundo wa Maendeleo ya Miaka Mitano na kuwa na Uchaguzi Mkuu chini ya chama kimoja. Mwaka huo tulijiandaa kupiga kura, mara yangu ya kwanza! TANU ilikuwa na wagombea wawili wa kiti cha mjini Tabora: Wakili Mahmoud Nasser Rattansey (m-Hindi) na m-Matumbi mzee Said (jina kamili limenitoka). Wakili Mahmoud Nasser Rattansey alishinda katika Uchaguzi Mkuu huo.
  Wakili Mahmoud Nasser Rattansey aliwahai kuwa mmoja wa watetezi wa Julius Kambarage Nyerere wakati wa kesi yake ya uchochezi na kashfa kwa ma-Disii wawili wakoloni. Mawakalili wengine walikuwa ni Denis Nowell Pritt, QC, (m-Uingereza) - aliyeletwa na chama cha Labour, aliyewahi kuwatetea akina Jomo Kenyatta na wenzake watano katika kesi ya Mau Mau na Ho Chi Minh wa Vietnam - na Kantilal Laxmichandi Jhaveri (m-Hindi).
  Ishirini na mbili, wanafunzi wengi mwaka 1964 tulihudhuria Maonyesho ya Biashara ya Saba Saba hapo mjini Tabora. Wanafunzi wengi wa Tabora (Wavulana na Wasichana) walishangaa sana kuona “matokeo ya ukubwa”!
  Waziri mmoja wa tangu uhuru (jina limehifadhiwa sijui kwa sababu gani) ndiye alikuwa mgeni rasmi. Siku ya mwisho ya kukagua vibanda, Waziri huyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa na viongozi wengine wa ngaziza juu wakitembea kwa miguu.
  Nyuma kulikuwa na gari la Mercdes-Benz la serikali la Mkuu wa Mkoa likifuata taratibu. Kwenye kiti cha nyuma walikaa wasichana wawili, ambao wengi tuliwatambua walikuwa ni wanafunzi wa Tabora (Wasichana) Darasa la 14.
  Tulishangaa sana kuona kituko hicho huku tukizimwa kwa tetesi kuwa mmoja wa hao wasichana alikuwa ni mchumba wa Waziri huyo! Hata hivyo, tulisikia tu tetesi kuwa kitendo hicho hakikumpendeza Hedmistresi wa Tabora (Wasichana) Barbro Johansson – m-Swidi m-misionari.
  Din webbläsare kanske inte stöder visning av den här bilden.
  Marehemu Mama Barbro
  Licha ya kuwa m-Bunge wa Kuteuliwa, Barbro Johansson anasifika kwa mambo mengine mawili: Mosi, alikuwa muasisi wa shule ya kwanza ya wasichana nchini Tanganyika hapo Kashasha, Bukoba). Pili, aliokoa Tabora (Wasichana) kutokana na tishio la kutaka kuifunga shule hiyo.
  Viongozi wa serikali wakati huo hawakuepe skandali za “dangerous liaisons” na wasichana wa shule sekondari. Kwa mfano, wakati huo huo, kutoka Mara wakuu wawili walijikuta wakisimama mbele ya Rais Julius Nyerere, mjini Mwanza, kujibu tuhuma za “les liaisons dangereuses” na wasichan wa Bwiru Sekondari.
  Wakati huo Hedmistresi Inkpen (Bwiru Wsichana) alipeleka majina na vitanmbulisho (documentary evidences) vya barua za mapenzi kutoka kwa wakuu hao wawili kuja kwa wapenzi wao hapo shuleni. Zaidi, wakati wa kurudi shuleni, wasichan hao wawili wakati mmoja waliletwa na gari la Mkuu wa Mkoa la Benz kutoka Musoma hadi hapo shuleni badala ya kusafiri kwa meli.
  Badala ya Benz la serikali kuwashusha mjini Mwanza na, pengine, wachuke teksi au ki-basi cha Mwanza Development Corporation ((MUDECO), hilo Benz liliwashusha hapo shuleni wanafunzi wengine wakiowaona wakishuka.
