Bongo Movie's bila Mzee Majuto walambwa 2-0

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
Timu ya Soka ya waigiza Filamu hapa nchi jana ktk uwanja wa Taifa imepokea kipigo cha goli 2-0 toka kwa timu ya wasanii wa Muziki wa kizazi kipya.

Wakicheza bila nahodha wao Amri Athuman ama King Majuto timu ya waigiza Filamu walionekana kupwaya sana ktk safu ya ushambuliiaji na kupelekea mabeki wa timu ya masharouharo muda mwingi kupumzika.

Nahodha Majuto anayesumbuliwa na Back Injury aliyoipata wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mechi hiyo amesema kwamba ni wazi kuwa kukosekana kwake uwanjani ndio sababu ya timu yake kupoteza mechi hiyo na akasema...''UNAONA BWANA, KAMA MIMI NINGEKUWA NIMESIMAMA PALE MBELE NI WAZI KUWA NINGEKUWA NAWAKUSANYA MABEKI WAWILI, NAWALALIA KISHA NAPIGA BUNDUKI...AU NARUDI KATIKATI NA KISHA NAANZA KUWACHUKUA MADEKI KWA CHENGA ZENYE UDHU NA KISHA NAACHIA MKWAJU''...

baada ya kusema hivyo alicheka na kutroti kama mchezaji wa ukweli vile na kisha akaendelea na porojo zake ''NAKUMBUKA MWAKA 75 NIKIWA NACHEZA NAMBA 9 YALIMWAGWA MAJARO NA KISHA MWANAUME NIKAJIKUNJUA TIC TAK...EE BWANA (akacheka kwa nguvu kisha akaendelea)...MOJA KWA MOJA GOLI, BASI MPIRA ULIVYOISHA WAREMBO WOOTE WAKAJA KWANGU...MARA HUYU ASEME MAJUTO TWENDE UKAOGE KWANGU, MARA YULE ASEME MAJUTO MIE LEO NIMEPIKA BIRIANI, MARA YULE ASEME MAJUTO BABU WEE TWENDE NKAKUCHUE....ILI MRADI SHALI MINAL BALAA''...Alimaliza mbwembwe zake huku akiachia cheko la karne.

Mechi hiyo ilikuwa mahsusi kwa ajili ya harambee ya kuwachangia ndugu zetu waliopata madhara kutokana na milipuko ya Mabomu huko Gongo la mboto.
 
Back
Top Bottom