Bongo Star Search 2008 Inasikitisha

Ni wazi kwamba kulikua na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uteuzi wa mshindi. Kuna kila harufu ya ufisadi na udanganyifu kwa kila stage ya mashindano haya. Mshindi anatangazwa wakati kura zinaendelea kupigwa bado, pia kutotangaza kura ni kupanga matokeo. Hii inafanana kidogo ya uchaguzi wa nchi jirani. Cha msingi baraza la sanaa pia linapaswa kuwajibika kwa kushindwa kusimamia vizuri uendeshaji wa mashindano haya. Baraza likijiuzulu sio vibaya sana kwa kushindwa kazi.Ieleweke pia hii ni biashara, kura tunazopiga tunakatwa hela,matangazo ya biashara na viingilio mlangoni ni mamilioni ya hela, ndio hizo hizo hutumia kuwalipa allowance,na washindi. Leo hii napiga kura na ninakatwa hela halafu wanaleta utani, pia Benchmark iwajibike kwa kua na baadi ya Majaji wenye wiwango vya chini, wangekua ni viwango vya wastani au juu wangeyaona haya yote. Pia wangeacha kuangalia eti mwele zako nimezimind, mpasua uko safi,Mmwaa weekend,sauti lako bovu haliyanifikisha n.k. Tuamke

Soma Hii Kutoka Global Publishers

Shindano lenye umaarufu mkubwa hivi sasa nchini la kumtafuta msanii chipukizi mwenye kipaji cha muziki, Bongo Star Search (BSS), limeingia lawamani kwa kuonesha kumjua mshindi mapema, katika fainali zilizovuta hisia za wengi zilizofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl, iliyopo ndani ya jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita.Licha ya lawama hiyo, lakini wananchi wengi bado wanaliunga mkono na kulikubali shindano hili, hasa pale lilipompa taji mwaka jana Mtoto wa Bagamoyo, Jumanne Idd katika fainali zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Ikumbukwe kuwa ni ufanisi uliooneshwa na waratibu wa shindano hilo ambalo lipo chini ya Kampuni ya Benchmark Production mwaka jana, ndiyo uliolijengea heshima na kuwafanya watu wengi kulifuatilia na kutumia muda wa hewani wa simu zao kwa kutuma sms kuchagua washindi.

Lawama zinazotolewa kwa fainali za safari hii, ni kauli zilizokuwa zikitolewa na majaji wakati washiriki walipomaliza zamu zao za kuimba, ambapo ilionekana majaji tayari walikuwa wanamjua mshindi atakuwa nani katika fainali za mwaka huu, licha ya ukweli kwamba kura zilikuwa zikiendelea kupigwa.

KAULI ZA MAJAJI ZILIKUWA HIVI!
Alipomaliza kutupa kete yake ya pili, mshiriki nambari 03, Rogers Lucas, jaji ambaye ni mwanamuziki mkongwe John Kitime, alimuambia kuwa baada ya BSS, asiache muziki. Ukiiangalia sentensi hiyo na kuichambua neno kwa neno, utagundua kuwa Kitime alikuwa na matokeo yanayoonesha kwamba Rogers si mshindi.

Kauli ya Jaji Mkuu, Madam Rita, nayo inathibitisha haya! Mara baada ya Rogers kumaliza kuimba, alimuambia kuwa laiti BSS ingekuwa inapata washindi wawili, naye angekuwemo. Sentensi hiyo nayo ilikuwa inaweka wazi kuwa mshindi alikuwepo ambaye wao walishamjua mapema.

Aidha, kauli za majaji Salama Jabir na Joachim Kimario ‘Master Jay’ walipokuwa wanawaponda washiriki Yohana Simon na Maangaza Nyange, kuwa waliimba chini ya kiwango, ni wazi ziliashiria kuwa mshindi wa kwanza mpaka wa tano, walikuwa wanamjua.

WATANZANIA KUHIMIZWA KUPIGWA KURA
Matokeo yalijulikana kabla ya kuingia Blue Pearl, lakini bado Watanzania walikuwa wakihimizwa kupiga kura ili kuchagua washindi. Kwa utaratibu huu, majaji hawakupaswa kuonesha wanamjua mshindi wakati kura zikiendelea kupigwa, kwani kitu chochote kingeweza kutokea na kubadilisha matokeo ya awali.

MAJAJI
Majaji Salama Jabir na Master Jay wanapaswa kujirekebisha na kuacha tabia zao za ‘kukandia’ katika shindano lenye hadhi kubwa sasa kama BSS. Madam Rita anatakiwa kuliangalia sauala hili mapema na ikiwezekana, mwaka ujao awapige chini na kuwachukua watu wenye heshima zao ambao watakidhi hadhi ya shindano.

