Majaji (Judges) wa Bongo Star Search wanadhalilisha Washiriki
Wanajamii,
Leo kwa mara ya kwanza nashuka katika jamvi hili nikiwa na maswali ya kuuliza. Napenda kuuliza kwa kuwa sina uhakika kama ninafahamu maana ya neno la kingereza celebrity yaa inaweza ikawa ni umaarufu au kusema ni mtu maarufu. Kama ndiyo hapa ndani ya nchi yetu nzuri Tanzania watakuwepo celebrity wengi sana. Lakini pamoja na kuwa nao kuna mambo yanafanywa na hao watu ninaowaita maarufu ambayo hayana maana kabisa katika jamii yetu. Hivi Juzi Jumapili ya tarehe 10 Mei, 2009 nilibahatika kutazama kipindi maarufu kwenye Luninga kinachokwenda kwa jina la Bongo Star Search kinachorushwa na Stesheni ya ITV. Kuna hawa watu maarufu ni maarufu kweli na hata kipindi chenyewe ni maarufu lakini kwa sasa naona kama kimekwishapoteza umaarufu.
Maswali yangu ni haya: Hivi nini maana ya kipindi Hiki? Kwa ajili ya nani? Je washiriki wale wanavyotendewa na hao majaji (Judges) au kwa lugha ya kawaida waamuzi ni sahihi? Iweje kutumia lugha chafu kwa washiriki? Kuna mifano kama miwili iliyojitokeza juzi ..moja kwa mwanadada na wa pili kwa mwanakaka .. walilalilishwa kwa kweli.
Mwanadada: Aliimba kwa kadiri ya uwezo wake. Wakati wa majaji kutoa comments zao .mmoja alidiriki kumwambia huyu dada hawezi kuimba anachodhani anaweza aende akazae tu Hii maana yake nini? Ndio kujaji kweli?
Halikadhalika;
Mwanakaka: kama alivyofanyiwa mwanadada naye kaambiwa akatafute ma sugar mummy kwa vile alikuwa smart Mtanashati ..inatisha
Sikuweza kujua kama kweli huyu Jamaa ana akili nzuri. Naomba nimtaje tu kwa sababu nia ni kumrekebisha na si kumsema vibaya. Ni kati ya wale majaji watatu anajiita P Funk. Mimi Binafsi na labda baadhi ya waliobahatika kutazama kipindi kile hafurahishi kwa comments zake. Anajaribu kuwe critique kama alivyokuwa Salama Jabir lakini si ki-hivyo. Ajaribu kuwa yeye asifanye vitu kwa kuiga lazima ataharibu.
Naomba tujadili hili kwa busara kwa ajili ya kuboresha kipindi vinginevyo sijaona maana yake kama hali itaendelea kama hivi. Umaarufu usiwe kero .