  Wakati Rais Nyerere alipotembelea Mkoa wa Mwanza, alikutana na viongozi mbali mbali ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao. Hedimistresi Inkpen alimweleza Mwalimu Nyerere shida aliyokuwa nayo katika kulea wasichana hapo shuleni kwake kutokana na “wakubwa na vigogo” kuwaharibu hao wasichana. Alimpa ushahidi wa barua kutoka kwa viongozi hao wawili wa Mkoa wa Mara.
  Mara moja, Mwalimu alitoa amri ya kuwaita viongozi hao wawili wa Mkoa wa Mara waje mjini Mwanza. Kutokana na habari za kuaminika, viongozi hao hawakujua kwan nini Rais alikuwa akiwaita ghafla hivyo. Walidhani, pengine, Mwalimu alikuwa akitaka kuwapandisha vyeo! Walifika mbele ya Mwalimu na bila kuwaficha alitoa barua zao kwa hao wasichana. Viongozi hao wawili wa Mkoa wa Mara walibaki wakitetemeka tu.
  Mwalimu aliwaagiza awakute Dar es Salaam. Habari za kuaminika kutoka kwa hao viongozi wenyewe zilieleza kuwa hawakujua hitima yao! Mwalimu aliwaondoa hapo mkoani. Mmoja alipelekwa u-balozini China, na mwingine akabadilishwa na kupelekwa huko mjini Mbeya.
  Ishirini na tatu, mwaka 1964 serikali iliamua kuanzisha Mafunzo ya Jeshi kwa vijana wa sekondari ma-Darasa toka 12 hadi 14. Hapo Tabora (Wavulana) mafunzo hayo yaliongozwa na ma-Afisa wa Polisi (nafikiria walikuwa kutoka Kikosi cha Kuzuia Fujo (Field Force Unit) wa mjini Tabora. Kwa muda wa miezi miwili hivi (kabla ya mkakati huo kuondolewa) walituenyesha, ki-kweli ili kutuondoa kutoka u-raia kwenda u-jeshi.
  Ishirini na nne, kutokana na maono na uongozi bora wa Rais Julius Kambarage Nyerere, tukiwa Darasa la 14, serikali ililegeza masharti ya kuingia Chuo Kikuu. Mwanafunzi alitegemewa kushinda Principal moja na Subsidiary moja badala ya Principals mbili na Subsidiary moja.
  Ishirini na tano, niliiaga Tabora (Wavulana) na Tabora mjini ya akina Kiko Kids na Unyanyembe (Tabora) Jazz Band na kurejea kwetu Musoma nilipopata kazi katika Barclays Bank, na kuahidiwa kupelekwa masomoni Uingereza. Lakini sikuwaamini Meneja Cowell (m-Uingereza) na Msaidizi wake Mazzarello (m-Goa) kuwa wangenipeleka kweli.
  Ishirini na sita, niliamua kujiunga na Mlimani only to be sent down baada ya miezi kama minne hivi, shauri ya Mgomo wa Jumamosi Oktoba 22, 1966. Nilirudi Musoma na kuchekwa na hao akina Meneja Cowell (m-Uingereza) na Msaidizi wake Mazzarello (m-Goa). Sana sana, chekwa hiyo ilifuatia kutangazwa kwa Azimio la Arusha na kutaifishwa kwa ma-benki ya ki-geni! Walinionyesha matayarisho waliyokuwa wameyafanywa kukidhi masomo yangu huko London: maombi ya shule na pasipoti!
  Hatimaye, tulisamehewa; tukarudi kwenye alma mater yetu Mlimani kutoka “Disapora”.
  The rest is history!
  Msomaji, asante sana kwa kunisoma. Huenda utanisoma tena!
  E-mail: [email protected]
  CHANZO: Kwanzajamii.com
   
 10. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,292
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 38
  hii ni safi ukiwa kwenye treni dar- lusaka
   
 11. umkhonto

  umkhonto Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  very interesting..no specific focal point,but there is a lot to learn about all aspects of life in those days..although there is a deliberate effort to conceal his identity..
   

Share This Page