Jaji msema hovyo wa nini? Anayeponda badala ya kutoa ushauri ni kwanini aendelee kuwepo? Alitumia busara gani Master Jay kwa kumuambia Maangaza kuwa zaidi ya mpasuo wa nguo yake, hana anachoweza katika muziki. Hii ni kauli ya kimuziki au ‘kukandia’?

Walishamjua mshindi mapema, ilikuaje wamponde Yohana mpaka kumkatisha tamaa, wakati mashabiki walikuwa wakimshangilia kwa nguvu? Madam Rita anatakiwa kutafuta majaji wanaoweza kutoa ushauri hata kisaikolojia, na siyo kukatisha tamaa. Wanaokosoa kwa kujenga na si wapondaji.

UKUMBI
Kamati ya maandalizi haikufikiria kwa makini kuhusu ukumbi muafaka wa shughuli kubwa kama ile. Ukumbi wa Blue Pearl ni mdogo na una joto jingi kiasi kwamba mashabiki walioingia walii shia kupata mateso badala ya kuburudika. Idadi ya watu waliobaki nje huku wakiwa na tiketi zao mkononi, ilikaribiana na ile ya waliokuwemo ndani, kwahiyo kuna watu waliolipa hela bila kuona shoo.

JUKWAA
Katika kipengele hiki, waandaaji wanastahili pongezi kwakuwa lilitengenezwa kimataifa na kumuwezesha kila mtu aliyepata nafasi ya kuingia ndani, kuona shoo bila matatizo.

SAFARI NDEFU
Madam Rita anastahili pia pongezi kwa kuianzisha BSS na kuifikisha hapa ilipo. Amewafungulia milango vijana wenye vipaji na kuweza kujipatia ajira. Mwaka jana alionesha mfano, mwaka huu pia amejitahidi, ukichanganya na kuwaleta wasanii ndugu kutoka Jamaica, Naila na Nyanda Thorbourne a.k.a Brick & Lace, ni safari ndefu kweli.

JUMANNE IDD NA MISOJI NKWABI NI NDUGU
Wanatoka kijiji kimoja ndani ya Wilaya ya Bagamoyo, Pwani. Na baada ya Misoji kutangazwa mshindi, Jumanne ‘alitusapraizi’ kuwa ‘mdada’ huyo ni ndugu yake kwasababu wanatoka kata na kijiji kimoja pia huwa wanaitana kaka na dada

Mkombozi;
Asante kwa link hio from global publishers, ila nataka nitofautiane na wewe kidogo kuhusu suala la BASATA kujiuzulu, personal i dont think kama kuna U mantiki wa BASATA kujiuzulu so far, ila tu as far as shindano linahusisha watanzania tulio wengi ambao ushiriki wetu wa kupiga kura invovles pesa then Benchmark they are supposed to te ACCOUNTABLE forour money! na hii itawezekana vipi basi?, its through kutangaza matokeo ya kila awamu ya kura ambazo kila mshiriki amepata!, then nafikiri kuwa na majaji ambao no reliable, sio every TOM AND JERRY akae pale na kubwabwaja tuu! unless otherwise mi nakwambia BSS no sooner will be a peace of crap!

Mimi ilo swala la Misoji na J4 kutoka kumoja wala sioni kama lina umhimu as far as mtu kashinda kiuhalali!, hata wawe wanatoka the same house no problem ila swala la msingi ni kujua DID SHE TRUELY DESERVE THAT?
 
Lengo la mashindano ni zuri lakini uendeshaji una mashaka sana
Tangu mwaka jana Jumane Idd alibebwa hata yule dada aliyekuwa wa pili alipewa kwa sababu ya ujauzito.KALA JEREMIA NA ABUBAKAR walistahili kuwa washindi mwaka jana JUMANNE anaweza kuimba nyimbo za wa2 nadhani tumedhibitisha kutokana na album yake ni mbovu pamoja na kupewa promosheni kubwa but hamna kitu
Nafikiri watu wamesikia nyimbo za KALA na ABUBAKARI wamapoof kuwa walistahili kushinda.
Mwaka huu mshindi alipangwa lazima awe MSICHANA
Huyo misobi hkustahili kuingia hata TOP10
Wasichana wote hakuna aliyestahili kuingia TOP 5
ROGERS LUCAS NDIYE ALIYESHINDA
 
it was a big joke, that girl try to imitate whitney, yaani niliziba masikio kwa aibu, hivi kwanini watanzania tunapenda kufanya vitu kwa ubabaishaji? why?
 
Back
Top Bottom