Bora mgambo kuliko jeshi la polisi la aina hii.

bakuza

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
490
100
Katika hali ya kuhuzunisha maana siwezi sema ni ya kuchekesha kwa sababu ni hatari kwa taifa na watu wake pale tunapokuwa na mkanganyo wa kusimamia haki na kweli ktk Taifa letu.Huu udhaifu umejitokeza mara nyingi kuanzia kwa Rais wa nchi,waziri mkuu,Spika wa bunge na hata watendaji wa chini yao.Hato yote tulifumbia macho tukijifariji kuwa hao wote ni viongozi wa kisiasa tukiamini kuwa siasa ni mchezo mchafu na uongo uliopotiliza kama walivyotuaminisha.
La haula....hatujakaa sawa na Jeshi letu la polisi likageuka chombo cha propaganda na siasa bila usajiri wa muda au wa kudumu toka kwa msajiri wa vyama baada ya kuanza kupeleka mambo yake kama wanasiasa wanchi hii,kwa kutoa kauli tofauti zinazokinzana tena toka kwa viongozi wa ngazi za juu.Hebu fatilia kauli za makamanda hawa wa polisi hapa chini
1.Kaimu Kamanda wa mkoa
"Machi 9 mwaka huu Kaimu kamanda wa mkoa wa Morogoro Hamisi Seleman alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.


2.Kamanda wa mkoa

"Machi 11 mwaka huu KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema "Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo"Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji".

"Hata silaha ambazo alikuwa nazo Waziri Malima ni za kawaida na anazimiliki kihalali" alisema Chialo.
Makubwa haya


Hivi nani muongo kati ya hawa je ni Naibu kamanda aliyeenda eneo la tukio kwa ukaguzi na upelelezi wa awali au kamanda wa polisi aliyepelekewa taarifa ofisini? Wahenga walishatwambia "ukitaka kuwa muongo uwe na kumbukumbu" na "Heri uyatima wa wazazi kuliko uyatima wa akili" Hebu unganisha dot ktk maandishi ya rangi nyekundu na utafakari je Jeshi la aina hii kuna haja ya kuwa nalo au tuvunje tuanze upya?

....Nawasilisha.......
 
Halafu jana wanatutangazia eti "waliomuibia" Naibu Waziri wanaswa. Waliomuibia walikuwa wangapi wakati nyie mlikuta nyayo za mtu mmoja?
 
Halafu jana wanatutangazia eti "waliomuibia" Naibu Waziri wanaswa. Waliomuibia walikuwa wangapi wakati nyie mlikuta nyayo za mtu mmoja?

Jeshi la kiinteligensia na hufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu....ebo..sipati picha.
 
Back
Top Bottom