Bongo nako kuna Wahafidhina japo ni wachache

Mchekechoni

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
279
19
Siasa za Tz(Bongo!) zimetawaliwa kwa kificho na mitazamo hasi ya kihafidhina na sio ya kiliberali kama chama tawala kinavyotaka wananchi waamini.

Mwelekeo huu wa kiutawala ndio haswa chanzo cha taifa letu kuwa nyuma kimaendeleo kwa jinsi ambavyo watawala wanakumbatia uozo wa kila aina na kushindwa kukata mirija ya kifisadi inayonyonya jasho la watanzania na raslimali zetu ambazo ndio utajiri wa nchi hii. Miaka 50 ya uhuru inaweza sasa kulinganishwa na just 5years of independence.

Hatua za kuchukua ili kuleta maendeleo ya haraka na kufidia muda uliopotezwa na watawala kupiga mark-tym bila ya kusonga mbele, ni pamoja na kuleta mapinduzi ya viwanda vidogovidogo katika wilaya zote nchini kwa kutumia wataalam wetu na malighafi tulizonazo, kupunguza mporomoko wa thamani ya fedha yetu na kushusha kiwango cha inflation.

Tunapoelekea kwenye kikao kijacho cha Bunge la Bajeti mambo haya ni muhimu yajadiliwe kwa kina na wabunge wetu ili kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli na ukuaji wa uchumi ulio tangible hata kwa mwananchi wa kipato cha chini.

Uhafidhina na ufisadi kwa pamoja ndio chimbuko la umaskini wetu, je wazalendo wenye uchungu sana na taifa hili hawatakuwa tayari kuifia nchi yao kama ilivyokuwa kwa kijana mwanamapinduzi Thomas Sankara wa kule Burkina Faso?

If anything, let it be. But in my case, I've vowed to die for my country! It's now or never, freedom is ours today!
 
Back
Top Bottom