jouneGwalu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,687
- 1,780
Imeshakuwa kawaida, kama kawaida yetu watz, Saiv ukisikiliza redio, ukisoma magazeti na karibia media zote zinapokuwa zina ripoti mambo ya burudani na hasa muziki, utasikia neno muziki wa "bongo fleva"
Bongofleva, inatafsirika kama ni muziki wa kibongo yaani wa kitanzania sababu saiv neno bongo limekuwa na maana ya Tanzania.
Sina tatizo kabisa na neno "bongofleva".
Binafsi linanikumbusha kipindi cha Mike Mhagama wa Radio One enzi zile za mwanzoni sana mwa miaka ya 2000,
Yeah, bongofleva lilikuwa jina la lipindi cha Mike Mhagama wa Radio One, Na hakukuwa na cha kukushtusha sababu karibia redio zote zilikuwa na vipindi vyake vilivyokuwa vinaenda na kasi ya mabadiliko ya kimuziki hasa hapa nyumbani.
Nakumbuka Eastafrika Redio kulikuwa na Dj JD kwenye kipindi chake cha The cruise alikuwa na session ya "bongo explosion"
Clouds fm kulikuwa na Boneventure Kilosa na Dj Steve B, wao kipindi chao kilikuwa kinaitwa "fleva ya bongo"
Redio Uhuru alikuwepo Sebastian Maganga, sikumbuki jina la kipindi na Times Fm simkumbuki mtangazaji wao maarufu wa kipindi hicho ila wao walikiita "bongo hits"
Vipindi hivyo vyote vilianzishwa sababu kwa muda husika muamko wa vijana wa kibongo kurekod nyimbo za "kisasa" ulikuwa mkubwa.
Hivyo nyimbo za wasanii wanaoimba "nyimbo za kisasa" (bila kuzingatia aina ya muzik msanii anaofanya) zikawa nyingi na zikawa na wapenzi wengi sana, hii ndio ilipelekea kuwepo kwa vipindi hivyo maalum.Kwa kutokea hapo naona unaweza ukaona kuwa kumbe "bongo fleva" ilimaanisha kuwa mkusanyiko wa nyimbo za vijana wa kitanzania, "kizazi kipya".
Kwa kulijua hilo waendeshaji wa vipindi hivyo, walivigawa vipindi vyao kwenye aina ya miziki kutokana na mwanamuziki alivyojitambulisha na alivyokidhi aina husika ya muziki, kwenye kipindi cha bongofleva au hivyo kukawa na bongo hip hop, bongo R n' B (hiyo ndio ilikuwa sanasana) na baadae ikaja bongo zouk.
Kwa mtiririko huo, ni inashangaza leo hii kusema Bongofleva ni aina ya mziki unaoimbwa na vijana wa kitz.
Aina Fulani ya muziki unatakiwa uwe na sifa za kufanana kimaadhi, vionjo, mpangilio, mirindimo na vitu vingine vyote vinavyoufafanua muziki husika ndio maana hip hop hata iimbwe kona gani ya dunia bado utajua tu hii ni hip hop, kitu hicho hamna kwenye bongofleva yetu.
Pia kuna mfano mzuri wa "GENGE" hii ni aina ya uimbaji (unahusisha aina ya rap) unaofanywa na jamaa wa Kenya, kwa kiasi fulani kikubwa wamefanikiwa sana kutengeneza aina ya muziki ambayo inasifa zinazoendana, kutokea kwenye mfano huo naona kwa wenzetu imekuwa rahisi sana kuliko wangejikita na "Kenya fleva" na uwepo wa GENGE haujazuia aina zingine za muziki.
Wadau husika hapa kwetu bongo, nadhani wanahitaji kuweka sawa vitu kwenye soko, hiyo itasaidia sana wanamuziki wenyewe, kwani kwa sasa ni kama wanafanya kitu wasichokifahamu hivyo ni vigumu wao kuwa bora sababu hamna standard za kuwapimia hii nayo inachangia sana wasanii (hasa wa hiyo bongofleva) wetu kufanya vibaya kwenye anga za kimataifa.
Bongofleva ni kitu tata bado, ndio maana wanamuziki wote makini na wanaojitambua hawapendi uwaite kwamba wanaimba bongofleva. Ndio maana Kikosi Cha Mizinga walikuwa watata sana katika kujenga mahusiano na wanaoimba hiyo Bongofleva, hata sasa kuna mstari wa wazi kati ya wanaoimba R n' B ( mfano Ramma D, Steve, Ben Pol nk) Hip-hop (mfano One, Stereo, Nickmbishi, Kala Pina, FidQ, Joh Makini nk)
Kwa wadau kuendekeza hii Bongofleva inapelekea hata watu wanaoimba aina nyingine kabisa ya muziki ambayo haijazoeleka hapa kwetu kusahaulika, kitu ambacho sio kizuri kwa jamii yetu, mfano wabongo wengi hatumjui Corolla Kinasha!
Huyo dada ni azina kubwa sana, nadhani ni miongoni mwa wanamziki wachache sana wanawake wa kiafrika wanaoimba Afrikan Jazz.
Tukifungua milango, nje ya Bongofleva kuna aina nyingi sana za muziki ambazo nadhani wabongo wanastahili kujifunza na kuzijua kwa kadiri inavyofahamika kuwa hatuna aina yetu ya muziki kama taifa na tusidanganyane, aina ya muziki wa taifa haitungwi kama tunavyotaka kulazimisha kupitia Bongofleva bali ni matokeo ya historia yenyewe!